PreGE2025 Chadema kutoshiriki Uchaguzi, hasara kwa CCM, Tume na jamii hizi hapa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Tumeccm na Polisiccm sasa wamebaka na kunajisi haki ya kuchagua na kuchaguliwa, uchaguzi utakuwa haramu kwani umejaa mbinu zote za kishetani
mbona CDM mmejibaka na kujinajisi wenyewe
 
Labda pia nipanue maelezo yangu kwa vifungu:

1. “Hasara kwa Chadema kwa kutoshiriki uchaguzi” ni hoja dhaifu – sababu ni Tume isiyo huru.​

Katiba ya JMT (1977), Ibara ya 21(1):​

“Kila raia ana haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi ama moja kwa moja au kwa njia ya wawakilishi waliowachagua kwa hiari yao.”

Haki hii haiwezi kuwa halali ikiwa uchaguzi hauna usawa, mipaka imewekwa kwa upendeleo, au usalama wa wagombea haupo.

Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343:​


Inampa Rais mamlaka ya kuteua Mwenyekiti wa Tume, Makamu na Wajumbe wengine wote — hali hii huondoa uhalisia wa uhuru wa tume.

Kwa mantiki hiyo:
Vyama vya upinzani vinapokataa kushiriki katika muktadha huo, havikiuki Katiba wala sheria, bali vinaweka msimamo wa kisiasa wa kupigania mazingira huru.



2. Demokrasia si kushiriki kwa lazima bali ni ushiriki wa haki, huru na usawa.​


Katiba ya JMT, Ibara ya 8(1)(c):​


"Serikali itawajibika kwa wananchi na itatoa fursa kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za Serikali."

Demokrasia ya kweli inahitaji:
  • Uhuru wa kujieleza, kukusanyika, na kupinga bila hofu.
  • Wagombea kupata fursa sawa za kutangaza sera bila kuzuiwa na vyombo vya dola.

Historia ya Afrika Mashariki (Kenya 2007, Zimbabwe 2008):
Vyama vilisusia uchaguzi au kutishia kususia, ndipo katika mazungumzo ya kisiasa (political settlements), ilizaliwa Tume huru au serikali ya mpito.




Hoja ya “mzunguko wa fedha za kampeni” ni matusi kwa akili za watu.​

​

Sheria ya Gharama za Uchaguzi, Sura ya 6:​


Inasimamia matumizi ya fedha kwenye kampeni, lakini si sababu ya msingi ya kufanya uchaguzi.


Uchaguzi si biashara ya kuuza kanga, bali ni mchakato wa kupima sera, uadilifu, na uwezo wa viongozi.

Kukataliwa kwa uchaguzi wa maigizo hakumaanishi kuvuruga uchumi, bali ni kutetea msingi wa utawala bora.



4. Kususia uchaguzi ni mbinu ya siasa safi ya kushinikiza mabadiliko.​

Ibara ya 20(1) ya Katiba:​


“Kila mtu anao uhuru wa kukusanyika na kushiriki katika chama chochote cha kisiasa...”

➡ Hii pia inamaanisha uhuru wa kuchagua kutoshiriki au kususia kwa malalamiko ya msingi.

Mfano wa kihistoria:​


Zimbabwe (2008) – MDC ya Morgan Tsvangirai ilisusia duru ya pili ya uchaguzi baada ya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya wafuasi wao. Dunia ililazimisha majadiliano yaliyosababisha “Government of National Unity”.



5. Ushindi wa CCM bila ushindani si uthibitisho wa uimara, bali ni udhaifu wa mfumo.​

Katiba Ibara ya 3(1):​


“Jamhuri ya Muungano ni ya mfumo wa vyama vingi vya siasa.”
Mfumo wa vyama vingi unakuwa wa kimazoea tu iwapo:

  • Vyama haviruhusiwi kushindana kwa haki,
  • Kimoja kinapewa rasilimali zote, na kingine kinazuiwa kiholela.

Historia ya Tanzania:
1995–2020: Uchaguzi umeendelea kuwa na dosari nyingi, huku Tume ikishindwa kusimamia haki kwa vyama vyote — lakini ni mwaka 2020 ambapo hali ilifikia kiwango cha “dola kupora uchaguzi waziwazi.”



6. Tume ya Uchaguzi haina uhalali wa kikatiba au wa kijamii katika hali ya sasa.​

Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT:​


Inaeleza mamlaka ya Tume, lakini haielezi uhuru wa kimuundo, wala uwakilishi wa vyama vyote.


➡ Tatizo kuu:
  • Wajumbe wote wa Tume huteuliwa na Rais (ambaye ni mgombea).
  • Wasimamizi wa uchaguzi ni Wakurugenzi walioteuliwa pia na serikali ya chama tawala.
Hali hii ni kinyume na kanuni za Kimataifa za uchaguzi huru:
  • SADC Principles and Guidelines on Democratic Elections
  • African Charter on Democracy, Elections and Governance


Hitimisho:​

Kutoshiriki uchaguzi wa kidhalimu si uoga wala kukata tamaa — ni hatua ya kisiasa ya kupinga uhalali wa mfumo unaonyonya wananchi kisiasa.


Ni kutumia Katiba kwa maana yake halisi,
Ni kutumia historia kujifunza mbinu za kupigania uhuru,
Ni kushinikiza mabadiliko ya kweli, ya kudumu, kwa njia ya amani lakini thabiti.
 
Ni Bora usishiliki shindano kuliko kushiliki shindano ambalo huwezi kushinda na mshindi Ana julikana
 
19-1, shall never be statistically significant, hata wangeshiriki wanakuwa kama hawajashiriki tu
 
Kitu ambacho unatakiwa kuelewa wakati wa uchambuzi wao

Chadema ,haitafifia kamwe na imejipambanua haiko Kwa ajili ya tamaa ya kutawala tu ,kupitia kataa Yao uchaguzi ,imewapa kukubaliwa na jamii maradufu

imeaminisha haipo Kwa ajili ya tamaa ya utawala tu ,bali inajali jamii
 
We poyoyo umeandika upupu tafuta kazi ya kufanya. Tuna vyama 19 na 18 vinashiriki uchaguzi, hao nyumbu wameamua kususa, demokrasia iko pale pale tena ni kubwa sana.
 
Na mtashuhudia uchaguzi wa baridi kuliko barafu.
Sioni hata sababu ya kupoteza pesa za kampeni kwa mtu ambae yuko serious na nchi yake.
We wachangie hao nyumbu hakuna atakayekuomba mchango wa hela ya kufanyia kampeni.
 
 

Attachments

  • 6026553-bf15b8f6f927c72fa16d6bb328a5e41f.mp4
    14.1 MB
Kura zipi nyingi kutoka wapi? Wakati wapiga kura hawatajitokeza kwa wingi
We ndio hautajitokeza, kimsingi wengi wenu mnaoandika humu si wapiga kura, hamna ht kadi ya kupigia kura. Watanzania wazalendo halisi wazalishaji wa nchi hii watapiga kura.
 
Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 
Ubarikiwe wewe na uzao wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…