CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike

Umeongea point moja ya msingi sana leo.
 
Ukihama chama kwa sababu ya flaiova, reli ya SG, Bombadia, barabara na vingine ambavyo ni wajibu wa serikali kuvitekeleza, basi wewe ni mjinga na hutambui haki zao za uraia pia hujui wajibu wa serikali yako. Wajibu wa upinzani ni kuisimamia serikali itekeleze mambo yake kwa mujibu wa katiba ya nchi.
 
Kama ccm wako vizuri waache vyama vyote viwe huru kufanya siasa! Waache Polisi ifanye Kazi yake, waache wakosoane kwa hoja! Nadhani mbowe wameshindwa kumhonga ili aharibu Chama kama alivyofanya Lipumba! Kusema hawezi kushinda siasa huwa zinabaridirika kama hali ya mgonjwa!!
 
Uko sahihi Petro.Tatzo kundi la Lowasa.Linawapa wakati mgumu sana CHADEMA
Wamlazimishe tu mzee kustaafu.La sivyo hawataweza kujirekebisha
 
siasa za kinafiki pia zinafanyika
 
Maelezo yako yoote ni mazuri saana kaka ila swali moja hivi uliwahi achwa na demu au mwananke? kama jibu ni ndio sababu ya msingi ilikuwa ni ipi? sio lazima unijibu lakini wengi wao huwa ni tamaa kwani wanaume wengi karibia woote tunafanana katika swala la vijitabia na matendo yetu tunatofautiana tu kwenye swala la uwekezaji yaani mali na kujikimu...na ndio maana unaona pamoja na clip zote za uzinzi zinazorushwa mtandaoni kwa sasa za wakili yule maarufu wa Arusha...bado mke wake hajaondoka mpaka sasa na haondoki ile angekuwa mke wa Mayala aone hiyo video sasa hivi ungekuwa Bachelor kama Gardner!
 
Tatizo la siasa zetu ni la "Zidumu Fikra za Mwenyekiti" na siyo "Zidumu Fikra Sahihi za Mwenyekiti"

Ninaamini kimoyo moyo wafuasi wa CDM wanakubali kwamba Lowassa ndiye chanzo cha sisi kama chama kupoteza dira, hatuna sera tena, ila hawawezi kulisema kwa sauti kwa sababu ni kosa kupinga maamuzi ya Mwenyekiti hata kama hayako sahihi.
 
Mayalla ni Njaa, kweli wee una njaa, hoja ni nini hasa, Kafulila anachekesha, aliwataja mafisafi wakati ufisadi aliouibu yeye, wakamwita Tumbili, na waliomwita tumbili bado wapo CCM hahahahaaaaaaaaaa. Hoja ya Kafulila ni Upinzani hawapambani na Rushwa, atwambie Pesa za Epa upinzania ndio ulisema Sio za umma? au CCM, na lile sakata lilisababisha aitwe Tumbili liliishaje? Juzi tu hapa alisema Tanesco bado wanawalipa wale jaama,

yaaaani simwelewi kabisa mayalla kusema wanaohama wana hoja, pamoja na Kafulila.
 
Umetoa maoni mazuri sana Paskali.Very constructive
 
kama kawaida yenu.Mnampuuza Paskali.Hamuangalii hoja zake.Please someni.Inawezekana hata hujasoma alichoandika
 

Paskali, niliwahi kuwakumbusha viongizi wa CHADEMA
Niwakumbushe viongozi wa CHADEMA
CHADEMA inaamini nini kwa sasa? lakini wao wamebaki kuwa SIKIO LA KUFA.
 
Huna lolote wewe.
Ni bora mtu Uwe moto au baridi kuliko kuwa VUGUVUGU kama ulivyo wewe.
 
Mkuu u are absolutely correct especially kwenye Way Forward kwa CDM.. Hapo hujaacha kitu kabisa Mkuu.. Bandiko Zuri Sana..
Salute sana Kaka.
 
Paskali, ni bahati mbaya sana umeichepusha hoja yako. Kwamba inawezekana nia yako ilikuwa kuweka ukosoaji wako binafsi kwa Chadema lakini ukaamua kutumia watu wanaohama, bahati mbaya ukashindwa kuonyesha hoja za wanaohama ili kuthibitisha wito wako wa kukitaka Chadema kijitafakari. Labda, ili uturudishe kwenye hoja yako, hebu tueleze sababu za kiongozi mmoja wa Chadema alizozitumia kuhama tuone sasa katika mjadala huu, kama Chadema wanaweza kuzitumia kujitafakari.
 

Umenena mkuu, na ndio maana mimi katika vitu navyofurahi ni kuona watu kama akina Masha wanaondoka...siku Lowasa na Sumaye wakiondoka Chadema nitafurahi sana...tubaki na Chadema yetu asili. Hawa watu wamekuwa mzigo sana, si kwa chama tu, ila hata kwa Taifa. Ingekuwa uamuzi wangu hata Nyalandu Lazaro hakufaa kupokelewa kama mwanachama wa CHADEMA kwa sasa.
 
Hivi ni kweli Chadema wanapinga kila kitu? Au ni uzembe wetu wa kuelewa hoja na kuwa na matamanio ya kusikia tunachokipenda?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…