CHADEMA Lake Zone imepotezwa na Uteuzi wa Dkt. Doto Biteko

CHADEMA Lake Zone imepotezwa na Uteuzi wa Dkt. Doto Biteko

busar

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2011
Posts
1,071
Reaction score
1,067
Asalam,
Siasa ni kazi inayohitaji ustadi mkubwa na tafiti nyingi ikiwemo kuzijua hisia za wananchi. Hizi kanuni muhimu sana

1. Kwenye Siasa nenda na agenda za wananchi (Nyerere J.K)
2. Kwenye Ongea lugha ya wananchi, usiongee lugha wanayoelewa, ongea lugha yao.

Kwa kanda ya ziwa CHADEMA wamefeli pakubwa. Kanda ya Ziwa kwa sehemu kubwa imerudi CCM kihamasa baada ya uteuzi huu wa juzi.

Makosa makubwa matatu ya CHADEMA wanayoendelea kuyafanya
1. Chama kimekaa, wakaamua kwenye vikao vyao kuwa waende wakahubiri Katiba mpya. Je ni suala la watanzani 60?
2. Kukosa consistency na political brain. TL anaenda Usukumani kumtukana Mtoto Pendwa Magufuli nyumbani kwao. Anatarajia nini ?
Hoja ya Bandari imeshindwa kujengwa vyema na political parties.

3. Chadema haina kundi die hard. Inataka kuwa kama CCM.

CHADEMA MSIPOBADILIKA MMEKWISHA
 
CCM na mentality yao ya "Silver Bullet" dhidi ya Wapinzani hahaha.. wakati wa Jiwe silver bullet ilikuwa ni kuwanunua Wapinzani woote ikashindikana.

Huwezi kumleta Dotto Biteko huku unapuuza ripoti ya CAG ya wizi wa matrioni ya fedha za Wananchi.
 
Kwamba Biteko ameongeza bei ya pamba au ameshusha bei ya bidhaa? hizi propaganda mnazoandika kwenye simu zenu na kupost hapa jf ni tofauti kabisa na hali ilivyo mtaani, njoo hapa mwandoya ujionee halisi na huyo Biteko hata watu hawamjui anafahamika tu maeneo ya Bukombe.
 
Kwanini Mbowe haachi kumtukana JPM ? Bora kuhadaiwa Dotto kuliko kuhadaiwa na Mbowe
Alimuachia kovu la kudumu.
Kumbomolea bilicana yake,kuharibu shamba lake la maua,kuharibu Mali,kumpa kesi feki ya ugaidi
 
Back
Top Bottom