CHADEMA kwawaka Moto! Mbowe arudi Dar!

Status
Not open for further replies.

Halisi,

CHADEMA ni chama cha kitaifa kwa sasa, hisia zako kuwa ni vema tukapoteza kule Tarime hakika mkuu hapo sijakuelewa, wana tarime ni wanamageuzi fikra zako kuwa huenda CCM ina nafasi kule Tarime hizo ni hadithi zako

Halisi tunajua kuwa na upenzi na ushabiki bila tija si vema, ni vema tukajikita kukiendeleza chama na kuepuka yale yote yanayoweza kuwapa watanzania kigugumizi.
 


Kwanini wengi wawe na nia mbaya kwa mmoja na si mmoja kwa wengi? Je mkataa wengi ni mchawi ama wengi wakataa mmoja ndio wachawi.Hii filosofia sijaipata vizuri.
Mwita :unaweza eleza kidogo kwanini unadhani CCM,CUF,TLP,NCCR,PPT hawakitakii mema CHADEMA?
 

Mwana wasu,
Unajua hivi vyama vingine(TLP,NCCR .na) havina mwelekeo kwa sasa, kwa hiyo wanajitahidi ili wapate umaarufu, sote ni mashahidi kuwa chama kama TLP hakika hakina mwelekeo, na ndiyo maana nikashauri kuwa ni vema basi Mbowe akajiweka pembeni na tukampata mtu mwingine badala yake, na hii inafanyika tu kwa sababu hawa wenzake wakose Mshiko, ama wewe unalitazamaje hilo?
 

Mkamap nimekusoma nami nangoja majibu ya mkuu kama wewe asante sana .
 

Mwanawasu

mimi nafikiri Mbowe hakubaliki wala nini miaka miwili na nusu iliyopita ktk uchaguzi mkuu alipata 5% ambayo ni sawa na takribani karibu ya watu laki moja sabina na tano elfu 175000 kati ya watu milion thelathin na tano (35,000,000)

Nitakubaliana na wewe ukisema Mbowe anakubalika ktk baadhi ya memba humu JF.
 

Mkama,
Hishima mbele mkuu, lengo letu sisi si kusema kuwa mbowe kapata ngapi ila hoja kwa sasa ni kumpata kiongozi mbadala atakaesukuma gurudumu hili, sisi sote ni mashahidi kwa yale mazuri Mboe aliyoyafanya, tungependa tumpate jemedari mwingine kabla hakujakucha.

Mbowe kafanya, ni ukweli usiopingika kuwa ndiye aliyesubutu kuleta upinzani wa kweli hata kutishia CCM, Lakini kwa kuwa hawa mafisadi wamekuja na style nyingine sasa yeye akae pembeni ili tuendelee kuwakimbiza hawa mafisadi.
 


Mwana wasu.
kwanza kabisa ukiangalia NCCR na CUF kwa miaka ya nyuma vilikua na nguvu sana kuliko CHADEMA ya leo.Nadhani umeshanipata nini nataka kuongelea.

Tatizo mimi ninaliona kwa wanasiasa wetu 1.nikutaka umaarufu 2.ving'ang'anizi 3.Mafisadi.

Umaarufu
Wanasiasa wetu wanafanya kazi kwa kutafuta umaarufu yani ma oportunists yani wanajikita zaidi sehemu ambapo kuna tatizo na wao kutumia tundu hilo si kwa ajili anawatakia mema wanannchi bali ili ajikweze ,nitakupa mfano ukiwa na mke wako akazini na jamaa fulani mtu mmoja anaweza kuja kukupa taarifa kwa nia njema na mwingine atakuja kukupa taarifa hizo si kwa nia njema bali ni ili apate kukuumiza .Nadhani umenipata
Ukitaka kuwagundua hawa wabunge/watu wa namna hii ni kuhoji je? ILANI zao za uchaguzi za mwaka 2005 walizoziuza kwa wananchi wamezitekeleza ?ama angalabu wamefikia nusu.

Ving'ang'anizi
Unajua unaweza kujiamini na ukawa na malengo mazuri lakini kwa bahati mbaya ukawa huna bahati ya kuungwa mkono ,kama wewe ni mwelevu ingekubidi ukae pembeni upishe wanaoungwa mkono.Mimi kama ningetokea nikawa mshauri wa wapinzani ningewashauri wenyeviti wote waliopo wa upinzani wote wajiuzulu isipokua Maalimu SELF wa CUF

Mafisadi

Wengi wao wanatumia hali ilivyo kufisadi fedha za chama ama yupo pale akiona jamaa serikali kafanya ufisadi yeye huku nje anabweka vibaya sana ili yule jamaa wa serikalini aliyefisadi 10% ampe anghalabu 4%.
 

Ukileta suala la asilimia za kura unakuwa haupo sawa. Hivi ni nani asiyejua kuwa CCM wanaiba KURA?, Hata wao wenyewe wanalijua hilo na hawabishi.

Hoja hapa ni kutaka kubadilisha FOCUS ya watanzania kutoka kwenye UFISADI. MBOWE Bado ni kiongozi makini nafikiri tunatakiwa kujenga hoja nzito zaidi ya hizi za KIFISADI kuweza kumfanya aachie ngazi.

Kama Hoja yako ina ukweli hebu jiulize swali moja Iweje LIPUMBA apate zaidi ya 10% of Votes na CUF Isiwe na kiti cha Ubunge hata kimoja Bara?. CCM Wanacheza ngoma ambayo baadae watakuja shindwa kujua kuwa sasa watikise mabega au wakate viuno?. WASHUGHULIKIE UFISADI, Na Ninakwambia CCM Ikiwasaliti mafisadi Imetoka madarakani na wao wanalijua hilo. Kwani ni wao ndio wanawapigia ngoma CCM waicheze.
 

Mkama,

Najua na wewe tayari umeshaathirika na hali hii ya kisiasa nchini mwetu, najua watu kama wewe mnaweza kuwa msaada mkubwa katika taifa letu, je ni lini hawa viongozi wetu wa upinzani wataligungua hili?

Mkama ujua tusipokuwa na upinzani imara taifa letu litakuwa katika hali ngumu na ndiyo maana nikashauri kwa kuwa CHADEMA kwa sasa ina sura ya kitaifa basi ni vema huyu mbowe akae pembeni akinusuru chama hiki chenye mwelekeo, ama wewe unalitazamaje hilo?
 

Hakika hii ni kweli, haiwezekani eti CUF haina kiti hata kimoja huku bara wapate 10%
 


Mwita
Ukiangalia wapinzani sio kwamba hawalioni wanaliona sana ila kwa vile malengo yao ni umaarufu na kujipatia fedha na si kwamba wanatafuta demokrasia ya kweli.Yani ni kama wasomi wetu serikalini si kwamba hawaoni wala hawajui mbinu ambazo zinaweza kutuondolea umasikini bali kwa umasikini wetu kwao ndio raha maana wanafalsafa yao ni bora tajiri kuzungukwa na masikini maana ataabudiwa kama miungu ,kuliko tajiri ndani ya midle class.

Maana kwa umasikini wetu wao kuingia mikataba ya 10% ni rahisi mno kuliko kwa taifa lenye matajiri na midle class.

Mimi sidhani kama upinzani wa chama utabadirisha matokeo,nafikiri matekeo yatabadirishwa na mtu mmoja ambaye atakua mzalendo wa kweli ,mfurukutwa ,mwenye nia ya kuondoa umasikini na anayeungwa mkono na watanzania wengi.
Nchi ngapi za afrika zimebadirisha na kuweka wapinzani,angalia Kibaki wa kenya wakati yupo upinzani alivyokua anaimba nyimbo za demokrasia lakini kaingia madarakani nini kimetokea?
 
Kweli, mafisadi waliapa kumshughulikia, chadema chini ya mbowe ndio waliongoza vita hiyo. Hii hela na aliyeandika huenda amelipwa. Mbowe anza kazi sasa bila kurudi nyuma. Tuko na wewe
 

Mkama,
Hapoa ndipo ninapopata shida kabisa ni lini sasa nchi yetu itakomboka toka mikononi mwa CCM? tunajua ndani ya ccm wamo watu wema na wenye mapenzi mema na nchi yao, na kwa kuwa viongozi wao wamelisaliti taifa kwao kuiuza nchi si tatizo sasa tufanye nini?

Na ndiyo maana namshauri Mbowe ajiweke pembeni kwani hawa mafisadi wameshaupeleka mkono wao ndani ya chama hiki chenye sura ya kitaifa.
Wasiwasi wangu 2005 CHADEMA Ilipata wabunge 6, na kwa sasa ccm watafanya kila wanaloliweza idadi hiyo ipate kushuka
 

Mkama,
Hapo ndipo ninapopata shida kabisa ni lini sasa nchi yetu itakomboka toka mikononi mwa CCM? tunajua ndani ya ccm wamo watu wema na wenye mapenzi mema na nchi yao, na kwa kuwa viongozi wao wamelisaliti taifa kwao kuiuza nchi si tatizo sasa tufanye nini?

Na ndiyo maana namshauri Mbowe ajiweke pembeni kwani hawa mafisadi wameshaupeleka mkono wao ndani ya chama hiki chenye sura ya kitaifa.
Wasiwasi wangu 2005 CHADEMA Ilipata wabunge 6, na kwa sasa ccm watafanya kila wanaloliweza idadi hiyo ipate kushuka
 
Lakini mbona wale wakongwe tuliowakuta hapa jamvni hawaigusi hii thread? ama ni tete? na kama ni tete MWKJJ,Jmush1, Pundit na wengineo tuambieni ifungwe?
 
Lakini mbona wale wakongwe tuliowakuta hapa jamvni hawaigusi hii thread? ama ni tete? na kama ni tete MWKJJ,Jmush1, Pundit na wengineo tuambieni ifungwe?

ni ngumu kukuunga ktk maada hii,nadhani unajua kwa nini.
 

Sasa unajichanganya kidogo mkuu. Sababu ulizotoa za kumtaka Mbowe ajiuzulu ndio hasa zinazomfanya awe na sifa za kumfanya aendelee kuwa kiongozi wa CHADEMA kuliko mwanachadema mwingine. Kama CCM wanamhara na kumwandama Mbowe hiyo ndiyo sifa tunayotaka kwa kiongozi wa upinzani. Kama wewe ni kiongozi wa upinzani na CCM hawakosi usingizi kwa ajili yako, wewe hufai kuwa kiongozi wa upinzani.

Halafu unakiri kwa maandishi yako kuwa Mbowe amefanya kazi kubwa ya kukuza demokrasia nchini, sasa cha ajabu unataka tena ajiuzulu.

Labda unisaidie kidogo hapa, wewe mwenzetu unataka sifa gani kwa kiongozi wa upinzani? Unataka kiongozi awe goigoi, asiyeikosesha CCM usingizi, anayesifiwa na akina Makamba, au namna gani, hebu tuweke sawa!
 

Sasa anayeshangaza hapa ni nani wewe au mimi, maada uliyotoa haina kichwa wala miguu, ningekuwa administrator ningekuvua hicho cheo ulicho nacho.HEBU ANGALIA ANALYISIS YA MDAU HALISI.

Kama umesoma na unawaza hivi!! wasomi hawawazi kama wewe: usjiweke upande wa chadema kwani ni wewe na siri yako.Ila maada hii haonyeshi kama wewe mpiganaji!! ni mtu wa kukata tamaa.Ingekuwa mimi wewe nisingeendelea kabisa kudebate humu ndani ningekaa kimya, maana NIMECHEMSHA, NIMESTUKIWA KAA CHINI UPYA TAFUTA MAADA NYINGINE, PEOPLE HERE ARE INTELLECTUALS

''If either player abandon the game by quitting the table in anger, or in an otherwise offensive manner; or by momentarily resigning the game; or refuses to abide by the decision of the Umpire, the game must be scored against him''.
Howard Staunton

Waberoya
 
Last edited:
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…