Daby
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 33,894
- 76,810
..binafsi sina tatizo na Wakenya kununua mazao yetu.
..hebu fikiria wasingeyanunua, mkulima hali ingekuwaje?
..naamini uzalishaji wa Tz unatosha ku-feed viwanda vya Tanzania pamoja na vilivyoko Kenya.
..Watanzania tujivunze kwamba kuwa na jirani mwenye uwezo ni jambo jema. Tujifunze changamoto wanazopitia USA dhidi ya jirani masikini kama Mexico, na jinsi USA inavyofaidika na jirani mwenye uwezo kama Canada.
..Au hapahapa, kati ya Kenya na Burundi ni jirani gani mwenye faida kubwa zaidi kwenye uchumi wa Tz? Inawezekana Burundi inatumia bandari yetu, lakini tukija ktk uchumi wa kaya Warundi wananunua mazao gani na kiasi gani kutoka kwetu?
..nakubaliana na hoja yako kuhusu upotevu wa mazao ambayo tunayavuna, na uhaba wa viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya wakulima wetu.
..tatizo langu ni kwamba Jpm na ccm focus yao haiko kwenye wakulima au viwanda. focus ya ccm iko kwenye miradi yao mikubwa ambayo itachukua miaka 10 mpaka 15 kukamilika. sasa wengine tunataka kuona mabadiliko ya kweli ktk kizazi chetu.
..CCM inaweza kuwa chama kizuri kabisa ikiwa kitakaa benchi awamu 1 u 2 halafu ndio kirudi madarakani.
Tukiwa na wapiga walau asilimia 50 wanafikiria kama wewe tutafika mbali mkuu. Hongera kwa hilo.
Fikira za Magufuli ni kama zako za kumwinua mwananchi wa chini. Tatizo ni njia zinatofautiana.
Bunge la bajeti uliskia vi-mega-wt tulivyonavyo? Viduchu saana.
Viwanda vya kuyachukua mazao yetu vinahitaji umeme. Nampa hongera kwa kuufikiria mradi utakao zalisha megawt za kutosha...huu ni mwanzo mzuri wa kumaliza tatizo la kilimo.
Lingine...tunahitaji miundo mbinu ya uhakika na ya haraka. Tukishavuna tutasafirishaje maana wakulima wengi wapo vijijini walaji mijini...ni jambo la kheri kuona amekarabati reli na kuanza ujenzi wa ya kisasa.
Sehemu ambayo naona tunachelewa...ujenzi wa hii miundombinu iende sambamba na elimu ya mapinduzi ya viwanda na kwa wakulima.
Kenya kukifanya kilimo biashara haijaanza leo. Miaka ya 90 huko vijijini Kenya wakulima walikuwa wakishavuna bamia zao, parachichi n.k wanazibeba wanaweka barabarani kuna magari maalum ya serikali yanasafirisha hadi sehemu husika. Sisi tulikuwa tunashangaa maana mazao yetu tulianza wenyewe kwa wenyewe kwa bei ya kutupwa.
Sijawahi kuwa mshabiki wa CCM ila nikiri JPM anafanya vizuri na anamaono.