CHADEMA kuweni makini na mapokezi ya Lissu wakati huu wa msiba, mnafanya kosa la kiufundi, mtawapa watu mtaji wa kiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu

Uyo Mkapa hakuwahi kukemea maovu yaliyofanyika kama lile la Lissu kupigwa risasi lakini pia alitukana watanzania waziwaazi kuwa ni wapumbavu na marofa sasa mtu kama uyo ya nini kumuomboleza katika msiba wake
Mkuu ukitulia utaona msingi wa hoja yangu ni nini.
 
Naona tatizo la kusifu kila kitu bila kutafakari mara mbili halipo kwa ccm peke yao kumbe hata huku upinzani nako Kuna tatizo lile lile kila kinacho semwa lazima kisifiwe na kiungwe mkono bila ya kuangalia kitaleta matokeo gani.
 
Nchi ipo kwenye maombelezo,itakuwa si vyema kuwa na aina au dalili yoyote ya shamra shamra wakati wa ujio wa Lissu.Chadema wawe makini.
Wewe hapo ulipo unalia? Au huendi bar? Au humpi Mumeo tendo la usiku kisa kuna msiba? Lazima mambo mengine yaendelee. Just kama ilivyokuwa kwa Corona. Hatuwezi kujifungia ndani tukaacha kwenda kumlaki mwamba eti kisa kuna msiba
 
Waache wawape watu chakusema, yani we bendera zinapepea nusu mlingoti hadi nchi jirani, watu wanaacha shughuli zao za kitaifa kwenye nchi zao huko wanakuja hapa nchini alafu eti wewe mtanzania unaenda kufanya maandamano ya mapokezi.
Wewe ni lofa kweli,mbona huzungumzii kura za maoni za ccm zinazoendelea
 
Yaani ww ni pimbi hatari ..yaani kumpokea Lissu kunahusiana vp na kifo Cha mkapa??? Tutakuja kuaga na isitoshe Lissu lazima atakuja kuaga pia ...usitutishe usitutishe usitutishe
 
Wewe ni lofa kweli,mbona huzungumzii kura za maoni za ccm zinazoendelea
Dah we jamaa aisee! Kwahiyo huoni tofauti ya hivo vikao na sherehe za mapokezi/ sijui maandamano ya amani?
 
Yaani ww ni pimbi hatari ..yaani kumpokea Lissu kunahusiana vp na kifo Cha mkapa??? Tutakuja kuaga na isitoshe Lissu lazima atakuja kuaga pia ...usitutishe usitutishe usitutishe
Kukurupuka ni kubaya sana mkuu sidhani hata kama umesoma uzi wote na kuelewa nilicho andika wewe.
 
Kukurupuka ni kubaya sana mkuu sidhani hata kama umesoma uzi wote na kuelewa nilicho andika wewe.
Nimekuelewa sana , kwanza msibani tutakuja licha mkapa alituchukia sana sana sisi wapinzani...lkn tutakuja hvyo hvyo tu na Lissu pia atakuja kuaga japo alimfunga kipindi anapambania madini ya nchi hii ....
 
Nimetua hapo JNIA mchana huu nikitokea Zanzibar hali ni shwari kabisa kila kona kuna jicho kali.

Hatari sana.
 
Dah we jamaa aisee! Kwahiyo huoni tofauti ya hivo vikao na sherehe za mapokezi/ sijui maandamano ya amani?
tofauti iko wapi,lissu ni mapokezi nani amesema sherehe,wewe unang'ang'ania chadema wakati ccm wanaendelea na kura,hebu balance shobo zako hata kama hupendi chadema ongea basi facts siyo unaegemea upande
 
Naona tatizo la kusifu kila kitu bila kutafakari mara mbili halipo kwa ccm peke yao kumbe hata huku upinzani nako Kuna tatizo lile lile kila kinacho semwa lazima kisifiwe na kiungwe mkono bila ya kuangalia kitaleta matokeo gani.

Mfano wako hauingii kwenye post yangu yoyote hapo juu, au umesoma post nyingine, ndio ukaja kuniquote mimi? Ni wapi nimesifia chochote hapo juu? Au ni madhara gani yatatokea kwa Lisu kupokelewa kwa amani, na kwa ustaarabu kuwa kuna msiba wa kada wa ccm aliyewahi kuwa rais wa Tanzania?
 
Wewe hapo ulipo unalia? Au huendi bar? Au humpi Mumeo tendo la usiku kisa kuna msiba? Lazima mambo mengine yaendelee. Just kama ilivyokuwa kwa Corona. Hatuwezi kujifungia ndani tukaacha kwenda kumlaki mwamba eti kisa kuna msiba

Upeo mdogo wa kufikiri,pole sana.Unaongea sana kwenye keyboard lakini viongozi wenu wakipata matatizo hakuna mwanachama wa kawada hata mmoja anaejitokeza wazi wazi kuwapambania,mnabaki kulia lia mitandaoni tu.Mimi ninayeona mbali,na ninaye thamini sana mchango wa Chadema katika Taifa hili naumia sana kuona hawa viongozi wanaumizwa kiasi hicho.
Pia Chama kipo katika harakati za uchaguzi,hakuna tena muda wa kupoteza kwenye hayo makesi ya kipuuzi watayowafunguliwa.Bila shaka barua ya Polsisiem umeiona.Labda utanielewa.
 
tofauti iko wapi,lissu ni mapokezi nani amesema sherehe,wewe unang'ang'ania chadema wakati ccm wanaendelea na kura,hebu balance shobo zako hata kama hupendi chadema ongea basi facts siyo unaegemea upande
Punguza hasira mkuu ya haja gani ku panic sasa.
Mimi nimekuuliza huoni utofauti ya vikao vya ndani na hayo mapokezi ya Lissu? ( Ni sherehe ndio au tunaweza kusema ni maandamano ya amani)
 
Tatizo lako ni kwamba chochote kitakachopangwa na Chadema kwako wewe kitakuwa kizuri tu. kama huoni kuwa kukusanyika uwanjani kwa mapokezi na nina hakika lazima zitakuwa ni kama sherehe tu naweza sema hivo na sina shaka hapatakosa mabango yenye jumbe tofauti tofauti huku wakati huo huo nchi ipo kwenye maomboleza bendera ziko nusu mlingoti basi utakuwa na matatizo fulani mkuu.
Unaposema kada wa ccm aliyewahi kuwa rais wa Tanzania unamaanisha nini? Inamaana siku wapinzani wakichukua nchi tutakuja pia tuseme kuwa mfano Mbowe ni kada wa Chadema ambaye ni rais wa Tanzania? Huoni kauli kama hizo zinamalengo ovu mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…