Mtanzania
Unaweza kusema ni vipengele vipi vya katiba ya CHADEMA vimekiukwa na kwa hoja zipi?
Kumbe ndugu yangu uko critical kwenye hii ishu ya Wangwe kwa sababu ya preconceived position yako kuhusu Mbowe?
Sasa mvue Mbowe pembeni, kumbuka Dr Slaa ndiye SG wa CHADEMA na alibariki Wangwe kusimamishwa.
Hebu fanya uchambuzi mpya wa Wangwe Vs CHADEMA maana baada ya kusimamishwa kwake wewe ni moja kati ya waliokuwa mstari wa mbele kupindukia upande wa kumtetea Wangwe hapa na kuiponda CHADEMA.
Je, bado unadhani hoja zako zote ulizotoa toka tarehe 29 Juni mpaka leo kuhusu Chacha Wangwe hapa ziko kama ulivyozisema ama kuna hoja ungependa uzitolee hoja mbadala?
Maanake some arguments are usually built under certain premises, when such underlying facts change, we are free to change the arguments
Asha
Asha,
Afadhali mimi nimeweka wazi jinsi ninavyomwona Mbowe as a politician.
Katiba kuna hilo la kumpa mtu siku 21 ili aandae utetezi kabla ya kumtimua. Sijasoma popote CHADEMA wakielezea.
Kuridhia kwa Dr. Slaa chini ya uenyekiti wa Mbowe si ndio huo huo uongozi wa pamoja? Pale ilikuwa ama zake Mbowe au Wangwe. Wengi wakajipanga upande wa Mbowe.
CHADEMA chini ya Dr. Slaa itakuwa tofauti kabisa.
Kuhusu Mbowe na Wangwe, hoja zangu ziko pale pale. Makosa ambayo Wangwe anadaiwa kufanya ni ya kisiasa, yanahusu mwelekeo wa chama. Kwa sehemu kubwa anatofautiana na mwenyekiti wake. Dawa ya ugomvi kama huo ilikuwa kurudi kwenye mkutano mkuu, kujiuzulu na kuomba kura upya. Mkutano mkuu ndio ungeamua umrudishe nani. Hiyo ndio njia pekee ya kuwafanya waropokaji kufyata mkia.
Mimi si muumini wa kufukuzana, in fact nimeshaandika mara nyingi kwamba viongozi imara huwa hawafukuzi watu, ni viongozi weak ambao wanaona positions zao ziko matatani ndio huwa wanakimbilia hizo hatua za ajabu ajabu za kufukuzana.
Pia nikusahihishe, mimi simtetei Wangwe, ila napinga kitendo cha Mbowe na kamati yake kumsimamisha Wangwe. I hope unaelewa kwamba hivyo ni vitu viwili tofauti.
Pia napinga hizi juhudi za kumwanika Wangwe nje nje hapa JF na kwenye magazeti ili wananchi wote wamwone hafai. Hizo ni personal attacks ambazo naona haziisaidii CHADEMA kama chama. Kama mmemsimamisha na mmetoa tamko inatosha, vinginevyo nimeona hapa JF ni kama mnatumia muda mwingi mno kutaka sisi wana JF tukubaliane na nyie kwa lugha nyingi SPINS zinatumika hasa.