CHADEMA
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 490
- 2,471
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA
Chama ch ma Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesikitishwa na kupokea kwa tahadhari kubwa matukio yanayotishia uvunjifu wa haki na uhuru nchini, kuhatarisha amani ya nchi na hata kuwa dalili zingine za wazi za kuharibu na kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020 na hivyo kinazitaka mamlaka zinazohusika kuchukua hatua za haraka kuzuia vitendo hivyo.
Kitendo cha Jeshi la Polisi Wilayani Kahama kuvamia msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu na kuwashambulia kwa silaha za moto wananchi waliokuwa wakitembea kwa amani kumsindikiza Mhe. Lissu kwenda hotelini na kuwatishia waandishi wa habari, ni mwendelezo wa vitendo vya jeshi hilo kukiuka Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na taratibu zingine za kisheria nchini.
Aidha, tukio la watu ambao hawajakamatwa, waliokuwa na silaha, kuwavamia Mgombea Ubunge wa Chadema, Jimbo la Chato na Katibu wa Chadema katika eneo hilo, kisha wakafanya uharibifu mkubwa wa mali na kutishia usalama wa viongozi hao, ni mwendelezo wa matukio dhidi ya Chadema na viongozi wake maeneo mbalimbali nchi nzima ambayo hakuna hatua zozote za kisheria zimechukuliwa.
Tukio hilo la kuvamia viongozi wa Chadema Jimbo la Chato usiku wa kuamkia leo, linafanana kwa namna moja ama nyingine na lile la kuvamiwa na kuchomwa moto kwa Ofisi ya Chadema Kanda ya Kaskazini, jijini Arusha. Matukio yote yamefanyika muda mfupi kabla Mgombea Urais wa Chadema Mhe. Lissu hajafika maeneo hayo kwa ajili ya vikao na mikutano inayohusu shughuli za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Chadema inayachukulia matukio yote hayo mawili yaliyotokea Kahama na Chato kuwa na tishio kwa usalama wa Mgombea Urais Mhe. Lissu na mwendelezo wa dalili za wazi za kuvuruga na kuharibu Uchaguzi Mkuu.
Pamoja na kulaani vikali matendo hayo yanayokiuka Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na taratibu zingine za kisheria za nchi yetu, Chadema inazitaka mamlaka zinazohusika ikiwemo NEC na Jeshi la Polisi kuchukua hatua za haraka kuzuia uhalifu huo unaovunja haki na kutishia amani wakati huu wa kampeni za Uchaguzi Mkuu. Kunyamazia vitendo hivyo itatafsiriwa kuwa vinafanyika kwa baraka za vyombo vyenye mamlaka ya kuzuia visitokee.
Imetolewa leo Jumanne Oktoba 13, 2020 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano