Uchaguzi 2020 CHADEMA kwa sera hii, mtakomba kura zote za wafanyakazi wa nchi hii, na haya ndio maneno tunayotaka kuyasikia yatayomuangusha Magufuli na CCM yake


Tukiwa na wapiga walau asilimia 50 wanafikiria kama wewe tutafika mbali mkuu. Hongera kwa hilo.

Fikira za Magufuli ni kama zako za kumwinua mwananchi wa chini. Tatizo ni njia zinatofautiana.

Bunge la bajeti uliskia vi-mega-wt tulivyonavyo? Viduchu saana.

Viwanda vya kuyachukua mazao yetu vinahitaji umeme. Nampa hongera kwa kuufikiria mradi utakao zalisha megawt za kutosha...huu ni mwanzo mzuri wa kumaliza tatizo la kilimo.

Lingine...tunahitaji miundo mbinu ya uhakika na ya haraka. Tukishavuna tutasafirishaje maana wakulima wengi wapo vijijini walaji mijini...ni jambo la kheri kuona amekarabati reli na kuanza ujenzi wa ya kisasa.

Sehemu ambayo naona tunachelewa...ujenzi wa hii miundombinu iende sambamba na elimu ya mapinduzi ya viwanda na kwa wakulima.

Kenya kukifanya kilimo biashara haijaanza leo. Miaka ya 90 huko vijijini Kenya wakulima walikuwa wakishavuna bamia zao, parachichi n.k wanazibeba wanaweka barabarani kuna magari maalum ya serikali yanasafirisha hadi sehemu husika. Sisi tulikuwa tunashangaa maana mazao yetu tulianza wenyewe kwa wenyewe kwa bei ya kutupwa.

Sijawahi kuwa mshabiki wa CCM ila nikiri JPM anafanya vizuri na anamaono.
 

..nakubaliana na mengi uliyoyasema.

..umezungumzia vi-mega-wt tulivyonavyo kuwa ni kiduchu.

..mimi kwa maoni yangu hata hivyo vichache tulivyonavyo hatuvitumii ipasavyo.

..lakini pia miaka mitano ya Jpm imeshanionyesha VIPAUMBELE vyake ni vipi, na i am not convinced kuwa vinaendana na vyangu.

..kwa mfano, stiegler's kwa maoni yangu tulitakiwa kuwa na miradi ya ukubwa wa kati ambayo inakamilika haraka lakini at the end inatupatia megawat zilezile ambazo stieglers itakuja kutupatia. pia sioni busara ya kununua ndege badala ya kuwekeza kwenye viwanda.

pia angalia atcl ilivyoathiriwa na mabeberu kutokusafiri kwasababu ya covid19. tungewekeza matrilioni kwenye viwanda au kilimo fedha yetu ingekuwa inazalisha sasa hivi.

..Vipaumbele vya Jpm haviwezi kubadilisha kwa haraka maisha ya wakulima wetu. Wananchi wataendelea kuwa wategemezi kwa serikali kwa muda mrefu unaokuja. Tunapozungumzia kuwa kama Ulaya maana yake ni kuwa na uwezo wa kulipa kodi, siyo kuwa na madaraja na matreni tusiyoyamudu gharama zake.
 
Mkuu hatakuwa wa Kwanza kuondoka kwa nguvu,may be ujinga na umbumbu ndo unakusumbua
Tatizo lenu mna karirishwa na nyinyi mna kubali kama majuha. Kwanza jiulize support utaitoa wapi wakati asilimia 90 ya wapiga kura nchini wapo nyuma ya Magufuli anzia hapo sasa
 
Unaonekana unampenda sana JPM mkuu??
Nampenda kuliko Marais wote wa awamu tatu waliotangulia! Namkubali Magu ktk kuliongoza taifa langu dhidi ya walanguzi na makuwadi wa mabeberu Kama TL, Mende, Sefu nk...Hawa ni wezi na ni wa hivyo Sana!
Magufuli ndio mpango mzima wa Mungu kulinusuru taifa letu!
 
Huyo Mungu ni wa Gamboshi anaye ruhusu watu wauwawe wapotezwe kina Azory Saanane wapigwe risasi kama Tundu Lisu??
Wasiojulikana wamekamatwa au unapotezea tukukumbushe??
Usijitoe ufahamu kama hujui labda unaandika ukiwa hapo Lumumba??
Huoni picha kubwa ndio maana huwezi pambanua ubora wa Magufuli! Watu wanauawa kwa risasi na kuonewa kote duniani...siyo kosa linaloweza kuunganishwa na Magufuli moja kwa moja! Hata hivyo ukiweka kwenye mizani mazuri na mabaya ya Magufuli utajua tumebarikiwa Kuwa na rais Bora kuliko maelezo Tz!
 
Nyie ndio wanufaika wa utawala wake... Hata akishinda ajue ukoo wangu mzima HATUMPENDI.
Hii ni hasira ya kupokonywa tonge mdomoni! 😂🤣😂 Jifunze Kuwa na kipato Hali ndg yangu utachukiwa wasiochukiwa shauri yako😂🤣😂!
 
Tume ikishatangaza matokeo hakuna kupinga kokote. Mi siamini kama CCM inaweza kutoka kwa kutumia njia ya kupiga kura kwa tume iliyopo.
Hata 2015 kwani Jiwe alishinda kihalali?
 
Acha kukariri, serikali imedhibiti mfumko wa Bei na imefanya kwa niaba yetu kubana matumizi ili kuijenga nchi kwa kuwekeza kwenye miradi tambuka itakayotunufaisha baadae! Mtazamo wako finyu wa kuangalia Leo tu bila kuiona kesho ndio shida inayokusibu! Maisha ya wafanyakazi sio mabaya Kama unavyoharibu kuamunishwa watu! Magufuli mwenyewe alijipunguzia mshahara wake mwenyewe kwa akili ya taifa...hebu niambie mfanyakazi gani mwingine wa kawaida aliyepunguziwa mshahara zaidi ya annual increments ambazo zitapandishwa kwa mkupuo soon!
Jikite kwenye hoja.tatizo kwa sasa serikali hii imeshindwa kuboresha maslahi ya wafanyakazi na kutoa ajira kwa vijana.
 
Hutaamini Kama hata kura yako pia utampa Magufuli kwa furaha😂🤣😂!
Kura yangu ni kwa Tundu Antipas Lissu. Mpaka sasa nimeshampigia kampeni na watu 10 tumeweka commitment kumpa kura zetu.

Nia yangu ni kumtafutia kura 5000. Nanamtafutia na atazipata kweli!
 
Sijui ni kwanini Mimi ninaamini kwenye matumizi ya nguvu kuiondoa ccm kuliko hizi sera zenu? Hivi Kati yenu nani anaamini 2015 Magu alishinda uchaguzi? Chadema hawajaanza kuwa na sera nzuri leo, elimu bure pia ilikuwa sera ya chadema
Hata mimi naamini ccm itaondolewa kwa makofi siyo sera tena.
 
Hivi unafikiri watz hasa watumishi hawajitambui kiasi hicho. Wengi wao wanajua uwezo wa serikali yao unafikiri ni kama wewe usiyejua kinachoendelea serikalini? Wanajua upatikanaji wa pesa za serikali kwa hiyo hiyo sera ni danganya toto tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…