CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

CHADEMA na nyie mmo kwenye "Zidumu fikra za Mwenyekiti na Politiburo".
Yaelekea Chacha kaingia kwenye uongozi wa juu wa CHADEMA kwa shingo upande ukiangalia mneno na mikiki iliyotumika kumfikisha hapo. Kama kweli swala ni wapi pesa ya ruzuku itumike, kaeni chini muone wapi pa kuwekeza kwa faida ya baadaye ya chama.
 
nimemfuatilia Chaha muda mrefu akiwa anatoa michango yake bungeni nikaona ni mtu asiyekuwa na malengo,haswa wakati huu wa bunge la bajeti hakuwa amejipanga kabisa.Na hili nadhani ni UGENI WA MADARAKA.Nafasi hizi tunazitaka sisi wanyonge za kupeleka mawazo yetu huko sebuleni ila naona mwenzangu chaha amechezea.
 
maana hili mla chaha kudai Ruzuku wakati NDESAMBURO amekikopesha chama zaidi ya 100 mil na Mbowe amekipa zaidi ya 500 mil na wapo kimya Then mtu analia na milion 65 naona amelewa madaraka huyo,kwakuwa amefikia kuwa makamu anaona atakuwa mwenyekiti soon!!!THATS WRONG CHACHA
 
CHADEMA nao wanapaswa kujifunza sasa. Nilitaraji kuwa Guninita aliporejea CCM lilikua somo tosha kwao. Nashindwa kuelewa ni kwa vipi hawa wanao cross toka vyama vingine wapokewe kwa kutuzwa vyeo. Guninita aliingia akapewa uenezi, alipoondoka akaja Akwilombe, akaukwaa. Nina hofu CHADEMA isije kuwa inashawishi wanachama wa vyama vingine kuhamia huko kwa hivi vyeo.
 

Mkuu ina maana unyonge wako unamaanisha unaweza ukawa kiongozi??
 

Hili la bangi ukitaka litumike usije kushangaa kuwa Mwenyekiti wako yupo.
 
Hili la bangi ukitaka litumike usije kushangaa kuwa Mwenyekiti wako yupo.

Mwenyekiti wangu? Yupi huyo. Ni IMANI yangu bado kwamba Mh. Wangwe kwa UMAKAMU ni cheo KIKUBWA MNO kwake. Au ni yale ya ANC na ZUMA kule Bondeni? Na MREMA na URAIS wa TZ?
 

Waheshimiwa wote mmekuja hapa jamii Forums kumkashifu Wangwe ina maana huko kamati kuu haikutosha? huko mlikuwa uso kwa uso mngempa vidonge vyake live kuliko kuja hapa na kauli mbiu ya kuwa Wangwe ni mzigo mzito, kama mnamuogopa kiasi hiki basi tumieni kanga kama wanawake wanavyofanya mtengeneze kanga za mafumbo.

Kitila anaweza kuvaa iliyoandikwa ' Zigo zito tumelitua mwaya ' na Zitto Kabwe iwe na maneno 'Utajiju na bangili zako' kuwa atajijua na bangi zake,

Mwenyekiti anaweza kuvaa inayosema 'Tulikwambia mpaka kitaeleweka ama kweli wewe ni kubwajinga' na Mnyika ' mcheza kwao hutunzwa au mvua usioijua imekunyeshea' mcheza kwao mwenyekiti lazima ashinde, wanawake hutumia kanga kufikisha ujumbe kuliko kumkabili mtu wanaemuogopa.

Maandishi yenu hapa yanaonesha kuwa Wangwe alikuwa anaishi katika mazingira magumu sana kama Makamu Mwenyekiti, kumbukeni yeye ana nguvu ya wanachama sio makao makuu wanaotumia JF ambao sio wanachama.
 

Kwani wewe ni msemaji wa Wangwe? Watu wanatoa maoni yao kulingana na issue at hand na hayo ni maoni yao kama nawe unavyotoa maoni yako ambayo mengi yanaonekana udaku tu na uzushi.
 
Kwani wewe ni msemaji wa Wangwe? Watu wanatoa maoni yao kulingana na issue at hand na hayo ni maoni yao kama nawe unavyotoa maoni yako ambayo mengi yanaonekana udaku tu na uzushi.

Tuko pamoja kuwa Wangwe katengenezewa Uzushi na Udaku. naweza kuwa msemaji wa Wangwe siku zote Mnyonge hupata watu wa kumsemea na Wangwe amewapata wengi sana kuanzia Es,Mtanzania na mimi.
kama alivyopata Mbowe wasemaji wewe,Tanzania Njema, kitila na wengine wengi sana.

kama watu wanatoa maoni yako kulingana na issue iliyopo,hukutenda haki kwa kutowauliza nao kama ni wasemaji wa Mbowe? Maneno yako aliulizwa Mtanzania na mwenzako jana kuwa yeye ni nani kwenye Chadema hadi anajadili?
 
Wangwe kapewa nafasi ya kujieleza na mtu yeyote anaweza kumsikia kwenye KLH news na vile vile Lissu naye. Wangwe amekubali adhabu aliyopewa na amesema hatima yake iko mikononi mwa wajumbe.
 
Wangwe nimemsikia kule klhnews ni kweli kaonewa kabisa!Chuki binafsi kabisa maana madai ya wangwe ni ya kweli
 

nimekuuliza swali kutokana na kile ulichoandika hapa:


Tanzania njema katoa maoni yake kisha wewe unasema kuwa amekuja kumkashifu Wangwe huku ukisema kuwa yeye ni memba wa kamati kuu ya Chadema. Swali hilo hilo linakuja kwako, je wewe ni msemaji wa Wangwe au ni memba wa kamati kuu ya chama kipi? .... I guess ni ccm.

Nimesoma ukidai kuwa Kitila aliwahi kuwa mwanachama wa NCCR na TLP kitu ambacho umekosa ushahidi hapa. Je utaleta ushahidi ulioombwa na Kitila?
 
Wangwe katoboa siri kasema hata ukienda makao makuu hadi madereva ni wachaga!kwi kwi kwi!Chadema subirini 2010!Kura za wachaga peke yao zitawapeleka ikulu!
 
Mkk kwenye ukweli lazima usemwe!

Kama wewe unaona kuwa huu ni ukweli na ni lazima uuseme basi nakuachia ukumbi kwenye issue ya ukabila na kukupa kombe kubwa la ushindi. Ukisoma hii thread utagundua makanusho mengi sana kwenye hili toka kwa watu kibao hapa.

Katika hili, endelea tu na rants mkulu yangu macho na masikio na huruma kidogo juu yako. Ninajua kuna mengi sana wana ccm mnaweza kuargue na chadema kuhusu sera. Sidhani kama la ukabila (ambalo si kweli) ni moja of them.

Kuna mtu alianzisha thread hapa kuwa ccm ni chama cha kiislam na kusema kuwa 75% ya viongozi wake ni waislam (na hoja hiyo ikapingwa maana haina nguvu). Ukienda huko yatakushinda mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…