Inasikitisha sana kuona watu wanapigania vitu wasivyoweza kuvitekeleza wao wenyewe.
Demokrasia ni tamu unapoililia lakini saa nyingine ngumu kui-practice unapokuwa madarakani. Ngoja tuone Chama Cha Demokrasia kinavyoleta Demokrasia ndani yake kabla ya kupewa nchi.
Hakuana cha demokrasia kwa vyama vyetu wote njaa tu na kutaka madaraka kwa malengo yao na si ya wananchi.
Tanzania ili iendelee inahitaji kiongozi Dikteta mwenye Determinations Maana tatizo la Tz kua masikini si tatizo la kifedha wala malighafi.
Maana sasa kila mmoja anatetea anapoguswa na si kutetea wananchi.Mfano hawa polisi Mchezo mchafu wa upekuzi ndio kawaida yao ,yani kule vijijini waliko wananchi akitofautiana na polisi ,polisi anakuja usiku kwako anaficha kadumu kagongo ama bangi anaichomeka kwenye kwenye nyumba yako ya nyasi.Harafu anakuja usubuhi na gobore anajidai kukusachi na anaelekea palepale alipoiweka na kukutia nguvuni ,huu ni mchezo wao wa miaka.Wanasiasa wademokrasia wanatetea mahala ambapo tu maslahi yao yanaguswa.Kazi kweli kweli.