CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Aliyepangwa kwenda msikitini leo kule Kinondoni ameshindwa ,ndio nilikuwa namaanisha hilo tuu kwani nilishasema kuwa mjadala wa Chacha sitauchangia tena.

Kauli yangu hapo isihusishwe na Mhe.Chacha wandugu...
 
Are we loosing the track? sasa naanza kufunguka macho kuwa baada ya mkakati A kufeli upo mkakati B , nami ngoja nijiandae kutengeneza Kombora C kwa ajili ya kulipua Mkakati B.

Nafuu na wewe umefunguka macho. Kuna watu wanaochezea akili mapenzi ya watu wengine chamani. Hawa ni wanaharakati maslahi wanaotakiwa kupatiwa hayo Makombora C.
 
Asha nakushukuru sana kwa posting yako kuhusu Katiba ya Chadema Ibara ya 6.3.5. Hata havyo naomba nirekebishe kidogo kuhusu 6.3.5(b). Nafasi inayokaimiwa kwa muda usiozidi miezi sita ni viongozi "walioteuliwa tu" tafsiri yako. Haihusiki na viongozi waliochaguliwa. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa Katiba ni uchaguzi unaofanyika na Mkutano Mkuu, na inapotokea nafasi inajazwa na Baraza Kuu na ndicho kilichofanyika kwa Mhe. Chacha. Nafasi hizo hazikufungwa kama zilivyo kwa viongozi wa kuteuliwa kama ilivyo kwa Ibara ya 6.3.5(b) .Hivyo Chacha bado ni Makamu Mwenyekiti kwa mujibu wa kifungu hicho. Swala la kufanyika kwa uchaguzi ni swala tofauti. Natumaini tafsiri ya Katiba imeeleweka vizuri.
 
kwa heshima na taadhima naomba uwaeleze hao kina kieleweke waache kutengeneza makombora (habari za uongo). Hii inashusha heshima ya chadema; wanatetea maslahi ya hicho chama na kuanza kuleta wasiwasi huenda habari wanazozileta humu mostly zimetengenezwa!
 
Unajua Kichunguu ile kamati kuu haikuitwa kumsimamisha Wangwe. <----->

Sasa haya ni mapyaa!!

Ilikuwa na ajenda zaidi ya kumi, suala la wangwe halikuwepo kabisa. <----->

Nazidi kuishiwa nguvu. Nani msema kweli sasa??

Huyu Wangwe alisababisha mwenyewe asimamishwe kwa mawenge yake, kama asingesimamishwa angetaka aendelee hata baada ya mwezi Julai, au angetaka mkutano wa Baraza Kuu uitishwe lakini haukuwepo kwenye ratiba. Nadhani afadhali CHADEMA haijafunika matatizo ya nidhamu ya chacha kwa kusema tu muda wake wa kukaimu umekwisha, imemchukulia hatua za kimaadili, imeonyesha mfano katika kuchukua hatua kuliko CCM wanaolindana.
Asha

Asha, nashindwa kukuelewa. Lipi ni lipi kati ya kuisha kipindi chake au kusimamishwa.
 
Asha nakushukuru sana kwa posting yako kuhusu Katiba ya Chadema Ibara ya 6.3.5. Hata havyo naomba nirekebishe kidogo kuhusu 6.3.5(b). Nafasi inayokaimiwa kwa muda usiozidi miezi sita ni viongozi "walioteuliwa tu" tafsiri yako. Haihusiki na viongozi waliochaguliwa. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa Katiba ni uchaguzi unaofanyika na Mkutano Mkuu, na inapotokea nafasi inajazwa na Baraza Kuu na ndicho kilichofanyika kwa Mhe. Chacha. Nafasi hizo hazikufungwa kama zilivyo kwa viongozi wa kuteuliwa kama ilivyo kwa Ibara ya 6.3.5(b) .Hivyo Chacha bado ni Makamu Mwenyekiti kwa mujibu wa kifungu hicho. Swala la kufanyika kwa uchaguzi ni swala tofauti. Natumaini tafsiri ya Katiba imeeleweka vizuri.

Hapo sasa imeeleweka vizuri sana.
 
kwa heshima na taadhima naomba uwaeleze hao kina kieleweke waache kutengeneza makombora (habari za uongo). Hii inashusha heshima ya chadema; wanatetea maslahi ya hicho chama na kuanza kuleta wasiwasi huenda habari wanazozileta humu mostly zimetengenezwa!

Mama kusema kuwa ninaleta habari za uongo ni kunishushia hadhi yangu , sijawahi kuweka habari za uongo hapa .

Pia hukunielewa ndio maana nilitoa clarification, na pia huyo unayemwambia kuwa awaambie waache atawapata wapi wakati hawajui?

The only thing to fear is fear by itselfu......By Mbowe JF posting.
 
habari za kutengeneza ni habari gani hizo?, unataka nikuletee ushahidi wa maandishi yako ambayo hujayajoa jana bali leo hii hii? spin kivingine useme kutengeneza ni kufanya log transformation.
 
Asha nakushukuru sana kwa posting yako kuhusu Katiba ya Chadema Ibara ya 6.3.5. Hata havyo naomba nirekebishe kidogo kuhusu 6.3.5(b). Nafasi inayokaimiwa kwa muda usiozidi miezi sita ni viongozi "walioteuliwa tu" tafsiri yako. Haihusiki na viongozi waliochaguliwa. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa Katiba ni uchaguzi unaofanyika na Mkutano Mkuu, na inapotokea nafasi inajazwa na Baraza Kuu na ndicho kilichofanyika kwa Mhe. Chacha. Nafasi hizo hazikufungwa kama zilivyo kwa viongozi wa kuteuliwa kama ilivyo kwa Ibara ya 6.3.5(b) .Hivyo Chacha bado ni Makamu Mwenyekiti kwa mujibu wa kifungu hicho. Swala la kufanyika kwa uchaguzi ni swala tofauti. Natumaini tafsiri ya Katiba imeeleweka vizuri.

Dr. Slaa,
Good to see you online. Ila hiyo sentence imenichanganya zaidi. Does it mean alivyosimamishwa Wangwe ni kinyume cha katiba ya CHADEMA? Una maana gani kusema kuwa kwa kulingana na hicho kifungu Chacha Wangwe bado ni Makamu wa M/kiti??
 
Nimekuelewa Dr Slaa. Nimeamini kwamba wewe unaijua katiba ya chama chetu. '

Kubwa Jinga

Manake ni kwamba bado ni makamu mwenyekiti. Ila ni Makamu Mwenyekiti aliyesimamishwa! Chacha hakufukuzwa.

Mod, nadhani huu mjadala ungefungwa sasa, mtoa hoja nimeridhika

Asha
 
Kubwajinga, nilikuwa nimetoa tafsiri sahihi ya Katiba ya Chadema, Toleo la 2004, Ibara ya 6.4.5(b). ambako Asha alikuwa anataka kujua kuwa kwa vile kifungu( b) kinazungumzia kuwa kukaimu kunatakiwa kusizidi miezi sita tangu kukaimu. Nilichofafanua ni kuwa tafsiri hiyo ya Asha haikuwa sahihi kwa kuwa si "blanket" bali kukuaimu kusikotakiwa kuzidi miezi sita ni kwa nafasi za "uongozi wa kuteuliwa" tu. Kwa msingi wa Katiba hiyo maana yake ni kuwa iwapo kusingelitokea yaliyotokea ndani ya kikao cha Kamati Kuu, yaani Kamati Kuu kupiga kura ya Kutokuwa na Imani, basi kikatiba Mhe. Chacha bado angelikuwa bado Makamu Mwenyekiti. Yaliyotokea kwenye Kamati Kuu si mjadala hapa, hivyo sitaki kulizungumzia hapa.
 
kwa heshima na taadhima naomba uwaeleze hao kina kieleweke waache kutengeneza makombora (habari za uongo). Hii inashusha heshima ya chadema; wanatetea maslahi ya hicho chama na kuanza kuleta wasiwasi huenda habari wanazozileta humu mostly zimetengenezwa!

Mama

Nimepitia michango yako mbalimbali na kubaini kwamba hoja zako ni propaganda mahususi za kulinda status quo. Hebu sema huo uwongo wa mpaka kieleweke uko wapi? Nao wengine ni wakina nani? Nimegundua wewe ni smooth operator unayejifanya neutral kumbe ni mweledi wa kupindisha hoja. I am marking all your words from now onwards. I had thought you are an ally in the war against ufisadi kumbe you are otherwise. I dont care which part are you or are you not but please simamia ukweli na usipindishe ukweli

Asha
 
Kubwajinga, nilikuwa nimetoa tafsiri sahihi ya Katiba ya Chadema, Toleo la 2004, Ibara ya 6.4.5(b). ambako Asha alikuwa anataka kujua kuwa kwa vile kifungu( b) kinazungumzia kuwa kukaimu kunatakiwa kusizidi miezi sita tangu kukaimu. Nilichofafanua ni kuwa tafsiri hiyo ya Asha haikuwa sahihi kwa kuwa si "blanket" bali kukuaimu kusikotakiwa kuzidi miezi sita ni kwa nafasi za "uongozi wa kuteuliwa" tu. Kwa msingi wa Katiba hiyo maana yake ni kuwa iwapo kusingelitokea yaliyotokea ndani ya kikao cha Kamati Kuu, yaani Kamati Kuu kupiga kura ya Kutokuwa na Imani, basi kikatiba Mhe. Chacha bado angelikuwa bado Makamu Mwenyekiti. Yaliyotokea kwenye Kamati Kuu si mjadala hapa, hivyo sitaki kulizungumzia hapa.

Dr. Slaa,
Tukiachana na yaliyotokea ndani ya Kamati Kuu;
  1. Je inayo madaraka kisheria kufikia uamuzi waliopitisha?
  2. Je Wangwe anao uwezo wa ku-appeal kusimamishwa kwake? What are the procedures, if any?
  3. Kuna adhabu gani kwa M/kiti kama ataonekana na yeye ana makosa?
  4. Unaweza kucomment nini juu ya wabunge wa kuteuliwa kwani tumeliongelea sana humu?
  5. Hebu tupe maoni yako juu ya huu mgogoro kama inawezekana bila kugusia yaliyotokea ndani ya Kamati Kuu?
 
Dr Slaa

Achana na huyu Kubwa Jinga anayeuliza maswali ambayo tayari ameshajibiwa hapa na Kitila, Zitto, Mnyika na Tundu Lissu- hata wewe katika nukuu zako za magazetini umeshayajibu.

Hebu nenda Bungeni huko wananachi wanakuhitaji zaidi kwenye mijadala juu ya ufisadi.

Kama anataka majibu aseme tu tutamjibu tena hapa

Asha,
Sidhani kama hivi ndio mijadala inavyoendeshwa. Dr. Slaa amekuja JF ili kujibu maswali yetu na kupata maoni yetu. Kama maswali yako yameshajibiwa, kwa nini asijibu na ya kwetu? Do you think you own him that you can tell him what to do? P'se be civil and you will be respected. These are serious issues that we are conversing.
 
Dr. Slaa,
Tukiachana na yaliyotokea ndani ya Kamati Kuu;
  1. Je inayo madaraka kisheria kufikia uamuzi waliopitisha?
  2. Je Wangwe anao uwezo wa ku-appeal kusimamishwa kwake? What are the procedures, if any?
  3. Kuna adhabu gani kwa M/kiti kama ataonekana na yeye ana makosa?
  4. Unaweza kucomment nini juu ya wabunge wa kuteuliwa kwani tumeliongelea sana humu?
  5. Hebu tupe maoni yako juu ya huu mgogoro kama inawezekana bila kugusia yaliyotokea ndani ya Kamati Kuu?

1. Kamati Kuu inayo hayo mamlaka kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA toleo la 2004 kifungu cha 6.3.6(f)Nanukuu- " Viongozi wa ngazi ya kitaifa waliochaguliwa na mkutano Mkuu wanaweza kusimamishwa uongozi endapo theluthu mbili ya wajumbe wa Kamati kuu watapiga kura ya siri ya kutokuwa na imani na kiongozi mhusika". Baraza Kuu ndilo litakuwa na uamuzi wa mwisho.

2. Anaouwezo wa kukata rufaa baraza kuu kwa kwa mujibu wa kipengele (d) na (e) za kufungu hicho, ndani ya siku kumi na nne. Sasa Chacha akikata rufaa baraza kuu lilishapangwa kufanyika Disemba 11 mwaka 2008.

3. Makosa Gani ya Mwenyekiti? Kwani yeye ndiye aliyemsimamisha? Chacha amesimamishwa na Kamati Kuu kwa kura 24 za kutokuwa na imani naye dhidi ya 7. Kwa hiyo si suala la Mbowe hapa ni suala la Kamati Kuu, na kamati kuu ilifikia uamuzi huu kwenye mjadala wa Taarifa ya Kamati ya Wazee na si hoja ya Mbowe au kiongozi yoyote binafsi!

4. Juu ya Wabunge wa Viti Maalum Dr Slaa alishazungumza kwa kina mwaka 2006 ikiwemo na vyombo vya habari na mjadala ulishafungwa na mkutano mkuu wa Agosti 13, 2006. Tadhali rejea maamuzi hayo kwa maelezo zaidi. Huu ni mjadala tofauti kabisa hapa, au fungue thread yako kwa ajili ya suala la viti maalum

5. Maoni ya Dr Slaa alishayotoa kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari Dodoma tarehe 29 June, na yalishajadiliwa sana hapa baada ya kuandikwa na vyombo vya habari. Sema kitu gani mahususi ambacho hujaelewa.

Kama umeridhika mwache mbunge wa wananchi aende bungeni kutumikia umma, mbona hujamuuliza maoni yake kuhusu orodha ya mafisadi alias list of shame?

Una lako jambo!

Kama ningetaka majibu yako ningekuuliza directly, lakini tumeshaona jinsi usivyoielewa katiba ya chama na umetetereka hapa na kuchanganya kila mtu. Ushabiki wako tunaukubali lakini intelect yako iko questionable ndio maana nilitaka kupata majibu ya mtu aliyebobea kwenye katiba ya chama.

Pia sidhani kama wewe unaweza kutoa maoni kwa niaba ya Dr. Slaa, kwani lolote utakalosema litakuwa ni la kwako binafsi na sio la mawazoni mwake.

Nashukuru kwa kuingilia kati mjadala lakini ningeomba umuachie Dr. Slaa kama anapenda kunijibu afanye hivyo. We are in JF where we dare to talk openly and no one has any monopoly over the other.
 
Una hamu ya kuzua mjadala mwingine nami? Now you go as far as questioning my intellect? Je, umeshindwa hoja wazua vioja. Hebu wewe mwenye intellect yachambue mapungufu ya majibu yangu niliyokupa kama hujapoteza muda wa Dr Slaa kujibu mambo ambayo ameshayajibu na yameshajibiwa sana tu humu!

Haya Kubwa Jinga

Utafsiri wako mbovu wa vifungu na arguments zako ndio zilizonifanya ni query uwezo wako kutoa majibu ya kuaminika. Kama tunaye mtaalamu kwa nini nihangaike na mtu ambaye majibu yake sitayaamini 100%. Maswali niliyouliza hayakuwa na ambiguity yoyote lakini nashindwa kuelewa kwa nini umeingilia kati a once smooth dialogue. I respect your opinion, but would have liked to hear Dr. Slaa answer my questions and not you.

Please, let this be the end of this exchange between us, as my interest is to use this opportunity and converse with Dr. Slaa. Have a good day.
 
RUZUKU, UKABILA WAIGAWA CHADEMA

CHADEMA ndicho chama pekee nchini kilichokuwa kinaonekana kutokuwa na migogoro, lakini hili la ruzuku na mengine yanaelekea kukigawa katika makundi mawili ya CHADEMA – MBOWE na CHADEMA – WANGWE.

Hali hii imejitokeza baada ya kutokea malalamiko ya wanachama wa CHADEMA kususu masuala kadhaa ya msingi. Masuala hayo yameibua mgawanyo uliozaa makundi hayo mawili na baadaye Mwenyekiti wa chama hicho FREEMAN MBOWE akatangaza kumsimamisha Makamu Mwenyekiti (CHACHA WANGWE).

Kwa tafakuri pana kila Mtanzania alitarajia kwamba kabla ya kumsimamisha Makamu Mwenyekiti, CHACHA WANGWE, Mwenyekiti wa chama hicho alitakiwa kujibu tuhuma moja baada ya ingine ili kujisafisha yeye mwenyewe pamoja na viongozi wengine wa juu wa CHADEMA.

Kimsingi,CHACHA WANGWE anamtuhumu MBOWE katika masuala yafuatavyo:-

Mosi, Kuna matumizi mabaya ya ruzuku (ufisadi wa ruzuku) ndani ya CHADEMA Makao Makuu. Hivyo, CHACHA WANGWE anamtaka Mwenyekiti FREEMON MBOWE atoe maelezo ya matumizi ya Ruzuku, ambayo ni fedha ya walipa kodi inayotolewa na serikali kwa vyama vyenye wabunge. Aidha WANGWE anamtaka MBOWE aonyeshe mapato na matumizi ya Ruzuku hiyo katika vikao vya chama au aunde kamati ya kuchunguza tuhuma hizo. Pia, WANGWE ana mashaka na hesabu zinazoonyesha mgawanyo wa matumizi ya ruzuku yanayopelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa kutoka chama cha CHADEMA.

Pili, CHACHA WANGWE hakubaliani na kitendo cha Mwenyekiti na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kuzuia ruzuku isifike mikoani. Anasema hali hii ina maana matawi ya chama yasifunguliwe na chama kisiwe na ofisi hali ambayo inadhoofisha chama. Vivyo hivyo, WANGWE hakubaliani na kitendo cha MBOWE kufuja fedha za chama kwa ziara za helkopta huku akiwaacha wagombea ubunge na udiwani wa chama chake hawana msaada wowote wa kifedha kutoka katika chama. Katika mazingira haya WANGWE anauliza nani anakihujumu chama kati ya MBOWE na WANGWE? Nani anadhoofisha CHADEMA?

Tatu, CHACHA WANGWE ana hoja kwamba MBOWE, anawajibika kuwaeleza watanzania, ni kwa vipi wabunge watano kati ya sita wa kuteuliwa (viti maalum) wote watoke mkoa wa Kilimanjaro ( MBOWE ni Mchaga wa Kilimanjaro). Ikumbukwe kwamba Tanzania bara ina mikoa 21 na Zanzibar mikoa 5. Kwa kawaida, idadi ya viti maalum inategemea idadi ya wabunge ambao chama kinapata katika uchaguzi mkuu, ambapo asilimia 90 ya viti vya ubunge zilizoleta viti maalum vya CHADEMA zilitoka kanda ya Ziwa. Hivyo, MBOWE kasahau kanda zilizosaidia CHADEMA ikipata viti maalum na kuvipeleka KILIMANJARO.

Nne, CHACHA WANGWE anamtaka MBOWE, aeleleze inakuwaje kati ya wakurugenzi nane wa Idara mbalimbali za CHADEMA wanne ni Wachaga wa Kilimanjaro?

Tano, WANGWE anamtaka MBOWE, aeleze umma wa watanzania inakuwaje Madereva wote wa Makao Makuu ya CHADEMA ni Wachaga kutoka Kilimanjaro?

Sita, WANGWE anataka MBOWE, ajibu tuhuma kwamba yeye mwenyewe, DR WILBROAD SLAA na PHILIMON NDESAMBULO wanajilipa fedha kwa ajili ya kurudisha gharama walizotumia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. WANGWE anauliza mbona wanachama wengine hawarudishiwi gharama hizo akiwemo yeye WANGWE? Je, huu siyo ufisadi? Je huku ni kutenda haki?

Saba, WANGWE anataka kujua ni kwa nini miaka minne iliyopita MBOWE alivunja tawi la CHADEMA mkoa wa DAR ES SALAAM na kubaki na CHADEMA Makao Makuu. Hatua hii imekifanya chama hicho kukosa viongozi na wawakilishi wa chama mkoa wa Dar ES salaam.

Nane, WANGWE anataka kujua kwa nini Wakurugenzi wote wa CHADEMA wameteuliwa na MBOWE badala ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya chama kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA. Aidha, Kwa Mujibu wa katiba ya CHADEMA kifungu 7.7.3 (vii), Katibu mkuu anatakiwa kuwajibika kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekti. Hata hivyo, DR SLAA ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA hakuwa akitoa ushirikiano kwa WANGWE hadi kufikia kumnyima ofisi alipoteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.

Tisa, Katika moja ya hatua za kumfukuza WANGWE katika Uongozi, Katibu Mkuu aliitisha kikao cha Kamati ya wazee wanne wa CHADEMA lakini kati yao wawili wakiwa wa kabila la Mwenyekiti . Wazee hao wa Kichaga ni EDWIN MTEI ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Wazee wa CHADEMA na PHILIMON NDESAMBULO. Hapo kulikuwa na mgongano wa kimaslahi (conflict of interest). Ikumbukwe kwamba, Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA Bw. EDWIN MTEI ni baba mzazi wa mke wa FREEMON MBOWE kwa maana kwamba MTEI ni mkwe wa MBOWE. Mke wa MBOWE anaitwa DR LILIAN EDWIN MTEI ( Hivi sasa anajulikana kwa jina la DR LILIAN FREEMON MBOWE) ni binti wa EDWIN MTEI.

Kumi, CHACHA WANGWE analalamika kwamba suala la kumfukuza liliibuka ghafla katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA wakati halikuwemo katika agenda. Inadaiwa kwamba MBOWE ndiye aliibua agenda hiyo. Kwa mujibu wa kanuni za CHADEMA, kama suala hilo lilitakiwa kuwa agenda ilitakiwa lijulishwe kwa wajumbe siku 21 kabla ya kikao ili wapate mawazo ya wanachama. Hata hivyo, liliibuka katika kikao bila mtuhumiwa CHACHA WANGWE kujiandaa. Aidha, katika kuhakikisha kuwa WANGWE anavuliwa madaraka yake kwenye kikao, baadhi ya viongozi waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho kwa mujibu wa katibu hawakupata mwaliko kwa sababu ilihofiwa kuwa wangekuwa upande wa WANGWE.

Kwa ufupi WANGWE anadai kwamba kuna ufisadi Makao Makuu ya CHADEMA. Kwamba MBOWE hajatoa maelezo kuhusiana na tuhuma hizo na badala yake anamtuhumu WANGWE kwamba anakigawa chama na kuamua kumsimamisha uongozi.

Katika uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti uliopita, CHACHA WANGWE hakuwa chaguo la Mwenyekiti MBOWE, lakini aliweza kushinda. Kutokana na kitendo cha CHACHA WANGWE kutangaza kwa mara ingine kugombea Uenyekiti wa CHADEMA katika uchaguzi wa Disemba 2008 amezidi kujenga maadui kutoka Makao Makuu ya chama hicho. Hofu ya MBOWE inatokana na ukweli kwamba, hivi sasa WANGWE anaungwa mkono na matawi mengi ya CHADEMA nchini kutokana na msiamamo wake wa kutenda haki na kusimamia ukweli daima.

Hivyo, MBOWE akamjengea zengwe kwamba, WANGWE anavujisha siri za chama lakini katika kikao cha Kamati Kuu hawakuweza kueleza siri ambazo WANGWE anadaiwa kuvujisha. Kwa sababu hiyo, WANGWE anadai kwamba hakuelezwa siri alizovujisha hatua ambayo inakidhi matakwa ya kisheria kwamba MBOWE amemhukumu WANGWE bila hatia. Hatua hii ina lengo la kukwaza ustawi wa demokrasia na utawala bora katika vyama vya siasa.

Katika hili la kuvujisha siri WANGWE anajitetea kwamba kama kuzungumza na wana CCM ni kosa basi mtu aliyetakiwa kuwajibika ni DR SLAA ambaye mke wake ni diwani wa kuchaguliwa wa CCM wakati mkewe CHACHA WANGWE ni mwanachama mwaminifu wa CHADEMA. Kitendo cha DR SLAA kuwa na mke mkereketwa wa CCM yamkini Nyaraka za siri za CHADEMA zinaweza kuangukia kirahisi kwa mkewe na hatimae CCM na pia wageni wa CHADEMA wanaofika nyumbani kwa DR SLAA ambako kuna tawi la CCM kwa maana ya mkewe DR SLAA ambaye anawajibika kuwakirimu wageni na hivyo kusikia mazungumzo yao. WANGWE anataka kujua ni nani kati yake na DR SLAA anaeweza kuvujisha siri za CHADEMA?

Aidha, imeonekana kwamba, kutokana na nafasi yake ya Ubunge WANGWE na wabunge wengine wa upinzani wanaweza kujipatia marafiki kutoka chama tawala CCM kama ambavyo Wabunge wa CCM wanaweza kuwa na marafiki kutoka vyama vya upinzani. Urafiki huu unaweza kuwa wa binafsi/kawaida kuliko mambo ya siasa kwa sababu ya uzalendo, hivyo tofauti ya itikadi siyo uadui bali ni suala la kusimamia ukweli kama ambavyo ZITTO KABWE alivyojumuika na wabunge wa CCM katika kamati ya madini ya Bomani.

Pia WANGWE anadai, kwamba kama kuzungumza na wana CCM ni kosa mbona MBOWE amewahi kuonekana akiwa katika mazungumzo na Rais JAKAYA KIKWETE hata kufikia kumkumbatia mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Halikadhalika MBOWE ameonekana katika mazungumzo na viongozi wengine wa CCM, vivyo hivyo wana CHADEMA wengine?

Kwa ujumla kashfa hizi zinakuja wakati bado baadhi ya Watanzania wanahoji uadilifu wa FREEMAN MBOWE. Kashfa ya kukopa na kushindwa kulipa deni la NSSF kwa muda stahiki ilitia mashaka ya uadilifu wa MBOWE kwa taifa lake. Hakika bila kujibu hoja nzito za WANGWE, Mwenyekiti MBOWE asitarajie kupata kura za Watanzania wenye fikra mbadala katika uchaguzi ujao ndani ya chama chake na asijisumbue kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Natoa mwito kwa MBOWE kuitisha mkutano wa waandishi wa Habari kujibu tuhuma moja baada ya nyingine. Vinginevyo MBOWE atakuwa ameingia katika kundi la Wenyeviti wa vyama vya siasa wanaoua demokrasia nchini.

Kwa upande mwingine, DR SLAA na KABWE ZITTO wamekuwa watu muhimu kwetu watanzania katika kutoa hoja zinazohusiana na ufisadi bungeni lakini inashangaza wameshindwa kudhibiti ufisadi wa MBOWE ndani ya CHADEMA na badala yake wamemwachia WANGWE pekee. Hakika watu hawa walitusaidia sana katika kuunda tume za kuchunguza Richmond na EPA inakuwaje kwa muda mrefu tangu Desemba 16, 2007 wanakalia ripoti ya Kamati ya Mziray iliyoundwa kuchunguza mambo yanayoweza kusababisha migogoro ndani ya CHADEMA? Kamati hiyo ilibaini ubaguzi wa kikabila na kidini katika CHADEMA lakini haikuwekwa wazi kwa Watanzania na wala haijafanyiwa kazi. Je tuwaelewe vipi viongozi hao wa CHADEMA? Ufisadi ni ule unaofanywa na viongozi wa serikali ya CCM tu? Je sio kweli kwamba Hisani siku zote inapasa kuanzia nyumbani???
 
Back
Top Bottom