CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Kule bungeni hatupeleki sura, bali watendakazi ambao ndio jeuri ya chama chetu,” anasema. Dk Slaa anasema shutuma zilizotolewa na Wangwe, ambaye alikuwa anagombea umakamu mwenyekiti, ni maneno tu ya kumtaka apate nafasi hiyo.



Mh. Dr. Slaa,
Hebu tufahamishe kama ulivyonukuliwa hapo juu kuwa, wakati wa uchaguzi Wangwe wakati ule aliyosema yalikuwa si ya kweli ingawa yalimsaidia kushinda uchaguzi.

Sasa inakuwaje hayo hayo yaliyompa uongozi ndio yanatumiwa leo hii kumuondoa kwenye uongozi? Je kuna mabadiliko yoyote kutoka kwenye manunng'uniko yake? Hebu tupe maelezo ili tuweze kuelewa kuwa Wangwe hakuonewa maana hivi sasa tunasikia wito wa kumfukuza uanachama ukitokea mkoani kwako. Nitakutumia ujumbe huu kwenye PM yako pia.
 
MKAMAP...hata kama Chadema kikikumbwa na migogoro, its not a TICKET kuwa CCM it has done something worth...

Kuhusu Kuunganisha Mada naona Ndugu yangu Mkjj ameshikwa na Hamaki, may be aje kuomba radhi kwa hamaki hizo, politics haziendi na hamaki...CCM nao wamekuja nayo kuwa wale wanaodakia Hoja ya Zanzibar ni Nchi wana ajenda ya Siasa..

Admin,Moderators na Kweli mada zimekuwa nyingi mpaka unaona adha kusoma. Its true that kila mmoja anapenda mada aloianzisha iwezekupata audience. Mie nashauri Mods wawe care ili kundi la wanaohisi kuonewa lisiwepo, kila mmoja awe na Haki sawa na wengine.

Ushauri wangu ni kuwa kama mada imekosa Hits ndani ya wiki 2 iwe archived, na ikitokea relevant mada imekuja later, basi kuunganisha ni muhim.
 
Chuma, sijahamaki, na huo ni msimamo wangu.

Kuna tabia ya watu kutaka kupigiwa magoti pale ambapo wanachokitaka hakifanyiki. Kwa kutumia gia ya "uchadema" wanataka watu watetemeke wakilalamika na wagwaye wakiandika. Jamii hi ya ndugu zetu wakiona jamboo haliendi wanavyotaka wana haraka ya kubatiza watu "msemaji wa Chadema" au "mwanachama wa Chadema" licha ya kwamba hawajui affiliation ya mtu.

Nimeona orodha aliyoitoa KJ hapo juu kuhusu Wangwe na Chadema. Mada zote nane zinahusiana na jambo moja tu nalo ni kufungiwa kwa Wangwe na kimsingi siyo tu zinahusiana bali zimefungana kimantiki. Vinginevyo Wangwe akikohoa mtu ataanzisha mada "Wangwe azuiliwa Kukohoa", Chadema wakisema "Wangwe ni chanzo cha vurugu" basi mada yake nayo ianzishwe. Hii haina mantiki ni kutapanya mawazo kiasi kwamba mtu anayetaka kufuatilia mwanzo wa jambo inakuwa kasheshe kupata logical flow.

Kumekuwa na mada ya Kubenea, kumekuwa na mada za UVCCM ambazo nazo kutokana na mantiki yake nimeona zimeunganishwa. Lakini hatujasikia wana CCM wakilalamika au waandishi wa habari kulalamika. Isipokuwa suala la Wangwe na Chadema.

Lakini kibaya zaidi ni hii dalili na mazoea kuwa kwa vile kitu hakiendii mtu anavyotaka basi JF ni ya kidikteta, ni ya chadema n.k! Ndio maana nimetoa wazo tu la kwangu binafsi, kuwa kama kweli kuna huo uonevu njia nyingine ni kutafuta mahali pengine ambako kutakuwa hakuna utaratibu, kila kitu kinakwenda na hakuna mtu wa kufuatilia jambo wala nini. KUja kukandia JF halafu kukesha kuendelea kuwa humu ni kilele cha uzugaji. Kama kuna jambo mtu anaona haliendi sawa basi tuna njia za kutoleana malalamiko, ushauri, mawazo, maoni, ombi n.k lakini kuanza kukandia kwanza siyo uungwana.

Kubwa zaidi ni kuwa kumekuwa na tabia ya muda sasa ambayo imekuwa ikiwaturn watu off kwa sababu ya huko kumwaga mada alimradi mtu anajisikia kaweka mada ya kwanza. Zile mada zinazotoka kwenye magazeti (articles) ma MoDs sasa yaonekana wanafuatilia logical consistence yake ili kuona wapi zinaingia na kufaa. Vinginevyo imekuwa ni kushindana kuona nani kaweka habari ya kwanza hapa na baadaye mwingine asiyechukua muda kusoma naye anaweka mwingine na mwingne naye anakuja na habari hiyo hiyo kwa jina jingine.

Binafsi nawashukuru ma MoDs kwa kazi nzuri, kubwa wanayofanya ya kuhakikisha kuna sanity hapa na jinsi ambavyo wamekuwa prompt kuhakikisha kuwa mtiririko wa mada unaendelea kuwa vizuri. Hili liwe somo kwetu sote kuwa kabla hujaanzisha mada au kabla hujaleta habari angalia kama wenzio wamekutangulia au tayari ina mahali pake. Kwa kufanya hivyo tutapunguza hii haja ya ma MODs kuunganisha unganisha mada zinazohusiana na zinazohusu jambo moja kwani sisi wenyewe tutaona ulazima wa kufanya hivyo.
 
Na wewe pia, maana CCM ndio imekusomesha tena wenda hata allowance ilikua inakupa kwenda middle school,chuo kikuu napo wenda CCM imekulipia gharama zote hata huko Us wenda usikute ni CCM hiyo hiyo ilikupeleka.

ni kweli 80% CCM ndipo imetufikisha hapa tulipo,Maana wengi wetu CCM ndio imetuleta ulaya na marekani na baada ya sisi kuunganika na hawa jamaa waupe ndio tunang'aka kwa CCM iliyotupa mwanga Badala ya kuipa njia mbadala zaidi ya kushambuliana.

wangetamba!
 
MKAMAP...hata kama Chadema kikikumbwa na migogoro, its not a TICKET kuwa CCM it has done something worth...

Kuhusu Kuunganisha Mada naona Ndugu yangu Mkjj ameshikwa na Hamaki, may be aje kuomba radhi kwa hamaki hizo, politics haziendi na hamaki...CCM nao wamekuja nayo kuwa wale wanaodakia Hoja ya Zanzibar ni Nchi wana ajenda ya Siasa..

Admin,Moderators na Kweli mada zimekuwa nyingi mpaka unaona adha kusoma. Its true that kila mmoja anapenda mada aloianzisha iwezekupata audience. Mie nashauri Mods wawe care ili kundi la wanaohisi kuonewa lisiwepo, kila mmoja awe na Haki sawa na wengine.

Ushauri wangu ni kuwa kama mada imekosa Hits ndani ya wiki 2 iwe archived, na ikitokea relevant mada imekuja later, basi kuunganisha ni muhim.


Mkuu Chuma,
Inakuwa jambo la kufurahisha wengi wetu tunapoona makosa na kukosoa bila kujali ni nani aliyefanya hayo makosa. Congra mkuu Chuma. Nashukuru kwa kumuomba MMJJ kuomba msamaha.

Binafsi nilishangazwa sana na hatua ya Mod, pamoja na support ya MMJJ, kuunganizha thread within 3mins ingawa ilikuwa na hoja tofauti kabisa na ilikounganishiwa ingawa ni kweli zote zinahusiana na CHADEMA na Wangwe.

Kiburi kilichoonyeshwa na Mwanakijiji kwa kusema kuwa asiyekubaliana na uamuzi haruhusiwi kulalamika bali aondoke JF, ni jambo la kusikitisha hasa ukitilia maanani kuwa demokrasia ndio iliyotukusanya hapa JF. Nashukuru kwa kuliona hilo. Kwa kweli kiburi hiki cha Mwanakijiji, kama cha akina Mramba, Lowassa n.k., kinahitaji kukemewa kwa nguvu zote na wana JF.

Wazo lako ni zuri sana la kuwepo kwa utaratibu unaoeleweka wa kuunganisha threads ili kila mtu aone ametendewa haki. Kuwe na muda maalum kabla ya kuunganishwa unless thread iwe haivutii wachangiaji.

Hadi hivi sasa nasubiri majibu ya Mod na nategemea atatupa na mtazamo wake juu ya wazo ulilotoa.
 
Chuma, sijahamaki, na huo ni msimamo wangu.

Kuna tabia ya watu kutaka kupigiwa magoti pale ambapo wanachokitaka hakifanyiki. Kwa kutumia gia ya "uchadema" wanataka watu watetemeke wakilalamika na wagwaye wakiandika. Jamii hi ya ndugu zetu wakiona jamboo haliendi wanavyotaka wana haraka ya kubatiza watu "msemaji wa Chadema" au "mwanachama wa Chadema" licha ya kwamba hawajui affiliation ya mtu.

Mkuu MMJJ,
Hiki kiburi cha kubeza mawazo ya haki ya mwanaJF umekitoa wapi. Nani kaomba kupigiwa magoti? Hivi ni kosa kwa mtu kuomba thread yake iachwe huru ili ijadiliwe au huko ndio kupigiwa magoti?

Tunapoomba demokrasia tuwe tayari na sisi kuwa wanademokrasia kwa vitendo.
 
KJ.. ni kitendo chenu (wewe na Mkamap) kukandia JF halafu wakati huo kuona ni chombo ambacho mawazo yenu yanapokelewa kama ya wengine. Mnafikiri mkikandia watu na JF au kuihusisha na Chadema basi ndio ma MoD wapige magoti ili wasifikiriwe kuwa ni Chadema. Ni jambo moja kutoa hoja au kuuliza kitu lakini ni jambo jingine kabisa kuwafanya watu duni.

Kama vile hatupigi magoti kwa mafisadi kwa vile wanachukizwa na tunachokifanya hatutapiga magoti au kutetemeka kwa woga kwa kuhusisha na chama chochote kile na hasa Chadema.

Kama unakiona hicho ni kiburi, ndugu yangu nakikiri hadharani. Lakini haya mambo ya kuikandia JF (siyo kuikosoa hata chembe) ni mambo ambayo binafsi nayapinga na nitaendelea kuyapinga. Kama kuna mtu anachukizwa na hilo, aniwie radhi, lakini nisivyopiga magoti kwa mwanadamu yeyote, sitoanza kupiga goti hilo sasa.

A lot is at stake than trying to appease few people for the few of being labeled a Chadema "spokesperson".

That is my stand and I'm sticking to it. Kuna mahali mistari mingine haivukwi.
 
Mkuu MMJJ,
Hiki kiburi cha kubeza mawazo ya haki ya mwanaJF umekitoa wapi. Nani kaomba kupigiwa magoti? Hivi ni kosa kwa mtu kuomba thread yake iachwe huru ili ijadiliwe au huko ndio kupigiwa magoti?

Tunapoomba demokrasia tuwe tayari na sisi kuwa wanademokrasia kwa vitendo.

Huko ndiko kupigiwa magoti, kwanini mtu afiikiri thread yake ni kuu mno kiasi kwamba haiwezi kuunganishwa, kuhamishwa, au kuwa edited? Hicho ndicho kiburi ambacho binafsi nakikataa. Kama hakuna miti mitakatifu isiyokatwa Tanzania, na hakuna miti hiyo hapa JF.

JF itaendelea kusimama na kutetewa.
 
Binafsi nawashukuru ma MoDs kwa kazi nzuri, kubwa wanayofanya ya kuhakikisha kuna sanity hapa na jinsi ambavyo wamekuwa prompt kuhakikisha kuwa mtiririko wa mada unaendelea kuwa vizuri.


Mkuu MMJJ,
Ni kipi cha kushangilia katika kukandamiza nguvu ya hoja?? Post niliyoleta ilikuwa ni mpya kabisaa na sio ajabu wengi hawajaisoma kama hawakupitia magazeti yote?

Hapa naipost tena thread nzima ili wanaJF waamue wenyewe kama hii thread haikufaa kuchangiwa angalau kwa muda kabla ya kuunganishwa au ni insane kufanya hivyo kama kiburi cha MMJJ kilivyonena hapo juu.






Kwa wale tunaopigania demokrasia ya kweli nchini, je hii ni demokrasia kufukuzana uanachama pale unapodai haki yako tena kwa kufuata sheria?

Kama Wangwe akiamua kwenda mahakamani kutafuta haki yake, je hii ni sababu ya kutosha kwa yeye kufukuzwa kwenye chama alichokijenga mkoani Mara hadi kupata ubunge na uongozi wa serikali ya mitaa?

Hawa wanaotoa misemo kwa misingi ya upendeleo ni vema sana waangalie wanachosema kisiwe ni kinyume kabisa na kile wanachohubiri kuwa wanakipigania. Demokrasia sio upande mmoja ni kila mahali na kwenye kila chama.



Wangwe atishiwa kutimuliwa Chadema

2008-07-19 08:58:41
Na Cynthia Mwilolezi, PST, Arusha




Viongozi wa Chadema Wilaya za Arusha Mjini na Vijijini wamesema iwapo Chacha Wangwe ataendelea na vitisho vya kupeleka chama mahakamani, achukuliwe hatua kali ikiwa pamoja na kuachishwa nafasi zote za uongozi alizonazo ndani ya chama.


Walisema sambamba na hilo, hata kumsimamisha uanachama, kwani heri kuwa na wanachama na hata wabunge wachache wanaokitumikia vyema chama na taifa, kuliko kuwa na wanachama wengi aina ya Bw. Wangwe wanaotaka kukisambaratisha chama na kuvuruga jitihada za kuwaondolea wananchi umaskini.


Hayo yamesemwa jana na Katibu mwenezi CHADEMA, wilaya ya Arusha, Bw. Samson Mwigamba na Mwenyekiti Baraza la Vijana CHADEMA, Wilaya ya Arusha, Bw. Zulfikri Mjema, wakati wakiongea na waandishi wa habari ofisini kwao.


Walisema kuwa wanamtaka Bw. Wangwe atulie bungeni ili kuwawakilisha wananchi wake wa jimbo la Tarime na Watanzania kwa ujumla tofauti na ilivyoripotiwa katika vyombo vya habari kwamba tokea asimamishwe umakamu mwenyekiti haonekani bungeni.


``Hii siyo sifa ya wabunge wa CHADEMA na asitumie muda wa kuwawakilisha wananchi kuzunguuka huku na kule na kufanya vita dhidi ya chama, kwani hicho ndicho alichochaguliwa na wananchi wa Tarime afanye hivyo,`` walisema.


Walisema anachokifanya Bw. Wangwe ni sawa na mtu ambaye wenzake wakiwa vitani, dhidi ya adui yeye anarudi nyumbani kwake kuanza kupigana na watu wa nyumbani mwake na kutangaza vita kati ya wanafamilia yake,`` walisema viongozi hao.


Walisema kuwa wanamshangaa kumwona Bw. Wangwe akihangaika kukipaka matope chama chao kwa kupitia vyombo vya habari, wakati wenzake wakiwa katika vita dhidi ya ufisadi, na wananchi wake wa Tarime wakiendelea kuuana kwa vita ya kugombania ardhi na wengine wakitaabika kwa kufukuzwa toka katika maeneo yao ili kuwapisha wawekezaji wa machimbo ya madini.


Viongozi hao walisema kuwa kama Bw. Wangwe aliona kuwa kamati kuu haikumtendea haki alikuwa na nafasi ya kukata rufaa kwenye baraza kuu, ambalo hujumlisha wajumbe wengi zaidi, likijumuisha hata wenyeviti wa wilaya kwa mujibu wa katiba hiyo, hapo angepata nafasi ya kujieleza vizuri na baraza kuu kuangalia kama kweli ameonewa na kamati kuu au la.
SOURCE: Nipashe
 
KJ.. ni kitendo chenu (wewe na Mkamap) kukandia JF halafu wakati huo kuona ni chombo ambacho mawazo yenu yanapokelewa kama ya wengine. Mnafikiri mkikandia watu na JF au kuihusisha na Chadema basi ndio ma MoD wapige magoti ili wasifikiriwe kuwa ni Chadema. Ni jambo moja kutoa hoja au kuuliza kitu lakini ni jambo jingine kabisa kuwafanya watu duni.



MMJJ,
Hebu onyesha wapi nilipokandia JF zaidi ya kuomba Mod afanye kazi yake?? Nafikiri kuna kiburi kinachoanza toka kwa baadhi ya members wanaojiona ni muhimu zaidi na hata Mods.

Kama kuna anayependa kuiunganisha JF na CHADEMA ana haki as long as anatoa ushahidi au sababu. Lakini hiki kiburi cha kuficha mawazo ya watu na kuwatishia kuwa waondoke JF ni jambo la kifisadi na linahitaji kupigwa vita.
 
Huko ndiko kupigiwa magoti, kwanini mtu afiikiri thread yake ni kuu mno kiasi kwamba haiwezi kuunganishwa, kuhamishwa, au kuwa edited? Hicho ndicho kiburi ambacho binafsi nakikataa. Kama hakuna miti mitakatifu isiyokatwa Tanzania, na hakuna miti hiyo hapa JF.

JF itaendelea kusimama na kutetewa.

Nani aliyesema kuwa thread yake haiwezi kuunganishwa?? Kinachopigiwa kelele hapa ni kwa thread kuunganishwa kabla hata haijajadiliwa (imechukua 30mins to be specific tokea kuanzishwa mpaka kuunganishwa). Kwanini wakati hapakuwepo thread nyingine yenye hicho kichwa cha habari na hata hilo somo for more than a week??.

Kwa hiyo kwa msemo wako ni kuwa Mod anapoombwa kutoa maelezo ndio kumpigia mtu magoti? Kazi za Mods ni zipi? Kwa nini angalau hakujibu maombi yangu?
 
KJ.. you'll be just fine...

I think MMJJ, you can do better than that.

Now that you have failed to show how I insulted (kukandia) JF, why not join my quest to persuade Mods to bring back the thread, so that we can let wanaJF cut it into pieces?
 
BACK TO TRACK.....! "CHADEMA WAMSIMAMISHA CHACHA WANGWE"
is it worth?
 
I think MMJJ, you can do better than that.

Now that you have failed to show how I insulted (kukandia) JF, why not join my quest to persuade Mods to bring back the thread, so that we can let wanaJF cut it into pieces?

mzee mada inaendelea hapa ilipo na nadhani, jifunze kukubali kuwa wakati mwingine maisha hayaendi tunavyotaka. Usijisikie vibaya. NImeisoma hiyo post uliyoiweka na binafsi naamini hapa ndipo mahala pake. Tuendelee kujadili hapa hapa.
 
HII ITAKUWA KWELI , KUWA UCHAGUZI WA MAKAMU MWENYEKITI NDIYO UNAYO ITIKISA CHADEMA....!
PEPSI (chadema) DARE FOR MORE (migogoro)....!
 
I think MMJJ, you can do better than that.

Now that you have failed to show how I insulted (kukandia) JF, why not join my quest to persuade Mods to bring back the thread, so that we can let wanaJF cut it into pieces?


K.J.

You are shouting - hii hasa ndiyo hoja ya nguvu - please cool down. I do concur with MKJJ. Thanx.
 
MODS

poleni na kazi na asanteni kwa kusikiliza maoni ya wanachama. Naombeni muunganishe hii pia na ile nyingine ambayo mmeungasha zingine. I mean, ile ya CHADEMA wamsimamisha Wangwe

Asha
 
I think MMJJ, you can do better than that.

Now that you have failed to show how I insulted (kukandia) JF, why not join my quest to persuade Mods to bring back the thread, so that we can let wanaJF cut it into pieces?


Stop pricking and picking on Mwanakijiji

Hebu kumbuka mwenyewe maneno yako Kubwa JINGA


Asha
 
Back
Top Bottom