CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?


mimi bado naamini ukileta uthibitisho watu watakuelewa zaidi kuliko story zote hizi mwenzangu. Leta kadi namba au vinginevyo ili kuthibitisha usemi wako.
 
Spendi, vyama vyenye style ya OFISI KTK BRIEF CASE!!!!

Yaani mtu mmoja akisafiri, chama kimesafiri. Akisema, chama kimesema. Asipomtaka mtu, chama hakimtaki mtu huyo. Akilala, chama kimelala!!! Mnh, mola apishie mbali, akifa chama kimekufwa!!!!!!
 
Fikiria, ndio washachukua innji. Kisha wanaanza kutimuana ktk baraza la mawaziri!! ikulu hapatoshi!!!!!. Duh!!!!!!

kutimuana ni sehemu ya kazi ya kujenga, sio kama JK anayeogopa kuchukua hatua anaendelea kuwa na serikali ya watu wasioelewana na wasiofanya kazi yoyote, hadi serikali inaparalise na kila mtu, hata mtoto mdogo anagundua kuwa mambo hayaendi.

Viongozi wakichemsha wanafukuzwa! Huo ndio uongozi wa kuchukua maamuzi.

HEKO MBOWE kwa kazi nzuri.
 

Mheshimiwa.

Sijasema kuwa ni ubaya kuhama vyama nimetoa mfano wa Mtemvu Abbas ni mbunge wa Temeke alianza Tadea 1992 akaenda UMD,NCCR,CUF na hatimaye CCM,Mtikila yuko DP na Ndesamburo yuko Chadema toka mwanzoni, James Mbatia hajabadilisha vyama kama Kitila.

mjadala wa Kitila umekuja baada ya mmoja wa wapenzi wa Chadema kusema kuwa Wangwe alikuwa NCCR na aliwasumbua huko. nikamjibu kwa kusema kuwa kwani Kitila Mkumbo alikuwa NCCR na TLP anasumbua?

Ni demokrasia kila mtu kuhamia chama anachokitaka hata iwe kila mwezi ila utulivu na subira vinahitajika sana kwenye siasa hata kwenye kazi za kawaida unaenda kwenye interview na kusema kuwa ndani ya miaka miwili umebadili kazi kumi, unawapa nafasi ya kukunyima kazi wakiamini utawakimbia kama ulivyokimbia huko kwingine.

somo hili litawasaidia wengi sana wanaopania kuingia kwenye ulingo wa kiasia kuwa kunahitajia uvumilivu na subira na tuwekeze sana kuliko kutegemea kuvuna, leo hii Mtemvu anaingia kundi la wanasiasa walizuunguka kwenye vyama vingi labda akifuatiwa na Kitila inaweza kuwa ni ishara ya kuonesha juhudi zao za kutaka mambo yaende vizuri ndani ya nchi yetu.

Kubwa jinga samahani sana kwa hili na wala sina maslahi na Wangwe ila haki lazima itendeke hata Saddam Hussein waliotaka kumuua waliweka mazingira ya kuhalalisha mauaji yao kama kumpeleka mahakamani wakati wamesha muhukumu.

naomba nishie hapa sitamjadaili zaidi RAIS wetu wa Daruso lakini kuyakimbia haya ndio baadae mtakuja kusema kuwa 'alikuwa mzigo' au alikuwa mvuta bangi au alikuwa ...... wa kisiasa.
 

Ungeweka ushahidi usingekuwa na sababu ya kuandika kitabu kizima. Watu hapa wakiona ushahidi huwa wanakubali. Sasa wewe unaeleza mengi lakini ushahidi hakuna na ndio maana bado watu wanakuuliza ushahidi wa madai yako hapa.
 
Mi sisemi hivyo lakini najua muda si mrefu kuna watu wakiingia humu watasema ni kwa kuwa tu si mchaga!

Wakuu,

Demokrasia ya nchi, chama au club husimamia katiba ya nchi hiyo, chama hicho au club husika.

Kwa kawaida inakuwa siyo busara kuweka njia ya kuingia bila ya kuwapo njia ya kutokea.

Mimi si mwanachama wa CHADEMA wala sijui katiba ya chama hicho inasemaje. Lakini, naamini hatua ya Bwana Wangwe kusimamishwa uongozi ni hatua ya kwanza.

Kusimamishwa uongozi si kufukuzwa uongozi. Kwa hiyo nafikiri hatua itakayofuatia ni hatua hiyo kufikishwa kwenye mkutano mkuu wa wanaongozwa, wenye chama na hao ndio watakaoamua kama wanathibitisha kusimamishwa kiongozi wao na kumfukuza kazi au watatengua kusimamishwa huko na wamwache aendelee kuwaongoza.

Kila likundi kina sheria zake za kufuatwa au kuvunjwa. JF hali kadhalika. Mara ngapi humu watu wamefungiwa na kufunguliwa? Mbona hatukusema JF ni kikundi cha wajinga?

Sheria tunazojiwekea mara zote zinakuwa msumeno. Zinakata huku na huko.
 

Je ni uongozi upi ambao unauongelea kwa ni imara na ulio bora na maisha ya Watanzania wengi wapi ambayo yameboreshwa?

Je una uhakika ya kwamba wengi wanapiga kura bila ya kujua kwa nini wanapiga kura ama wanapiga kuchagua yule wanayemuona anafaa kwa wakati huo.?

chadema wamemsimamisha Chacha kwa madai kwamba anakiuka maadili waungwana mnaamua kulalamika sana hili jambo ati linaua upinzani...

Kwa nini mazuri yote ambayo Upinzani unafanya kujijenga mayachukulia kama mawazo 'negative'? Chenge pamoja na kashfa za Ufisadi aliporudi katika Baraza la Mawaziri mlifurahia, hakusikitika kama ambavyo mnafanya sasa?

CHADEMA ni shamba lenye miche inayochipua na katu hatutokubali kuyaacha magugu yamee na kukua na miche bora! tunategemea mavuno mema kwa kile tulichokipanda na si vinginevyo!
 
good news! MWKJJ kama ungekuwa na kituo cha TV, nadhani kingekuwa hot kuliko TBC!!
 
Wapinzani wa chadema mnanichekesha sana. Hivi nyie mnayaamini vipi maneno ya Wangwe?
Si kafukuzwa na chama? kwani kafukuzwa na Mbowe? mbona wengi uelewa ni mdogo?
Wangwe kafukuzwa na Chama. Na kwa sababu mdomo tu ni mali yake na haukufukuzwa ana mamlaka nao kuutumia kwa jinsi aonavyo yeye.
Mwisho bado naamini Chadema itabaki imara bila Wangwe.
Lakini ccm inayoogopa kuwafukuza mafisadi eti kwa kukiokoa chama, wataishia kuiporomosha Danganyika yetu.
 

Kikwete akiwa Raisi na Lowasa Waziri Mkuu kilitokea nini baada ya Mtendaji Mkuu wa Serikali kuvurunda...

CCM kuwa na mbegu kama hizi ndio zinachangia uchafu wa Chama kwa kukumbatia Uozo! Kujisafisha ni wajibu kabla ya aibu ya harufu mbaya kukukumba!
 
wenyeviti wa vyama vingi vya upinzani ni kama miungu ukitaka ukione cha moto wakosoe, hivyo demokrasi ni ndogo ndiyo maana CCM itaendelea kongoza tu. Demokrasi ndani ya CCM IPO JUU na jamaa wanaweza kukosoana kwa kiasi kikubwa kulinganisha upinzani.
huo ni mtazamo wangu tu
 

mmmmmmmhhhhhh unasema kweli?😳
 

Yanapatina sehemu gani? kwenye Klh news? napata tabu kuyapata.
 
Mwkjj,
Kwa mara nyingine tena hongera kuwa mstari wa mbele katika kupambanua mchele na pumba. Tunayasubiri kwa makini.
 
Mwanakijiji, Kesho mda gani ili tuchungulie?
 
Ungeweka ushahidi usingekuwa na sababu ya kuandika kitabu kizima. Watu hapa wakiona ushahidi huwa wanakubali. Sasa wewe unaeleza mengi lakini ushahidi hakuna na ndio maana bado watu wanakuuliza ushahidi wa madai yako hapa.

Sio wote wanaelewa darasani, nimetoa darasa na wenye kuelewa wamelewa ni mwaka 2000 ndio alikwenda TLP,muulize Zitto Kabwe labda utamuelewa.

Nitumie email yako nikwambie jina analotumia Mbowe kwenye mtandao kama tulivyokubaliana.
 
Yatakuwa hewani kuanzia mapema asubuhi... kwa walioko Marekani bila ya shaka itakuwa ni late tonite.
 

Any summary?
 
Kwa wale mlioko US na sehemu nyingine ambazo mtakuwa macho nitarusha mahojiano yangu na Tundu na Wangwe kuanzia saa nne kamili EST nikiwa natangaza "live"..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…