Maluo,
Heshima mbele mkuu,
Najua kama si jaziba na uzembe wa kufikiri ulionao basi itakuwa ni ufuasi na ushabiki wa kisiasa unaotawala fuadi yako, Bado tuna imani kubwa sana na tena sana na mwenyekiti wetu, na tunathamini mchango wake wa kukilea na kukikuza chama hiki cha CHADEMA chenye sura ya kitaifa tanzania nzima, Maluo naomba ufahamu tu kwa dokezo kuwa CHADEMA ndiyo chama mbadala wa CCM, Wasomi wote wamo ndani ya chama hicho japo ni kwa KIVULI
Nimeshasema kuwa kwa kuwa chama hiki kimeshakuwa na sura ya kitaifa na kwa kuwa watanzania wote wanakikubali kwa sasa, na hata Hao CCM nao wanakikubali basi na kwa kuwa hawa mafisadi wanatumia propaganda kumchafua Mbowe eti ana ukabila na mengineo mengi, basi ndiyo maana nikasema kuna haja sasa ya kuutafuta uongozi mpya na si vinginevyo
Asante sana
pia naomba kusema jambo moja tu kuwa the Late Mwl Nyerere aliwahi kusema kuwa hakuna jambo baya kama mtu kufilisika kimawazo na ukiona mtu amefilisika kimawazo haswa kwa wana siasa ujue jambo la kwanza atazungumzia ukabila na hilo ndilo limejitokeza kwa wale ambao wamefilisika kimawazo wamekosa mtizamo chanya wamekuja na mawazo ya kikabila je hii inaweza kuwa sera mbadala ya maendeleo yapi???
mimi nakubali chama kipo katika sura ya kitaifa na kina mwelekeo mzuri na wale wenye kumiliki vyombo vya habari ambavyo ni mamluki ya ukabila ndiyo haswa waliofilisika kisera na kimawazo wanaoleta sera ambayo haina mantiki katika demokrasia wala kiuchumi bali matokeo yake ni kulazimisha muda wa watu kutumika kujibu hoja zisizo na impact katika maendeleo ya jamii bali ni source of distructions