CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

FIKRA MGANDO OHH NO MBADALA ?

Upo kwa ajili ya kazi maalumu , nalitegemea hilo kuwa hivyo ila majibu yalishatolewa soma thread za nyuma utaweza kupata majibu ya kina ya hizo propaganda unazoziita tuhuma za Mh.Wangwe.

Pili kwa kuwa jana ulikutana naye mshauri Mh.Wangwe aende bungeni kutetea wananchi wake wa Tarime kwani walimpa kazi ya kuwawakilisha ,sasa Wizara ya madini ilipitisha bajeti bila hata wananchi wa Nyamongo kutetewa juu ya dhuluma wanazofanyiwa na North Mara ambao ni BARRICK .
 
RUZUKU, UKABILA WAIGAWA CHADEMA

CHADEMA ndicho chama pekee nchini kilichokuwa kinaonekana kutokuwa na migogoro, lakini hili la ruzuku na mengine yanaelekea kukigawa katika makundi mawili ya CHADEMA – MBOWE na CHADEMA – WANGWE.

Hali hii imejitokeza baada ya kutokea malalamiko ya wanachama wa CHADEMA kususu masuala kadhaa ya msingi. Masuala hayo yameibua mgawanyo uliozaa makundi hayo mawili na baadaye Mwenyekiti wa chama hicho FREEMAN MBOWE akatangaza kumsimamisha Makamu Mwenyekiti (CHACHA WANGWE).

Kwa tafakuri pana kila Mtanzania alitarajia kwamba kabla ya kumsimamisha Makamu Mwenyekiti, CHACHA WANGWE, Mwenyekiti wa chama hicho alitakiwa kujibu tuhuma moja baada ya ingine ili kujisafisha yeye mwenyewe pamoja na viongozi wengine wa juu wa CHADEMA.

Kimsingi,CHACHA WANGWE anamtuhumu MBOWE katika masuala yafuatavyo:-

Mosi, Kuna matumizi mabaya ya ruzuku (ufisadi wa ruzuku) ndani ya CHADEMA Makao Makuu. Hivyo, CHACHA WANGWE anamtaka Mwenyekiti FREEMON MBOWE atoe maelezo ya matumizi ya Ruzuku, ambayo ni fedha ya walipa kodi inayotolewa na serikali kwa vyama vyenye wabunge. Aidha WANGWE anamtaka MBOWE aonyeshe mapato na matumizi ya Ruzuku hiyo katika vikao vya chama au aunde kamati ya kuchunguza tuhuma hizo. Pia, WANGWE ana mashaka na hesabu zinazoonyesha mgawanyo wa matumizi ya ruzuku yanayopelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa kutoka chama cha CHADEMA.

Pili, CHACHA WANGWE hakubaliani na kitendo cha Mwenyekiti na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kuzuia ruzuku isifike mikoani. Anasema hali hii ina maana matawi ya chama yasifunguliwe na chama kisiwe na ofisi hali ambayo inadhoofisha chama. Vivyo hivyo, WANGWE hakubaliani na kitendo cha MBOWE kufuja fedha za chama kwa ziara za helkopta huku akiwaacha wagombea ubunge na udiwani wa chama chake hawana msaada wowote wa kifedha kutoka katika chama. Katika mazingira haya WANGWE anauliza nani anakihujumu chama kati ya MBOWE na WANGWE? Nani anadhoofisha CHADEMA?

Tatu, CHACHA WANGWE ana hoja kwamba MBOWE, anawajibika kuwaeleza watanzania, ni kwa vipi wabunge watano kati ya sita wa kuteuliwa (viti maalum) wote watoke mkoa wa Kilimanjaro ( MBOWE ni Mchaga wa Kilimanjaro). Ikumbukwe kwamba Tanzania bara ina mikoa 21 na Zanzibar mikoa 5. Kwa kawaida, idadi ya viti maalum inategemea idadi ya wabunge ambao chama kinapata katika uchaguzi mkuu, ambapo asilimia 90 ya viti vya ubunge zilizoleta viti maalum vya CHADEMA zilitoka kanda ya Ziwa. Hivyo, MBOWE kasahau kanda zilizosaidia CHADEMA ikipata viti maalum na kuvipeleka KILIMANJARO.

Nne, CHACHA WANGWE anamtaka MBOWE, aeleleze inakuwaje kati ya wakurugenzi nane wa Idara mbalimbali za CHADEMA wanne ni Wachaga wa Kilimanjaro?

Tano, WANGWE anamtaka MBOWE, aeleze umma wa watanzania inakuwaje Madereva wote wa Makao Makuu ya CHADEMA ni Wachaga kutoka Kilimanjaro?

Sita, WANGWE anataka MBOWE, ajibu tuhuma kwamba yeye mwenyewe, DR WILBROAD SLAA na PHILIMON NDESAMBULO wanajilipa fedha kwa ajili ya kurudisha gharama walizotumia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. WANGWE anauliza mbona wanachama wengine hawarudishiwi gharama hizo akiwemo yeye WANGWE? Je, huu siyo ufisadi? Je huku ni kutenda haki?

Saba, WANGWE anataka kujua ni kwa nini miaka minne iliyopita MBOWE alivunja tawi la CHADEMA mkoa wa DAR ES SALAAM na kubaki na CHADEMA Makao Makuu. Hatua hii imekifanya chama hicho kukosa viongozi na wawakilishi wa chama mkoa wa Dar ES salaam.

Nane, WANGWE anataka kujua kwa nini Wakurugenzi wote wa CHADEMA wameteuliwa na MBOWE badala ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya chama kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA. Aidha, Kwa Mujibu wa katiba ya CHADEMA kifungu 7.7.3 (vii), Katibu mkuu anatakiwa kuwajibika kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekti. Hata hivyo, DR SLAA ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA hakuwa akitoa ushirikiano kwa WANGWE hadi kufikia kumnyima ofisi alipoteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.

Tisa, Katika moja ya hatua za kumfukuza WANGWE katika Uongozi, Katibu Mkuu aliitisha kikao cha Kamati ya wazee wanne wa CHADEMA lakini kati yao wawili wakiwa wa kabila la Mwenyekiti . Wazee hao wa Kichaga ni EDWIN MTEI ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Wazee wa CHADEMA na PHILIMON NDESAMBULO. Hapo kulikuwa na mgongano wa kimaslahi (conflict of interest). Ikumbukwe kwamba, Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA Bw. EDWIN MTEI ni baba mzazi wa mke wa FREEMON MBOWE kwa maana kwamba MTEI ni mkwe wa MBOWE. Mke wa MBOWE anaitwa DR LILIAN EDWIN MTEI ( Hivi sasa anajulikana kwa jina la DR LILIAN FREEMON MBOWE) ni binti wa EDWIN MTEI.

Kumi, CHACHA WANGWE analalamika kwamba suala la kumfukuza liliibuka ghafla katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA wakati halikuwemo katika agenda. Inadaiwa kwamba MBOWE ndiye aliibua agenda hiyo. Kwa mujibu wa kanuni za CHADEMA, kama suala hilo lilitakiwa kuwa agenda ilitakiwa lijulishwe kwa wajumbe siku 21 kabla ya kikao ili wapate mawazo ya wanachama. Hata hivyo, liliibuka katika kikao bila mtuhumiwa CHACHA WANGWE kujiandaa. Aidha, katika kuhakikisha kuwa WANGWE anavuliwa madaraka yake kwenye kikao, baadhi ya viongozi waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho kwa mujibu wa katibu hawakupata mwaliko kwa sababu ilihofiwa kuwa wangekuwa upande wa WANGWE.

Kwa ufupi WANGWE anadai kwamba kuna ufisadi Makao Makuu ya CHADEMA. Kwamba MBOWE hajatoa maelezo kuhusiana na tuhuma hizo na badala yake anamtuhumu WANGWE kwamba anakigawa chama na kuamua kumsimamisha uongozi.

Katika uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti uliopita, CHACHA WANGWE hakuwa chaguo la Mwenyekiti MBOWE, lakini aliweza kushinda. Kutokana na kitendo cha CHACHA WANGWE kutangaza kwa mara ingine kugombea Uenyekiti wa CHADEMA katika uchaguzi wa Disemba 2008 amezidi kujenga maadui kutoka Makao Makuu ya chama hicho. Hofu ya MBOWE inatokana na ukweli kwamba, hivi sasa WANGWE anaungwa mkono na matawi mengi ya CHADEMA nchini kutokana na msiamamo wake wa kutenda haki na kusimamia ukweli daima.

Hivyo, MBOWE akamjengea zengwe kwamba, WANGWE anavujisha siri za chama lakini katika kikao cha Kamati Kuu hawakuweza kueleza siri ambazo WANGWE anadaiwa kuvujisha. Kwa sababu hiyo, WANGWE anadai kwamba hakuelezwa siri alizovujisha hatua ambayo inakidhi matakwa ya kisheria kwamba MBOWE amemhukumu WANGWE bila hatia. Hatua hii ina lengo la kukwaza ustawi wa demokrasia na utawala bora katika vyama vya siasa.

Katika hili la kuvujisha siri WANGWE anajitetea kwamba kama kuzungumza na wana CCM ni kosa basi mtu aliyetakiwa kuwajibika ni DR SLAA ambaye mke wake ni diwani wa kuchaguliwa wa CCM wakati mkewe CHACHA WANGWE ni mwanachama mwaminifu wa CHADEMA. Kitendo cha DR SLAA kuwa na mke mkereketwa wa CCM yamkini Nyaraka za siri za CHADEMA zinaweza kuangukia kirahisi kwa mkewe na hatimae CCM na pia wageni wa CHADEMA wanaofika nyumbani kwa DR SLAA ambako kuna tawi la CCM kwa maana ya mkewe DR SLAA ambaye anawajibika kuwakirimu wageni na hivyo kusikia mazungumzo yao. WANGWE anataka kujua ni nani kati yake na DR SLAA anaeweza kuvujisha siri za CHADEMA?

Aidha, imeonekana kwamba, kutokana na nafasi yake ya Ubunge WANGWE na wabunge wengine wa upinzani wanaweza kujipatia marafiki kutoka chama tawala CCM kama ambavyo Wabunge wa CCM wanaweza kuwa na marafiki kutoka vyama vya upinzani. Urafiki huu unaweza kuwa wa binafsi/kawaida kuliko mambo ya siasa kwa sababu ya uzalendo, hivyo tofauti ya itikadi siyo uadui bali ni suala la kusimamia ukweli kama ambavyo ZITTO KABWE alivyojumuika na wabunge wa CCM katika kamati ya madini ya Bomani.

Pia WANGWE anadai, kwamba kama kuzungumza na wana CCM ni kosa mbona MBOWE amewahi kuonekana akiwa katika mazungumzo na Rais JAKAYA KIKWETE hata kufikia kumkumbatia mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Halikadhalika MBOWE ameonekana katika mazungumzo na viongozi wengine wa CCM, vivyo hivyo wana CHADEMA wengine?

Kwa ujumla kashfa hizi zinakuja wakati bado baadhi ya Watanzania wanahoji uadilifu wa FREEMAN MBOWE. Kashfa ya kukopa na kushindwa kulipa deni la NSSF kwa muda stahiki ilitia mashaka ya uadilifu wa MBOWE kwa taifa lake. Hakika bila kujibu hoja nzito za WANGWE, Mwenyekiti MBOWE asitarajie kupata kura za Watanzania wenye fikra mbadala katika uchaguzi ujao ndani ya chama chake na asijisumbue kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Natoa mwito kwa MBOWE kuitisha mkutano wa waandishi wa Habari kujibu tuhuma moja baada ya nyingine. Vinginevyo MBOWE atakuwa ameingia katika kundi la Wenyeviti wa vyama vya siasa wanaoua demokrasia nchini.

Kwa upande mwingine, DR SLAA na KABWE ZITTO wamekuwa watu muhimu kwetu watanzania katika kutoa hoja zinazohusiana na ufisadi bungeni lakini inashangaza wameshindwa kudhibiti ufisadi wa MBOWE ndani ya CHADEMA na badala yake wamemwachia WANGWE pekee. Hakika watu hawa walitusaidia sana katika kuunda tume za kuchunguza Richmond na EPA inakuwaje kwa muda mrefu tangu Desemba 16, 2007 wanakalia ripoti ya Kamati ya Mziray iliyoundwa kuchunguza mambo yanayoweza kusababisha migogoro ndani ya CHADEMA? Kamati hiyo ilibaini ubaguzi wa kikabila na kidini katika CHADEMA lakini haikuwekwa wazi kwa Watanzania na wala haijafanyiwa kazi. Je tuwaelewe vipi viongozi hao wa CHADEMA? Ufisadi ni ule unaofanywa na viongozi wa serikali ya CCM tu? Je sio kweli kwamba Hisani siku zote inapasa kuanzia nyumbani???

Mpaka Kieleweke

Mwambie Fikra Mbadala aje kwanza huku ajibu haya:https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=15327

Namkaribisha sana JF,naona kilimchomleta leo ni ku-post tu huo ujumbe walioupeleka Mwananchi ukakataliwa!

PM
 
RUZUKU, UKABILA WAIGAWA CHADEMA

CHADEMA ndicho chama pekee nchini kilichokuwa kinaonekana kutokuwa na migogoro, lakini hili la ruzuku na mengine yanaelekea kukigawa katika makundi mawili ya CHADEMA – MBOWE na CHADEMA – WANGWE.

Hali hii imejitokeza baada ya kutokea malalamiko ya wanachama wa CHADEMA kususu masuala kadhaa ya msingi. Masuala hayo yameibua mgawanyo uliozaa makundi hayo mawili na baadaye Mwenyekiti wa chama hicho FREEMAN MBOWE akatangaza kumsimamisha Makamu Mwenyekiti (CHACHA WANGWE).

Kwa tafakuri pana kila Mtanzania alitarajia kwamba kabla ya kumsimamisha Makamu Mwenyekiti, CHACHA WANGWE, Mwenyekiti wa chama hicho alitakiwa kujibu tuhuma moja baada ya ingine ili kujisafisha yeye mwenyewe pamoja na viongozi wengine wa juu wa CHADEMA.

Kimsingi,CHACHA WANGWE anamtuhumu MBOWE katika masuala yafuatavyo:-

  1. Mosi, Kuna matumizi mabaya ya ruzuku (ufisadi wa ruzuku) ndani ya CHADEMA Makao Makuu. Hivyo, CHACHA WANGWE anamtaka Mwenyekiti FREEMON MBOWE atoe maelezo ya matumizi ya Ruzuku, ambayo ni fedha ya walipa kodi inayotolewa na serikali kwa vyama vyenye wabunge. Aidha WANGWE anamtaka MBOWE aonyeshe mapato na matumizi ya Ruzuku hiyo katika vikao vya chama au aunde kamati ya kuchunguza tuhuma hizo. Pia, WANGWE ana mashaka na hesabu zinazoonyesha mgawanyo wa matumizi ya ruzuku yanayopelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa kutoka chama cha CHADEMA.
  2. Pili, CHACHA WANGWE hakubaliani na kitendo cha Mwenyekiti na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kuzuia ruzuku isifike mikoani. Anasema hali hii ina maana matawi ya chama yasifunguliwe na chama kisiwe na ofisi hali ambayo inadhoofisha chama. Vivyo hivyo, WANGWE hakubaliani na kitendo cha MBOWE kufuja fedha za chama kwa ziara za helkopta huku akiwaacha wagombea ubunge na udiwani wa chama chake hawana msaada wowote wa kifedha kutoka katika chama. Katika mazingira haya WANGWE anauliza nani anakihujumu chama kati ya MBOWE na WANGWE? Nani anadhoofisha CHADEMA?
  3. Tatu, CHACHA WANGWE ana hoja kwamba MBOWE, anawajibika kuwaeleza watanzania, ni kwa vipi wabunge watano kati ya sita wa kuteuliwa (viti maalum) wote watoke mkoa wa Kilimanjaro ( MBOWE ni Mchaga wa Kilimanjaro). Ikumbukwe kwamba Tanzania bara ina mikoa 21 na Zanzibar mikoa 5. Kwa kawaida, idadi ya viti maalum inategemea idadi ya wabunge ambao chama kinapata katika uchaguzi mkuu, ambapo asilimia 90 ya viti vya ubunge zilizoleta viti maalum vya CHADEMA zilitoka kanda ya Ziwa. Hivyo, MBOWE kasahau kanda zilizosaidia CHADEMA ikipata viti maalum na kuvipeleka KILIMANJARO.
  4. Nne, CHACHA WANGWE anamtaka MBOWE, aeleleze inakuwaje kati ya wakurugenzi nane wa Idara mbalimbali za CHADEMA wanne ni Wachaga wa Kilimanjaro?
  5. Tano, WANGWE anamtaka MBOWE, aeleze umma wa watanzania inakuwaje Madereva wote wa Makao Makuu ya CHADEMA ni Wachaga kutoka Kilimanjaro?
  6. Sita, WANGWE anataka MBOWE, ajibu tuhuma kwamba yeye mwenyewe, DR WILBROAD SLAA na PHILIMON NDESAMBULO wanajilipa fedha kwa ajili ya kurudisha gharama walizotumia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. WANGWE anauliza mbona wanachama wengine hawarudishiwi gharama hizo akiwemo yeye WANGWE? Je, huu siyo ufisadi? Je huku ni kutenda haki?
  7. Saba, WANGWE anataka kujua ni kwa nini miaka minne iliyopita MBOWE alivunja tawi la CHADEMA mkoa wa DAR ES SALAAM na kubaki na CHADEMA Makao Makuu. Hatua hii imekifanya chama hicho kukosa viongozi na wawakilishi wa chama mkoa wa Dar ES salaam.
  8. Nane, WANGWE anataka kujua kwa nini Wakurugenzi wote wa CHADEMA wameteuliwa na MBOWE badala ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya chama kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA. Aidha, Kwa Mujibu wa katiba ya CHADEMA kifungu 7.7.3 (vii), Katibu mkuu anatakiwa kuwajibika kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekti. Hata hivyo, DR SLAA ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA hakuwa akitoa ushirikiano kwa WANGWE hadi kufikia kumnyima ofisi alipoteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.
  9. Tisa, Katika moja ya hatua za kumfukuza WANGWE katika Uongozi, Katibu Mkuu aliitisha kikao cha Kamati ya wazee wanne wa CHADEMA lakini kati yao wawili wakiwa wa kabila la Mwenyekiti . Wazee hao wa Kichaga ni EDWIN MTEI ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Wazee wa CHADEMA na PHILIMON NDESAMBULO. Hapo kulikuwa na mgongano wa kimaslahi (conflict of interest). Ikumbukwe kwamba, Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA Bw. EDWIN MTEI ni baba mzazi wa mke wa FREEMON MBOWE kwa maana kwamba MTEI ni mkwe wa MBOWE. Mke wa MBOWE anaitwa DR LILIAN EDWIN MTEI ( Hivi sasa anajulikana kwa jina la DR LILIAN FREEMON MBOWE) ni binti wa EDWIN MTEI.
  10. Kumi, CHACHA WANGWE analalamika kwamba suala la kumfukuza liliibuka ghafla katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA wakati halikuwemo katika agenda. Inadaiwa kwamba MBOWE ndiye aliibua agenda hiyo. Kwa mujibu wa kanuni za CHADEMA, kama suala hilo lilitakiwa kuwa agenda ilitakiwa lijulishwe kwa wajumbe siku 21 kabla ya kikao ili wapate mawazo ya wanachama. Hata hivyo, liliibuka katika kikao bila mtuhumiwa CHACHA WANGWE kujiandaa. Aidha, katika kuhakikisha kuwa WANGWE anavuliwa madaraka yake kwenye kikao, baadhi ya viongozi waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho kwa mujibu wa katibu hawakupata mwaliko kwa sababu ilihofiwa kuwa wangekuwa upande wa WANGWE.

Hii habari ni nzuri na imeandikwa kwa ufasaha. Read Please.

Mimi kama mwangaliaji hakuna upande ambao nitauona unaridhisha kwenye hili. Mzee mwanakijiji tungeomba umlete Mbowe redioni kwako kama ulivyfanya kwa Wangwe ili ajibu hayo maswali 10 hapo juu.
 
KubwaJinga, yote aliyosema Asha ni sahihi na ninakubaliana naye. Sina la kuongeza if you have specific question, I have no objection and in the interest of transparency will provide the necessary answers to the best of my ability. Hakuna hofu kupeana taarifa sahihi. Tunaitaka Serikali itupe taarifa sahihi katika masuala yote ya ufisadi na sisi wenyewe tuwe tayari kutoa majibu sahihi tunapohitajika kufanya hivyo. Uongozi ni dhamana na nimeapa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Msahafu wa dini yangu kuwa daima nitasema kweli na kweli tupu. Tujenge nchi ni yetu wote.
 
Dr. Slaaa kuna hoja imeibuliwa kuwa Wangwe anavujisha siri ya Chadema kwa watu wa CCM ktk sense ya kukutana nao, nae Wangwe anasema Mkeo ni DIWANI wa CCM...kuna possibility kuwa mkeo akawa na siri nyingi anawapa CCM....hapo unaweza kutuelewesha vipi wanJF...
 
Ni kweli mke wa Dr Slaa ni Diwani wa CCM Viti Maalum kata ya Busuto, kumbuka Dr Slaa kabla ya kujiunga na CHADEMA alikuwa CCM ambapo alipochoka na ufisadi wao kwenye kura za maoni akahama.

Lakini hajawahi kutuhumiwa kwa namna yoyote kuvujisha siri za CHADEMA kwenda CCM kwa kuwa tu ana mke CCM.

Dr Slaa anajua mipaka ya kazi yake, hata shughuli zake za kichama anazifanyia ofisi ama katika maeneo ya faragha.

Na wala Chacha hajahukumiwa kwa kuwa karibu na CCM kwa maana ya kufahamiana. Ingekuwa hivyo angehukumiwa kuwa na urafiki wa muda mrefu na Sarungi mbunge wa CCM.

Inaposemwa kwamba Chacha amevujisha siri CCM manake ni kwamba kuna ushahidi wa wazi wa hilo.

Yeye mwenyewe amekiri mbele ya umma kwamba alivuka bahari na kwenda kukutana na Kaborou nyumbani kwa Kabarou.

Sasa kuna ushahidi wa vikao hivyo vilikuwa vinajadili siri za CHADEMA kwa kushirikiana na wanaojiita waliokuwa viongozi wa Dar es salaam.

Ushahidi kuwa anatoa nyaraka kwa watu wa CCM mmeuona wenyewe kwenye gazeti la fisadi Rostam Azizi kuhusiana na Taarifa ya Mziray.

Kuna tofauti kati ya kufahamiana na kuvujisha siri. Kila kiongozi wa CHADEMA hakatazwi kuwa na marafiki CCM lakini hakuna anayeruhisiwa kuvujisha siri.

Unless useme: ni siri gani Dr Slaa amevujisha kwa mkewe? Lakini kuna ushahidi wa siri alizuvujisha Chacha Wangwe!

Asha
 
Kwa sisi tulio nje ya mifumo ya vyama vya kisiasa, inatusikitisha sana kuona mikoroganyo inapotokea ndani ya mojawapo ya vyama vinavyotegemewa kuleta demokrasia nchini. Hivi karibuni tumeona mvutano ndani ya chama cha CHADEMA kati ya upande unaomuunga mkono mwenyekiti wa chama hicho, Mh. Freeman Mbowe na upande mwingine akiwapo aliyekuwa makamu wake ambaye amevuliwa madaraka, Mh. Chacha Wangwe.

Tumesoma nyaraka na maoni mbali mbali juu ya shutuma za kila upande lakini kila kukicha tunashindwa kuelewa lipi ni lipi. Kati ya nyaraka kuu zilizoleta shutuma mbalimbali, zipo tatu ambazo zinaweza kuitwa nyaraka kuu juu ya huu mgogoro, ambapo mbili zinampendelea Mh.Mbowe na moja ikimuunga mkono Mh. Wangwe.

Hizi ni sura mbili za shutuma zikielekezwa kila upande. Nimejaribu kuzifupisha lakini msomaji anaweza kutumia kibinyio kwenye kila kariri ili zimfikishe nilipozitoa ili azisome kwa urefu wake wote.

Maswali mbali mbali yamejitokeza, na ningeshauri kila mwenye maswali ya ziada aongezee ili wahusika waweze kutujibu. Unaweza kulielekeza kwa upande unaopendelea kama unaona swali lako ndipo linakohitaji jibu;
  1. Kuna ushahidi gani wa Rostam Aziz kuhusishwa na huu mgogoro?
  2. Hiyo ripoti ya tume ya Mziray, kwa nini isiwekwe wazi na kujadiliwa ukweli au uongo wake?
  3. Je haingekuwa vema kwa Mh. Mbowe naye kufanya mahojiano na MMJJ (KLH) ili kujibu shutuma zilizoelekezwa kwake?
  4. Je hapangeweza kufikiwa utatuzi mwingine wowote badala ulio bora na kukinusuru chama kisigawanyike badala ya kumfukuza Mh. Wangwe hasa tukitilia maanani kuwa uchaguzi uko karibu?
  5. Ni kwa nini Mziray kama amepika ripoti kwa kutumia pesa ya Rostam Aziz, asichukuliwe hatua za kinidhamu kama alivyofanyiwa Mh. Wangwe?
  6. Kama malalamiko ya Mh. Wangwe juu ya wabunge wa kuteuliwa, madereva na wakurugenzi, je haingekuwa vema kurekebisha hizo nafasi badala ya kumfukuza Wangwe na kuanzisha mgogoro?
  7. Kwenye mahojiano na KLH, Wangwe alipendekeza kuwa angalau TShs. 100,000 (jumla TShs. 14 million approx.), zitengwe kwa ajili ya kila wilaya, je hili sio wazo zuri ili kuwa na matawi yatakayovuta wanachama kila pande ya nchi badala ya CHADEMA kuwa chama cha mikoa fulani tu?
  8. Kwa chama chenye mapato madogo kama CHADEMA, je sio wazo zuri kuachana na Helcopter ambayo ni ya gharama kubwa sana na kutumia njia nyingine kuhamasisha wananchi?
Haya ni yangu machache na ninategemea kusikia mengi zaidi toka kwa wahusika. Hapo chini nazinukuu baadhi ya hizo nyaraka:

Zinazomuunga Mkono Bw. Freeman Mbowe

1.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
NA
KUSIMAMISHWA KWA MHESHIMIWA CHACHA ZAKAYO WANGWE (MB.) KUWA KAIMU MAKAMU MWENYEKITI WA TAIFA (BARA) WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

Ndugu wanahabari na wananchi wenzangu,

Tarehe 28 Juni 2008 Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo katika kikao chake cha kawaida kilimsimamisha Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe kama Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Taifa (Bara) wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kumpigia kura ya siri ya kutokuwa na imani naye. Huu ni uamuzi mzito na ambao haujawahi kufanywa katika historia ya miaka 16 ya CHADEMA. Tunapenda kuwafahamisha wananchi wetu kwamba uamuzi huu mzito ulichukuliwa baada ya mjadala na tafakuri ya muda mrefu. Kamati Kuu ya chama chetu ilifikia hatua hiyo dhidi ya baada ya kuridhika na ushahidi kwamba Mh. Chacha Wangwe amekiuka maadili ya uongozi na hivyo kupoteza sifa mahsusi za kuendelea kuwa kiongozi wa kitaifa wa CHADEMA kwa sababu zifuatazo:

1. Amekuwa akijihusisha na/au kushiriki katika vikundi na/au vitendo vya uchonganishi na/au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa chama na/au wanachama wake.

2. Amekuwa akitoa tuhuma nzito lakini zisizokuwa na msingi dhidi ya viongozi wenzake wa kitaifa na watendaji wa chama pasipo kupitia vikao halali na wala kuzingatia taratibu za chama

3. Amekuwa akikashifu chama, viongozi na watendaji wake bila kutofautisha kashfa na ukosoaji wa kisiasa na/au wa kiutendaji

4. Kuvujisha siri za vikao halali vya chama kwa watu wanaotaka kuhujumu chama

Ndugu wananchi na wanahabari,

Kamati Kuu ya CHADEMA haikufikia uamuzi huu mzito kwa haraka na/au bila kufikiria kwa kina madhara yake kwa chama na kwa taifa letu. Kamati Kuu imefikia uamuzi huu baada ya jitihada mbali mbali za kumsaidia Mh. Chacha Zakayo Wangwe kujisahihisha na kujirudi kushindikana kabisa. Jitihada hizi mbali mbali ni kama vile:

a. Vikao mbali mbali na vya muda kati yake mwenyewe, Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu kujadili tofauti na/au migongano kati yao na/au ndani ya chama;

b. Kusuluhishwa na Kamati ya Wazee wa Chama ambapo Mh. Wangwe alitakiwa kuandika maandishi kwamba ataacha vitendo vyake dhidi ya chama, viongozi wa kitaifa na watendaji wa chama;

c. Kamati Kuu ya chama kumuonya kuacha vitendo vyake hivyo dhidi ya chama;

d. Baada ya jitihada zote hizi kushindikana, Kamati Kuu ilimsihi kujiuzulu kwa hiari yake yeye mwenyewe na hivyo kujiepusha na adha ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na kusimamishwa na Kamati Kuu.

Kwa vitendo na matukio yote haya, Kamati Kuu ya CHADEMA imejikuta haina njia yoyote ile ya kuepuka mgogoro mkubwa zaidi na usio na maana au msingi zaidi ya kumchukulia hatua za kinidhamu Mh. Chacha Zakayo Wangwe. Kwa matendo haya ni wazi Mh. Chacha Zakayo Wangwe amepoteza sifa mahsusi za kuendelea kushikilia dhamana kubwa ya uongozi ambayo vikao halali vya chama vilimpatia. Kamati Kuu imelazimika kutumia mamlaka yake ya kikatiba ya kumsimamisha uongozi wa kitaifa Mh. Wangwe kwa kumpigia kura ya siri ya kutokuwa na imani naye. Azimio la kumsimamisha Mh. Wangwe kuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti Taifa (Bara) liliungwa mkono na wajumbe ishirini na nne kati ya thelathini na moja waliohudhuria na kushiriki katika kikao cha Kamati Kuu. Idadi hii ni zaidi ya theluthi mbili ya kura za wajumbe wa Kamati Kuu inayohitajika kikatiba ili kumsimamisha uongozi kiongozi yeyote wa kitaifa kama alivyokuwa Mh. Chacha Zakayo Wangwe. Kamati Kuu imechukua hatua hii ngumu na nzito ili kukiokoa chama kutokana na migogoro ambayo imesambaratisha vyama vingine vya siasa hapa nchini.

Asanteni sana
-----------------------------------------------
Freeman A. Mbowe
MWENYEKITI

2.
Naona hatimaye Waraka huu umeletwa JF. Huu ndio Waraka alioandika Balillle na kumpa Mzee Yusuph Halimoja, ndio waraka ambao Chacha Amekuwa akipita katika vyombo vya habari kutoa hoja zake akiusoma.
Katika waraka huu mtaona ule mkakati niliowadokeza wa kumweka Mbowe mwenyewe kikaangaoni, hii ilikuwa ni baada ya mkakati wa mwanzo wa kumng'oa kwanza Dr Slaa kushindwa.
Katika waraka huu Kamati ya Mziray imetajwa, mtakumbuka niliwaeleza siku za nyuma kuhusu hili. Hii ndio njia mpya ya Wagawe, Uwatawale inayoendelea.
Na katika taarifa hii Balille anafanya spinning sasa kuwa ripoti hii iliminywa toka mwezi Disiemba kumbe ukweli ni kuwa ni Mwenyekiti wa Kamati Bwana Mziray ndiye ambaye katika vikao vyote vya kamati kuu vilivyofuata hakutaka kuleta ripoti yake mpaka Mkakati na Rostam wa kumtoa Dr Slaa Dodoma Juni 28 akaipeleka ripoti hiyo Dodoma siku moja kabla ya kikao ili ripoti hiyo isipitie kwenye sekretariati kama zilivyo nyaraka nyingine za kamati kuu.

Sasa kuhusu taarifa ya Mziray, pamoja na kuwa ilifika dodoma bila kupitia sekretariati mwenyekiti Mbowe akiamini katika demokrasia alikubali ijadiliwe(kwa mujibu wa wachambuzi hili lilikuwa kosa la kisiasa la mbowe).
Taarifa hiyo ilijikita katika kusema CHADEMA kuna ubaguzi wa ukabila, elimu na dini. Kwamba CHADEMA inapendelea zaidi wasomi katika kugawa nafasi za utumishi makao makuu na hata viti maalumu. Pia taarifa ili eleza kuhusu ukabila kwa kutumia takwimu zilizotajwa hapo juu.
Mjadala ulipoanza ikabainika kwamba Kamati ya Mziray iliandika taarifa za uwongo kabisa na majungu kwa kutoa takwimu na hoja za uwongo. Kura zikapigwa na wajumbe 29 wa Kamati Kuu wakaikataa hiyo taarifa kama si nyaraka ya chama(total dismissal). Wajumbe wawili tu wakapiga kura za ndio, Mwenyekiti wa kamati Mziray na mjumbe wa Kamati Mzee Shilembi wa Shinyanga. Hata wajumbe wengine wawili wa kamati hiyo waliikataa ripoti hiyo, Katibu wa Kamati mama Sophia Khatau alipiga kura ya hapana na Wakili Mbogoro Mjumbe wa kamati naye alikataa kwa kuwa hakushiriki kwenye vikao vya Kamati. Mjumbe mmoja toka Pemba wa Kamati hiyo alifariki kabla ya Kamati kuwasilisha kazi yake.

Zinazomuunga Mkono Bw. Chacha Wangwe

3.
RUZUKU, UKABILA WAIGAWA CHADEMA

CHADEMA ndicho chama pekee nchini kilichokuwa kinaonekana kutokuwa na migogoro, lakini hili la ruzuku na mengine yanaelekea kukigawa katika makundi mawili ya CHADEMA – MBOWE na CHADEMA – WANGWE.

Hali hii imejitokeza baada ya kutokea malalamiko ya wanachama wa CHADEMA kususu masuala kadhaa ya msingi. Masuala hayo yameibua mgawanyo uliozaa makundi hayo mawili na baadaye Mwenyekiti wa chama hicho FREEMAN MBOWE akatangaza kumsimamisha Makamu Mwenyekiti (CHACHA WANGWE).

Kimsingi,CHACHA WANGWE anamtuhumu MBOWE katika masuala yafuatavyo:-
  1. Mosi, Kuna matumizi mabaya ya ruzuku (ufisadi wa ruzuku) ndani ya CHADEMA Makao Makuu. Hivyo, CHACHA WANGWE anamtaka Mwenyekiti FREEMON MBOWE atoe maelezo ya matumizi ya Ruzuku, ambayo ni fedha ya walipa kodi inayotolewa na serikali kwa vyama vyenye wabunge. Aidha WANGWE anamtaka MBOWE aonyeshe mapato na matumizi ya Ruzuku hiyo katika vikao vya chama au aunde kamati ya kuchunguza tuhuma hizo. Pia, WANGWE ana mashaka na hesabu zinazoonyesha mgawanyo wa matumizi ya ruzuku yanayopelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa kutoka chama cha CHADEMA.
  2. Pili, CHACHA WANGWE hakubaliani na kitendo cha Mwenyekiti na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kuzuia ruzuku isifike mikoani. Anasema hali hii ina maana matawi ya chama yasifunguliwe na chama kisiwe na ofisi hali ambayo inadhoofisha chama. Vivyo hivyo, WANGWE hakubaliani na kitendo cha MBOWE kufuja fedha za chama kwa ziara za helkopta huku akiwaacha wagombea ubunge na udiwani wa chama chake hawana msaada wowote wa kifedha kutoka katika chama. Katika mazingira haya WANGWE anauliza nani anakihujumu chama kati ya MBOWE na WANGWE? Nani anadhoofisha CHADEMA?
  3. Tatu, CHACHA WANGWE ana hoja kwamba MBOWE, anawajibika kuwaeleza watanzania, ni kwa vipi wabunge watano kati ya sita wa kuteuliwa (viti maalum) wote watoke mkoa wa Kilimanjaro ( MBOWE ni Mchaga wa Kilimanjaro). Ikumbukwe kwamba Tanzania bara ina mikoa 21 na Zanzibar mikoa 5. Kwa kawaida, idadi ya viti maalum inategemea idadi ya wabunge ambao chama kinapata katika uchaguzi mkuu, ambapo asilimia 90 ya viti vya ubunge zilizoleta viti maalum vya CHADEMA zilitoka kanda ya Ziwa. Hivyo, MBOWE kasahau kanda zilizosaidia CHADEMA ikipata viti maalum na kuvipeleka KILIMANJARO.
  4. Nne, CHACHA WANGWE anamtaka MBOWE, aeleleze inakuwaje kati ya wakurugenzi nane wa Idara mbalimbali za CHADEMA wanne ni Wachaga wa Kilimanjaro?
  5. Tano, WANGWE anamtaka MBOWE, aeleze umma wa watanzania inakuwaje Madereva wote wa Makao Makuu ya CHADEMA ni Wachaga kutoka Kilimanjaro?
  6. Sita, WANGWE anataka MBOWE, ajibu tuhuma kwamba yeye mwenyewe, DR WILBROAD SLAA na PHILIMON NDESAMBULO wanajilipa fedha kwa ajili ya kurudisha gharama walizotumia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. WANGWE anauliza mbona wanachama wengine hawarudishiwi gharama hizo akiwemo yeye WANGWE? Je, huu siyo ufisadi? Je huku ni kutenda haki?
  7. Saba, WANGWE anataka kujua ni kwa nini miaka minne iliyopita MBOWE alivunja tawi la CHADEMA mkoa wa DAR ES SALAAM na kubaki na CHADEMA Makao Makuu. Hatua hii imekifanya chama hicho kukosa viongozi na wawakilishi wa chama mkoa wa Dar ES salaam.
  8. Nane, WANGWE anataka kujua kwa nini Wakurugenzi wote wa CHADEMA wameteuliwa na MBOWE badala ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya chama kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA. Aidha, Kwa Mujibu wa katiba ya CHADEMA kifungu 7.7.3 (vii), Katibu mkuu anatakiwa kuwajibika kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekti. Hata hivyo, DR SLAA ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA hakuwa akitoa ushirikiano kwa WANGWE hadi kufikia kumnyima ofisi alipoteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.
  9. Tisa, Katika moja ya hatua za kumfukuza WANGWE katika Uongozi, Katibu Mkuu aliitisha kikao cha Kamati ya wazee wanne wa CHADEMA lakini kati yao wawili wakiwa wa kabila la Mwenyekiti . Wazee hao wa Kichaga ni EDWIN MTEI ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Wazee wa CHADEMA na PHILIMON NDESAMBULO. Hapo kulikuwa na mgongano wa kimaslahi (conflict of interest). Ikumbukwe kwamba, Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA Bw. EDWIN MTEI ni baba mzazi wa mke wa FREEMON MBOWE kwa maana kwamba MTEI ni mkwe wa MBOWE. Mke wa MBOWE anaitwa DR LILIAN EDWIN MTEI ( Hivi sasa anajulikana kwa jina la DR LILIAN FREEMON MBOWE) ni binti wa EDWIN MTEI.
  10. Kumi, CHACHA WANGWE analalamika kwamba suala la kumfukuza liliibuka ghafla katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA wakati halikuwemo katika agenda. Inadaiwa kwamba MBOWE ndiye aliibua agenda hiyo. Kwa mujibu wa kanuni za CHADEMA, kama suala hilo lilitakiwa kuwa agenda ilitakiwa lijulishwe kwa wajumbe siku 21 kabla ya kikao ili wapate mawazo ya wanachama. Hata hivyo, liliibuka katika kikao bila mtuhumiwa CHACHA WANGWE kujiandaa. Aidha, katika kuhakikisha kuwa WANGWE anavuliwa madaraka yake kwenye kikao, baadhi ya viongozi waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho kwa mujibu wa katibu hawakupata mwaliko kwa sababu ilihofiwa kuwa wangekuwa upande wa WANGWE.
Kwa ufupi WANGWE anadai kwamba kuna ufisadi Makao Makuu ya CHADEMA. Kwamba MBOWE hajatoa maelezo kuhusiana na tuhuma hizo na badala yake anamtuhumu WANGWE kwamba anakigawa chama na kuamua kumsimamisha uongozi.

Hivyo, MBOWE akamjengea zengwe kwamba, WANGWE anavujisha siri za chama lakini katika kikao cha Kamati Kuu hawakuweza kueleza siri ambazo WANGWE anadaiwa kuvujisha.

Aidha, imeonekana kwamba, kutokana na nafasi yake ya Ubunge WANGWE na wabunge wengine wa upinzani wanaweza kujipatia marafiki kutoka chama tawala CCM kama ambavyo Wabunge wa CCM wanaweza kuwa na marafiki kutoka vyama vya upinzani.

Natoa mwito kwa MBOWE kuitisha mkutano wa waandishi wa Habari kujibu tuhuma moja baada ya nyingine. Vinginevyo MBOWE atakuwa ameingia katika kundi la Wenyeviti wa vyama vya siasa wanaoua demokrasia nchini.

Kwa upande mwingine, DR SLAA na KABWE ZITTO wamekuwa watu muhimu kwetu watanzania katika kutoa hoja zinazohusiana na ufisadi bungeni lakini inashangaza wameshindwa kudhibiti ufisadi wa MBOWE ndani ya CHADEMA na badala yake wamemwachia WANGWE pekee. Hakika watu hawa walitusaidia sana katika kuunda tume za kuchunguza Richmond na EPA inakuwaje kwa muda mrefu tangu Desemba 16, 2007 wanakalia ripoti ya Kamati ya Mziray iliyoundwa kuchunguza mambo yanayoweza kusababisha migogoro ndani ya CHADEMA?

Hapa naongezea mahojiano ya Mwanasheria Tundu Lissu na Mh. Chacha Wangwe, walipohojiwa na KLH. Bonyeza hapa.
 
Unahitaji kupata mahojiano ya Wangwe na TBC Radio..., halafu ukitafuta kwa muda kidogo utaona kuna mada nyingi zaidi humu zilizoupande wa Wangwe. So it is not 2:1 kama unavyojaribu kusuggest..

Kuhusu hoja za Fikra Mbadala nilijaribu kuzichambua hapa moja baada ya nyingine na baadhi ya maswali uliyoyauliza yana majibu yake hapa:

RUZUKU, UKABILA WAIGAWA CHADEMA

Once again... wangeanza kwa kututafsiria wanaposema "Ukabila" wanamaanisha nini kwa sababu kaw muda wote ambao nimekuwa nikisoma jambo hili wanazungumzia kana kwamba tunakubaliana maana ya ukabila ni nini. Naamini kwa kuwasoma vizuri kwao ukabila si hisia za kabila moja kujitukuza dhidi ya mengine, au kujiona bora na wanastahili zaidi kuliko makabila mengine bali kwao ukabila is simply idadi. It has nothing to do with vitendo vya kabila fulani dhidi ya makabila mengine.

CHADEMA ndicho chama pekee nchini kilichokuwa kinaonekana kutokuwa na migogoro, lakini hili la ruzuku na mengine yanaelekea kukigawa katika makundi mawili ya CHADEMA – MBOWE na CHADEMA – WANGWE.

Huyo aliyeigawa katika makundi hayo ndiye mwenye lengo la kuonesha kugawanyika? Kwanini isiwe CHADEMA - KATIBA na CHADEMA - MALALAMISHI; Kwanini isiwe CHADEMA - UMOJA na CHADEMA - UTENGANO? n.K NI wazi jibu ni kuwa watu na watu ndio wanajitengenezea agenda.

Hali hii imejitokeza baada ya kutokea malalamiko ya wanachama wa CHADEMA kususu masuala kadhaa ya msingi.

Malalamiko ya wanachama wa Chadema au mwanachama mmoja. Hadi hivi sasa sijasikia mwanachama mwingine wa Chadema aliyetoa tuhuma au madai hayo ukiondoa mtu mmoja. Basi hao wengine wajitokeze na wenyewe angalau wampe nguvu huyo mwanachama mmoja. Hao "wanachama" wako wapi?

Masuala hayo yameibua mgawanyo uliozaa makundi hayo mawili na baadaye Mwenyekiti wa chama hicho FREEMAN MBOWE akatangaza kumsimamisha Makamu Mwenyekiti (CHACHA WANGWE).

Well, it went back to the two! Hakuna makundi as far as one can see; kuna mtu anayejidhania kundi na kuna chama ambacho kina uongozi ambao uko msimamo mmoja. Halafu Wangwe hakuwa Makamu Mwenyekiti alichaguliwa Kukaimu tu.

Kwa tafakuri pana kila Mtanzania alitarajia kwamba kabla ya kumsimamisha Makamu Mwenyekiti, CHACHA WANGWE, Mwenyekiti wa chama hicho alitakiwa kujibu tuhuma moja baada ya ingine ili kujisafisha yeye mwenyewe pamoja na viongozi wengine wa juu wa CHADEMA.

Hili ni wazo zuri, lakini unapotakiwa kujibu tuhuma basi utoe ushahidi wa tuhuma hizo kusema namtuhumu fulani hivi halafu uoneshe msingi wa tuhuma hizo ni kejeli. Tunaposema kwa mfano kuna matumizi mabaya ya fedha katika serikali hatusemi hewan, tunachukua ripoti ya Mkaguzi Mkuu na kuiweka hadharani na kusema ripoti hii inasema hivi, namba ni hizi, na authority ya hiyo namba ni hizi. Tuhuma za Wangwe zina msingi huo?

Kimsingi,CHACHA WANGWE anamtuhumu MBOWE katika masuala yafuatavyo:-

hebu tuziangalie tuhuma hizo na kama zina "msingi"

Mosi, Kuna matumizi mabaya ya ruzuku (ufisadi wa ruzuku) ndani ya CHADEMA Makao Makuu.

Vyama vya kisiasa vinatakiwa kutoa ripoti ya matumizi ya fedha za ruzuku kwa Msajili wa vyama vya siasa nchini. Chadema ni mojawapo ya vyama hivyo vya siasa. Katika mwaka wa fedha ulioisha Juni 30, 2007 Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali ilionesha kuwa kuna zaidi ya Shilingi Bilioni 13 ambazo vyama vya kisiasa havikutokea maelezo jinsi gani walizitumia. Bilioni hizi 13 zinahusisha fedha siyo za Chadema tu bali CCM, CUF, TLP n.k

Kwa hiyo, Chacha ana hoja hapa na yeye angeweza kutumia ripoti ya mkaguzi mkuu kama msingi wake wa kuhoji matumizi ya ruzuku inayoenda kwenye chama chake.

Hivyo, CHACHA WANGWE anamtaka Mwenyekiti FREEMON MBOWE atoe maelezo ya matumizi ya Ruzuku, ambayo ni fedha ya walipa kodi inayotolewa na serikali kwa vyama vyenye wabunge. Aidha WANGWE anamtaka MBOWE aonyeshe mapato na matumizi ya Ruzuku hiyo katika vikao vya chama au aunde kamati ya kuchunguza tuhuma hizo. Pia, WANGWE ana mashaka na hesabu zinazoonyesha mgawanyo wa matumizi ya ruzuku yanayopelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa kutoka chama cha CHADEMA.

Chacha amekuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya chama chake na ameushika umakamu. Inaonekana yeye ameona vitu ambavyo watu wengi hawajahi kuviona. Kama yeye ana msingi wa madai basi aseme na kujenga hoja kuwa Chama kilipokea kiasi fulani cha ruzuku, vitabuni imeoneshwa hivi, na matumizi yake yameoneshwa vile na haiingii akilini.

Kama kweli alikuwa ananita ya kutatuta ukweli suala la ruzuku haliendi mbali, angeenda kwa Msajili wa vyama vya siasa, angefungua kesi, n.k ili kuweza kupata taarifa hizo. Akienda kwa Msajili wa Vyama vya Kisiasa na kuuliza kuhusu Chadema kama kinatoa ripoti ya matumizi ya ruzuku kama inavyotakiwa na kama angeweza kuona ripoti hiyo. Hiyo ndiyo njia rahisi ya kuonesha jinsi ruzuku inavyotumika. Yawezekana Wangwe hajui ilipo ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa na majukumu yake?

Pili, CHACHA WANGWE hakubaliani na kitendo cha Mwenyekiti na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kuzuia ruzuku isifike mikoani.

Mwanzoni ilikuwa ni "Mbowe" sasa wameamua kuongeza na "Dr. Slaa" na muda si mrefu watamuongeza na "Zitto" na wakiona haviendi wataongeza "Kamati Kuu nzima" n.k Swali ambalo Wangwe angelijibu kwanza kabla ya kuendelea na kauli yake ni lini, wapi, na kwa amri gani ambayo Dr. Slaa na Mbowe walifanya "kitendo" cha kuzuia ruzuku isifike mikoani. Hapa kwa kumsaidia anaweza akatoa barua, email, mazungumzo, kikao, au ushahidi wowote kuwa kuna agizo au uamuzi kama huo uliochukuliwa na watu hao wawili bila kumhusisha yeye kama Kaimu Makamu Mwenyekiti.

Anasema hali hii ina maana matawi ya chama yasifunguliwe na chama kisiwe na ofisi hali ambayo inadhoofisha chama.

Sasa hili la kufungua matawi ya chama halihusiani na fedha moja kwa moja, kwani matawi mangapi ya vyama vingine yanayofunguliwa na fedha toka makao makuu? Ni hoja ya kilaghai kutaka kufanya watu waamini kuwa bila fedha toka Makao Makuu matawi hayafunguliwi. Kosa kubwa la Chadema hadi hivi ni kuwa wameshindwa kuwatia moyo mashabiki wao mikoani na wilani kujianzishia matawi yao wao wenyewe. Matawi yanayoanzishwa kwa misingi ya kupewa fedha mikoani yatakufa fedha hizo zikikoma!

Nadharia hii ya Wangwe siyo tu haina msingi lakini is impractical. Matawi yanaanzishwa na mashabiki, na kwa kadiri yanavyoongezeka hadi pale yanapofikia ngazi fulani ndivyo pesa ya kuendeshea inapoanza kutolewa. Hata CCM na mabilioni yake ya fedha haitoi ruzuku kwenye matawi yake, vinginevyo wangefilisika!

Zaidi ya yote hili wazo kuwa matazi yanaanzishwa kutoka juu halina msingi, matawi ya vyama huanza kuanzia kweny shina ambako wananchi wenyewe wanaamua kuanzisha tawi la chama chao. kwa wale wanakumbuka watakumbuka jinsi gani vyama vya NCCR na CCM vilivyokuwa vinashindana kufungua matawi na hata kule Zanzibar mashindano ya CUF na CCM. NI mara ngapi fedha toka makao makuu zimetumika kufungua matawi vijijini au mitaani? Kwanini Chadema itakiwe kutumia fedha kidogo ya ruzuku kufungua matawi vijijini?

Hoja ya Wangwe ingekuwa ya msingi kama angesema uongozi wa makao makuu haujahamisha wanachama kufungua matawi sehemu mbalimbali nchini na hivyo kukosa wanachama wengi zaidi na mapato yanayotokana na mauzo ya kadi na michango ya wanachama. That is a more valid argument than saying Makao Makuu haijatuma fedha za kuanzisha matawi! this is ab absurdo

Vivyo hivyo, WANGWE hakubaliani na kitendo cha MBOWE kufuja fedha za chama kwa ziara za helkopta huku akiwaacha wagombea ubunge na udiwani wa chama chake hawana msaada wowote wa kifedha kutoka katika chama.

Hii nayo ni hoja dhaifu. Kama Kamati Kuu au ile ya uchaguzi (whatever final authority is ) waliacha Mbowe atumie helikopta kufanya kampeni hilo ni kosa lao wao wenyewe. Wangwe mwenyewe ni sehemu ya Kamati hiyo. Njia pekee ya kumbebesha lawama Mbowe ni kuonesha kuwa viongozi wengine wote walikataa na walipiga kura ya kukataa lakini Mbowe AKAWALAZIMISHA aidha kwa ahadi au vitisho. Na kama waliogopa kumsimamia (akiwemo Wangwe) basi Mbowe ana ubavu mkubwa sana na hao wengine hawana ubavu wa kumpinga. Hilo linasema zaidi kuhusu wao kuliko yeye.

Hata hivyo, kama maamuzi yalichukuliwa kwa pamoja na uamuzi wa kutumia helikopta ulipitishwa kwa pamoja basi hapa ndio collective responsibility inapokuja. Hivyo Mbowe, Wangwe, Zitto, Slaa na wengine waliopitisha uamuzi huo wanawajibika moja kwa moja kwa kuwaacha "wagombea ubunge na udiwani wa chama chake hawana msaada wowote wa kifedha kutoka katika chama." Ina maana kile anachomtuhumu Mbowe, na yeye anahusika.

Katika mazingira haya WANGWE anauliza nani anakihujumu chama kati ya MBOWE na WANGWE? Nani anadhoofisha CHADEMA?

kama wote walihusika na mchakato wa kuruhusu hiyo chopa, the answer is simple uongozi mzima wa Chadema akiwemo Chacha Wangwe.

Tatu, CHACHA WANGWE ana hoja kwamba MBOWE, anawajibika kuwaeleza watanzania, ni kwa vipi wabunge watano kati ya sita wa kuteuliwa (viti maalum) wote watoke mkoa wa Kilimanjaro ( MBOWE ni Mchaga wa Kilimanjaro).
I

There it is! "Mbowe ni Mchagga wa Kilimanjaro"! Sitaki kujua wachagga wengine wanatoka wapi. Hili la Wabunge wote "kutoka mkoa wa Kilimanjaro" limeshajibiwa mara nyingi sana kiasi kwamba hata sitojaribu kuelezea. Tukumbuke tu kuwa kwa Wangwe madai ya ukabila kwake ni idadi. Period. Kuna Ukabila pale penye idadi ya watu wengi wa kabila moja mahali fulani. Ukifiria sana msimamo huu utashangaa ni sehemu ngapi tanzania kuna ukabila!

kumbukwe kwamba Tanzania bara ina mikoa 21 na Zanzibar mikoa 5. Kwa kawaida, idadi ya viti maalum inategemea idadi ya wabunge ambao chama kinapata katika uchaguzi mkuu, ambapo asilimia 90 ya viti vya ubunge zilizoleta viti maalum vya CHADEMA zilitoka kanda ya Ziwa. Hivyo, MBOWE kasahau kanda zilizosaidia CHADEMA ikipata viti maalum na kuvipeleka KILIMANJARO.

Mbowe ndiye aliyefanya maamuzi haya? Au ndiye mwenye kubebeshwa lawama hizo. Kwanini asiseme chombo au watu waliotoa uamuzi huu ili tuweze kuona msingi wake. Maana huyu Mbowe inawezekana ana nguvu kubwa sana kiasi watu kama kina Mbowe wanashindwa kumhoji humo humo ndani.

Nne, CHACHA WANGWE anamtaka MBOWE, aeleleze inakuwaje kati ya wakurugenzi nane wa Idara mbalimbali za CHADEMA wanne ni Wachaga wa Kilimanjaro?

Hili ni suala la ajira, lakini well bado tatizo ni "Wachagga wa Kilimanjaro" na kama mtu haoni sumu ya ukabila na chuki dhidi ya Wachagga wa "kilimanjaro" sijui iwekwe vipi ili ionekane.

lakini kama nilivyosema hapo juu kuwa kwa Wangwe Ukabilla ni idadi anaonesha namba. Basi si wangetoa na majina ya hao wakurugenzi ili tuweze kuamua kuona ukweli (validit) wa hoja yake? Hao wakurugenzi ni kina nani na je ni kweli ni Wachagga, na kweli wanatoka "Kilimanjaro"?

Tano, WANGWE anamtaka MBOWE, aeleze umma wa watanzania inakuwaje Madereva wote wa Makao Makuu ya CHADEMA ni Wachaga kutoka Kilimanjaro?

Once again tatizo siyo ajira ya watanzania bali walioajiriwa ni "wachagga" wa kutoka Kilimanjaro. Hata hivyo hili ni rahisi kwani tunayo majina ya madereva wa makao makuu.

1.Juma waziri- kutoka nachingwea.
2.Pella Ngunagwa-huyu sijui katoka wapi ila ni kusini.
3.Waziri Simba -Mkwere bagamoyo.
4.Baraka Daud -Tanga.
5.Olvary Karia -mchagga.kibosho
6.Kalikisha -Kigoma.

Sasa njia pekee ya dai hili kuwa na nguvu ni kwa Wangwe kutoa majina yake ya madereva wa makao makuu na kuonesha kuwa ni "Wachagga wa Kilimanjaro". Haitoshi tu kusema bali angalau aoneshe chembe ya ushahidi wa madai kama haya kuwa "Madereva wote".

Sita, WANGWE anataka MBOWE, ajibu tuhuma kwamba yeye mwenyewe, DR WILBROAD SLAA na PHILIMON NDESAMBULO wanajilipa fedha kwa ajili ya kurudisha gharama walizotumia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. WANGWE anauliza mbona wanachama wengine hawarudishiwi gharama hizo akiwemo yeye WANGWE? Je, huu siyo ufisadi? Je huku ni kutenda haki?

Hili ni swali zuri lakini lina ufundi. Je kuna wanachama ambao waliamua kukikopesha fedha chama fedha ambazo wanatarajia kulipwa? Kama wapo wanachama hao na ni kweli waliingia makubaliano na chama, wakatia sahihi na masharti yapo na wakatoa fedha hizo, swali kwanini wasilipwe? Jambo pekee ambalo Wangwe anaweza kulionesha ni kusema kuwa hakuna makubaliano yoyote ya kukikopesha chama na hivyo malipo wanayojilipa hayana msingi wa kisheria.

In that case kinachofanyika ni wizi na Wangwe ana haki ya kwenda mahakamani siyo kulalamika. Kwa mpambanaji kama yeye anajua wapi pa kukimbilia.

Kuhusu wanachama wengine, swali ni hilo hilo je na wao waliingia mkataba wa kukikopesha chama na hadi sasa hawalipwi? Ni kina nani hao na waliingia mkataba huo lini na kwa makubaliano gani?

Saba, WANGWE anataka kujua ni kwa nini miaka minne iliyopita MBOWE alivunja tawi la CHADEMA mkoa wa DAR ES SALAAM na kubaki na CHADEMA Makao Makuu. Hatua hii imekifanya chama hicho kukosa viongozi na wawakilishi wa chama mkoa wa Dar ES salaam.

kwa mara nyingine tena, anampa nguvu kubwa sana Mbowe. Wanachama wa Chadema Dar wako wapi kutoa malalamiko haya? Kama kuna mtu anataka kuanzisha tawi dar kwanini wasianzishe? Je ni kweli Mbowe ndiye aliyevunja tawi hilo? Hapa tunahitaji habari zaidi maana mtu mwenye nguvu ya kuvunja tawi zima na viongozi wenzie kama kina Wangwe wakawa wanamuangalia basi wamempa nguvu za kidikteta; aidha wanahitaji kubadili Katiba au kumuondoa madarakani!

Nane, WANGWE anataka kujua kwa nini Wakurugenzi wote wa CHADEMA wameteuliwa na MBOWE badala ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya chama kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA.

Hapa inabidi atuoneshe angalau hiyo Katiba inasema nini kuhusu Wakurugenzi wa Chama. Kwa kuisoma kwangu kwa haraka inasema kuwa Kamati Kuu itakuwa ina jukumu la kuwateua "Wakurugenzi wa Idara Kuu za Chama Makao Makuu"

Sasa kama kweli Mbowe ndiye aliyewateua wakurungezi hao (note a fine difference from what the constitution says and what Wangwe alleges) basi tatizo bado liko kwenye uongozi mzima wa Chadema kwa kumuacha Mbowe avunje Katiba na badala ya kumshtaki au kujenga hoja ya kuondolewa madarakani kwa kuvunja Katiba mtu anaamua kulalamika pembeni. Kumbuka hapo juu tayari ameshadai kuwa wakurunzi wanne ni "Wachagga wa Kilimanjaro".

Aidha, Kwa Mujibu wa katiba ya CHADEMA kifungu 7.7.3 (vii), Katibu mkuu anatakiwa kuwajibika kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekti. Hata hivyo, DR SLAA ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA hakuwa akitoa ushirikiano kwa WANGWE hadi kufikia kumnyima ofisi alipoteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.

Nimeangalia kwenye Katiba iliyoko kwenye tovuti yao na sijaona kipengele hicho ambacho kinasema Katibu Mkuu anatakiwa kuwajibikwa kwa Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti. Kipengele hicho kinasema hivi:

7.7.3 Viongozi Wakuu wa Ngazi ya Taifa watakuwa wafuatao:
(a) Mwenyekiti wa taifa
(b) Makamu Mwenyekiti Bara
(c) Makamu Mwenyekiti Zanzibar
(d) Katibu Mkuu
(e) Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
(f) Naibu Katibu Mkuu (Bara)

yawezekana Katiba iliongezwa kipengele kidogo cha (iii). Mwenye nacho naomba akiweke na kusema kinasemaje.

Tisa, Katika moja ya hatua za kumfukuza WANGWE katika Uongozi, Katibu Mkuu aliitisha kikao cha Kamati ya wazee wanne wa CHADEMA lakini kati yao wawili wakiwa wa kabila la Mwenyekiti . Wazee hao wa Kichaga ni EDWIN MTEI ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Wazee wa CHADEMA na PHILIMON NDESAMBULO. Hapo kulikuwa na mgongano wa kimaslahi (conflict of interest). Ikumbukwe kwamba, Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA Bw. EDWIN MTEI ni baba mzazi wa mke wa FREEMON MBOWE kwa maana kwamba MTEI ni mkwe wa MBOWE. Mke wa MBOWE anaitwa DR LILIAN EDWIN MTEI ( Hivi sasa anajulikana kwa jina la DR LILIAN FREEMON MBOWE) ni binti wa EDWIN MTEI.

I give up on this one! Tuambie basi hao wengine nao wa makabila gani?

Kumi, CHACHA WANGWE analalamika kwamba suala la kumfukuza liliibuka ghafla katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA wakati halikuwemo katika agenda. Inadaiwa kwamba MBOWE ndiye aliibua agenda hiyo.

Inadaiwa na nani, na yeye au na mtu mwingine.?

Kwa mujibu wa kanuni za CHADEMA, kama suala hilo lilitakiwa kuwa agenda ilitakiwa lijulishwe kwa wajumbe siku 21 kabla ya kikao ili wapate mawazo ya wanachama. Hata hivyo, liliibuka katika kikao bila mtuhumiwa CHACHA WANGWE kujiandaa. Aidha, katika kuhakikisha kuwa WANGWE anavuliwa madaraka yake kwenye kikao, baadhi ya viongozi waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho kwa mujibu wa katibu hawakupata mwaliko kwa sababu ilihofiwa kuwa wangekuwa upande wa WANGWE.

very vague.. taja majina au nafasi yoyote au viongozi ambao hawakufika kwa sababu walifichwa habari hizo. Kwa mujibu wa kanuni za Chadema, sasa basi angalau taja hizo kanuni ziko wapi. Kwa mujibu wa hiyo Katiba mahali pekee ambapo suala la siku 21 lipo ni hapa:

Mapendekezo ya marekebisho ya Katiba yatafikishwa kwa kamati za Wilaya sio chini ya siku 30 kabla ya tarehe ya Mkutano Mkuu unaohusika kujadili mabadiliko. Kamati za Wilaya zitatakiwa kurejesha maoni yake katika siku 21 tangu tarehe ya mapendekezo kutumwa.

Hivyo suala la siku 21 halihusiani na vikao vya kawaida bali suala la kubadilisha Katiba.

Kwa ufupi WANGWE anadai kwamba kuna ufisadi Makao Makuu ya CHADEMA. Kwamba MBOWE hajatoa maelezo kuhusiana na tuhuma hizo na badala yake anamtuhumu WANGWE kwamba anakigawa chama na kuamua kumsimamisha uongozi.

Ingekuwa kwenye mpira wa basketball hapa ndipo ile horn ya kumiss basket inapolia.. ng'eeee!

Katika uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti uliopita, CHACHA WANGWE hakuwa chaguo la Mwenyekiti MBOWE, lakini aliweza kushinda.

Wow! sasa si ndio uzuri wa demokrasia? Kwani hadi Mwenyekiti akukubali ndio uona uhalali wa wewe kuwepo. As long as umeshinda fair and square si Mbowe wala Slaa ambao wanaweza kufanya lolote nje ya taratibu za kikazi.

Kutokana na kitendo cha CHACHA WANGWE kutangaza kwa mara ingine kugombea Uenyekiti wa CHADEMA katika uchaguzi wa Disemba 2008 amezidi kujenga maadui kutoka Makao Makuu ya chama hicho.

Hakuna baya mtu kujipigia panda. Angalau tunaweza kuona nini kinafanyika. It is all about election. Ni kuhusu kuchaguliwa tu na kuwa on top!

Hofu ya MBOWE inatokana na ukweli kwamba, hivi sasa WANGWE anaungwa mkono na matawi mengi ya CHADEMA nchini kutokana na msiamamo wake wa kutenda haki na kusimamia ukweli daima.

Hadi leo sijasikia matawi yaliyojitokeza kumuunga mkono Wangwe, maana hata tawi la kwake Tarime wameanza kumgeuka. Natoa wito kwa matawi yanayomuunga Wangwe kujitokeza na kumuunga mkono hadharani. Lakini hili swali la "kutenda haki na kusimamia ukweli" tungewauliza wachagga ambao wanajikuta wanatakiwa kufanya kazi na Wangwe kama wanajisikia kutendewa haki na kufanyiwa mambo kwa ukweli. Sitoshangaa kama Wangwe anaweza kumkataa dereva Mchagga akipatiwa!

Hivyo, MBOWE akamjengea zengwe kwamba, WANGWE anavujisha siri za chama lakini katika kikao cha Kamati Kuu hawakuweza kueleza siri ambazo WANGWE anadaiwa kuvujisha. Kwa sababu hiyo, WANGWE anadai kwamba hakuelezwa siri alizovujisha hatua ambayo inakidhi matakwa ya kisheria kwamba MBOWE amemhukumu WANGWE bila hatia. Hatua hii ina lengo la kukwaza ustawi wa demokrasia na utawala bora katika vyama vya siasa.

Katika hili la kuvujisha siri WANGWE anajitetea kwamba kama kuzungumza na wana CCM ni kosa basi mtu aliyetakiwa kuwajibika ni DR SLAA ambaye mke wake ni diwani wa kuchaguliwa wa CCM wakati mkewe CHACHA WANGWE ni mwanachama mwaminifu wa CHADEMA. Kitendo cha DR SLAA kuwa na mke mkereketwa wa CCM yamkini Nyaraka za siri za CHADEMA zinaweza kuangukia kirahisi kwa mkewe na hatimae CCM na pia wageni wa CHADEMA wanaofika nyumbani kwa DR SLAA ambako kuna tawi la CCM kwa maana ya mkewe DR SLAA ambaye anawajibika kuwakirimu wageni na hivyo kusikia mazungumzo yao. WANGWE anataka kujua ni nani kati yake na DR SLAA anaeweza kuvujisha siri za CHADEMA?

Aidha, imeonekana kwamba, kutokana na nafasi yake ya Ubunge WANGWE na wabunge wengine wa upinzani wanaweza kujipatia marafiki kutoka chama tawala CCM kama ambavyo Wabunge wa CCM wanaweza kuwa na marafiki kutoka vyama vya upinzani. Urafiki huu unaweza kuwa wa binafsi/kawaida kuliko mambo ya siasa kwa sababu ya uzalendo, hivyo tofauti ya itikadi siyo uadui bali ni suala la kusimamia ukweli kama ambavyo ZITTO KABWE alivyojumuika na wabunge wa CCM katika kamati ya madini ya Bomani.

Pia WANGWE anadai, kwamba kama kuzungumza na wana CCM ni kosa mbona MBOWE amewahi kuonekana akiwa katika mazungumzo na Rais JAKAYA KIKWETE hata kufikia kumkumbatia mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Halikadhalika MBOWE ameonekana katika mazungumzo na viongozi wengine wa CCM, vivyo hivyo wana CHADEMA wengine?

Kwa ujumla kashfa hizi zinakuja wakati bado baadhi ya Watanzania wanahoji uadilifu wa FREEMAN MBOWE. Kashfa ya kukopa na kushindwa kulipa deni la NSSF kwa muda stahiki ilitia mashaka ya uadilifu wa MBOWE kwa taifa lake. Hakika bila kujibu hoja nzito za WANGWE, Mwenyekiti MBOWE asitarajie kupata kura za Watanzania wenye fikra mbadala katika uchaguzi ujao ndani ya chama chake na asijisumbue kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Natoa mwito kwa MBOWE kuitisha mkutano wa waandishi wa Habari kujibu tuhuma moja baada ya nyingine. Vinginevyo MBOWE atakuwa ameingia katika kundi la Wenyeviti wa vyama vya siasa wanaoua demokrasia nchini.

Katika hili ni wazi kuwa ni suala binafsi sana kati ya Wangwe na Mbowe at least kwa upande wa Wangwe. Ushauri wangu ni kuwa nyinyi watu wawili tu muitane Ngurdoto yenu na mkae mzungumze, no TV no radio, no newspaper na mkimaliza mje na msimamo wenu, mambo ya kukubaliana mkubaliane ya kupingana mpingane, lakini inaonekana kuna mambo mawili yanayowahusu ninyi watu wawili. It is more personal than professional.

Kwa upande mwingine, DR SLAA na KABWE ZITTO wamekuwa watu muhimu kwetu watanzania katika kutoa hoja zinazohusiana na ufisadi bungeni lakini inashangaza wameshindwa kudhibiti ufisadi wa MBOWE ndani ya CHADEMA na badala yake wamemwachia WANGWE pekee.

WoW shujaa amesimama na kujitangaza kuwa kazi anaifanya peke yake! Well, wakati mwingine mtoto anaweza kuingia chumbani na akaanza kupigana na jinamizi la chini ya uvungu, jinamizi ambalo ni yeye pekee analiona!

Hakika watu hawa walitusaidia sana katika kuunda tume za kuchunguza Richmond na EPA inakuwaje kwa muda mrefu tangu Desemba 16, 2007 wanakalia ripoti ya Kamati ya Mziray iliyoundwa kuchunguza mambo yanayoweza kusababisha migogoro ndani ya CHADEMA? Kamati hiyo ilibaini ubaguzi wa kikabila na kidini katika CHADEMA lakini haikuwekwa wazi kwa Watanzania na wala haijafanyiwa kazi. Je tuwaelewe vipi viongozi hao wa CHADEMA? Ufisadi ni ule unaofanywa na viongozi wa serikali ya CCM tu? Je sio kweli kwamba Hisani siku zote inapasa kuanzia nyumbani???

Kama Wangwe ana ripoti hiyo, basi aitoe, kama Mziray (yeye siyo mtu wa Kilimanjaro?) na yeye aitoe ili kijulikane kilichomo.
 
1. Kumi, CHACHA WANGWE analalamika kwamba suala la kumfukuza liliibuka ghafla katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA wakati halikuwemo katika agenda.

2. Inadaiwa kwamba MBOWE ndiye aliibua agenda hiyo. Kwa mujibu wa kanuni za CHADEMA, kama suala hilo lilitakiwa kuwa agenda ilitakiwa lijulishwe kwa wajumbe siku 21 kabla ya kikao ili wapate mawazo ya wanachama.

3. Hata hivyo, liliibuka katika kikao bila mtuhumiwa CHACHA WANGWE kujiandaa.

4. Aidha, katika kuhakikisha kuwa WANGWE anavuliwa madaraka yake kwenye kikao, baadhi ya viongozi waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho kwa mujibu wa katibu hawakupata mwaliko kwa sababu ilihofiwa kuwa wangekuwa upande wa WANGWE.

So far ninaamini maneno yote ya pande mbili ni hisia tu bado hatujapata ukweli, ninasema hivi kama haya maneno juu ni ya kweli, basi huko kuna tatizo kubwa na sio dogo na yanahitaji kutatuliwa sasa kwenye hii tatizo.
 
Dr.W.Slaa Dr.W.Slaa has no status.

Re: Chacha Wangwe si Makamu Mwenyekiti-Katiba ya CHADEMA

1. kuhusu Katiba ya Chadema Ibara ya 6.3.5. Hata havyo naomba nirekebishe kidogo kuhusu 6.3.5(b). Nafasi inayokaimiwa kwa muda usiozidi miezi sita ni viongozi "walioteuliwa tu" tafsiri yako.

2. Haihusiki na viongozi waliochaguliwa. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa Katiba ni uchaguzi unaofanyika na Mkutano Mkuu, na inapotokea nafasi inajazwa na Baraza Kuu na ndicho kilichofanyika kwa Mhe. Chacha.

3. Nafasi hizo hazikufungwa kama zilivyo kwa viongozi wa kuteuliwa kama ilivyo kwa Ibara ya 6.3.5(b) .Hivyo Chacha bado ni Makamu Mwenyekiti kwa mujibu wa kifungu hicho.

4. Swala la kufanyika kwa uchaguzi ni swala tofauti. Natumaini tafsiri ya Katiba imeeleweka vizuri.

Mheshimiwa saafi sana kwa kutuweka sawa hapa maana sheria ni sheria na hapa naona iko wazi na very clear! Tupo ukurasa mmoja hapa.
 
Kaishiwa hoja huyu ameshaamua kuleta vioja. Anajifanya ananijua kuliko ninavyojijua mwenyewe. His intention was to blacken my name and character and he thought I would let it go just like that. Ukweli siku zote hujitenga. Anafikiri ataficha uzushi wake kwa kuibua madai mengine.
wewe uliyeshindwa chaguzi zote za CCM hadi ukahamia TLP ndio umeishiwa hoja. ungekuwa na hoja ungechaguliwa.
 
So far ninaamini maneno yote ya pande mbili ni hisia tu bado hatujapata ukweli, ninasema hivi kama haya maneno juu ni ya kweli, basi huko kuna tatizo kubwa na sio dogo na yanahitaji kutatuliwa sasa kwenye hii tatizo.

FMES

Soma kwanza katiba ya CHADEMA. Hilo suala la ajenda kutumwa siku 21 ni suala la Mkutano Mkuu wa CHADEMA. Halihusiani kabisa na Kamati Kuu ambacho ni kikao cha utendaji. Pamoja na kwamba halihusiani na hilo bado ajenda zilitumwa kabla. Pia kwa mujibu wa taratibu za vikao vya kiutendaji kupitisha ajenda ni ajenda ya kwanza baada ya ufunguzi. Na hivyo ndivyo ilivyo kwa vikao vya CHADEMA.

Ni kweli kumsimamisha Chacha Wangwe haikuwa ajenda. Ajenda ilikuwa ni Taarifa ya Wazee kuhusu Viashiria Vya Mgogoro vinavyotokana na Mwenendo, Matendo Na Maneno ya Makamu Mwenyekiti. Baada ya Taarifa hii ambayo imetokana na vikao vingi vya wazee ambavyo Chacha Wangwe naye alishiriki vikilenga kumrekebisha ndipo ilipoibuka hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.

Ukweli ni kuwa wazee hawakutaka hatua zozote za kinidhamu kuchukuliwa juu yake. Hii ni kwa sababu katika vikao naye alikiri mambo yote na kusema kwamba atarudi katika mstari, na alisema pia hana ugomvi na Mwenyekiti Mbowe. Akaombwa na Mzee Makani aandike ukurasa mmoja juu ya hiyo understanding and consesus ili iwe kama ushahidi. Kwa siku nyingi akakumbushwa hakuandika. Kwenye Kamati Kuu baada ya taarifa ya wazee kuwasilishwa akaikana taarifa ya wazee, akawakana wazee, akamwambia Mzee Mtei kuwa hata kama yeye ni mwasisi hawezi kumsikiliza kwa kuwa sasa yeye yuko juu. Akamtukana Profesa Baregu kwa kumwambia tu anyamaze kwa kuwa ni "Mhaya Tu"(alimnukana pia matusi ya nguoni siyataji), Mama Chiku Abwao alipoingilia kati naye akatukanwa. Mwenyekiti wa Madiwani wa CHADEMA Tanzania ambaye pia ni Naibu Meya Wa Halmashauri ya Kigoma Ujiji alipoingilia kati naye akasemwa Vibaya na Chacha.

Hapo ndipo ilipopendekezwa kwamba kwa hali ilivyofikia ajiuzulu mwenyewe kulinda heshima yake. Akagoma kujiuzulu! Akasema yeye tayari yuko juu atapambana naye. Hapo ndipo kikao kilipoamua kupiga kura ya kutokuwa na imani kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA 6.3.6(f) chini ya kipengele hicho kura ya kutokuwa na imani si lazima ije kama ajenda inayojitegemea; kura ya kutokuwa na imani inapigwa kutokana na hali ya mambo au jambo fulani linalowakosisha viongozi wengine imani juu ya kiongozi fulani.

Sasa imani kwa Chacha ilipotea kutokana na mtiririko wa mambo toka asubuhi ya tarehe 28 mpaka taarifa ya wazee ilipojadiliwa kwa masaa zaidi ya matano. Na kabla ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani alipewa wasaa wa kujieleza, na ndipo alipotukana. Na ndipo alipoamka na kutaka kumpiga Tundu Lissu kwenye kikao.

Kwa hiyo Katiba ilifuatwa. Kama anadhani haikufuatwa akate tu rufaa kwenye baraza kuu naaamini wajumbe wa CHADEMA watamsikiliza. Na kama haamini baraza kuu basi aende tu mahakamani, lakini kwa maelezo niliyoyasoma toka kwa Mbowe, Tundu Lissu, Dr Slaa, Profesa Baregu, Bob Makani katika Tanzania Daima, Mwananchi, Mtanzania na Mwanahalisi na jinsi ambavyo nimelinganisha na Katiba. Taratibu zote zilufuatwa. Anapoteza muda wake na anajaribu kutafuta uhalali tu ili hata baraza kuu likitupa rufani yake au mahakama ikitupa bado apate cha kusema.

Kuhusu uhalali wa wajumbe, muulizeni ni mjumbe gani huyo au wajumbe gani ambao hawakuwa halali au ni wepi halali hawakualikwa. Mbona hasemi? Ni mwongo tu huyo Chacha. Anatafuta mahali pa kutokea, kwa kifupi ana tapa tapa. Rostam na Ballile ni vyema wakambana vizuri zaidi aeleze ni wajumbe gani hao na kwa katiba ipi badala tu ya kutoa sweeping statement ya kutweza vikao halali vya CHADEMA na maamuzi yake.

Mnakumbuka jinsi nilivyobanana na Zitto kabwe hapa kuhusu matamshi yake juu ya uchumi kukua, sasa natangaza rasmi kwammba nguvu ile ile ya mjadala wake kati yangu na yeye wa hoja naihamishia kwenye kueleza udhaifu na uongo wa hoja za Chacha Wangwe, Ballile na wapambe wake. Asha wa mipasho nimerudi rasmi kwa heshima ya Chacha Wangwe

Asha
 
Kwenye Kamati Kuu baada ya taarifa ya wazee kuwasilishwa akaikana taarifa ya wazee, akawakana wazee, akamwambia Mzee Mtei kuwa hata kama yeye ni mwasisi hawezi kumsikiliza kwa kuwa sasa yeye yuko juu. Akamtukana Profesa Baregu kwa kumwambia tu anyamaze kwa kuwa ni "Mhaya Tu"(alimnukana pia matusi ya nguoni siyataji), Mama Chiku Abwao alipoingilia kati naye akatukanwa. Mwenyekiti wa Madiwani wa CHADEMA Tanzania ambaye pia ni Naibu Meya Wa Halmashauri ya Kigoma Ujiji alipoingilia kati naye akasemwa Vibaya na Chacha.

Sasa imani kwa Chacha ilipotea kutokana na mtiririko wa mambo toka asubuhi ya tarehe 28 mpaka taarifa ya wazee ilipojadiliwa kwa masaa zaidi ya matano. Na kabla ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani alipewa wasaa wa kujieleza, na ndipo alipotukana. Na ndipo alipoamka na kutaka kumpiga Tundu Lissu kwenye kikao.

... lakini kwa maelezo niliyoyasoma toka kwa Mbowe, Tundu Lissu, Dr Slaa, Profesa Baregu, Bob Makani katika Tanzania Daima, Mwananchi, Mtanzania na Mwanahalisi na jinsi ambavyo nimelinganisha na Katiba. Taratibu zote zilufuatwa.

Ulipoeleza hapo juu nilifikiri ulikuwepo.

Ni hivi, kama unataka kutu convince Chacha kaharibu huwezi kwenda kuchukua hadithi za yule anaesema Chacha kaharibu halafu ukategemea hiyo itakuwa balanced narration of what transpired.

Na hayo ma tabloid ya Tanzania Daima, Mwananchi, Mtanzania na Mwanahalisi, hao ni wadaku as far as I'm concerned, ambao sidhani hata walikuwepo kwenye mkutano.

Na magazeti mengine hayo si nasikia ni ya Mbowe. Sasa kweli unaweza kuyaleta kama kielelezo kweli?

Tundu Lissu alihadithia kilichotokea na hakusema alitaka kupigwa ila majibizano ya Wangwe.

Narration yako ni ya upande mmoja. To say the least.
 
Maswali mbali mbali yamejitokeza, na ningeshauri kila mwenye maswali ya ziada aongezee ili wahusika waweze kutujibu. Unaweza kulielekeza kwa upande unaopendelea kama unaona swali lako ndipo linakohitaji jibu;
  1. Kuna ushahidi gani wa Rostam Aziz kuhusishwa na huu mgogoro?
  2. Hiyo ripoti ya tume ya Mziray, kwa nini isiwekwe wazi na kujadiliwa ukweli au uongo wake?
  3. Je haingekuwa vema kwa Mh. Mbowe naye kufanya mahojiano na MMJJ (KLH) ili kujibu shutuma zilizoelekezwa kwake?
  4. Je hapangeweza kufikiwa utatuzi mwingine wowote badala ulio bora na kukinusuru chama kisigawanyike badala ya kumfukuza Mh. Wangwe hasa tukitilia maanani kuwa uchaguzi uko karibu?
  5. Ni kwa nini Mziray kama amepika ripoti kwa kutumia pesa ya Rostam Aziz, asichukuliwe hatua za kinidhamu kama alivyofanyiwa Mh. Wangwe?
  6. Kama malalamiko ya Mh. Wangwe juu ya wabunge wa kuteuliwa, madereva na wakurugenzi, je haingekuwa vema kurekebisha hizo nafasi badala ya kumfukuza Wangwe na kuanzisha mgogoro?
  7. Kwenye mahojiano na KLH, Wangwe alipendekeza kuwa angalau TShs. 100,000 (jumla TShs. 14 million approx.), zitengwe kwa ajili ya kila wilaya, je hili sio wazo zuri ili kuwa na matawi yatakayovuta wanachama kila pande ya nchi badala ya CHADEMA kuwa chama cha mikoa fulani tu?
  8. Kwa chama chenye mapato madogo kama CHADEMA, je sio wazo zuri kuachana na Helcopter ambayo ni ya gharama kubwa sana na kutumia njia nyingine kuhamasisha wananchi?
Haya ni yangu machache na ninategemea kusikia mengi zaidi toka kwa wahusika.

1. Ushahidi wa Rostam Aziz na Kaborou kuhusika: si lazima hapa utolewe hapa Jambo Forum, Kubwa Jinga umezidi kuwa kuwadi wa watu hawa! Michango yako humu inakuanika ulivyo. Dr Slaa na wenzako, msianike ushahidi wowote hapa. Huyu jamaa anataka kujua mikakati yenu awapekelekee Rostam na Balille. Ushahidi endeleeni kuutoa kwenye vikao vyenu vya chama. Na kama wao wanataka kuuona si waende mahakamani kwa kuchafulia majina yao ushahidi utatolewa huko? Rostam, Kaborou na Chacha- nendeni mahakamani kwa kusingiziwa!

2. Ripoti ya Mziray imeshawekwa wazi kwenye gazeti la Fisadi Rostam la Rai vipande kwa vipande toka wiki iliyopita. Na imechapwa kwa ukamilifu wake kwenye gazeti dada la mafisadi la Majira. Wewe hujaisoma? Kama bado wasiliana na rafiki yako Bwana Balille akupe nakala? Dr Slaa hawezi kuitoa hapa ripoti ambayo imekataliwa na kamati ya Chama as no document, atakuwa ameihalalisha kuwa ni nyaraka ya chama. Weka wewe

3. Mbowe hawezi kufanya mahojiano na MMJJ kujibu tuhuma zisizokuwepo. Tundu Lissu ameshaeleza bayana kwanini Wangwe amesimamishwa. Kama una tuhuma mpya zaidi ya zile ambazo Dr Slaa, Tundu Lissu, Zitto nk wameshazitolea ufafanuzi hapa ziweke. Kama huna, nyamaza!

4. Hio ndio njia bora zaidi. Chacha Wangwe hajafukuzwa, amesimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu na kukiuka katiba, kanuni, maadili na itifaki ya CHADEMA. CHADEMA sio kama CCM, Chenge ametuhumiwa na ufisadi lakini mpaka sasa ni kinara wa Kamati ya Maadili ya Chama Cha Mafisadi, mnasubiri mpaka uchaguzi wa chama chenu ndio mchukue hatua? CHADEMA ni tit for tat nidhamu mbele! Uchaguzi na hatua za kinidhamu ni mambo mawili tofauti

5. Mziray amechukuliwa hatua kwa ripoti yake kukataliwa na wajumbe wamemkaripia. Tatizo la Chacha ni tofauti na la Mziray, yeye amepotosha taarifa ndani ya vikao vya chama. Chacha amepeleka siri za chama kwa kaborou na rostam, amekosa uwajibikaji wa pamoja, amekiuka maamuzi ya chama, amechochea makundi, ameleta matusi na ugomvi vikaoni, amepingana na maamuzi halali ya chama nk na hivyo Kamati Kuu ya Chama kukosa imani naye kama makamu mwenyekiti. Haya ni Makosa tofauti kabisa na adhabu ni tofauti kabisa! Sasa kumchukulia hatua mkosaji sio kuanzisha mgogoro, kuendelea kulea makosa ni kuweka msingi wa migogoro mibaya zaidi kwa taasisi. CCM imezoea kulindana ndio maana CHADEMA kuchukua hatua imeonekana ni mgogoro.

6. Kurekebisha nafasi za wakurugenzi, madereva na wabunge wa viti maalimu namna gani? Kama ni wakurugenzi, toka 2005 mpaka 2006 mwishoni CHADEMA ilikuwa na mkurugenzi mchagga mmoja tu kati ya 8, wasukuma wakiwa wawili Mnyika na Tumbo. Mwaka 2007, CHADEMA ikaongeza mkurugenzi mmoja mhitimu wa shahada ya Ualimu UDSM na Waziri Mkuu wa zamani wa wanafunzi bwana John Mrema kuwa Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri, hapo hapo ikamuomba Mbunge Suzan Lyimo ambaye alikuwepo bungeni Tayari kuwa Mkurugenzi wa Kurugenzi Mpya ya rasilimali kwa gharama zake mwenyewe. Hapo ndipo walipoongezeka wachagga kuwa watatu kati ya Tisa, wakati huo huo ikamteua Mama Kaihula toka Mbeya kuwa mkurugenzi wa Wanawake. Sasa ukabila unakujaje hapo? Madai yanayotolewa na Chacha kuwa kuna wakurugenzi wanne wachagga ni ya uongo kabisa. Madai ya Chacha na Mziray kuwa Mnyika ni Mchagga ndiyo yanatumika kuhalalisha uwongo huo. Sasa kama Chacha Si mkabila ni nini? Kuhusu Viti Maaliumu, uteuzi ulifanyika 2005;unataka CHADEMA iwakate vichwa wale wabunge wa viti maalum wachagga watatu kati ya sita walioteuliwa kwa sifa na vigezo ambavyo vimeshaelezwa humu? Tayari CHADEMA imeshaweka utaratibu mbadala wa kupata wabunge wa viti maalimu 2010 kupitia uchaguzi katika Baraza la Wanawake wa CHADEMA, suala hili lilishapatiwa ufumbuzi na Mkutano Mkuu 13 Agosti, 2006. Madai ya Chacha na Mziray kuwa wabunge watano kati ya Sita ni wachagga ni ya uwongo na uzushi wenye kupandikiza ukabila. Kuhusu Madereva, imeelezwa wazi kwa majina kati ya madereva watano, mchagga ni mmoja tu. Na hakuna aliyeajiriwa kwa uchagga wake. Watu wa kusini na pwani, ni wengi zaidi kwa nini huzungumzii ukabila wa kuwapendelea watu wa nachingwea?. Hata dereva wa sita, aliyepatiwa Chacha wangwe kama Makamu mwenyekiti naye ametolewa Kigoma!. Hivyo Madai ya Chacha na Mziray yanayoratibiwa na Ballile na Kaborou kwa ufadhili wa Rostam kwamba madereva wote ni wachagga ni ya uwongo wa kuchochea ukabila. Kuhusu uteuzi mbona Mwenyekiti Mbowe alipoteua wahaya wawili Profesa Baregu na Balozi Ngaiza Kuwa wajumbe wa Kamati Kuu hamkusema kuwa ni ukabila? Shame on you kwa kuleta mgawanyiko katika taifa letu!

7. Kuhusu Ruzuku. Imedhirika wazi kuwa Madai ya Chacha kuwa ruzuku haipelekwi Wilayani na Mikoani ni ya uwongo kabisa baada ya wilaya yake ya Tarime kusema wazi wao wanapokea laki nne kila mwezi, nini laki moja. Kigoma wao Mzee kasisiko mwenyekiti wa Mkoa amesema wilaya zake zote zinapokea ruzuku kati ya laki 1 mpaka 4 kutegemea na idadi ya madiwani na kura za wilaya katika matokeo ya 2005. Nao Temeke wameweka wazi kuwa wanapokea ruzuku. Chacha ni mtu asiyejua mambo yalivyo katika CHADEMA anasema milioni 14 zipelekwe ruzuku kila mwezi. Kwa Taarifa yake CHADEMA tayari inatumia kati ya milioni 13 mpaka 15 kila mwezi kupeleka ruzuku ya fedha taslimu kwenye wilaya mbalimbali nchini. Na kwamba wilaya zote zilizotimiza masharti yaliyowekwa na baraza kuu ya kufungua akaunti na kuwa na kamati ya utendaji zinapewa ruzuku toka mwaka 2007. Chama kimeweka utaratibu huu wa kuweka fedha kwenye akaunti badala ya kuwapa viongozi fedha binafsi mkononi. Pia chama kinatoa ruzuku ya vifaa ya uenezi bendera, katiba, vipaza sauti, gharama za magari au kufanya ziara kati ya milioni 5 mpaka 10 kwa mwezi. Hivyo, shilingi takribani milioni 25 kila mwezi zinatumika kama ruzuku kwa wilaya na mikoa. Chacha Wangwe alishiriki mkutano Mkuu wa chama Agosti 13 mwaka 2006 ambao ulipisha Mpango Mkakati wa CHADEMA 2006 mpaka 2010 ambapo ilikubaliwa kuwa Matumizi ya Makao Makuu ya Chama yawe asilimia 15 tu ya ruzuku ya Chama. Chacha Wangwe amekuwa mjumbe wa baraza kuu toka wakati huo mpaka leo na kila mwaka anakaa kwenye vikao kupitisha bajeti ya mwaka na taarifa ya fedha na anajua kabisa kwamba wakati wote ni asilimia 15 tu imetengwa kwa matumizi ya chama makao makuu na amekuwa akipitisha taarifa za fedha zikionyesha utekelezaji huo kwa kupiga kura. Hakuna siku amewahi kupiga kura ya hapana kati ya mwaka 2005 mpaka 2007 mwishoni. Kwa mara ya kwanza Chacha Wangwe amepiga kura ya hapana kwenye kikao cha Kamati Kuu Juni 28 mwaka 2008 pale Dodoma katika masuala mawili- moja kupinga kusimamishwa kwake na pili kuunga mkono taarifa ya Mziray! Nilikosea jana kidogo, taarifa ya Mziray iliungwa mkono na kwa kura tatu tu, ya Mwenyekiti wa Kamati Bwana Mziray, ya Mjumbe wa Kamati bwana Shilembi na ya Chacha Wangwe. na wajumbe 28 walipiga kura ya kuikataa taarifa hiyo kama ripoti ambayo haipo(total dismissal), kati ya wajumbe hao 28 ni pamoja na wakina Profesa Baregu, Balozi Ngaiza, Makani nk mpaka Katibu wa Kamati Mama Sophia Khatau toka Lindi naye aliikataa taarifa kuwa ni ya uzushi, majungu nk

8. Kuhusu helikopta, toa maoni yako lakini hili ni Azimio la Mkutano Mkuu Agosti 13, 2008 kuwa chama kitaendelea kutumia helikopta. Na iko kwenye mkakati wa miaka mitano wa chama. Na Baraza kuu la Chama mwaka 2007 kilifanya tathmini ya Ziara ya Zitto baada ya kusimamishwa bungeni na wabunge wa CCM ambayo ilimwezesha kuzunguka nchi nzima kueleza ukweli kuhusu Buzwagi na likabaini ni njia nzuri na ya haraka na ya nafuu na kikaazimia kuendelea kutumia helikopta. Hii ilikuwa ni Disemba 2007, juzi juzi tu. Mwaka 2006 Chacha alipiga kura ya kuunga mkono matumizi ya Helikopta, Mwaka 2007 Disemba wakati wa kampeni za makamu mwenyekiti Chacha alipinga helikopta kama ajenda zake za kisiasa, lakini baada ya kubaina kwenye taarifa ya fedha urahisi wa ziara ya helikopya na mafanikio yake katika kumzungusha Zitto kura zilipopigwa, wajumbe wote walipiga kura ya ndio. Chacha akaogopa kupiga kura ya hapana maana kura zilikuwa za wazi, akanyamaza kimya, hakupiga kura. Kesho yake baada ya kuchaguliwa akizungumza na waandishi wa habari CHADEMA makao makuu, Chacha aliunga mkono matumizi ya helikopta!. Sasa likaja suala la Kiteto mwaka 2008. Chama hakikutaka kutumia helikopta, lakini Kimesera alipoumwa, Helikopta ikatumika kuwezesha kampeni zake siku za Mwisho. CCM nayo ikatumia helikopta iliyoletwa na Rostam kwa zaidi yaidi ya milioni 100 kwa siku zile chache. CHADEMA ilitumia chini ya milioni 20 kwa helikopta katika kipindi chote. Chacha akaja juu kupindukia kwenye kamati kuu kwa chama kutumia helikopta, masikini Chacha Wangwe alikuwa hajasoma taarifa ya fedha ya gharama za kampeni za Kiteto siku zote kuwa gharama za helikopta zilikuwa ni mchango binafsi wa Mwenyekiti Mbowe wala haikuwa ruzuku ya Chama. Alipoambiwa asome ripoti na kuona ukweli kuwa helikopta ilitumika Kiteto kama Mchango binafsi wa Bwana Mbowe kwenye kampeni akainamisha kichwa chini kwa aibu. Sasa kama Mtu binafsi ameumua kuchangia helikopta kwenye kampeni, vipi ikataliwe wakati ruzuku ya chama imetumika kuwapekeka madiwani wa CHADEMA kwenye kampeni za nyumba kwa nyumba huko Kiteto?
Sasa ni vyema Chacha na Ballile wakikutana na Rostam kabla ya kuanza kulalamikia ya CHADEMA wamuulize kwanza, iweje helikopta yake aliyopeleka Kiteto imetumia takribani mara kumi ya gharama ya Helikopta ya CHADEMA wakati ya CHADEMA imetumika siku nyingi zaidi? Je, Rostam hajawafisadi CCM kupata sifa alizopewa na Komba kwenye NEC za kupeleka helikopta iliyochangia ushindi wa CCM Kiteto pamoja na kufadhili uwizi mwingine wa kura kupitia kadi za kura alizoununua Msekwa?

Asha
 
Ulipoeleza hapo juu nilifikiri ulikuwepo.

Ni hivi, kama unataka kutu convince Chacha kaharibu huwezi kwenda kuchukua hadithi za yule anaesema Chacha kaharibu halafu ukategemea hiyo itakuwa balanced narration of what transpired.

Na hayo ma tabloid ya Tanzania Daima, Mwananchi, Mtanzania na Mwanahalisi, hao ni wadaku as far as I'm concerned, ambao sidhani hata walikuwepo kwenye mkutano.

Na magazeti mengine hayo si nasikia ni ya Mbowe. Sasa kweli unaweza kuyaleta kama kielelezo kweli?

Tundu Lissu alihadithia kilichotokea na hakusema alitaka kupigwa ila majibizano ya Wangwe.

Narration yako ni ya upande mmoja. To say the least.

Nimetumia credible sources, kwako wewe kuhani Majira na Rai ndio credible zaidi?

gazeti la Mbowe ni moja tu hapo Tanzania Daima.

Mpigie simu Tundu Lissu umuulize kama Chacha hakutaka kumpiga. Tundu Lissu mwenyewe amekiri kwenye mahojiano na mwanahalisi kuwa Chacha alinyanyuka kutaka kumpiga. Kwani mwanakijiji alimuuliza hilo swali akakataa kujibu?

Profesa Baregu mwenyewe amekiri kwenye mahojiano yake na Mtanzania kuwa Chacha alitumia lugha chafu kikaoni. Nadhani amekwepa tu kusema kwamba alinitukana. Nilishatoa namba yake hapa, hebu muulizeni binafsi kama hakumtukana.

Mzee Makani ni mwanasheria naye alieleza ukweli. Mimi nilichofanya ni kuvuta kumbukumbu tu ya coverage ya magazeti mbalimbali na kuongezea details kwa kadiri ya maongezi yangu na baadhi ya wajumbe wa Kamati

Asha
 
Nimetumia credible sources, kwako wewe kuhani Majira na Rai ndio credible zaidi?

Mpigie simu Tundu Lissu umuulize

Profesa Baregu
mwenyewe amekiri kwenye mahojiano yake na Mtanzania kuwa Chacha alitumia lugha chafu kikaoni.

Mzee Makani ni mwanasheria naye alieleza ukweli...

Hao wote ndio alleged victims!

Juma anashitaki Baraka kampiga.

Kutafuta ukweli, unarudi kwa Juma kumuuliza "eti Juma ulipigwa na Baraka?"

Juma keshadai alipigwa huwezi kumuuliza yeye tena. Wala Baraka.

Muulize Roza kama alikuwepo. Third party!

(Unawajua Juma na Roza na Baraka?)
 
Kwa sisi tulio nje ya mifumo ya vyama vya kisiasa, inatusikitisha sana kuona mikoroganyo inapotokea ndani ya mojawapo ya vyama vinavyotegemewa kuleta demokrasia nchini. Hivi karibuni tumeona mvutano ndani ya chama cha CHADEMA kati ya upande unaomuunga mkono mwenyekiti wa chama hicho, Mh. Freeman Mbowe na upande mwingine akiwapo aliyekuwa makamu wake ambaye amevuliwa madaraka, Mh. Chacha Wangwe.

[IZE]

Wewe kubwa JINGA ndio usikitike na 'mgogoro' wa CHADEMA! Wewe kubwa JINGA ambaye toka uingie hapa JF wakati wote kazi yako ni kuiponda CHADEMA, wewe au mwingine.

Naipenda staili yako ya kubomoa, ya kung'ata kama hung'ati. Kujifanya unajali kumbe hujali. Huu mkakati wa kinafiki, ni staili hiyo hiyo inatumiwa na mwenzako KUHANI mkuu! Waumini wa hoja alizoleta FIKRA MBADALA, kumbe LOL!.

Unajifanya wajali kuwa hutaki mgogoro kumbe lengo lako ni kupandikiza hisia kwamba kuna mpasuko ndani ya CHADEMA ili watu wapoteze imani. Ili wengine wasio msimamo waanze kushabikia madai ya kizandiki ya Chacha Wangwe.

Hapa hakuna mgogoro wa CHADEMA wala hakuna mpasuko, sasa ukiwa na mtu mmoja upande mmoja na chama kwa upande wa pili, kuna mpasuko hapo au kuna hatua za kinidhamu zimechukuliwa?

Kwa taarifa yako unaoitwa upande wa Chacha ni kikundi cha watu watatu walioko kwenye orodha ya malipo ya Rostam Aziz na mashabiki wao 20 kati yao 17 wakiwa ni wanachama wa kawaida wa CHADEMA wafundi gereji pale Ndugumbi. Huu ndio unaitwa upande, kwa bahati mbaya Majira, Rai na Mtanzania wamepuliza hilo puto mpaka sasa watu wanadhani ni dude kubwa kweli. Subiri baraza kuu na mkutano mkuu ndio utaamini maneno yangu. Sasa hiki kikundi cha watu watatu kiko zidi ya maelfu ya wanaCHADEMA makini.

Hakuna mgogoro CHADEMA ni kiongozi mmoja asiye na nidhamu amechukuliwa hatua, sasa hata mtu aliyejipaka kinyesi bado anaweza kupita barabarani na akawa na washabiki, wengine wakimcheka na wengine wakichekelea. Ndicho kinachoendelea hivi sasa.

Asha
 
Hao wote ndio alleged victims!

Juma anashitaki Baraka kampiga.

Kutafuta ukweli, unarudi kwa Juma kumuuliza "eti Juma ulipigwa na Baraka?"

Juma keshadai alipigwa huwezi kumuuliza yeye tena. Wala Baraka.

Muulize Roza kama alikuwepo. Third party!

(Unawajua Juma na Roza na Baraka?)

Kama wote hao ni victims basi akaulizwe Rostam Aziz atakuwa na jibu mwafaka!

Maana naona Chacha Wangwe mtu mmoja anaaminiwa kuliko wajumbe watano wa kikao ambao walikuwepo na ni watu wa kuheshimia katika jamii! Basi waulizwe wakina Rostam Aziz na Kaborou.

Last choice, nikuunganisha na Naibu Meya wa Halmashuri ya Kigoma Bwana Shaban Mambo ambaye pia ni mwenyekiti wa Madiwani wote wa CHADEMA?

Au nikuunganishe na Mwenyekiti wa Ruvuma Bwana Fuime au Wa Iringa Dr Kapwani au wa Kigoma Bwana Kasisiko? Chagua yupi, maana hawa wote walikuwepo kikaoni na wanaweza kuthibitisha maneno yangu!

Ndio maana mi nilishasema siku nyingi hapa, wewe ni KUHANI wa MARUHANI, huupendi ukweli unaohusu CHADEMA. Unatoa hoja nzuri unapojadili ufisadi lakini linapokuja suala la CHADEMA basi ni kawaida yako kutoa hoja maruhani

Umekosea tena.

Hao madiwani wote ni wale wale. Upande uliomuondoa na kudai umetaka kupigwa. Ni Ngedele. Usiwapelekee kesi ya Nyani.

(Nimeongea figuratively hapo, maana hamchelewi ku twisti vitu nyinyi watu.)

Rostam na Kaborou hawahusiki hapa. Unatumia hoja-tasnifa, umepungukiwa na hoja murua? Unanichekesha.

Na kama unaamini CHADEMA wanapigana na ufisadi, huwezi kusema mtu anatoa hoja nzuri za kupambana na ufisadi halafu wakati huo huo mtu huyo huyo anakataa ukweli wa CHADEMA. Ni kujipinga. Njoo na hoja nyingine, hiyo pia mbovu.

Naomba sources za neutral parties.

Na sio wanaosema wametaka kupigwa, wala majarida ya waandishi, au watu wowote ambao hawakuwepo mkutanoni.

Kama vile Asha Abdallah.
 
Umenidhirihishia wewe ni Kuhani wa maruhani kweli kweli. Yani hujajibu hoja yangu hata moja umekazania vioja tu.

Neutral parties kwako wewe ni wakina nani kama wajumbe wote wa kamati huwataki?

Sasa kama kikao zaidi ya 2/3 kimepiga kura ya kutokuwa na imani basi huwezi kupata mtu neutral kwa mtazamo wako. Na kama hivyo ndivyo basi tuwahoji watu ambao hawakuwepo kwenye kikao uzungumzie yaliyotokea kwenye kikao ambacho hawakuwepo!

Ndio usivyotaka lakini ukweli ni kuwa ndivyo unavyotaka.

Ukweli upi huo wa CHADEMA ambao tumeukataa? Lakini uwongo tutaukataa uwe ni kuhusu CCM, CHADEMA au hata shetani.

Leo mmejidhihirisha hapa kuwa kuhani MKUU WA MARUHANI na kubwa JINGA lenu moja.

FMES chunga sana na watu hawa, karibu watakuingiza katika ufalme wao. Endelea kuwa mtu huru ndugu yangu wasiukuingize kutetea mikakati ya Rostam ya kujisafisha kwa gharama za kuichafua CHADEMA.

Kubwa JINGA ameleta tuhuma na maswali, mimi nimejibu zote- waambie yeye na Kuhani Mkuu wa maruhani wazipinge kwanza hoja zangu kwa hoja moja baada ya nyingine

Asha
 
Back
Top Bottom