CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Mbona CCM wamemfukuza uanachama yule mwenyekiti wa kata ya Manzese?

Mbona CCM wamemchukulia hatua naibu meya Yakob?

Kubwa Jinga tatizo lako wewe ni kuwa wanachama na viongozi wa CHADEMA wakilalamika na kutaka hatua zichukuliwe unakuja hapa haraka haraka na kuja kusema kuwa huko hakuna demokrasia.

Mbona hili nalo husemi kuwa kufukuzana ni kubaya?

Kubwa Jinga acha unafiki wako, kuwa principal ambayo itakuwa inaongoza msimamo pamoja na fikra zako la sivyo hutakuwa na tofauti na MAFISADI kweani hawa ndio ambao hawana principal za maisha yao.

Kujibizana na hawa ni sawa na kusukuma mlima kwani hawaoni upande wa pili.
 
Mkamap: Ni vigumu sana kuyaangalia haya mambo objectively kama hadi leo unaamini kwamba CCM ndiyo iliyokusomesha. Ok, let's assume this ludicrous claim is true, so what- Wanastahiki fadhila??!

Sikujua kwamba propaganda za CCM ziliwaingia wengi namna hii. Aibu!!
 
Mkamap: Ni vigumu sana kuyaangalia haya mambo objectively kama hadi leo unaamini kwamba CCM ndiyo iliyokusomesha. Ok, let's assume this ludicrous claim is true, so what- Wanastahiki fadhila??!

Sikujua kwamba propaganda za CCM ziliwaingia wengi namna hii. Aibu!!

Tukisahau tunakotoka, itakuwa vigumu sana kufika tunakotaka kwenda.
 
NAUMIA KWA SABABU WACHAGA WANAPIGWA VIPYA VITA
Siku hizi
1 Wachaga hawastahili kushika nyazifa zozote, wakishika tu UKABILA
2 Nasikia kuna mkakati madhubuti hata ya kuhakikisha namba ya wachaga wanaojiunga shule inapungua kwa kuweka PASS MARK kubwa kwa shule za KASKAZINI, kwa hiyo kama wewe unaitwa MASAWE utahijaka kupata maksi za juu ili uendelee na Masomo, mfano Mr X (kutoka lindi (120%), mr Y (kutoka Moshi 150%) Mr X anachaguliwa lengo ni kuwianisha idadi ya makabila yaliyosoma (Huu ndio ukabila tena mkubwa sana.
3 Chacha anawabagua wachaga CHADEMA, anataka KIGEZO cha UKABILA kiwe ni sifa ya mtu kuchaguliwa UONGOZI huu ni Ukabila na chuku ya Chacha dhidi ya wachaga
4 Yaani mtu aogope kugombea nafasi CHADEMA kisa mwenyekiti ni Mchaga hizi fikra finyu sana kuziunga mkono.
5 Hii chuki dhidi ya haka kabila ni Lazima iishe
 
Na wewe pia, maana CCM ndio imekusomesha tena wenda hata allowance ilikua inakupa kwenda middle school,chuo kikuu napo wenda CCM imekulipia gharama zote hata huko Us wenda usikute ni CCM hiyo hiyo ilikupeleka.

ni kweli 80% CCM ndipo imetufikisha hapa tulipo,Maana wengi wetu CCM ndio imetuleta ulaya na marekani na baada ya sisi kuunganika na hawa jamaa waupe ndio tunang'aka kwa CCM iliyotupa mwanga Badala ya kuipa njia mbadala zaidi ya kushambuliana.

Samuel Chitalilo would have said exactly the same, with confidence!
 
NAUMIA KWA SABABU WACHAGA WANAPIGWA VIPYA VITA
Siku hizi
1 Wachaga hawastahili kushika nyazifa zozote, wakishika tu UKABILA
2 Nasikia kuna mkakati madhubuti hata ya kuhakikisha namba ya wachaga wanaojiunga shule inapungua kwa kuweka PASS MARK kubwa kwa shule za KASKAZINI, kwa hiyo kama wewe unaitwa MASAWE utahijaka kupata maksi za juu ili uendelee na Masomo, mfano Mr X (kutoka lindi (120%), mr Y (kutoka Moshi 150%) Mr X anachaguliwa lengo ni kuwianisha idadi ya makabila yaliyosoma (Huu ndio ukabila tena mkubwa sana.
3 Chacha anawabagua wachaga CHADEMA, anataka KIGEZO cha UKABILA kiwe ni sifa ya mtu kuchaguliwa UONGOZI huu ni Ukabila na chuku ya Chacha dhidi ya wachaga
4 Yaani mtu aogope kugombea nafasi CHADEMA kisa mwenyekiti ni Mchaga hizi fikra finyu sana kuziunga mkono.
5 Hii chuki dhidi ya haka kabila ni Lazima iishe

Huu sasa ni zaidi ya ukabila na ni uongo wa hali ya juu! Stop this baseless lamentations and concentrate on the issues!
 
Mkamap: Ni vigumu sana kuyaangalia haya mambo objectively kama hadi leo unaamini kwamba CCM ndiyo iliyokusomesha. Ok, let's assume this ludicrous claim is true, so what- Wanastahiki fadhila??!

Sikujua kwamba propaganda za CCM ziliwaingia wengi namna hii. Aibu!!

Kitila
Mimi napenda sana kujadili na wewe maana wenda pamoja kua una chama lakini unayaangalia mambo si kiushabiki wa chama bali kiu halisia wa mambo.

Kitila lazima tukubaliane chama kinachoongoza ndicho serikali ya kwamba serikali inafanya mambo ya ilani ya chama kwa namna nyingine serikali ni chama tawala na chama tawala ndio serikali.

Ktk upande wa elimu sera ya serikali kweli ni nzuri japo inaangushwa na baadhi ya watu wenye tamaa na mafisadi ,Tz kwa afrika ni nchi ya pili ama ya tatu kutoka mwisho kwa umasikini lakini serikali yake bado inawapa udhamini wanafunzi wa elimu ya juu nje na ndani ya nchi.

Katafute nchi nyingine afrika inayofanya hivyo na kama zipo ni chache mno wenda zisidi hata tatu.

Bado naamini umakini wa serikali ktk elimu ya juu pamoja na serikali kua masikini ya mwisho ndiyo bado unaona UDSM bado inang'ang'ania Top ten ,nakubali pia mchango wa wahadhili lakini mkono wa serikali ndio msingi.

Mwl Kitila pamoja na maneno mengi na elimu yetu kudidimia lakini bado naamini elimu yetu ipo juu kwa afrika ,Maana nimekutana na watu karibu elfu tatu hivi kutoka nchi mbalimbali za afrika wakati tunajifunza language school hapa Natambua ubora wa elimu ya bongo pamoja na serikali kua masikini.

Nisiandike mengi sana lakini kwa kawaida utajiri wa nchi unaenda rank za vyuo swali kwako kwanini TZ ni masikini lakini chuo chake UDSM kimeng'ang'ania kuifanya TZ kwa ubora wa nchi kua ya tatu??

Unaposema CCM na serikali yake haikutusomesha wewe na mimi unamaanisha nini??
 
Kitila
Mimi napenda sana kujadili na wewe maana wenda pamoja kua una chama lakini unayaangalia mambo si kiushabiki wa chama bali kiu halisia wa mambo.

Kitila lazima tukubaliane chama kinachoongoza ndicho serikali ya kwamba serikali inafanya mambo ya ilani ya chama kwa namna nyingine serikali ni chama tawala na chama tawala ndio serikali.

Ktk upande wa elimu sera ya serikali kweli ni nzuri japo inaangushwa na baadhi ya watu wenye tamaa na mafisadi ,Tz kwa afrika ni nchi ya pili ama ya tatu kutoka mwisho kwa umasikini lakini serikali yake bado inawapa udhamini wanafunzi wa elimu ya juu nje na ndani ya nchi.

Katafute nchi nyingine afrika inayofanya hivyo na kama zipo ni chache mno wenda zisidi hata tatu.

Bado naamini umakini wa serikali ktk elimu ya juu pamoja na serikali kua masikini ya mwisho ndiyo bado unaona UDSM bado inang'ang'ania Top ten ,nakubali pia mchango wa wahadhili lakini mkono wa serikali ndio msingi.

Mwl Kitila pamoja na maneno mengi na elimu yetu kudidimia lakini bado naamini elimu yetu ipo juu kwa afrika ,Maana nimekutana na watu karibu elfu tatu hivi kutoka nchi mbalimbali za afrika wakati tunajifunza language school hapa Natambua ubora wa elimu ya bongo pamoja na serikali kua masikini.

Nisiandike mengi sana lakini kwa kawaida utajiri wa nchi unaenda rank za vyuo swali kwako kwanini TZ ni masikini lakini chuo chake UDSM kimeng'ang'ania kuifanya TZ kwa ubora wa nchi kua ya tatu??

Unaposema CCM na serikali yake haikutusomesha wewe na mimi unamaanisha nini??

Stop Whinning! Ulisomeshwa kwa kodi yako na chama kilikuwa kimoja wakati huo. Hata ingekuwa CHAUSTA kodi yako ingekusomesha tu!

Asha
 
moderator & Mmjj,
sikutegemea Mawazo Yenye Upupu Kiasi Hiki Toka Kwa Alias 'mwanahabari Maarufu Wa Jf', Mwanakijiji. Natumaini Aliyosema Ni Mawazo Binafsi Na Sio Msimamo Wa Jf.

mmjj Kama Msemaji Wa Chadema, Unofficial, Hili Linawezekana Ikawa Ndio Utaratibu Wa Chadema Wanaoutumia Kwa Wasioafikiana Nao Na Hivyo Watakavyowaambia Watz Watakapolalamikia Demokrasia Ikiwa Wakipewa Nafasi. Kama Ni Hivyo Basi Ni Bora Tukabaki Na Mafisadi Tunaowajua Kuliko Kuwakaribisha Wapya Wanaojifanya Watakatifu Mpaka Tu Pale Utakapogusa Sehemu Zao Nyeti?

  1. kati Ya Threads Zilizounganishwa, Nafikiri Nyingi Zake Zilifaa Kusimama Peke Yake Angalau Kwa Wiki Chache Kabla Ya Kuwa Achived, Nimeshangaa Kuona Ya Kwangu In 2 Mins Ikawa-achived, Ni Kwa Nini?
  2. kwa Nini Mvuto Wa Topic Uondolewe Kwa Kuunganishwa Na Thread Ambayo Kichwa Chake Cha Habari Hakina Mvuto Kulingana Na Nyakati??
  3. kwa Nini Maombi Ya Mleta Thread Yasisikilizwe Pale Anapoomba Thread Yake Iwe Independent Kwa Muda Kabla Ya Kuunganishwa?? Ugumu Au Ubaya Uko Wapi Hapa, Moderator??
moderator, Hili La Kuiachia Thread Ining'inie Yenyewe Nimekufahamisha Wazi Na Nikakutumia Pm, Vipi Imekuwa Vigumu Kujibu?? Natumaini Majibu Ya Mmjj Hayakuwakilishi Na Utanipatia Mimi Pamoja Na Wanaukumbi Majibu Yenye Kueleweka.

hapa Naorodhesha Baadhi Tu Ya Threads Zilizounganishwa. Sielewi Kwa Nini Zimeunganishwa Na Ile Ya Mtu Aliyekuwa Banned, Kama Ndio Introduction Ya Thread Lakini Ikapewa Tittle Tofauti. Naomba Utufahamishe Jinsi Ulivyofikia Hapa Maana, Pia Sidhani Kuwa Hizi Thread Zote Na Nyingine Nisizoziorodhesha Zilihitaji Kuunganishwa Within Two Min Baada Ya Kuwa Posted Wakati Kila Moja Inaelezea Jambo Tofauti??

  1. mbowe Ampiga Vita Chacha Wangwe
  2. chadema Wamsimamisha Chacha Wangwe
  3. wangwe Alonga Tatizo Ni Mbowe !!!!
  4. baada Ya Chadema Kumwaga Ugali...wangwe Amwaga Mboga
  5. mpasuko Wa Kisiasa Ndani Ya Chadema?
  6. chadema Mtimueni Wangwe - Nccr
  7. chacha Wangwe Si Makamu Mwenyekiti-katiba Ya Chadema
  8. wangwe Atishiwa Kutimuliwa Chadema

Mimi Niliweka Yangu Ya Chadema Wajiloga Wenyewe Ilikuwa Habari Ya Kisiasa Ikaondolewa Ndani Ya Second Na Kupelekwa Kwenye Utani,

Kuna Thread Ya Chadema Na Udikteta Makao Makuu Hiyo Ilifutwa Sehemu Za Hoja Na Kubaki Sehemu Za Majibu Tu, Ni Ukweli Wa Wazi Kuna Kaupendeleo Hapa. Huwezi Kuwaambia Watu Waondoke Wakati Wametumia Muda Wao Kuwekeza Hapa Jf, Fmes Tukimwambia Aondoke Kwa Vile Ni Ccm Itakuwa Ni Kutokumtendea Haki Jamaa Kawekeza Sana Hapa Na Kutuvuta Wengi Lakini Kwa Vile Hayuko Chadema Anapewa Low Profile,
Muziki Wa Rege Muasisi Si Bob Marley Imekuwa Ikifichwa Sana. Fmes Anaandika Kwa Uhodari Na Uoni Sio Anaandika Tu Kukipigia Debe Chama Chake,kwenye Kukosoa Anakosoa,lakini Wengine Wamekuwa Kama Kasuku Wako Hapa Kuimba Nyimbo Nzuri Za Mwenyekiti Wa Chadema Kiasi Cha Kumfanya Kama Malaika Hana Mapungufu Hata Ya Ukabila Wanayatafutia Misamiati Mizuri.
 
Mkamap: Ni vigumu sana kuyaangalia haya mambo objectively kama hadi leo unaamini kwamba CCM ndiyo iliyokusomesha. Ok, let's assume this ludicrous claim is true, so what- Wanastahiki fadhila??!

Sikujua kwamba propaganda za CCM ziliwaingia wengi namna hii. Aibu!!

Mheshimiwa Rais wetu, mbona hata wewe ulikuwa ukipiga propaganda kuwa CCM ni chama makini ni pale tu ulipogombea Uenyekiti wa UVCCM-mkoa wa Dsm na ukashindwa vibaya kwa kupata kura moja tu naamini ilikuwa yako mwenyewe ndio ukahama CCM,
uliomba na ujumbe wa baraza kuu ukakosa.uliyokuwa ukiyaamini wewe jana wenzako wanayaamini leo.
hukutakiwa kusema wewe maneno haya,wanatakiwa kusema kama kina Mnyika au Zitto amabao hawajawahi kugombea uongozi CCM.
 
Kitila

Unaposema CCM haikutusomesha wewe na mimi unamaanisha nini??

Mkamap, CCM ingekuwa na ubavu na utashi wa kusomesha ingeanza kumsomesha Makamba.

On a serious note, usiwatukane watanzania wanaojinyama mambo kibao ili walipie elimu, afya, n.k kwa kupitia kodi zao.

Jamani tuache hizi imani potofu. Hakuna chama cha siasa chenye hela za kusomesha watu. Dola (hata ya kichaa kama ya Amini) yeyote duniani lazima itatoza kodi kwa ajili ya elimu, afya, ulinzi, n.k. Sasa unapoona polisi barabarani unasema ni polisi wa CCM? Ukipewa vidonge hospitali unasema vidonge vya CCM?

Ndio maana wenzetu wazungu hutakuta hata siku moja wanasema hela za serikali au serikali inalipia hiki, always wanasema pesa za walipa kodi (tax payers' money). Wanajua kwamba serikali ni conduit tu ya kupitishia hizo hela, na sio hiari au upendelo, ni kazi ambayo wanalipwa. In fact ungewaambia Wamarekani leo kwamba elimu yao inalipiwa na Republicans au Waingereza wanasomeshwa na Labour ingekuwa ni tusi la ajabu!
 
Mkamap, CCM ingekuwa na ubavu na utashi wa kusomesha ingeanza kumsomesha Makamba.

On a serious note, usiwatukane watanzania wanaojinyama mambo kibao ili walipie elimu, afya, n.k kwa kupitia kodi zao.

Jamani tuache hizi imani potofu. Hakuna chama cha siasa chenye hela za kusomesha watu. Dola (hata ya kichaa kama ya Amini) yeyote duniani lazima itatoza kodi kwa ajili ya elimu, afya, ulinzi, n.k. Sasa unapoona polisi barabarani unasema ni polisi wa CCM? Ukipewa vidonge hospitali unasema vidonge vya CCM?

Ndio maana wenzetu wazungu hutakuta hata siku moja wanasema hela za serikali au serikali inalipia hiki, always wanasema pesa za walipa kodi (tax payers' money). Wanajua kwamba serikali ni conduit tu ya kupitishia hizo hela, na sio hiari au upendelo, ni kazi ambayo wanalipwa. In fact ungewaambia Wamarekani leo kwamba elimu yao inalipiwa na Republicans au Waingereza wanasomeshwa na Labour ingekuwa ni tusi la ajabu!

kwani yakifanyika mabaya kama vita ya IRAQ inatajwa serikali au REPUBLICAN wametupeleka vitani?
AU huwa ni Labour ya BLAIR imepeleka nchi vitani na imepoteza pesa kiasi kadhaa?
CCM inawezekana ilisimamia vizuri ilani yake, kama ambavyo ingeweza kutumia fungu hilo kwa jambo lingine ila ikaweka mkazo kwenye elimu.
msikilize obama anasema akiingia pesa zake zitaenda kwenye elimu,afya na nyumba na si vita.
 
Jana nilieleza kuwa Wangwe asingeweza kupata haki yake mbele ya wale wajumbe watano Ngaiza,Baregu,Ndesamburo, Makani na Mtei na akipeleka kw suala hilo mahakamani kwenye kipengele cha Judicial Review anatashinda kesi kuwa walimuondoa walikuwa na maslahi au ukaribuni na Mbowe hiyo ni point kubwa.

Wewe kumsema kuwa mimi muongo na Kitila ni kweli sio sahihi, angekuja mtu ambaye ni Independent angesema kuwa mimi muongo ingeleta nguvu,lakini inajulikana wazi kuwa pesa za makao makuu ya Chadema zinatumiwa vibaya kuwanufaisha kina Mnyika na group lao kuliko kutumika majimboni, Hilo group yuko Kitila na timu yao kwa michango yako humu, wewe ni sehemu ya timu hiyo,mtu ambaye uko kwenye mission moja utaacha kusema kuwa ni mkweli?

Unajua ukienda mahakamani ushahidi wa mke wako, au ndugu yangu hautakiwi sababu utakuwa wa upendeleo, ukiomba kazi huwezi kusema kuwa ndugu yako au rafiki yao ndio refarii wako, hawezi kutoa maelezo ya ukweli.
Kitila hawezi kuwa mkweli kwa kauli yako wewe mwenzake kwenye mission ya kumtoa Wangwe.
WAKATABAHU!!!
walianza mbali kumuombea na kumpangia mabaya.
 
Waheshimiwa wote mmekuja hapa jamii Forums kumkashifu Wangwe ina maana huko kamati kuu haikutosha? huko mlikuwa uso kwa uso mngempa vidonge vyake live kuliko kuja hapa na kauli mbiu ya kuwa Wangwe ni mzigo mzito, kama mnamuogopa kiasi hiki basi tumieni kanga kama wanawake wanavyofanya mtengeneze kanga za mafumbo.

Kitila anaweza kuvaa iliyoandikwa ' Zigo zito tumelitua mwaya ' na Zitto Kabwe iwe na maneno 'Utajiju na bangili zako' kuwa atajijua na bangi zake,

Mwenyekiti anaweza kuvaa inayosema 'Tulikwambia mpaka kitaeleweka ama kweli wewe ni kubwajinga' na Mnyika ' mcheza kwao hutunzwa au mvua usioijua imekunyeshea' mcheza kwao mwenyekiti lazima ashinde, wanawake hutumia kanga kufikisha ujumbe kuliko kumkabili mtu wanaemuogopa.

Maandishi yenu hapa yanaonesha kuwa Wangwe alikuwa anaishi katika mazingira magumu sana kama Makamu Mwenyekiti, kumbukeni yeye ana nguvu ya wanachama sio makao makuu wanaotumia JF ambao sio wanachama.
Walimtengeneza kanga marehemu Wangwe.
 
Wangwe ni mzigo hatari ambao CHADEMA wanapaswa kuubwaga chini mapema kabla ya madhara zaidi. Chama chenye malengo ya muda mrefu kama CHADEMA walipaswa kuwa makini katika kurecruit watu kama hawa kwa kuwajua na kuangalia athari zao kwa nchi na chama chao. Kwa ninavyamjua Wangwe hata kadi hawakupaswa kumpa.

Walichokifanya CHADEMA sasa ni muhimu hata kama kitaleta madhara kwa sasa lakini kitawasaidia kuendeleza mipangoa yao ya muda mrefu badala ya kuachia wahuniwahuni wachache wanaochukulia siasa kama ushindani wa simba na yanga ama ubishani wa kijiweni SAIGON kuharibu mipango ambayo ikifanikiwa italisaidia taifa letu na chama chao.

Uamuzi wa CHADEMA kumshughulikia WANGWE sasa ndio aina ya uongozi inayohitajika nchini yenye uwezo wa kuthubutu kuchukua maamuzi magumu hata kama wanajua kuwa yataumiza chama chao. Kikwete na wenziwe wanaogopa kuwashughulikia mafisadi walijenga ngome CCM wanapaswa kuiga mfano huu.

Kwa hao wanafiki wa CCM wanaotaka kumfanya Wangwe shujaa wao ingawa ni hivi karibuni tu walikuwa wakilaani taarifa za CHADEMA kukataa kuachia uenyekiti wa manispaa ya KIGOMA umamuzi ambao ulishurutishwa na siasa za kihuni za WANGWE, nawashauri wampokee nyumbani (CCM) kwa nderemo na vifijo.

Hata hivyo CHADEMA bado mna vichaka vingi zaidi vya kusafisha kabla ya kujenga imani kwa watanzania kama mnaweza kuwa tofauti na huu uhuni tulio nao sasaaaa.

Tanzanianjema
Nakubali mzigo mzito.
 
Web Master Funga Hii Topic Kwani Hatuwezi Kujadili Mtu Aliyefariki Dunia Tumpe Heshima Yake.
 
Huyu naona ni pandikizi la CCM na amewekwa ili kukivuruga CHADEMA. Wasipokuwa makini kweli atawavuruga. Akiendelea kuongea upupu wake ambao hauna maslahi kwa CHADEMA ni bora kumtosa tu.

Web Master Funga Hii Topic Kwani Hatuwezi Kujadili Mtu Aliyefariki Dunia Tumpe Heshima Yake.



duh!


sasa democrasia iko wapi? wangapi wamekufa na bado wanaendelea kujadiliwa?
 
KAULI YA MWISHO YA MAREHEMU CHACHA WANGWE KWA
MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE

HII NI TAARIFA YA MHESHIMIWA WANGWE KUHUSU JARIBIO LA MWENYEKITI WA CHADEMA, FREEMAN MBOWE KUMVUA WADHIFA WAKE NA UANACHAMA WA CHADEMA ALIYOTARAJIA KUISOMA KWA WATANZANIA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA KUFIKA DAR ES SALAAM, DHAMIRA AMBAYO ILIKATISHWA NA MAUTI YALIYOTOKANA NA INAYOSEMEKANA KUWA NI AJALI YA KUPANGWA, ENEO LA PANDAMBILI, WILAYA YA KONGWA DODOMA TAREHE 28 JULAI, 2008.

Taarifa hii ilikuwa isomwe Dar es salaam, tarehe 29 Julai, 2008 siku moja kabla ya ajali iliyomuua CHACHA WANGWE

UTANGULIZI

Jumamosi, June 28 mwaka huu wajumbe kadhaa wa Kamati Kuu ya CHADEMA walidai kuwa wamesitisha Umakau Mwenyekiti wangu katika kikao kilichofanyika mjini Dodoma siku hiyo. Kesho yake Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. FREEMAN MBOWE akaitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutaja sababu za kunisimamisha uongozi.

Inatosha tu kusema kuwa sababu zote alizotoa ni za uzushi kama ile inayodai kuwa mimi navujisha siri za chama kwa viongozi wa CCM bila hata kutaja siri hizo, au kusema nimezitoa lini, wapi, na kwa kiongozi yupi?

Kikao hicho kinachosemekana kunisimamisha uongozi, kilikuwa na wajumbe 31 ambao takribani nusu hawakuwa na uhalali wa kupiga kura kinyume cha katiba na kanuni za CHADEMA kwa vile walikuwa wameandaliwa kwa kazi hiyo. Wajumbe 7 walikataa kushiriki njama hizo.

Kufuatia jaribio hilo la kunivua uongozi kutokubalika kwa wanachama walio wengi wa CHADEMA , Mwenyekiti MBOWE na wafuasi wake wameendelea kuhaha kwa kuongeza sababu nyingine mbalimbali ili kuhalalisha njama zao. Sasa hivi wameingia hatua ya kuwashawishi wanachama wa Tarime eti wanifukuze uanachama.

Kwa kuzingatia katiba, kanuni na taratibu za CHADEMA, nilichokifanya mimi baada ya kubaini njama zao ni kukata rufaa kwa Baraza Kuu la Chama, kupinga upotoshaji unaofanywa chini ya uongozi wa Mhe. MBOWE anayeonekana kutaka kuendesha chama kinyume na matarajio ya wanachama walio wengi.

Hivyo basi zipo habari za uhakika kuwa kikao hicho cha Baraza Kuu hakitaitishwa ama kabisa, au kitacheleweshwa kwa makusudi, kwa visingizio mbalimbali ikiwemo kutokuwa na fedha za kukidhi gharama za kikao hicho.

Naomba nikiri kuwa ninakerwa sana na mtiririko mzima wa sakata hili linalozua mgogoro unaokiyumbisha chama. Ukweli ni kwamba mimi niligombea Umakamu Mwenyekiti nikiwa na agenda ya kufufua uhai wa chama kwa kukaripia vitendo visivyostahili katika kuendesha chama. Agenda yangu haijabadilika. Yote niliyoyasema wakati nagombea nafasi hii yanafahamika kwa wana CHADEMA wote. Walikuwepo walioyalalamikia na walikuwepo walioyapongeza matamshi yangu hayo.

Mwisho wa yote wana CHADEMA waliridhika kuwa ajenda yangu ilikuwa sahihi na hivyo wakanichagua kuwa Makamu Mwenyekiti. Hivyo basi hata kama ni kweli kuwa ulikuwepo mvutano wakati wa kampeni ile, lakini hilo ni jambo la kawaida katika uchaguzi. Nijuavyo mimi hayo yalitakiwa yawe si ndwele nasi tugange yajayo kwani wanachama walikwisha fanya uamuzi halali kupitia kura zao.

Baada ya kuingia kwenye wadhifa wa Makamu Mwenyekiti Taifa, nilifanikiwa kuzungumza na Mhe. MBOWE kuhusu mambo, hususan yale, niliyoyapigania wakati wa kinyang’anyiro kile na kumuomba tukae chini na kutafuta jinsi ya kufanikisha azma hiyo.

Ni imani yangu kuwa waraka huu utawasaidia wanaCHADEMA wenzangu na watanzania wote kwa ujumla, kuelewa vizuri ukweli wa mambo niliyoyapigania kabla ya kuwa Makamu Mwenyekiti, na ninayoendelea kuyasimamia hivi sasa nikiwa Makamu Mwenyekiti, na inshallah nitakayoyatekeleza baadae kama Taifa Mwenyekiti wa CHADEMA.

Kimsingi mambo tunayotofautiana na Mhe. MBOWE ni haya yafuatayo:-

MATUMIZI YA RUZUKU

CHADEMA hupata ruzuku ya Tshs. 66,000,000 kwa mwezi (Milioni sitini na sita). Mimi nasema si haba hasa tukizingatia chama kilikotoka. Naamini kuwa kiasi hiki cha fedha kikisimamiwa vizuri kinaweza kukirahisishia chama kujieneza katika ngazi zote toka Tawi, Wilaya, Mkoa na Taifa.

Si kweli kwamba matatizo yote yatamalizwa na fedha hizi lakini basi hata ofisi za chama zinaweza kuwa hai nchi nzima kitu ambacho kwa sasa hakipo. Mahesabu yanaonesha kuwa mtaji wa laki moja (Tshs.100,000/=) kwa wilaya moja nchini inatosha, hivyo kwa Wilaya 126 kwa mwezi jumla yake ni Tshs. milioni 12 (Tshs. 12,600,000/= ) zinahitajika ( Wilaya 126 x 100,000 kila wilaya = 12,000,000/=)

Hata tukisema tupeleke kiasi hicho kwa kila jimbo la uchaguzi jumla yake ni Tshs. Milioni 23 (Tshs. 23,000,000/=) kwa maana ya majimbo 213 x 100,000 = 23,000,000/=. Mhe. MBOWE anasema hizo ni pesa nyingi sana kwa uimarishaji wa chama. Mimi nasema hapana, kiwango hiki kwa kila Wilaya au Jimbo la uchaguzi ni muafaka kwani haba na haba hujaza kibaba.

Chini ya uongozi wa Mhe. MBOWE na wafuasi wake hawastaajabu kuwa kati ya Tshs. 374,144,000.40 zilizopatikana kama ruzuku katika ya Januari 1 na Juni, 30, 2008, Tshs. 350,000,000/= zilitumika Makao Makuu ya CHADEMA na Tshs. 25,000,000/= tu ndizo zilikwenda Wilayani kuimarisha chama.

Mimi naona mgao huu unayatukuza Makao Makuu ya CHADEMA isivyostahili wakati huo huo ukidhalilisha chama nchi nzima.

MADENI YA UCHAGUZI

Kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Mhe. MBOWE alitufahamisha wanachama kuwa alikuwa anakidai chama US $ 181,949.00 sawa na Tshs. 218,338,546. Mpaka sasa chama kimekwisha mlipa Tshs. 175,000,000/=

Baada ya kupata wadhifa wa Makamu Mwenyekiti, na kwa kuzingatia takwimu zionekanazo hapo juu katika kulinganisha matumizi ya fedha Wilayani na Makao Makuu niliamua kumshauri MBOWE asitishe kujilipa deni kutokana na fedha za ruzuku kwani siamini kuwa kulipa madeni yaliyopita kunaendana na utaratibu wa usimamizi wa fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa toka serikalini.

Mhe. MBOWE alichachamaa na ndipo nilipomshauri kuwa kama ni hivyo basi atuthibishie pesa hizo anazodai alikikopesha chama ziliingia kwenye akaunti gani ya CHADEMA, kupitia hundi ipi, na lini? Nilimuomba pia kutaja ni kikao gani cha chama kiliidhinisha matumizi ya fedha hizo kwani kama hakuna ushahidi wa maidhinisho, ni dhahiri kuwa matumizi hayo hayakudhibitiwa na chama na kwa mantiki hiyo kuyafanya kuwa matumizi binafsi ya Mhe. MBOWE.

Vilevile, nilimueleza kuwa matumizi ya fedha hizo alizodai alikikopesha chama yalikuwa yakinuka harufu ya UFISADI. Stakabadhi zote kuhusiana na matumizi hayo zilionesha kuwa gharama za aidha ununuzi na / au ukodishaji wa vifaa hivyo, hazikutofautiana na viwango wanavyolipishwa watalii kwa huduma kama hizo, kwa maana ya gharama ya juu sana.

Na kwa kuwa hata baada ya kuwa Mhe. MBOWE amekwisha lipwa zaidi ya nusu ya deni alilodai kuikopehsa CHADEMA, vifaa vyote yakiwemo magari, vipaza sauti na kadhalika vimebakia kuwa mali yake binafsi, basi bila kumficha nilimueleza kuwa huko ni kukinyonya chama kwa kukigeuza kitega uchumi cha watu binafsi.

Kuhusu suala la kulipa madeni kupitia ruzuku ya serikali, nilimuomba Mhe. MBOWE afuatilie kwa Msajili wa Vyama vya siasa ili tupate ufafanuzi kama kweli fedha za ruzuku ya serikali kwa vyama vya siasa, inaweza kutumika kulipia madeni ya viongozi wa vyama hivyo yatokanayo na uchaguzi ili CHADEMA isiathirike kisheria.

Niseme kweli hapa kwamba, kwa vile wanaCHADEMA wengi walinichagua kuwa Makamu Mwenyekiti, na hata mimi mwenyewe tulikuwa wagombea wa nafasi za ubunge, udiwani n.k katika uchaguzi wa mwaka 2005 ningefarijika sana iwapo na sisi tungerejeshewa angalau chochote cha kufidia gharama zetu, kwa maana kwamba kama chama kimeamua kurudisha gharama hizo kiwalipe wote badala ya kulipa madeni kwa wateule wachache.

UTEUZI WA WABUNGE WA VITI MAALUM

Naamini ukweli wa suala hili hauna mjadala. Kwamba Mhe. MBOWE na wafuasi wake walighushi orodha ya majina ya viti Maalum badala ya kupeleka yaliyopendekezwa na Kamati Kuu sio siri. Naamini hata Mhe. MBOWE anakubaliana nami kuwa suala hili si moja ya siri anazodai nimevujisha!

Yamesemwa mengi juu ya mtafaruku uliojitokeza kuhusu viti maalum hadi baadhi ya waasisi wa chama wakataka kujitoa na hivyo kumlazimisha Mwenyekiti Taifa ( FREEMN MBOWE) na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kukiomba radhi kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kwa kukiuka katiba, kanuni na maadili ya chama katika suala hili la kugushi viti maalum.

Ni ukweli ulio wazi kuwa kitendo hicho cha upendeleo bado kina iumiza taswira ya CHADEMA. Chama kinaonekana kuendekeza ujanja ujanja kiasi kwamba watu na binti zao, wakwe zao, shemeji zao, waume wenzao, wachumba wa shemeji zao, wake wenza na kwa kiwango kikubwa watu wa kabila moja ndiyo wamekuwa sura ya CHADEMA bungeni.

Katika hili nilichoweza kumueleza Mhe. MBOWE ni kuwa chaguzi mbalimbali tangu za Mitaa, Ubunge na Urais zinakaribia ni vizuri tufanye bidii kusambaza nguvu zetu nchi nzima tuwe na mtaji wa kura maeneo mengi ili kashfa kama hii isijirudie. Hii ni kwa msingi kuwa chama kikijitanua kutakuwa hakuna sababu ya kuwaona watu wa eneo fulani tu kuwa ndiyo mhimili wa CHADEMA na hivyo zikitokea fursa itakuwa rahisi chama kuwakilishwa na mtandao wake mpana badala ya koo au kabila fulani.

Sasa kwa kuwa kuimarisha chama kitaifa maana yake ni matumizi ya fedha, nalo hili likawa nongwa ingawa kwa mtazamo wa Makao Makuu kulipa madeni kwa wateule wachache si nongwa. Cha ajabu ni kwamba Mhe. MBOWE hakukana kuwa hili la viti maalum na hata upangaji wa ajira kwa ukabila una leta athari mbaya kwa mustakabali wa CHADEMA.

Katika maongezi yangu nae nilikuwa wazi nilipotahadharisha kuwa:

1. Watanzania wakiendelea kuona kwamba CHADEMA inaendeshwa kwa misingi ya kikabila hawatajiunga na chama chetu na tutakosa wafuasi.
2. Watanzania wakiona kuwa sisi tumeweka mbele ukabila kuliko utaifa hawatatupa madaraka na kutawala kwa kuhofia yale yanayotokea nchi jirani kama Rwanda, Burundi, Kenya na kadhalika ambako nafasi za raia wote zimehodhiwa na kabila moja na hatma yake watu wamechinjana kama kuku kwa kupinga hilo.

Pia nilimwambia kwamba, kwa jinsi sura ya uteuzi wa Wakurugenzi na watendaji wengine wa Makao Makuu inavyoonekana, sasa tayari chama chetu kimebatizwa jina la CHAMA CHA WACHAGA, na hii si kuwatendea haki raia wengine na makabila yao ambao wataonekana kama punguani kujihusisha na chama na ukabila.

Yote haya ninayosema kuhusu ukabila, upendeleo na kadhalika sio dhana tu. Kufuatia malalamiko mengi yaliyokuwa yakisikika nchi nzima kuhusu masuala haya, Kamati Kuu ya CHADEMA ilikwisha unda Tume kutafuta ukweli wa mambo hayo. Tume hiyo ya watu watano iliongozwa na Mhe. Merky Lugendo Mziray ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA nayo imekwisha toa taarifa yake kwamba Makao Makuu ya CHADEMA yanatawaliwa na ubaguzi wa kikabila, kidini na kielimu.

UTENDAJI WA KIBABE

CHADEMA ni chama kilicho njia panda kwa sasa kutokana na utendaji wa kibabe wa Mhe. MBOWE. Ninafahamu jinsi vyama vingine vya upinzani hapa nchini kama vile NCCR – Mageuzi vilivyoporomoka haraka haraka mithili ya nyumba ya mabua. Chama NCCR – Mageuzi kilifikia mahali pazuri tu hadi watu wakaanza kufikiria kuwa kingekuwa chama mbadala kwa CCM. kwa bahati mbaya uchu wa madaraka, ulafi wa ruzuku, na tabia za kimangimeza kwa pamoja vikakiathiri hadi kupoteza umaarufu wake.

Na hata vyama vingine vya upinzani vina dalili hizo hizo japo kwa viwango vinavyotofautiana. Ila badala ya kujichunguza na kujua kasoro zetu, kila siku vyama vyetu, vimekuwa vikidai kuwa ni chama tawala ndicho kinachoviroga, kama ambavyo Mhe. MBOWE ameanza kuweweseka kupitia vyombo vya habari.

Napenda kuthibitisha kuwa katika mgogoro unaopaliliwa sasa na Mhe. MBOWE ndani ya CHADEMA kutokana na ufisadi, ufuska, ulevi wa madaraka na umangimeza chanzo chake ni tabia yake ya kuendesha chama kibabe. Mathalan kumzuia Martin Mung’ong’o Mkurugenzi aliyechaguliwa kwa kura kutofanya kazi zake ndani ya chama, madai ya kupigana na watendaji wa chama ndani ya baa na vitendo vingine vya aina hiyo ni ushahidi tosha wa hulka hii. Hadi sasa Mhe. MBOWE amefanikiwa kukizuia chama hiki kisifanye kazi ya siasa mkoa wa Dar es salaam kwa miaka minne.

Ninavyoongea hivi sasa CHADEMA imekuwa ikikimbia vikao vya Democratic Union of Afrika (DUA), Muungano wa Vyama Vya Upinzani, uliofanikisha CHADEMA kujuana na Conservative Party ya Uingereza na Republican ya Marekani. Vyama dada hivi vyote vinaulalamikia uongozi wa CHADEMA kwa kufuja fedha ya misaada na kuwasilisha kwao risiti za kugushi, kama ilivyofanyiwa Conservative Party baada ya kutoa msaada wa Tshs. 78,000,000 kwa ajili ya ununuzi wa baiskeli na pikipiki ambazo hazikununuliwa.

Katika mkutano wa Kamati Kuu ya CHADEMA huko Dodoma hivi majuzi tu, Mhe. MBOWE kwa kauli yake aliwatisha wajumbe kuwa alikuwa amethibiti uwezekano wowote wa wajumbe kujisikia huru kwa kutoa mawazo ambayo yangepingana na ajenda yake aliyoitoa ghafla kikaoni kunisimamisha Umakamu Mwenyekiti.

Mhe. MBOWE Alikifahamisha kikao kuwa alitoa taarifa kwa IGP, SAID MWEMA kuwa kuna wahuni ambao walitaka kuuchafua mkutano wake, naye IGP akahakikisha kuwa mkutano ule unalindwa kwa kiwango cha kushtua kama ambavyo hata vyombo vya habari vimethibitisha.

Hayo ni baadhi tu ya mambo yanayobainisha Mhe. MBOWE ni kiongozi wa aina gani.

HITIMISHO

Kama nilivyokwisha sema hapo awali, sijaacha na sintoacha ajenda yangu ya kufufua uhai wa CHADEMA kwani ndiyo ahadi iliyofanikisha kuchaguliwa kwangu kuwa Makamu Mwenyekiti Taifa. Nilipopata wadhifa huo nilianza kuitekeleza ajenda hiyo kupitia mahojiano na Mwenyekiti MBOWE kuhusu matumizi ya ruzuku, madeni ya uchaguzi, uteuzi wa wabunge wa viti maalum, nafasi za ajira Makao Makuu, na kuhusu mwenendo wa chama Mkoa wa Dar es salaam.

Nilijikuta katika mvutano mkubwa kila nilipogusa eneo lolote katika haya. Nakiri kuwa kwa kiwango kikubwa sikuwa na uwezo wa kubadili mambo hayo yaliyokuwa yakiratibiwa kwa ukaribu na Mhe. MBOWE na wafuasi wake kwani sikupewa ushirikiano wa aina yoyote na chama pale Makao Makuu. Ni vigumu kuamini, lakini ni kweli kuwa sikuwa na ofisi Makao Makuu, sikupewa vitendea kazi kama magari, vipaza sauti na/au vyombo vya habari, na sikuwahi kupata taarifa yoyote ya kiutendaji toka Makao Makuu.

Kwa kuzingatia yote hayo, naomba nichukue fursa hii kuwashukuru kwa dhati wanachama wa CHADEMA mkoa wa Dar es salaam ambao kwa pamoja tulisimama kidete kufufua uhai wa chama hapa jijini. Niseme tu ushirikiano wao wa hali na mali uliniwezesha kushughulikia masuala muhimu ya kitaifa na kimataifa.

Rai yangu kwa wana CHADEMA na wale wote wanaokitakia mema chama chetu na nchi yetu kwa ujumla ni kwamba kazi ya kupigania demokrasia ya kweli ndani na nje ya chama, kukiepusha chama na vitendo vya ukabila, migogoro, ubadhirifu, umangimeza, ufisadi na ubaguzi wa aina yoyote bado inaendelea na nawaombeni mniunge mkono kwa hali na mali katika vita hii. Naamini tutashinda.

Mungu Ibariki CHADEMA
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika




====Chacha Wangwe amekufa lakini waraka wake huu utawasaidia WanaCHADEMA na watanzania kuelewa ukweli wa mambo aliyokusudia.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom