IsayaMwita
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 1,127
- 140
Mawazo yako yana maana kubwa hasa kwa hali ya sasa ya Tarime. Kwa kweli Chadema ina kazi sana kushinda Tarime chini ya Mbowe baada ya CCM kuungana na CUF, TLP na NCCR Mageuzi kumpinga Mbowe.
Lakini, katika vita ni lazima kuwapo na maamuzi magumu na ya kudumu na si vyema sana kukubali kuzidiwa nguvu na upepo. Alipojiuzulu Lowassa, wafuasi na mashabiki wake na hata yeye binafsi (hadi sasa) waliamini kwamba kujiuzulu kwake kutamuibua SHUJAA ambaye atafanikiwa kuwamaliza maadui zake na yeye kurudi kwa kishindo katika siasa dakika za majeruhi na kuibuka kuwa RAIS..... Mawazo hayo SI SAHIHI maana tayari kujiuzulu kwake kumetoa picha halisi ya kuwa FISADI na hilo ni gumu kulifuta kama ambavyo sasa SUMAYE anapata shida kufuta tuhuma zilizopikwa na MTANDAO. Dhambi ya kuchafuana imewarudia kina EL kwa kasi na imekua sumu kwao. Tukirudi kwenye mada, kwa sasa Mbowe akijiuzulu itakuwa ni KUWAPA nguvu wapinzani wake na wenye malengo ya kusambaratisha upinzani wa kweli na itakua vigumu kuiepusha CHADEMA na kujiuzulu kwa Mbowe na hivyo Chadema itakufa, jambo ambalo ni hatari kwa demokrasia, maslahi na USALAMA wa TAIFA. Hakuna anayetaka hili litokee kwa sasa. Kwa sisi tusio na vyama tunadhani ni vyema Mbowe akajipanga na kufanya mambo kadhaa ya msingi yatakayomuwezesha kukabiliana na wimbi la kampeni chafu hasa kwa kuwa Watanzania walio wengi wana imani na Chadema na wamegundua kuna njama za kundi dogo la wana-CCM wanaotaka kuua upinzani wa kweli.
Ni vyema kwa sasa Mbowe akapambana kwa mbinu zote na si kujiuzulu ili kuwachanganya. Ni bora kupoteza hata jimbo la Tarime (japo iko kazi) ili kuimarisha upinzani kuelekea 2010 na si kwa maslahi ya wakati huu pekee au kwa kukubali kufuata upepo na kucheza ngoma inayopigwa na MAFISADI.
Mutakumbuka dua yangu ya wakati wa RICHMOND na leo naifufua tena.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WALAANI MAFISADI. MUNGU ULIYETUKUKA IVUNJE YAO DHAMIRA MAFISADI, WASIWEZE KUSIMAMA, WASIONE JAPO WANA MACHO, WASISIKIE JAPO WANA MASIKIO, WASITEMBEE JAPO WANA MIGUU, WAENDELEE KUSAMBARATIKA NA KUPUKUTIKA
Halisi,
CHADEMA ni chama cha kitaifa kwa sasa, hisia zako kuwa ni vema tukapoteza kule Tarime hakika mkuu hapo sijakuelewa, wana tarime ni wanamageuzi fikra zako kuwa huenda CCM ina nafasi kule Tarime hizo ni hadithi zako
Halisi tunajua kuwa na upenzi na ushabiki bila tija si vema, ni vema tukajikita kukiendeleza chama na kuepuka yale yote yanayoweza kuwapa watanzania kigugumizi.