PreGE2025 Chadema kutoshiriki Uchaguzi, hasara kwa CCM, Tume na jamii hizi hapa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
TOFAUTI YA MIMI NA WEWE NI KUBWA SANA, MIMI NON PARTISAN NA SI MWANACHAMA WA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA, SO I AM FREE KUTOA MAWAZO YANGU HATA KAMA YANAKUUMIZA, HASA KWA HILI LA CHADEMA KU-COMMIT SUICIDE DELIBERATELY HALAFU INALAUMU CCM, MI NASEMA BLUNTLY MMEFANYA MAAMUZI AMBAYO SI SAHIHI MNGEINGIA ULINGONI TO FIGHT A FIGHT MNGEKUWA MMEWATENDEA HAKI WATANZANIA.
Unawahitaji Chadema washiriki uchaguzi bila mabadiliko?? Unawahitaji Wanachadema wauawe wangapi kwenye chaguzi ndipo uwaelewe??

Uchaguzi siyo vita ni ushindani wa hoja kwenye kunadi sera. CCM haiwezi tena kunadi sera zake bila kutumia mitutu ya bunduki pamoja na mahakama kuwanyamazisha Washindani/Wapnzani wao.

Tulio wengi tumechoshwa na maigizo ya uchaguzi. Ni bora CCM waendelee kuteuana kuliko kutangaza uchaguzi wa maigizo kupitia Tume ya Uchaguzi mchongo na Wapinzani tukabaki salama. Hatuko tayari tena kuuawa au kupoteza ndugu zetu kisa chaguzi.
 
Wengi wapi?? Chadema wapiga kura hawanaga zaidi ya wafanya propaganda mitandaoni

Unaukumbuka uchaguzi mdogo wa Mbeya vijijini? Baada ya CHADEMA kuenguliwa uchaguzi ukafa.
 
Unawahitaji Chadema washiriki uchaguzi bila mabadiliko?? Unawahitaji Wanachadema wauawe wangapi kwenye chaguzi ndipo uwaelewe??

Uchaguzi siyo vita ni ushindani wa hoja kwenye kunadi sera. CCM haiwezi tena kunadi sera zake bila kutumia mitutu ya bunduki pamoja na mahakama kuwanyamazisha Washindani/Wapnzani wao.

Tulio wengi tumechoshwa na maigizo ya uchaguzi. Ni bora CCM waendelee kuteuana kuliko kutangaza uchaguzi wa maigizo kupitia Tume ya Uchaguzi mchongo na Wapinzani tukabaki salama. Hatuko tayari tena kuuawa au kupoteza ndugu zetu kisa chaguzi.
I support G55, fight the fight within the battle field, so pumzikeni nje, karibuni tena 230/31
 
Na:Mathias Byabato

Binafsi uwa siandiki sana kuhusu mambo ya siasa. Leo nimeona nisaidie muktadha kadri ya uelewa wangu. Kwa watu wanaojua mantiki na umuhimu demokrasia katika taifa lolote wanajua hasara kadhaa zitazojitokeza iwapo itasalia hivi hivi Kwa chadema kutoshiriki uchaguzi wowote 2025 hadi 2030.

Kwa wasiojua ni kwamba jamii ya kawaida, Taifa,CCM,Serikali na Tume watapata hasara kubwa kuliko chadema yenyewe.

Twende sawa.

Chadema
Kwa chadema hasara kubwa wanayoweza kupata ni kukosa ushawishi,uongozi na kupungua nguvu iwapo tu madai yao hayatetelezwa kabisa hadi 2030. Madai makubwa ni kutokuwepo Tume huru ya Uchaguzi,uwanja sawa WA ushindani kati yao na CCM,Sheria za uchaguzi na watu wao kutopotea au kufa kutokana na michakato ya Uchaguzi.

Iwapo tu yatatekelezwa Kwa kipindi hicho chadema itapanda thamani sana. Kama Hali itasalia hivi hivi na madai yao basi chadema itakuwa imejimaliza.

Aidha Chadema itapoteza nafasi ya kushiriki katika siasa za kitaifa, hivyo kupunguza umaarufu na msaada wake kati ya wafuasi. Wengi wanaweza kuona chama kama kisichokuwa na mkakati au uwezo wa kuongoza.
Kutengwa na Mifumo ya Uongozi: Kwa kususia, chama hakitapata wabunge, madiwani, au nafasi za urais, hivyo kitapoteza fursa ya kuwa na sauti katika Bunge au mabaraza ya uongozi, na hivyo kupunguza uwezo wake wa kuleta mabadiliko.

CCM

Kwa Chama Tawala
Kukosekana kwa Ushindani wa Kisiasa: Chama tawala kitapata ushindi rahisi bila upinzani wa maana, lakini hii inaweza kusababisha ukosefu wa changamoto za kiwango cha juu, na hivyo kupunguza ubora wa sera zao na uongozi.Watajihesabu wamemaliza uchaguzi mkuu baada ya ule WA ndani. Bajeti yao ya Uchaguzi mkuu itafumuliwa sana. Watakuwa na jukumu la kuanza kusoma mbinu za kuendesha siasa Kwa kutazama hoja za vyama vingine nje ya chadema.

~Changamoto za Uhalali:~ Ushindi bila upinzani wa nguvu unaweza kutiliwa shaka kimataifa na ndani ya nchi, na kuathiri uhalali wa chama tawala kama CCM. Wanaweza kuonekana kama wamechukua mamlaka bila ridhaa ya kweli ya wananchi.

Hapatakuwepo na siasa za hoja. Kuibua hoja na kujibiwa. Kuna suala la kuibuliwa Kwa vijana wenye nguvu kisasa hapa itakuwa ngumu kuwapata. Vijana wapya wenye nguvu kisasa wanapatikana kutokana na siasa ngumu za ushindani. Mbinu za ujasusi WA kisiasa nk hazitakuwepo.Watu kama akina Katambi,Kitila Mkumbo,Kafulila,Waitara,mashinji,Wasira ,zitto,Halima mdee nk ni mazao ya kuwepo ushindani kati ya CCM na Chadema.

Itakuwa ni ngumu sana Kwa CCM kuwa na hoja Mpya za kila siku KATIKA kampeini ambazo uibuliwa na wapinzani WA kweli kwao. Wapo ACT Wazalendo,CUF nk lakini bado hawakuwa na nguvu ya mtandao kama Chadema.

Taifa
Kudhoofika kwa Demokrasia: Kukosekana kwa chama cha upinzani chenye nguvu kushiriki kutasababisha demokrasia dhaifu, kwani uchaguzi hautakuwa wa ushindani wa kweli. Hii inaweza kuleta mfumo wa karibu na chama kimoja, ambao unaweza kuathiri uhuru wa kisiasa.
Kupungua kwa Uwakilishi wa Maoni Mbalimbali: Wananchi wanaounga mkono Chadema watapoteza sauti yao katika mifumo ya utawala, na hivyo kusababisha kutokuwepo kwa uwakilishi wa maoni tofauti, ambayo ni msingi wa taifa lenye ushirikiano. Nchi yetu ni ya mfumo WA vyama vingi. Hali hii itaonesha jicho baya kimataifa.

Kwa jamii
Kutakuwa na tatizo la Uchumi kwani Mzunguko wa Fedha za Kampeni utapungua.
Kampeni za uchaguzi huchochea uchumi wa ndani kupitia matumizi ya fedha kwenye huduma kama usafiri, matangazo, mikutano, na bidhaa za kampeni. Kutoshiriki Kwa chadema kutasababisha kupungua kwa mzunguko wa fedha, na kuathiri wafanyabiashara wadogo, wauzaji wa chakula, na watoa huduma.
Pia kuna kupungua kwa Mapato ya Biashara za Ndani kwani biashara zinazotegemea kampeni, kama vile hoteli, kampuni za uchapishaji, na wauzaji wa fulana,kanga, zitapata hasara kubwa kwa sababu hakutakuwa na mahitaji makubwa ya huduma zao kwa kiwango cha kawaida.

Kwa Serikali
Kupungua kwa Imani ya Umma: Serikali inayoundwa baada ya uchaguzi usio na ushindani wa kweli inaweza kukosa imani ya umma, hasa kati ya wafuasi wa upinzani. Hii inaweza kusababisha mgawanyiko wa kijamii na kuathiri utulivu wa kisiasa.
Changamoto za Utawala wa Kimataifa: Serikali itakabiliwa na shinikizo la kimataifa kutokana na uchaguzi usioonekana kuwa huru na wa haki, na hivyo kuathiri uhusiano na wafadhili au washirika wa kimataifa.

Kwa Tume ya Uchaguzi
Kutokuwa na Uhalali: Tume ya Uchaguzi inaweza kushutumiwa kwa kushindwa kusimamia uchaguzi wa ushindani, na hivyo kupoteza uaminifu wa umma. Maswali yanaweza kujitokeza kuhusu uwezo wake wa kuendesha uchaguzi wa haki.
Kupungua kwa Maana ya Uendeshaji Uchaguzi: Bila ushiriki wa chama chenye nguvu, uchaguzi unaweza kuonekana kama wa “kawaida” badala ya tukio la kitaifa lenye maana. Hii inaweza kupunguza umuhimu wa tume na kazi yake katika kuimarisha demokrasia.

Hivyo Kwa ufupi.
Uamuzi wa chama cha upinzani chenye nguvu kama Chadema kususia au kuzuiwa kushiriki uchaguzi mkuu utaleta athari mbaya zinazoathiri wadau wote wa kisiasa na kiuchumi. Chama cha upinzani kitapoteza nguvu na ushawishi, chama tawala kitakosa changamoto za maana, taifa kitapoteza msingi wa demokrasia, uchumi utakosa mzunguko wa fedha, serikali itapoteza imani, na tume ya uchaguzi itakosa uhalali. Ili kuepuka hasara hizi, ni muhimu kwa vyama vyote kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi ili kuhakikisha ushindani wa haki na demokrasia imara.

Tukubali kupoteza?.

Mathias Byabato
Bukoba
0754527358
Nimependa ulivyoandika bila ushabiki. Duh utakuwa na kipaji na siyo limbukeni
 
Utaenda kupoteza muda kwenye chaguzi za maigizo?? October ni mbali lkn wahusika wana matokeo tayari.
Bora mmezira, so mtakuwa na project ya "No reform no election" bila bugudha for solid 5 years, in fact imekuwa ni blessing in disguise for CDM
 
CCM hawajali hata wakipata 200%.

They just dont care about voters
 
CCM hawajali hata wakipata 200%.

They just dont care about voters
Ni kweli maana huwa hawashindi kihalali. Huwa wanataka wapiga kura wawe wengi vituoni ili hata wakiiba uchaguzi ionekane wao ndio wenye wapiga kura. Kwao idadi ya wapiga ikiwa ndogo inasababisha ukweli wa wao kuwa na wapiga kura wachache kuvuja.
 
Turnout itakuwa ndogo sana na wabunge wengi na madiwani watashinda kwa kura chache hata raisi samia atapata kura chache unless watajiongeza kama kawaida yao kuongeza kura za ccm,
Wananchi wataona ccm inashindana na vyama dhaifa na nina Imani wengi hawataenda kupiga Kura, na mwaka huu wananchi ndio wataamini kuwa ccm huwa wanaiba kura,licha ya low Turnout ila utasikia Samia kapita kwa kura nyingi sanaa,
 
19-1, shall never be statistically significant, hata wangeshiriki wanakuwa kama hawajashiriki tu
Kwa maths kibishi za CDM uko sahihi, kwa sababu nyie mnaamini ni "odds man out " but life will go on with or without CDM, because your are not indispensable
 
Turnout itakuwa ndogo sana na wabunge wengi na madiwani watashinda kwa kura chache hata raisi samia atapata kura chache unless watajiongeza kama kawaida yao kuongeza kura za ccm,
Wananchi wataona ccm inashindana na vyama dhaifa na nina Imani wengi hawataenda kupiga Kura, na mwaka huu wananchi ndio wataamini kuwa ccm huwa wanaiba kura,licha ya low Turnout ila utasikia Samia kapita kwa kura nyingi sanaa,
Vyama vinavyoshiriki 17 ni less important kuliko uwepo wa CDM? , mnajidanganya sana, hata CUF walifikiri hivyo wako wapi sasa, we need just 2 political parties to contest
 
Back
Top Bottom