Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Niko Mbeya Mjini kwa siku tatu hivi na nimeona upepo wa siasa za hapa. Siko upande wa CCM wala CDM. Nawashauri tu CDM kuwa wana nafasi kubwa ya kushinda Jimbo la Mbeya Mjini iwapo wataweka mgombea mwingine nje ya Joseph Mbilinyi aka Sugu. Kuna sababu tatu :-
1. Mbunge aliyekaa kwenye jimbo zaidi ya kipindi kimoja mara nyingi wapiga kura humchoka, wanataka ingizo jipya
2. Watu wengi wanadai Sugu HAKUFANYA lolote kwenye miaka 10 aliyokuwa Mbunge zaidi ya kujenga hoteli yake
3. Wengine wanaona hana uwezo kwa vile kisomo chake kidogo na ana pata umaarufu kwa sababu za kisela tu
NB:
CHADEMA kwa ujumla ina nafasi kubwa ya kushinda Jimbo la Mbeya Mjini kwa kuwa Mbunge wa CCM aliyepo sasa hivi licha ya kuwa Spika lakini hakubaliki sana kwa sehemu kubwa ya Mbeya. Anakubalika kata zilizopo Uyole za Itezi, Iduda, Igawilo tu. Anaonekana ni Mbunge aliyeletwa na Mwendazake lakini siyo kwa kura za wana Mbeya.
Pili Tulia achafuka sana kwa namna alivyoshughulikia suala la Bandari kwa DP WORLD na suala la Luaga Mpina kuhusu sukari.
KIUJUMLA kama kungekuwa na DEMOKRASIA ya kweli kwenye vyama vyote CHADEMA na CCM, hawa Watajwa wote wawili HAWAFAI kuchaguliwa kugombea viti vya ubunge wa Mbeya Mjini