Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mahakama ya Rufaa inatarajiwa kusoma uamuzi wa kesi ya Saidi Issa Mohamed dhidi ya CHADEMA leo Aprili 15, 2026. Chama kimesema kimepokea taarifa hiyo kutoka mahakamani na kuahidi kuujulisha umma kuhusu matokeo ya uamuzi huo mara tu utakapotolewa.
Kesi hii inahusiana na mgawanyo wa mali na rasilimali za chama (Na. 8323/2025), ambapo kuna madai ya kutokuwepo kwa usawa kati ya Bara na Zanzibar. Licha ya mapingamizi ya chama, Mahakama imeruhusu shauri hilo kuendelea huku viongozi mbalimbali, akiwemo Tundu Lissu, wakihusishwa katika hatua za kisheria zinazoendelea.
===
Chama kimepokea taarifa kutoka Mahakama ya Rufaa, Dodoma, kuhusu kesi ya Saidi Issa Mohamed dhidi ya Chadema kuwa Mahakama hiyo inatarajiwa kusoma uamuzi wake leo.
Chama kitauarifu umma wa Watanzania kuhusu uamuzi wa mahakama mara tu utakapokuwa umetolewa
View attachment 3573010
Uko sahihiHii taarifa itakuwa Chadema wameipata ghafla toka mahakamani, mahakama siku hizi zinatoa maamuzi kwa kuvizia.
Mbona ghafla na bila taarifa. Ukiona hivi ujue ni Nganda 6 kama alivyosema Rugemeleza Nshala .Mahakama ya Rufaa inatarajiwa kusoma uamuzi wa kesi ya Saidi Issa Mohamed dhidi ya CHADEMA leo Aprili 15, 2026. Chama kimesema kimepokea taarifa hiyo kutoka mahakamani na kuahidi kuujulisha umma kuhusu matokeo ya uamuzi huo mara tu utakapotolewa.
Kesi hii inahusiana na mgawanyo wa mali na rasilimali za chama (Na. 8323/2025), ambapo kuna madai ya kutokuwepo kwa usawa kati ya Bara na Zanzibar. Licha ya mapingamizi ya chama, Mahakama imeruhusu shauri hilo kuendelea huku viongozi mbalimbali, akiwemo Tundu Lissu, wakihusishwa katika hatua za kisheria zinazoendelea.
===
Chama kimepokea taarifa kutoka Mahakama ya Rufaa, Dodoma, kuhusu kesi ya Saidi Issa Mohamed dhidi ya Chadema kuwa Mahakama hiyo inatarajiwa kusoma uamuzi wake leo.
Chama kitauarifu umma wa Watanzania kuhusu uamuzi wa mahakama mara tu utakapokuwa umetolewa
View attachment 3573010
TumekusikiaChadema ije na uzi mmoja wa hiyo kesi, ili tufuatilie ilianzia wapi, ikaweje mpaka hukumu yake. CHADEMA wakusanye mwenendo wa hiyo kesi, iwekwe kwenye uzi mmoja, watu tufuatilie.
Chadema wasikubali kesi zao ziwe za kuvizia vizia, waanike mwenendo wa kesi hizi mitandanoni.
Itakuwa hukumu ya ajabu kuwahi kutolewa. Maelekezo tupuUamuzi utakuwa maelekezo
Hivi majaji walikuwa akina naniUko sahihi
Tutawaanika hapa woteHivi majaji walikuwa akina nani
Kifupi wamemkimbia Tundu Lissu... Angewachachafya vibaya sana!Uamuzi utakuwa maelekezo