CHADEMA kwawaka Moto! Mbowe arudi Dar!

Status
Not open for further replies.

Asante sana
pia naomba kusema jambo moja tu kuwa the Late Mwl Nyerere aliwahi kusema kuwa hakuna jambo baya kama mtu kufilisika kimawazo na ukiona mtu amefilisika kimawazo haswa kwa wana siasa ujue jambo la kwanza atazungumzia ukabila na hilo ndilo limejitokeza kwa wale ambao wamefilisika kimawazo wamekosa mtizamo chanya wamekuja na mawazo ya kikabila je hii inaweza kuwa sera mbadala ya maendeleo yapi???

mimi nakubali chama kipo katika sura ya kitaifa na kina mwelekeo mzuri na wale wenye kumiliki vyombo vya habari ambavyo ni mamluki ya ukabila ndiyo haswa waliofilisika kisera na kimawazo wanaoleta sera ambayo haina mantiki katika demokrasia wala kiuchumi bali matokeo yake ni kulazimisha muda wa watu kutumika kujibu hoja zisizo na impact katika maendeleo ya jamii bali ni source of distructions
 

Maluo,

Nimetangulia kukujibu kwa usemi huu kuwa, kama si ushabiki na fikra butu ulizonazo basi fuadi yako inaongozwa na upenzi pasipo mshiko, lengo na dhamira hapa ni kutaka kuutangazia umma kuwa hapa CHADEMA kuna demokrasia ya kweli, kwa maana ya kuwa kama M/kiti wetu ajiuzulu kwa haya yanayotajwa kwa sasa, atawapa hamasa wasomi na wapenda demokrasia kitimkia ndani ya chama hiki chenye mwelekeo kwa sasa.

Hakuna kificho kuwa CCM wanafanya kila wanaloweza ili kukitokomeza chama hiki, na tusisahau kama CHADEMA Kitatokomea tusitegemee chama mbadala kwa siku za karibuni.

Ni chama cha CHADEMA Kwa kupitia wabunge wake ndiyo wameweza kuibua ufisadi na maovu katika taifa letu.

Mungu ibariki Tanzania Mungu ikomboe Tanzania.
 
sidhani kama kujiuzulu kwa mbowe ndio kutakinusuru chama!! kwa mtazmo wangu hapa zifanyike jitihada za makusudi kupunguza ubaguzi katika chama ndio nusura pekee na wala sio kujiuzulu kwa mbowe! ni Mtazamo wangu!
 
sidhani kama kujiuzulu kwa mbowe ndio kutakinusuru chama!! kwa mtazmo wangu hapa zifanyike jitihada za makusudi kupunguza ubaguzi katika chama ndio nusura pekee na wala sio kujiuzulu kwa mbowe! ni Mtazamo wangu!

Mpogolo

Kweli hayo ni mawazo yako, mpogolo naomba usikae pembeni njoo tulisukume kugurudumu ndani ya chama hiki, tumekataa kuwa neno ukabila lisitajwe ndani ya chama chetu.

Tunajua wafanyakazi wote wa taifa letu hawaiungi serikali yao mkono hata kidogo.

Waalimu wataifa hili wote kwa pamoja hawaitaki serikali yao, ni serikali hii ambayo inawanyima maslahi yao, kuongezewa mshahara ni hadithi kwao na ndiyo maana tunasema kwa kuwa tuna chama mbadala wa CCM tumekimbilia humu ili kuleta mageuzi ya kisera na pia kiutawala kwa siku za usoni

Nchii hii ni ya wachache, wale tu wanasiasa wa CCM wa ngazi ya juu, utasikia wamerithishana mali zetu na mengineyo.

Sasa kwa kupitia chadema yote yanawezekana.

Tutatoa magugu yote na pia tutapata mstikabali na hatima ya chama chetu.
 

Kuwapata watu wa kujadili KUJIUZULU kwa Mbowe na si KIKWETE, wakati Kikwete nchi na CCM imemshinda kuliko ilivyowahi kwa watangulizi wake akiwamo fisadi Mkapa
 
Kuwapata watu wa kujadili KUJIUZULU kwa Mbowe na si KIKWETE, wakati Kikwete nchi na CCM imemshinda kuliko ilivyowahi kwa watangulizi wake akiwamo fisadi Mkapa

Halisi,

Sasa nimeupata mtizamo wako, yaani unaweza kumlinganisha JK na ndugu yetu Mbowe? hakika utakuwa hautendei Mbowe haki, watu hawa wenye mitizamo tofauti, hisia tofauti na hata itikadi tofauti.

Mkuu tunaposema CCM nchi imewashinda nandiyo maana tunasema CHADEMA ni chama mbadala naona hauelewi, unatumia ulazima wakati sisi tunadhani nini kifanyike CHADEMA izidi kuboreka, tumia tu akili kidogo, leo Mbowe akawaita waandishi na kuwatangazia kuwa amejiuzulu unadhani CCM watamchukuliaje? nadhani hapo watashangaa na pia watamuona kama kweli mwana mageuzi, si lazima m/kiti wetu azidi kuwa kwa muda mrefu.
 
Mkuu Halisi,

Kwani Mbowe ameifanyia nini CHADEMA?
Je kaifanyia nini nchi yetu zaidi ya kuleta mambo ya ukabila CHADEMA?
nionavyo ni kheri Mbowe aachie ngazi,yeye pamoja na Dr. slaa.walmpikia majungu Marehemu chacha Wangwe mpka wakahakikisha anag'oka kw ambinu ya kumsimamisha kwanza.
 

Gembe,

Najua si tatizo lako ni tatizo la uelewa wako, hisia zako zimefungamana na haya unayoyaamini.

Gembe usijisahau kuwa una shule humo kichwani mwako, vipi kale kamasta umekamaliza?

Pole sana ndugu yangu, naomba ujue kuwa CHAMA CHA CHADEMA ndiyo chama mbadala yA CCM.

Lengo la kumtaka m/kiti wetu akae pembeni ni hoja za wana CHADEMA na si vinginevyo, tumegundua(ccm) mnataka kutumia hoja za kipuuzi ili kukipiku CHADEMA

Tunamshukuru Mungu kuwa M/kiti wetu ni msikivu na ataendelea kuyatafakari haya yanayosemwa kwa sasa.
 

NAPINGA KWA NGUVU ZANGU ZOTE KUJIUZULU KWA MBOWE KWA SABABU ZIFUATAZO:
1.itakuwa ni kuendekeza imani potofu zilizoko nchini kwetu kuwa mtu yeyote maarufu akifa basi kuna mkono wa mtu
2.itakuwa ni kutomtendea haki mbowe kwa tuhuma zisizo na uthibitisho wa kinadharia wala wa kisayansi
3.kwenye siasa kuna makundi na misuguano mbalimbali.ndio maana kuna kuwa na chaguzi za ndani ya vyama ili kupata mwenye wafuasi wengi na wa nje ya vyama.waoshindana ni watu na siyo mawe.wamezaliwa na watakufa.kama watakufa basi tunaoshindana nao tukaambiwa tumewauwa ina maana yuache siasa wote kwa kuwa hakuna ambaye hatokufa siku moja na hakuna hajuaye lini mtu unaye mpinga atakufa.
4.imani za kuuwana kishirikina au kwa namna yeyote ile ni lazima zikemewe kwa nguvu zote kwa kuwa ni aibu kwa jamii yetu na ni fedheha kubwa kwa familia na kwa anaesingiziwa.

Ata hivyo hili ni fundisho pia kwenu wana chasdema ambao nanyi individually mlikuwa mkiwasingizia sana watu wa vyama vingine pale anapokufa mtu...binafsi najua jinsi inavyouma sana lakini mara zote unakuwa strong zaidi mara baada ya tuhuma.Mbowe rafiki yangu na ndugu yangu,hizi ndio siasa za nchi zetu masikini.ujumbe wangu kwako:
Courage brother donot stumble
Though the pass be dark as night
there is a star to guide the humble
Trust in God and do the right.

Some will love you some will hate you
some will flatter you some will slight you
Cease from men and look above God
Trust in God and do the right.

Perish policy perish canning
perish all that fears the light
whether winning or loosing
Trust in God and do the right
 

NCHIMBI,

Haya ndiyo yaliyojaza fuadi yako, mtizamo wako butu, sijui umeielewa mada? pole sana ndugu yangu.

Sisi wanachadema tutaendelea kubolesha ili tupate ushindani zaidi, kujiuzulu kwa m/kiti wetu ni sera wala si ushabiki wa ninyi Mafisadi, Mbowe kashaona na atafanya maamuzi yake hasa tukiendelea kumshauri ili chama chetu kipone.

Ninasema tena najua CCM mtafanya kila linalowezekana kutaka kukipiku chama chetu 2010 hata kile kidogo tulichonacho, fikra zetu hazijasahau, mlifanya hivyo kwa NCCR na ndiyo maana mafisadi sasa mnajitahidi kukichafua chama hiki cha chadema, najua Mola yu pamoja nasi.

Tunaendelea kutafakari ni jinsi gani CCM wasivyokuwa na haya jamani, wamesahau kwa kupitia vyama vya upinzani mengi yameweza kuibuliwa, tumegundua uozo kwa taifa letu

Mungu ibariki Tanzania

Mungu inusuru Tanzania
 
Well,Hili suala la kusema Mbowe ajiuzulu ni sawa kama kuna hoja za kutosha.so far hakuna hoja za maana maanke yote yanaonekana ni uzushi.Mbowe ajiuzulu kwa lipi maanke kama ishu ni hii yaWangwe basi inabidi kauli ibadilike iwe kamati kuu ya CHADEMA ijiuzulu.


NCHIMBI,

Tunaomba usije ukafikiri kwa hizo hoja zako hapo juu za kujifanya uko upande wa mhe.Mbowe zitakufanya uonekane kashfa zinazokuandama kule kwenu zitazuia mawazo ya watu huru ndani ya chama chako huko kwenu kujenga hoja za kukuwajibisha.Ubabe wako ndani ya UVCCM ni wa kweli acha kujisogeza huku ili uonekane unaonewa.

Back to the point,Suala la CHADEMA kujitanua nchi nzima ndilo la msingi sasa ikizingatiwa zaidi kuna local government's election next year.

Pia kwanza kuna hili suala la Kufungua matawi nje ya Nchi,mpaka sasa huku India tuna Tawi moja lakini bado kadi hazijatolewa.Idadi kubwa ya wanachama ni wanafunzi wa mwaka wa pili na wa Tatu ambao next year watakua home.

Vijana wengi wanavutiwa na CHADEMA kutokana na sera na pia hoja za Wabunge wa CHADEMA Bungeni zinavuta hisia za vijana wengi.sasa leo hii hii stori ya kutaka Mbowe a-resign nadhani haijengi sana kwa muada huu hasa pale ambapo hoja haziwezi kusimama

Hebu Dr.W.Slaa tafadhali tunaomba utupe mkakati wa kujiandaa na election zijazo hasa katika viti vya ubunge!
 
ni ngumu kukuunga ktk maada hii,nadhani unajua kwa nini.

Naona mkuu,hao unataka kuleta masuala ya hisia.

Haya masuala ya kutawaliwa na hisia ndiyo yaliyopelekea hadi Msanii Jk akachemka na kuliaibisha Taifa kule Ufaransa aliposema hajui ni kwa nini tu Maskini.Kwa kweli tulionekana sisi ni watu tunaotakiawa tuandikwe kwenye Guinnes book records kwa kumchukua mpita njia ambae hajui matatizo yetu na kumuweka ikulu.

Sumaye nae baada ya ile shule yake ya Harvad,tena after ten(10) years in office as PM akatoa bonge la kauli ati,'Finally,nimejua kwa nini Tanzania ni Maskini'.Kama si kuongoza nchi kwa hisia ni nin maanke.Yaani alivyokua busy akiwa Pm kumbe alikua hajui antaka ku-accomplish nini?
 
Eddy nadhani msemo "no research no right to speak" una appy vizuri hapa. Hivi ni kitu gani kinamkataza kuendesha magari yake binafsi yawe Jaguar au nini na unataka agawe hata yake binafsi kwa wengine? Ujue Mbowe ni mfanyibiashara mkubwa, mwenye uwezo wake hata kabla ya kuingia Chadema, and has made many sacrifices to elevate Chadema to where it is Today. Chacha alikuwa Mbunge, mwenye haki ya kukopa Gari Standard kwa gharama ya Watanzania kama alivyo Mbunge mwingine yeyote. Kauli kama hizi ambazo hazijafanyiwa utafiti na zinazotaka kujenga Sentiments za kugawa Watanzania, jambo ambalo hatujalizoea ni za hatari sana. Tulililiwa sana na Mafisa kwa mawazo kama haya, tunaacha kujadili muhimu na kupelekwa kusiko na maana ili tusahau kulinda rasilimali za Taifa. Taifa zima linakuwa maskini kwa vile hata sisi wenyewe tunapiga vinanda kwa 'tunes' zisizo zetu.
Kinachoitwa 'Danguro' I wish Eddy ukapata muda ukapatembelea kidogo tu ili msemo wa no research ufanye kazi, lakini ujue wenzio wakati wako tayari kwenye sayari wengine wasiwe kwenye 'tembe' kama la kule kwetu. Tuna kazi kubwa wakati huu kuliko wakati wowote ule kuachana na itikadi zetu na kujadili real issues kwa ajili ya watoto wetu na kwa ajili ya Taifa hili. Maneno hayo ni tusi kwa Watanzania wana Chadema, ambao katika vikao vyao halali walimchagua na mtu ambaye labda hajui inside story ya Chama hicho akarukia maneno yaliyopandikizwa na kutumia tu kwa tune ya wale anaowapalilia. Chopper ingelikuwa mbaya kama inavyosemwa CCM wasingelileta tena kwa kukiuka taratibu zote za nchi za kiusalama na za kiuhamiaji dakika za mwisho wakati wa Uchaguzi mdogo wa Kiteto. Ukiona mtani wako anapigia sana kelele jambo ujue linamwumiza sana. Chopper itaendelea kwa miaka mingi ijayo watani wa Chadema, whoever they are and whereever they are!
 



Bravo Dr,

Hili suala huyu mtu alishajibiwa kitambo maanke suala la Magari inategemea na background za akina Mbowe na wangwe kabla hawajaingia kwenye siasa.Hili sio tatizo la kichama kabisa.

Sasa Kuna hili suala la bajeti za chama kipindi cha kampeni.Mkuu ni kwa nini mikakati hii isiwe inawekwa mapema na kama ni kutumia Chopper hata ikiwezkana election ijayo ziwe zaidi ya tatu ili kuhakikisha wananchi wengi wanapata muda mwingi kusikiliza sera kwa muda murefu.Hata ikiwezekana kikanda.

Pia matumizi ya Bendi na wasanii mbali mbali maanke unajua watanzania wengi wanapenda starehe bila ngoma hawaji kwenye kampeni.

Pia campaign team na kitengo cha propaganda viandaliwe mapema ili kulizidi kundi la akina Tambwe Hiza
 
Ben Thanks. It is to early to spill out out strategies and I think you agree with me. Mikakati ya Chama inatolewa na au baada ya kuidhinishwa na vikao husika vya Chama kwa mujibu wa Katiba ya Chadema.
 
Nimekuelewa Mkuu.
Tafadhali hebu cheki PM yako nimekutumia ujumbe
 
Gembe thanks. Una hakika ya mawazo lakini unaweza kuwasaidia sana wasomaji wako ukiwaeleza kinagaubaga walimpikia Marehemu Chacha Wangwe majungu yapi hasa? You can do this country justice kama utaweza ku 'substantiate angalau chache tu ili JF wote tuzielewe vizuri!
 
BEN, asante kwa ushauri.Point noted and taken
 

Nimemkashifu au kumshutumu nani hapa? Sijamkataza mtu kutoa maoni yake kwa sababu hicho ndicho nilichokifanya mimi (kutoa maoni), sasa kwa nini niwakataze wengine kitu ambacho mimi ninakifanya?
Sijajifunga katika itikadi yoyote kisiasa, nimemua niwe huru
 

Hisia za Gembe zinafahamika, Dr.W.Slaa, usiumize kichwa kwa huyu ndugu yetu, wakati sisi tunaendeleza fikra zilizo hai yeye analeta majungu na utani hapa jamvini,

Dr.W.Slaa, Mkuu umenishangaza sana umeijadli mada lakini ukaruka hoja yenyewe, sisi tunafikiri nini kifanyike ili chama kiboreke, kwa sasa unaona tulivyojeruhiwa na bado unaona Mafisadi wanataka kutumia hoja za kipuuzi kutusambaratisha.

Dr.W.Slaa,Upiganaji wako ni mithiri ya Simba dume, hauogopi chochote, taifa kwa sasa litakwenda Mbele kwa sasa umejitoa muanga wala usijali, huruma zako kwa watoto wa kitanzania zimethibitika,haijalishi mwisho wako baba

Dr.W.Slaa, wewe ni malaika uliyeshushwa hapa duniani kwa bahati tu, hakika tutaendelea kukuheshimu na michango yako katika ujenzi wa Taifa letu.

Dr.W.Slaa,sasa imefika wakati wa kumwambia M/kiti wetu akae pembeni, kwa kuwa kashifa hizi zinazomwandama kwa makusudi kabisa toka kwa CCM, ili kupoze umaarufu wake, mwambie akae pembeni

Mungu ibariki Tanzania

Mungu inusuru Tanzania
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…