CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?



Kwa hiyo ni kweli kuwa hakukuwa na agenda ya kumsimamisha, lakini ilitenegnezwa pale pale kwenye mkutano kama anavyodai baada ya kukamiwa na mwenyekiti, ambacho ni kinyume na katiba, au?
 
FMES chunga sana na watu hawa, karibu watakuingiza katika ufalme wao. Endelea kuwa mtu huru ndugu yangu wasiukuingize kutetea mikakati ya Rostam ya kujisafisha kwa gharama za kuichafua CHADEMA.

Rostam hawezi kuitumia Chadema kujisafisha na matatizo yake ndani ya CCM, Rostam siye aliyemchagua Wangwe kuwa makamu, kama kuna mahali ameingia ni baada ya kuona huko ndani mna matatizo ambayo hayajashughulikiwa when the right times demanded,

Chadema sio a threat kwa CCM, isipokuwa kuna baadhi ya viongozi kama Zitto na Dr. Slaaa ambao baadhi ya viongozi mafisadi wangependa kuzizima hoja zao na hizo ni individuals efforts, sio chama kiziama cha CCM, no way!

Kuingizwa kwenye ufalme wa mtu humu forum kwa sababu ya maoni yangu kuhusu Chadema, unless kuna something sikielewi as of your words!
 
Kwa hiyo ni kweli kuwa hakukuwa na agenda ya kumsimamisha, lakini ilitenegnezwa pale pale kwenye mkutano kama anavyodai baada ya kukamiwa na mwenyekiti, ambacho ni kinyume na katiba, au?

Field Marshal ES

Najua wewe ni mtu wa hoja, na ni mtu wa kusoma. Niwapi nimesema katiba imekiukwa? Nimeeleza kwa kirefu kuwa Katiba imefuatwa.

Wala suala hilo halikutengenezwa kikaoni na wala halikuanzishwa na Mwenyekiti.

Katiba ya CHADEMA kifungu 6.3.6(f) inatoa mamlaka ya Kamati Kuu kupiga kura wakati wowote kura ya kutokuwa na imani na kiongozi wa kitaifa ili kumsimamisha uongozi.

Ndio hayo mamlaka yalitumika. Na yalitokea wakati wa Ajenda ya kujadili Taarifa ya Kamati ya Wazee kuhusu Viashiria vya Mgogoro vilivyotokana na Matendo, Maneno na Maamuzi ya Makamu Mwenyekiti, Bwana Chacha Wangwe!

Kutokana na maneno, manendo na maamuzi yake Chacha Wangwe ndipo ikapigwa kura ya kutokuwa na imani naye, na hoja hii haijatolewa na Mwenyekiti, ilitolewa na wajumbe wengine kabisa wakina Chiku Abwao, Mjumbe wa Kamati Kuu toka Iringa na Naibu Meya wa Kigoma Bwana Chacha Wangwe nk. Wazee wa Chama wakasema hiyo haitakuwa heshima kwake, wakamuomba ajiuzulu Mwenyewe, Chacha akagoma na kuwasema vibaya wazee hao. Hapo ndio Kamati Kuu ikamua kupiga kura 2/3 ya kumsimamisha.

Haikuwa uamuzi kama ule wa Mkapa wa kuondoa jina la Malecela Dodoma ambao haukufuata Katiba ya CCM, huu ulikuwa ni uamuzi wa kikatiba kabisa wa kumwajibisha kiongozi aliyeenda kinyume na katiba.

Nashangaa watu hawakuwa mstari wa mbele kumwambia Malecela apite kwenye vyombo vya habari na mikoani kusema ameonewa lakini hapa wako mstari wa mbele kutaka Chacha Wangwe aliyewajibishwa kwa kukiuka kanuni, maadili na itifaki kuzunguka kwenye vyombo vya habari na mikoani wakati ambapo adhabu yake ilifuata katiba ya CHADEMA.

Asha
 

Kusema CHADEMA sio threat wa CCM inadhihirisha kwamba mwanachama wa Chama Cha Mafisadi huwa haachi asili.

Kwamba chama ambacho kila Vikao vya juu vya CCM vikikaa lazima vikataje na kujadili mwelekeo wake sio threat, are you serious!

Kwamba CHADEMA sio threat halafu CCM kama chama kinatoa matamko ya kumjibu Mbowe, ya kuwajibu viongozi wengine wa CHADEMA wakina Dr Slaa, Zitto nk is grossly understatement.

Kusema kwamba CHADEMA sio threat kwa CCM wakati huo huo CCM kutumia nguvu kubwa kushindana na CHADEMA kila uchaguzi mdogo unapojitokeza ni hadithi ya mbuni kufunika kichwa kwenye mchanga!

Mbona hupinga maelezo ya Paparazi Muwazi jinsi Rostam Aziz alivyomsaidia fedha Chacha Wangwe kwenye kampeni zake za Makamu Mwenyekiti na baada ya hapo, na jinsi anavyomsaidia baada ya kusimamishwa kuendeleza ajenda zake? Nashauri suala hili ukabishane kwanza na Paparazi Muwazi kule maana yeye yuko tayari kutoa data zaidi. Mlengwa hapa ni Dr Slaa, pengine yote ni picha ya kihindi!

Kwamba CCM kama Chama hakizimi hoja ya ufisadi! No way, Hujaona jinsi ambavyo Makamba na Mwanri wakati huo walipoyakataa masuala yote ya EPA, Richmond kuwa ni uwongo since 2006-2007? Hujaona sasa Chiligati naye alivyoingia mtego huo? Kama CCM haiwalindi Mafisadi mbona NEC imeshindwa kuchukua hatua? Au mmegawanyika makundi makubwa mawili ndani ya chama chenu?

Ama kweli, mtoto wa kondoo ni kondoo!

Asha
 
wewe uliyeshindwa chaguzi zote za CCM hadi ukahamia TLP ndio umeishiwa hoja. ungekuwa na hoja ungechaguliwa.


Jamani mbona mnamuonea Kitila wangu? Watu hapa wameeleza kuwa hajawahi kuwa TLP na yeye mwenyewe amethibitisha hilo jamani? Mmeshindwa kujibu hoja sasa mnaanza kumshambulia Kitila?

Asha
 
Mheshimiwa saafi sana kwa kutuweka sawa hapa maana sheria ni sheria na hapa naona iko wazi na very clear! Tupo ukurasa mmoja hapa.

Great! Maana wengine hapa wanadhani Chacha amefukuzwa bila kufuata taratibu kumbe ukweli ni kuwa amesimamishwa tu kwa kufuata katiba ya CHADEMA kifungu 6.3.6(f)

Asha
 
Ama kweli, mtoto wa kondoo ni kondoo!

ninajaribu kusoma mengine kwanza, lakini so far I like this comment, kwa sababu ndiyo hasa niliyokuwa ninasema jana kuwa ukianza kwenda hiyo angle sasa na mimi ninakuwa sina njia ila kukufuata huko huko kwenye hiyo angle ya ID, sasa umeanza mwenyewe!

Mimi ni member huru hapa na ni wajibu wangu kutoa maoni yangu as I see fit, haya maneno juu sio hoja ya siasa tunayojadili hapa..ila ni personal attack, sasa I will let this pass lakini sio next time!

Kwa sababu sina tatizo kuwa kondoo, lakini siwezi kuwa bendera kwa ujira mdogo sana
 

Mengi kati ya haya hufanywa na baadhi ya viongozi wachache ndani ya CCM kwa ajili ya kujikomba kwa mwenyekiti lakini hazijawahi kuwa collective ideas za CCM as chama,

uchaguzi ni uchaguzi hakuna anayeweza kupuuzia uchaguzi, lakini ukiiisha tu ni wakati wa kutawala, Wangwe kutumiwa na Rostam ni kwa sababu ya makosa ya Chadema kuruhusu au kufuga matatizo ndani yake kwa muda mrefu bila ya kuyagusa, off course Mwalimu alisema sana kuwa mficha ugonjwa hufichuliwa na kifo,

Chadema ni chama cha siasa, kuwa na matatizo ni kitu cha kawaida the ishu ni jinsi wanavyolittatua tatizo, siamini kuwa kwa kudai kuishinikiza CCM na Rostam, ndani ya matatizo yake Chadema inajisaidia in anyway, kuna wakati wa ku-deal na CCM na kuna wakati wa ku-deal na matatizo ya ndani ya chama ni vitu viwili tofauti,

U-threat wa chama kimoja cha siasa against kingine huonyeshwa na matokeo ya uchaguzi, ninawaombea sana Chadema na kulitatua hili la Wangwe kwa usalama, kwa sababu Wangwe anaweza kuwagwa na kuwamegua that itakuwa ni hasara kwa taifa,

hatuombei hayo lakini wajitahidi kutatua haya ya Wangwe kwa amani! kama ni CCM ni kweli huwa tuna makundi toka enzi za Mwalimu, na hiyo ndio demokrasia yenyewe lakini tuna tatizo la viongozi mafisadi wachache hiyo sio siri, lakini pia tunajitahidi kuyatatua matatizo yetu bila kusingizia chama wala mtu mwingine!
 

Heeh! Kumbe nimegonga ikulu eeeh. Ulisema mwenyewe humu JF kuwa wewe ni mtoto wa CCM sasa kama umesema mwenyewe mimi kusema mtoto wa kondoo ni kondoo imekuwa kosa?

Salaleeeeeeeeeee haya endelea. Jibu hoja zangu basi

Asha
 

I humbled the sincerity you have shown now!

Nami napunguza mipasho for now.

Naamini CHADEMA wanayatatua matitatizo yao ya ndani vizuri tu. Tatizo linapokuja pale mtu kama Rostam anapotumia mtu mmoja wa ndani kutoa masuala ya ndani nje na kuyapotosha kuchanganya uwongo kibao. Hapo lazima chama kitoke nje na kuweka mambo sawa.

Kama upande wa pili ungekuwa na uwezo wa kununua watu wa CCM viongozi waandamizi kufanya kama anayofanya Wangwe unadhani CCM ingekuwaje? Maana haya yanasemwa kuhusu CHADEMA ni punje ndogo sana ya yale yaliyoko CCM. Tena yale ya ndani ya CCM ya Mafisadi ni uozo uliovuka mipaka.

Cha msingi tuijenge nchi yetu. Ndio maana nikakuomba usiingie kwenye kundi la kina Kubwa Jinga na Kuhani ambao lengo lao ni kubomoa upinzani tu bila sababu zozote za msingi.

Wewe you are greater than that. Tuendelee kuilinda CHADEMA kwa manufaa ya taifa letu. Chama hiki ndio kimbilio kwa wote ndani ya CCM ambao hawakubaliani na Chama hicho kuendelea kugeuzwa genge la mafisadi.

Luv ya!

Asha
 
CHADEMA mkiendelea kusigana hivi mnatengeneza OMBWE la UONGOZI ambalo kwa hakika wapinzani wenu watalitumia kuwasaidia kujimaliza au wao kuwamaliza. Ninyi sasa hivi mnamwona RA tu, wanaotaka mmalizane wako wengi.
 
I humbled the sincerity you have shown now! Nami napunguza mipasho for now.

Sina sababu yoyote ya kuwa na mipasho na wewe, mimi ninajadili taifa tu hapa hayo ya mipasho ni yako ya kujaribu kutishia ili watu waogope kuuliza maswali serious kuhusu chadema na matatizo yake, maana nimeona mara nimekuwa kondoo, mara ninatumiwa hayo ni ya kawaida wala hayanisumbui,

nimesema toka mwanzo kuwa Chadema watatue matatizo bila kusingizia Rostam kwa sababu yalikuwepo huko Chadema hata kabla Rostam hajaingia kwenye siasa za bongo za taifa
 


Yalikuwepo yapi hayo? Unaweza kunieleza hayo matatizo ambayo unataka CHADEMA wayatatue?

Uliza tu maswali serious kuhusu CHADEMA, Kubwa JINGA aliuliza ya kwake nimemjibu yote. Ya kwako ni yapi? Uliza tu tujadili mustakabali wa taifa!

Wapi nimesema kwamba wewe unatumika? Nilichosema ni kwamba mtoto wa kondoo ni kondoo na kwamba wakati mwingine unaonyesha ukada wako. Hakuna mahali nimesema wewe unatumika! Unless kama unanitafsiri nisivyo sema.

Na kuhusu mipasho wewe ndio umeanzisha kwa kusema kwamba CHADEMA si chochote kile, kwa kusema CHADEMA kama chama haina kitu ila kuna watu wawili tu Zitto na Dr Slaa ndio wanashindana na baadhi ya mafisadi ndani ya CCM. Mimi nawewe nani ameanza?

CHADEMA inatatua matatizo yake ndani bila kumsingizia Rostam wala nani, haya matatizo yalishatatuliwa toka 2006, sasa inapotokea mtu kama Wangwe au yoyote yule akaenda kinyume na maamuzi ya chama iwe kwa nia yake binafsi au kwa kutumia lazima atachukuliwa hatua. Na inapotokea watu wakaamua kuzitumia hatua hizo kama fimbo ya kuichafua CHADEMA lazima kuweka wazi.

Wewe unadhani kwanini Rai na Mtanzania kwa uratibu wa Balille wako mstari wa mbele kuandika habari za kuichafua CHADEMA hata pale wanapoelezwa kabisa kabla kwamba taarifa hizi na hizi si za kweli ukweli ni huu, ushahidi ni huu lakini bado wanaandika ule uwongo ulitaka CHADEMA inyamaze? Au umesahau kwamba hawa ndio waliokuwa mstari wa mbele kuandika makala na habari za kuwasafisha Lowassa na Rostam?

Asha
 
kuna kila dalili ya moto kuwaka ndani ya chadema...kama hazitafanyika juhudi za makusudi za kuumaliza mgogoro huu yatakuwa yaleyale ya akina NCCR-Mageuzi na TLP.Cha msingi hapa wanachama wa chadema mliomo humu JF muwashauri viongozi wenu watafute suluhu ya mgogoro huu na dhambi mbaya hapa ni ukabila kuliko hata ufisadi...kama mtaendelea kupigana jihadi ya kutetea hali hali hii kana kwamba hakuna mgogoro ndani ya chadema basi mnakiua hichi chama kilichoanza kujipatia umaarufu nchini hasa tanzania bara.tunajua kule visiwani CUF wapo imara kwa upande wao kule.
 

Mtizedi

Unadhani wanachama wa CHADEMA humu ni mbumbumbu wa kukukabali hoja yako wewe uliye nje ya chama kuwa kuna mgogoro ndani ya chama wakati wao ni wanachama wanakaa vikao vya chama na wanajua kuwa hakuna mgogoro ila mtu mmoja tu amechukuliwa hatua za kinidhamu? Mnaka mpandikize mgogoro kwa maneno ya nje? chukua kadi ya uanachama uingie kwenye vikao ili uone kama kuna mgogoro.

Karibu CHADEMA, chama cha demokrasia na maendeleo. Na mwaka huu ni wa uchaguzi wa chama, karibu ugombee, nilishatoa mwito hapa wa watu kugombea toka mwanzoni mwa mwaka huu kuanzia ngazi ya msingi

Asha
 

hahahhahahhaahahahahaa.......

mwanakijiji naona haya maswala ya ukabila wa chadema yatakupunguzia heshima yako kubwa uliyojijengea miongoni mwa internet communities duniani na hata hapa JF.
Ushauri wa bure usitumie nguvu nyingi kutetea haya mambo kama yapo au hayapo unatakiwa kuyakemea ili yaondoke ndani ya chadema na sio kutumia tani za nguvu na nishati kuyatetea,yatakuvunjia heshima bure...ni kazi kubwa kuutetea ukabila ...

otherwise nakubaliana na baadhi ya points zako ulizotoa hapo juu
 

Umeamua kumtisha Mwanakijiji ili aogope kusimamia ukweli? Hebu acha uzushi wako huko. Ukweli ni mmoja tu hauna itikadi.

Hebu ingia hapa pia usome na ya kwangu. Umejidhihirisha kuwa uko kazini. Karibu sana JF hapendwi mtu, zinapendwa hoja tu:https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=245335#post245335

Una maswali?

Asha
 

Hivi CHADEMA Tatizo ni WANGWE tu ama Pia kamati yote ya Mziray na Mziray mwenyewe pia na wazee aliowataja PM.Ipi ni SPIN nzuri??
 
Hivi CHADEMA Tatizo ni WANGWE tu ama Pia kamati yote ya Mziray na Mziray mwenyewe pia na wazee aliowataja PM.Ipi ni SPIN nzuri??

Wangwe sio tatizo ila wangwe mwenyewe ndio ana matatizo na amechukuliwa hatua za kinidhamu. Mziray is not an issue, although Chacha Wangwe alitaka kumtumia Mziray kutimiza malengo yake. Ukweli ni kwamba Kamati kuu ili dismiss kinachoitwa kamati ya Mziray ambacho hakikuwepo kwa kweli.

Kamati iliundwa ya watu watano: Mziray Mwenyekiti, Mama Khatau toka lindi Katibu, wajumbe Mbogoro, Shilembi na Muhsin toka pemba. Sasa yakatokea yafuatayo. Bwana Mziray akaandika ripoti yake kwa kushirikiana na Shilembi. Katibu wa Kamati akakataa kusaini, bwana Muhsin akafariki baadaye, Wakili Mbogoro hakushiriki hata kikao kimoja cha kamati. Sasa kuna kamati hapo! Hebu acheni mzaha, ndio maana nawapongeza kamati kuu kwa ku-dismiss hiyo ripoti na wajumbe kutoa makaripio kwa Mziray. Kwa hiyo ngazi ya Chacha kupandia kumwondoa Dr Slaa ikaporomoka! Na mkakati ukakatika! Sasa arudi mezani akajipange upya, akirudi atakuwa na nidhamu na atafanya kazi kwa uwajibikaji wa pamoja. Sasa hapo kuna mpasuko gani ndani ya CHADEMA? Mpasuko lazima kuwe na makambi makubwa kadhaa sasa kuna kambi gani kama ni Chacha dhidi ya CHADEMA kwa kuwa tu amechukuliwa hatua za kinidhamu?

Asha
 

haya mama chadema.....but ushauri wa bure fanyeni suluhu ya migogoro ndani ya chadema ....usitumie nguvu nyingi kufunika moto utaungua buree..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…