Kaka
Pascal Mayalla, nakubaliana na hoja yako. Lakini, ugonjwa mkubwa uliobaki na kuwasumbua CHADEMA ni kuwepo kwa Lowassa na kundi lake. Kundi la Lowassa likiondoka kwa kuhamia chama kingine au kuanzisha chama chao, CHADEMA itarejea kwenye njia yake. Hakika, uwepo wa Lowassa na kundi lake ni jambo gumu sana kwa CHADEMA kwakuwa inakuwa na muda mwingi wa kujibu tuhuma kuliko kujijenga.
Petro E. Mselewa, na mimi nakubaliana na wewe kwamba Team Lowassa ndiyo inayousumbua uongozi wa CHADEMA, na ndio walio wengi hata humu JF. Lugha yao ni moja tu ya kupinga kila kitu kwa kebehi, dharau, lawama, lialia, uzushi, nk kwa kila aina ya lugha chafu.
Viongozi wa CHADEMA Team Lowassa, watambue kuwa Lowassa aliwaandaa angie Ikulu kwa kutumia migongo yao, kupitia tikiti ya CCM, kwa kuwa alikuwa amejekwisha jenga mizizi na mtandao wa ufisadi. CCM ililiona hilo, ikamkata na genge lake.
Viongozi wa CHADEMA Asilia wanalijua hilo ila walimpokea Lowassa kama mtaji wao kisiasa. Na hakika wamevuna siyo tu majimbo zaidi bungeni, pia wanaongoza halmashauri kubwa nchini.
Tofauti ya makundi haya mawili unaonekana sasa kwa jinsi ya utendaji wa Serikali ya CCM inayongozwa na Rais Magufuli, akitambua kuwa nguvu yake ni Watanzania wenyewe. Inapambana na kundi/genge la mafisadi chini ya Lowassa, na wakati ule ule ikiendesha mabadiliko ya kiuchumi, moja ya agenda kuu za CHADEMA asilia.
Team Lowassa, wengi humu, kila lifanyalwo na Magufuli kwao ni mwimba. Wanasahau kuwa matatizo anayopambana nayo Rais Magufuli mengi yamefanyika wakati wa awamu zilizopita, ambazo Sumaye na Lowassa walikuwa Mawaziri Wakuu. Baadhi ya matatizo hayo:
1) Kesi za kimataifa, ambazo leo zinapelekea mali za Taifa kukamatwa.
2) Mikataba mibovu ya usimamizi wa maliasili ya nchi.
3) Ukwepaji kodi na matumizi mabaya na mali ya umma.
4) Urasmu na uzembe Serikalini na Taasisi zake
5) Na mengine mengineyo anayopambana nayo.
Kila lililo na mwanzo lina mwisho. CHADEMA Asilia wakati ndio huu, ngoeni mizizi yote ya Team Lowassa!
nk: Vijana Mnyika, Lissu, na Msigwa unganeni na wazee akina Mwesigwa na Safari kwa kazi hiyo ya kuleta mabadiliko ndani ya CHADEMA au kuiondoa Team Lowassa. Tayari Katambi na Kafulila wameungana na Mkumbo kuonesha mlango, japo walipaswa kufanya mageuzi ndani. Tatizo alikimbiwi ila hukabiliwa. Tatizo lichukuliwe kama changamoto, mwishowe ni fursa ya mabadiliko.