Gembe
JF-Expert Member
- Sep 25, 2007
- 2,483
- 167
sioni hata mantiki ya huu mjadala kuendelea.
Mwambie aliyeuanzisha aufunge
sioni hata mantiki ya huu mjadala kuendelea.
wewe unataka nani aje athibitishe?nani anaweza pia kuthibitisha tuhuma za pesa za EPA?
tukianza kusema hivyo basi tuache na yale ambayo hatuna uhakika nayo,ila yaliyosemwa ni kweli?
hiyo mbona ishu ndogo na inawezekana?mie nafikirir tuangalie nadhalia ya jambo lenyewe na wangwe alikuwa akisema nini kuhusu CHADEMAGembe;
Do not be Naive, E&Y Audit report explains everything about EPA, We want a signed Wangwe's Document to verify its authenticity.
hiyo mbona ishu ndogo na inawezekana?mie nafikirir tuangalie nadhalia ya jambo lenyewe na wangwe alikuwa akisema nini kuhusu CHADEMA
Mimi naweza kuamini kuwa huu ni waraka wa Wangwe kweli kwani sentiments zake siyo ngeni na lugha yake haitofautiani na jinsi Wangwe anaandika. Swali langu hata hivyo ni walioupata wameupata wapi wakati tuliambiwa kila kitu kiliibwa pale kwenye ajali? Kama kuna mtu alikuwa nao kabla ya safari ni nani huyo, na kama kuna mtu ulimfikia baada ya ajali ni nani huyo? na wote hao waliupata wapi kwanza?
Kwa sababu kama kuna mtu mbaya ambaye aliupata waraka huu masaa machacha kabla ya Wangwe kulazimika kuondoka na akaona uzito wa madai yake ni wazi angeweza kuchukua kitu chochote na kufanya kweli ili aiharibu Chadema kabisa kwani sasa mwandishi "wake" hayupo kutetea alichoandika au kusema "hapana hicho sikukiandika".
Gembe, unafikiri waraka huu umepatikana lini? Kabla ya kifo au baada ya kifo..?
hili ni swali ambalo tunatakiwa tumuulize aliyeleta waraka huuMimi naweza kuamini kuwa huu ni waraka wa Wangwe kweli kwani sentiments zake siyo ngeni na lugha yake haitofautiani na jinsi Wangwe anaandika. Swali langu hata hivyo ni walioupata wameupata wapi wakati tuliambiwa kila kitu kiliibwa pale kwenye ajali? Kama kuna mtu alikuwa nao kabla ya safari ni nani huyo, na kama kuna mtu ulimfikia baada ya ajali ni nani huyo? na wote hao waliupata wapi kwanza?
Kwa sababu kama kuna mtu mbaya ambaye aliupata waraka huu masaa machacha kabla ya Wangwe kulazimika kuondoka na akaona uzito wa madai yake ni wazi angeweza kuchukua kitu chochote na kufanya kweli ili aiharibu Chadema kabisa kwani sasa mwandishi "wake" hayupo kutetea alichoandika au kusema "hapana hicho sikukiandika".
Gembe, unafikiri waraka huu umepatikana lini? Kabla ya kifo au baada ya kifo..?
hili ni swali ambalo tunatakiwa tumuulize aliyeleta waraka huu
hili ni swali ambalo tunatakiwa tumuulize aliyeleta waraka huu
Mwanakijiji
Mzee nimekusoma, kweli huyu kautoa wapi huu waraka jamani? Da........... hapa kuna siri nzito, hawa watakuwa wanajua kitu.
Kuanzia ule waraka wa CCM kabla ya kifo cha marehemu, hapa kuna jambo
Gembe Uko wapi uyajibu haya Mkuu?
Waraka wa Madini ,kwa taratibu za Buneg Mhe. spika anweza kuwa nao.ila huu ni warak wa Mbowe na viongozi wote wa juu wa CHADEMA na wale wenye mlengo wa kumnyenyekea Mtu.
Kwanini hatujiulizi kwanini baaada ya wangwe kuandika waraka huu wa kuuponda uongozi wa CHADEMA alikufa kabla hajufikisha mbele ya watu?
Je kuna kiongozi yeyote wa CHADEMA alijua?Ndiyo walijua sababua lsiahawaambi baadhi ya watu..
Mkuu Mwanakijiji,
kuna jambo moja ambalo ningesema wazi,Baadhi ya wanachama wa CHADEMA ni wanafiki sana,unakumbuka therad ile ya wangwe kusimamishwa,watu kama kina MK walileta mapema resolution ya kusimamishwa kwa wangwe,sijui waliitoa wapi ambapo ilikuwa ni jmuda mchache baada ya kikao cha dodoma,inaonesha kuna mbinu chafu zilipangwa kabla.
Ukiendelea kupitia thread ile ambayo kwa sasa haionekani(Invisible kulikoni).utagundua jinsi wana CHADEMa ambo wako hapa JF walivyomdhihaki wangwe na hili ndilo kosa kubwa walilofanya,nina mshukuru sana kitila kwa kutoka nje na kuelezea upungufu walioufanya CHADEMA.
kwa maoni yangu CHADEMA Hawakustahili kufanya jambo lile wakati walikuwa wakishindana na chana tawala katika hoja za ufisadi,navyokwambia sasa hoja ya ufisadi ilimalizwa haswa na ugomvi wa CHADEMA kwa kiasi kikubwa magazeti yakabalidili mwelekeo mzima,kifo ndiyo basi tena ukawa mwisho wa mafisadi kujadiliwa.
Mie siyo kwamba nakumbatia ufisadi wala CCM(ambacho ni chama changu) ,ila siku zote nimekuwa nikitaka tujadili hoja zinazohusu wizi wa mali zetu kama watanzania,tujadili kwanini nchi na rasilimali zetu zote ila bado uchumi wetu uko chini?nyie mkaamua kuwaunga mkono kujadili kile walichokitaka,wameshashinda tena na hili ni bao la tobo.
Ndugu watanzania wenzangu,wana mapinduzi wenzangu kuna haja sasa ya kuanzisha mijadla ya kitaifa yenye kuleta tija na ambayo tutaifuatilia mpaka mwisho.Bajeti Muhimu zimepita ila zilizo na madudu kibao kwa kuwa tulipenda sana kukitetea chama zaidi,na mtu kwa ujumla,Hibvi kweli leo tumekuwa watumwa wa kuja kumtete mtu hapa?
tukate ishu
Kwa hiyo unakiri kwamba kuna waraka wa kisiasa na hoja yenye maslahi ya Taifa?
[/COLOKAULI YA MWISHO YA MAREHEMU CHACHA WANGWE KWA
MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE
HII NI TAARIFA YA MHESHIMIWA WANGWE KUHUSU JARIBIO LA MWENYEKITI WA CHADEMA, FREEMAN MBOWE KUMVUA WADHIFA WAKE NA UANACHAMA WA CHADEMA ALIYOTARAJIA KUISOMA KWA WATANZANIA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA KUFIKA DAR ES SALAAM, DHAMIRA AMBAYO ILIKATISHWA NA MAUTI YALIYOTOKANA NA INAYOSEMEKANA KUWA NI AJALI YA KUPANGWA, ENEO LA PANDAMBILI, WILAYA YA KONGWA DODOMA TAREHE 28 JULAI, 2008.
Taarifa hii ilikuwa isomwe Dar es salaam, tarehe 29 Julai, 2008 siku moja kabla ya ajali iliyomuua CHACHA WANGWE
Sitaki kuingia kwa ndani katika maneo yaliyomo ndani ya waraka huu lakini swali langu la kwanza ni TUTAAMINI VIPI kuwa huu waraka ndiyo ilikuwa isomwe Dar siku moja kabla ya kifo chake? Naomba uthibitisho hapa.
UTANGULIZI
Jumamosi, June 28 mwaka huu wajumbe kadhaa wa Kamati Kuu ya CHADEMA walidai kuwa wamesitisha Umakau Mwenyekiti wangu katika kikao kilichofanyika mjini Dodoma siku hiyo. Kesho yake Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. FREEMAN MBOWE akaitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutaja sababu za kunisimamisha uongozi.
Inatosha tu kusema kuwa sababu zote alizotoa ni za uzushi kama ile inayodai kuwa mimi navujisha siri za chama kwa viongozi wa CCM bila hata kutaja siri hizo, au kusema nimezitoa lini, wapi, na kwa kiongozi yupi?
Kikao hicho kinachosemekana kunisimamisha uongozi, kilikuwa na wajumbe 31 ambao takribani nusu hawakuwa na uhalali wa kupiga kura kinyume cha katiba na kanuni za CHADEMA kwa vile walikuwa wameandaliwa kwa kazi hiyo. Wajumbe 7 walikataa kushiriki njama hizo.
Kufuatia jaribio hilo la kunivua uongozi kutokubalika kwa wanachama walio wengi wa CHADEMA , Mwenyekiti MBOWE na wafuasi wake wameendelea kuhaha kwa kuongeza sababu nyingine mbalimbali ili kuhalalisha njama zao. Sasa hivi wameingia hatua ya kuwashawishi wanachama wa Tarime eti wanifukuze uanachama.
Kwa kuzingatia katiba, kanuni na taratibu za CHADEMA, nilichokifanya mimi baada ya kubaini njama zao ni kukata rufaa kwa Baraza Kuu la Chama, kupinga upotoshaji unaofanywa chini ya uongozi wa Mhe. MBOWE anayeonekana kutaka kuendesha chama kinyume na matarajio ya wanachama walio wengi.
Hivyo basi zipo habari za uhakika kuwa kikao hicho cha Baraza Kuu hakitaitishwa ama kabisa, au kitacheleweshwa kwa makusudi, kwa visingizio mbalimbali ikiwemo kutokuwa na fedha za kukidhi gharama za kikao hicho.
Naomba nikiri kuwa ninakerwa sana na mtiririko mzima wa sakata hili linalozua mgogoro unaokiyumbisha chama. Ukweli ni kwamba mimi niligombea Umakamu Mwenyekiti nikiwa na agenda ya kufufua uhai wa chama kwa kukaripia vitendo visivyostahili katika kuendesha chama. Agenda yangu haijabadilika. Yote niliyoyasema wakati nagombea nafasi hii yanafahamika kwa wana CHADEMA wote. Walikuwepo walioyalalamikia na walikuwepo walioyapongeza matamshi yangu hayo.
Mwisho wa yote wana CHADEMA waliridhika kuwa ajenda yangu ilikuwa sahihi na hivyo wakanichagua kuwa Makamu Mwenyekiti. Hivyo basi hata kama ni kweli kuwa ulikuwepo mvutano wakati wa kampeni ile, lakini hilo ni jambo la kawaida katika uchaguzi. Nijuavyo mimi hayo yalitakiwa yawe si ndwele nasi tugange yajayo kwani wanachama walikwisha fanya uamuzi halali kupitia kura zao.
Baada ya kuingia kwenye wadhifa wa Makamu Mwenyekiti Taifa, nilifanikiwa kuzungumza na Mhe. MBOWE kuhusu mambo, hususan yale, niliyoyapigania wakati wa kinyanganyiro kile na kumuomba tukae chini na kutafuta jinsi ya kufanikisha azma hiyo.
Ni imani yangu kuwa waraka huu utawasaidia wanaCHADEMA wenzangu na watanzania wote kwa ujumla, kuelewa vizuri ukweli wa mambo niliyoyapigania kabla ya kuwa Makamu Mwenyekiti, na ninayoendelea kuyasimamia hivi sasa nikiwa Makamu Mwenyekiti, na inshallah nitakayoyatekeleza baadae kama Taifa Mwenyekiti wa CHADEMA.
Kimsingi mambo tunayotofautiana na Mhe. MBOWE ni haya yafuatayo:-
MATUMIZI YA RUZUKU
CHADEMA hupata ruzuku ya Tshs. 66,000,000 kwa mwezi (Milioni sitini na sita). Mimi nasema si haba hasa tukizingatia chama kilikotoka. Naamini kuwa kiasi hiki cha fedha kikisimamiwa vizuri kinaweza kukirahisishia chama kujieneza katika ngazi zote toka Tawi, Wilaya, Mkoa na Taifa.
Si kweli kwamba matatizo yote yatamalizwa na fedha hizi lakini basi hata ofisi za chama zinaweza kuwa hai nchi nzima kitu ambacho kwa sasa hakipo. Mahesabu yanaonesha kuwa mtaji wa laki moja (Tshs.100,000/=) kwa wilaya moja nchini inatosha, hivyo kwa Wilaya 126 kwa mwezi jumla yake ni Tshs. milioni 12 (Tshs. 12,600,000/= ) zinahitajika ( Wilaya 126 x 100,000 kila wilaya = 12,000,000/=)
Hata tukisema tupeleke kiasi hicho kwa kila jimbo la uchaguzi jumla yake ni Tshs. Milioni 23 (Tshs. 23,000,000/=) kwa maana ya majimbo 213 x 100,000 = 23,000,000/=. Mhe. MBOWE anasema hizo ni pesa nyingi sana kwa uimarishaji wa chama. Mimi nasema hapana, kiwango hiki kwa kila Wilaya au Jimbo la uchaguzi ni muafaka kwani haba na haba hujaza kibaba.
Chini ya uongozi wa Mhe. MBOWE na wafuasi wake hawastaajabu kuwa kati ya Tshs. 374,144,000.40 zilizopatikana kama ruzuku katika ya Januari 1 na Juni, 30, 2008, Tshs. 350,000,000/= zilitumika Makao Makuu ya CHADEMA na Tshs. 25,000,000/= tu ndizo zilikwenda Wilayani kuimarisha chama.
Mimi naona mgao huu unayatukuza Makao Makuu ya CHADEMA isivyostahili wakati huo huo ukidhalilisha chama nchi nzima.
MADENI YA UCHAGUZI
Kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Mhe. MBOWE alitufahamisha wanachama kuwa alikuwa anakidai chama US $ 181,949.00 sawa na Tshs. 218,338,546. Mpaka sasa chama kimekwisha mlipa Tshs. 175,000,000/=
Baada ya kupata wadhifa wa Makamu Mwenyekiti, na kwa kuzingatia takwimu zionekanazo hapo juu katika kulinganisha matumizi ya fedha Wilayani na Makao Makuu niliamua kumshauri MBOWE asitishe kujilipa deni kutokana na fedha za ruzuku kwani siamini kuwa kulipa madeni yaliyopita kunaendana na utaratibu wa usimamizi wa fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa toka serikalini.
Mhe. MBOWE alichachamaa na ndipo nilipomshauri kuwa kama ni hivyo basi atuthibishie pesa hizo anazodai alikikopesha chama ziliingia kwenye akaunti gani ya CHADEMA, kupitia hundi ipi, na lini? Nilimuomba pia kutaja ni kikao gani cha chama kiliidhinisha matumizi ya fedha hizo kwani kama hakuna ushahidi wa maidhinisho, ni dhahiri kuwa matumizi hayo hayakudhibitiwa na chama na kwa mantiki hiyo kuyafanya kuwa matumizi binafsi ya Mhe. MBOWE.
Vilevile, nilimueleza kuwa matumizi ya fedha hizo alizodai alikikopesha chama yalikuwa yakinuka harufu ya UFISADI. Stakabadhi zote kuhusiana na matumizi hayo zilionesha kuwa gharama za aidha ununuzi na / au ukodishaji wa vifaa hivyo, hazikutofautiana na viwango wanavyolipishwa watalii kwa huduma kama hizo, kwa maana ya gharama ya juu sana.
Na kwa kuwa hata baada ya kuwa Mhe. MBOWE amekwisha lipwa zaidi ya nusu ya deni alilodai kuikopehsa CHADEMA, vifaa vyote yakiwemo magari, vipaza sauti na kadhalika vimebakia kuwa mali yake binafsi, basi bila kumficha nilimueleza kuwa huko ni kukinyonya chama kwa kukigeuza kitega uchumi cha watu binafsi.
Kuhusu suala la kulipa madeni kupitia ruzuku ya serikali, nilimuomba Mhe. MBOWE afuatilie kwa Msajili wa Vyama vya siasa ili tupate ufafanuzi kama kweli fedha za ruzuku ya serikali kwa vyama vya siasa, inaweza kutumika kulipia madeni ya viongozi wa vyama hivyo yatokanayo na uchaguzi ili CHADEMA isiathirike kisheria.
Niseme kweli hapa kwamba, kwa vile wanaCHADEMA wengi walinichagua kuwa Makamu Mwenyekiti, na hata mimi mwenyewe tulikuwa wagombea wa nafasi za ubunge, udiwani n.k katika uchaguzi wa mwaka 2005 ningefarijika sana iwapo na sisi tungerejeshewa angalau chochote cha kufidia gharama zetu, kwa maana kwamba kama chama kimeamua kurudisha gharama hizo kiwalipe wote badala ya kulipa madeni kwa wateule wachache.
UTEUZI WA WABUNGE WA VITI MAALUM
Naamini ukweli wa suala hili hauna mjadala. Kwamba Mhe. MBOWE na wafuasi wake walighushi orodha ya majina ya viti Maalum badala ya kupeleka yaliyopendekezwa na Kamati Kuu sio siri. Naamini hata Mhe. MBOWE anakubaliana nami kuwa suala hili si moja ya siri anazodai nimevujisha!
Yamesemwa mengi juu ya mtafaruku uliojitokeza kuhusu viti maalum hadi baadhi ya waasisi wa chama wakataka kujitoa na hivyo kumlazimisha Mwenyekiti Taifa ( FREEMN MBOWE) na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kukiomba radhi kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kwa kukiuka katiba, kanuni na maadili ya chama katika suala hili la kugushi viti maalum.
Ni ukweli ulio wazi kuwa kitendo hicho cha upendeleo bado kina iumiza taswira ya CHADEMA. Chama kinaonekana kuendekeza ujanja ujanja kiasi kwamba watu na binti zao, wakwe zao, shemeji zao, waume wenzao, wachumba wa shemeji zao, wake wenza na kwa kiwango kikubwa watu wa kabila moja ndiyo wamekuwa sura ya CHADEMA bungeni.
Katika hili nilichoweza kumueleza Mhe. MBOWE ni kuwa chaguzi mbalimbali tangu za Mitaa, Ubunge na Urais zinakaribia ni vizuri tufanye bidii kusambaza nguvu zetu nchi nzima tuwe na mtaji wa kura maeneo mengi ili kashfa kama hii isijirudie. Hii ni kwa msingi kuwa chama kikijitanua kutakuwa hakuna sababu ya kuwaona watu wa eneo fulani tu kuwa ndiyo mhimili wa CHADEMA na hivyo zikitokea fursa itakuwa rahisi chama kuwakilishwa na mtandao wake mpana badala ya koo au kabila fulani.
Sasa kwa kuwa kuimarisha chama kitaifa maana yake ni matumizi ya fedha, nalo hili likawa nongwa ingawa kwa mtazamo wa Makao Makuu kulipa madeni kwa wateule wachache si nongwa. Cha ajabu ni kwamba Mhe. MBOWE hakukana kuwa hili la viti maalum na hata upangaji wa ajira kwa ukabila una leta athari mbaya kwa mustakabali wa CHADEMA.
Katika maongezi yangu nae nilikuwa wazi nilipotahadharisha kuwa:
1. Watanzania wakiendelea kuona kwamba CHADEMA inaendeshwa kwa misingi ya kikabila hawatajiunga na chama chetu na tutakosa wafuasi.
2. Watanzania wakiona kuwa sisi tumeweka mbele ukabila kuliko utaifa hawatatupa madaraka na kutawala kwa kuhofia yale yanayotokea nchi jirani kama Rwanda, Burundi, Kenya na kadhalika ambako nafasi za raia wote zimehodhiwa na kabila moja na hatma yake watu wamechinjana kama kuku kwa kupinga hilo.
Pia nilimwambia kwamba, kwa jinsi sura ya uteuzi wa Wakurugenzi na watendaji wengine wa Makao Makuu inavyoonekana, sasa tayari chama chetu kimebatizwa jina la CHAMA CHA WACHAGA, na hii si kuwatendea haki raia wengine na makabila yao ambao wataonekana kama punguani kujihusisha na chama na ukabila.
Yote haya ninayosema kuhusu ukabila, upendeleo na kadhalika sio dhana tu. Kufuatia malalamiko mengi yaliyokuwa yakisikika nchi nzima kuhusu masuala haya, Kamati Kuu ya CHADEMA ilikwisha unda Tume kutafuta ukweli wa mambo hayo. Tume hiyo ya watu watano iliongozwa na Mhe. Merky Lugendo Mziray ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA nayo imekwisha toa taarifa yake kwamba Makao Makuu ya CHADEMA yanatawaliwa na ubaguzi wa kikabila, kidini na kielimu.
UTENDAJI WA KIBABE
CHADEMA ni chama kilicho njia panda kwa sasa kutokana na utendaji wa kibabe wa Mhe. MBOWE. Ninafahamu jinsi vyama vingine vya upinzani hapa nchini kama vile NCCR Mageuzi vilivyoporomoka haraka haraka mithili ya nyumba ya mabua. Chama NCCR Mageuzi kilifikia mahali pazuri tu hadi watu wakaanza kufikiria kuwa kingekuwa chama mbadala kwa CCM. kwa bahati mbaya uchu wa madaraka, ulafi wa ruzuku, na tabia za kimangimeza kwa pamoja vikakiathiri hadi kupoteza umaarufu wake.
Na hata vyama vingine vya upinzani vina dalili hizo hizo japo kwa viwango vinavyotofautiana. Ila badala ya kujichunguza na kujua kasoro zetu, kila siku vyama vyetu, vimekuwa vikidai kuwa ni chama tawala ndicho kinachoviroga, kama ambavyo Mhe. MBOWE ameanza kuweweseka kupitia vyombo vya habari.
Napenda kuthibitisha kuwa katika mgogoro unaopaliliwa sasa na Mhe. MBOWE ndani ya CHADEMA kutokana na ufisadi, ufuska, ulevi wa madaraka na umangimeza chanzo chake ni tabia yake ya kuendesha chama kibabe. Mathalan kumzuia Martin Mungongo Mkurugenzi aliyechaguliwa kwa kura kutofanya kazi zake ndani ya chama, madai ya kupigana na watendaji wa chama ndani ya baa na vitendo vingine vya aina hiyo ni ushahidi tosha wa hulka hii. Hadi sasa Mhe. MBOWE amefanikiwa kukizuia chama hiki kisifanye kazi ya siasa mkoa wa Dar es salaam kwa miaka minne.
Ninavyoongea hivi sasa CHADEMA imekuwa ikikimbia vikao vya Democratic Union of Afrika (DUA), Muungano wa Vyama Vya Upinzani, uliofanikisha CHADEMA kujuana na Conservative Party ya Uingereza na Republican ya Marekani. Vyama dada hivi vyote vinaulalamikia uongozi wa CHADEMA kwa kufuja fedha ya misaada na kuwasilisha kwao risiti za kugushi, kama ilivyofanyiwa Conservative Party baada ya kutoa msaada wa Tshs. 78,000,000 kwa ajili ya ununuzi wa baiskeli na pikipiki ambazo hazikununuliwa.
Katika mkutano wa Kamati Kuu ya CHADEMA huko Dodoma hivi majuzi tu, Mhe. MBOWE kwa kauli yake aliwatisha wajumbe kuwa alikuwa amethibiti uwezekano wowote wa wajumbe kujisikia huru kwa kutoa mawazo ambayo yangepingana na ajenda yake aliyoitoa ghafla kikaoni kunisimamisha Umakamu Mwenyekiti.
Mhe. MBOWE Alikifahamisha kikao kuwa alitoa taarifa kwa IGP, SAID MWEMA kuwa kuna wahuni ambao walitaka kuuchafua mkutano wake, naye IGP akahakikisha kuwa mkutano ule unalindwa kwa kiwango cha kushtua kama ambavyo hata vyombo vya habari vimethibitisha.
Hayo ni baadhi tu ya mambo yanayobainisha Mhe. MBOWE ni kiongozi wa aina gani.
HITIMISHO
Kama nilivyokwisha sema hapo awali, sijaacha na sintoacha ajenda yangu ya kufufua uhai wa CHADEMA kwani ndiyo ahadi iliyofanikisha kuchaguliwa kwangu kuwa Makamu Mwenyekiti Taifa. Nilipopata wadhifa huo nilianza kuitekeleza ajenda hiyo kupitia mahojiano na Mwenyekiti MBOWE kuhusu matumizi ya ruzuku, madeni ya uchaguzi, uteuzi wa wabunge wa viti maalum, nafasi za ajira Makao Makuu, na kuhusu mwenendo wa chama Mkoa wa Dar es salaam.
Nilijikuta katika mvutano mkubwa kila nilipogusa eneo lolote katika haya. Nakiri kuwa kwa kiwango kikubwa sikuwa na uwezo wa kubadili mambo hayo yaliyokuwa yakiratibiwa kwa ukaribu na Mhe. MBOWE na wafuasi wake kwani sikupewa ushirikiano wa aina yoyote na chama pale Makao Makuu. Ni vigumu kuamini, lakini ni kweli kuwa sikuwa na ofisi Makao Makuu, sikupewa vitendea kazi kama magari, vipaza sauti na/au vyombo vya habari, na sikuwahi kupata taarifa yoyote ya kiutendaji toka Makao Makuu.
Kwa kuzingatia yote hayo, naomba nichukue fursa hii kuwashukuru kwa dhati wanachama wa CHADEMA mkoa wa Dar es salaam ambao kwa pamoja tulisimama kidete kufufua uhai wa chama hapa jijini. Niseme tu ushirikiano wao wa hali na mali uliniwezesha kushughulikia masuala muhimu ya kitaifa na kimataifa.
Rai yangu kwa wana CHADEMA na wale wote wanaokitakia mema chama chetu na nchi yetu kwa ujumla ni kwamba kazi ya kupigania demokrasia ya kweli ndani na nje ya chama, kukiepusha chama na vitendo vya ukabila, migogoro, ubadhirifu, umangimeza, ufisadi na ubaguzi wa aina yoyote bado inaendelea na nawaombeni mniunge mkono kwa hali na mali katika vita hii. Naamini tutashinda.
Mungu Ibariki CHADEMA
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika
Nimeusoma waraka huu hauna tofauti na ule ambao uliandikwa katika gazeti la Mwananchi ukidaiwa kusambazwa na CCM, na nikinukuu habari hiyo. ulianza kusambazwa Julai 27, 2008 na CCM kwa kutumwa Fax toka ofisi ya makamba kwenda Dar ofisi moja ya SGMA ICT.
Je, makamba alikuwa ameupata wapi siku moja kabla ya kusomwa na Wangwe mwenyewe na kama ndivyo je alikuwa akimtumia nani na kwa faida gani?
====Chacha Wangwe amekufa lakini waraka wake huu utawasaidia WanaCHADEMA na watanzania kuelewa ukweli wa mambo aliyokusudia.
Jmush1,
Hili liinchi bora tuliuze tugawane, haiwezekani mtu maka Gembe atuambie hivi mara vile sasa sisi tushike wapi jamani?
Cha muhimu ni kwa wazalendo kuwaelewesha wananchi kuwa kwenye issue hii kuna siasa na maslahi ya Taifa...Hivyo Isaya Mwita huna haja ya kuishiwa na nguvu sasa...Badala yake pigeni moyo konde na muwaeleze wananchi ukweli kuwa tishio la Wangwe halikuwa waraka wa kisiasa kwa chadema...Bali kilio cha hoja yake....Kilio kilichoonyeshwa wazi na spika kwa niaba ya wazalendo...Kilio hicho...Si kilio cha kisiasa kwani hoja ya msingi aliyoiwakilisha marehemu inapoelekea kutaka kuuwawa kwa kigezo cha kifo cha mtoa hoja ni jambo la kisikitisha.
Kama kweli ccm mafisadi hawachezi na usalama wa Taifa...Basi waache mchezo mchafu mara moja na wahakikishe siasa haitumiwi kuligawa Taifa na kusababisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Ninapomaliza kuisoma thread hii nashindwa kabisa kujizuia kuamini kwamba haya si maneno ya marehemu, sioni kwanini mtu mwingine ambaye si marehemu apoteze muda wake kuandika yote haya huku akijidai yeye ndiye Wangwe? Motive behind? Hata hivyo sidhani kama chama chochote kilicho serious na mambo yake kingekimbilia kutaka kujua aliyeyaandika haya badala ya kujibu hoja zilizotolewa, hata kama hoja hizi zingekuwa zimetolewa anonymously bado ingekuwa ni muhimu kwa chama kurespond. Shame Chacha died before all these became public........na hapa ndio utaamini kuwa marehemu hana haki, I can bet everything here will be vehemently denied bse there is no one to hit back, sioni hata mantiki ya huu mjadala kuendelea.