CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike

Huyu ndio mwiba wa FISIEM[emoji196] wanaomba leo kesho adondoke
hahahaha.eti mwiba.mwiba kivipi? ana kipi kipya? amechafua CHADEMA hadi sasa haieleweki
alafu aliwaambia eti mpige kura yeye atazilinda..Hhahaha..what happened?
This guy is just overrated.Na hio overrating ndio iliwachanganya chadema hadi kupokea zigo la mavi
 
Biashara zinaendelea mkuu.... binafsi kosa walilofanya ni pale ambapo wanapinga Udikteta alafu wanafuta.... msimamo hamna..... katiba inavunjwa wanalalamika alafu wakakaa kimya...... kura zinaibiwa hata wakishinda hawatangazwi(Wenyeviti huko Arusha?)wanabaki kulalamika .Ila kamati kuu ikae chini ijitathmini kuna shida sehemu.
 


My brother Paskali, nikuombe kwa muda wa siku chache ujaribu kufanya jambo hili nitakalokuomba kama your young sister who is learning something from you. Can you stretch your mind and allow something new to get in? In the Bible there is a very powerful verse which says it is impossible the old wine skin to hold new wine. Viriba vya zamani haviwezi kutunza divai mpya. Sasa fanya utafiti mfupi wa kutathimini kama wale viongozi wote wanaohamia ccm kutoka upinzani, kuwa wamepata hisia na mapenzi halisi ya kuipenda ccm au what is behind the scene. Ukifanya hivyo my brother come here with a new thread please. But this is my precaution don't try to fight against the truth
 
Mayalla wewe mkabila watu wananunuliwa kipi cha maana alichofanya mkabila mwenzio mbaka mtu avutike huyu ni rais wa hovyo tangu kupata uhuru
 
Tatizo kubwa ni kuwafunga mdomo CHADEMA kuzungumzia na kukemea ufisadi. Sasa CCM inajifanya ndiyo inayopambana na ufisadi kutokana na CHADEMA kuzibwa mdomo.

Wakili unatia aibu,hivi unaweza kuainisha ni wapi chadema wameshindwa kuzungumzia ufisadi au rushwa ? ule ushaidi aliotoa nassari wa mkuu wa wilaya anahonga madiwani autoshi kuonyesha cdm inapambana na rushwa ? arafu hyo hyo mkuu wa wilaya ndio anapandishwa cheo arafu unasema ccm ndio inajipambambanua kupambana na ufisadi,mbona unasiasa za kitoto sana,kama humpendi lowasa useme tu na sio kusingizia mambo mengine
 
Hakuna kitu ni njaa tu Kama jina lako hivi ccm inapinga ufisadi upi chenge anadunda tu ngeleja na Wengine wengi mkuu wa wilaya kutoa rushwa na kununua madiwani anapandishwa cheo kuna dhamira ya kupinga ufisadi Ama maigizo tu kuchota watu wenye narrow mind hawawezi kureason? ccm hii ambayo haki yake Kuishi Siyo kipaumbele kila Mara miili kibao inaokotwa coco beach mpaka sasa hatujaambiwa ni police ni kina Nani wala waziri wa mambo ya ndani bado watu wanarudi ccm badala ya kumrudia Mungu mnachekesha waliokufa ccm ipi inaonea wafanyakazi kuhusu mafao yao wakistaafu wapewe 40% nyingne wachukuwe kidogo mpaka watakapo kufa ndo hii ccm ya kurudi kweli mayala ninahoja kibao za kukubishia na kukuthibitishia kuwa Hakuna sababu ya kurudi ccm badala ya kumrudia Mungu
 
Paskali, Ushauri wako mzuri sana. Ni vizuri kuvikosoa vyama ili vijirekebishe na kusahihisha mapungufu yake. Shida tu ni kwamba hii Chadema tunayoikosoa sasa iko strangled. Ni sawa na mzazi kumfungia jiwe zito mtoto wa miezi 8 anayejifunza kutambaa, na kisha akaendelea kulalamika kwa nini mtoto huyo hatambai!
 
And njaa Huyo jamaa Kama chadema Hakina hoja kwa nini hujuma zinaendelea kwa nguvu mpaka watu kupigwa risasi wansheria wanavamiwa Lakini mamlaka Kimya ila Najua unatafuta vyeo utapata kutokana na jina lako
 
Paskali, niliwahi kuwakumbusha viongizi wa CHADEMA
Niwakumbushe viongozi wa CHADEMA
CHADEMA inaamini nini kwa sasa? lakini wao wamebaki kuwa SIKIO LA KUFA.

Chama cha siasa akiwez kuwa na agenda moja miaka nenda miaka rudi.sasa kama wewe hujui chadema inaamini nini unafanya nini katika huu uzi ? Paskali na nyie watu mmekaa mbele ya komputa kukisema chama cha siasa ambacho wamezuiwa kufanya siasa,wanachaguliwa maneno ya kuongea na kutwa wanakamtwa na polisi ila bado wanapambana, lakin nyie hata kwenye mtaa wenu hamjaweza kufanya mabadiliko kutwa huku kuisema chadema ambayo kila uchaguzi inaongezeka.kama kweli unaitakia mema hii nchi iambie serikali iruhusu demokrasia na ijiendeshe kwa uwazi tuone survival ya CCM kwenye politics
 
Msingi wa Chadema ulijengwa katika ukanda na ukabila kama ambavyo msingi wa Cuf ulivyojengwa katika udini na Upemba kwa maana hiyo vyama hivi lazima vitajimaliza vyenyewe na kamwe wasiisingizie CCM!!
CHADEMA haina ukanda wala udini; Mwenyekiti Taifa ni Mkristo; wenyeviti wenza Safari na Mohammed waislam. Katibu Mkristo ila Naibu Zanzibar Mwislam. Waasisi wa chama Bob Makani na ndiye Katibu Mkuu wa Kwanza alikuwa Mwislam na Msukuma wa Shinyanga; Makamu Mwenyekiti wa kwanza Ngwilupipi Mnyakyusa wa Mbeya. Huo Ukanda unaosema uko wapi? Rudi ukasome usikurupuke mkuu. Mawazo ya Mayalla yako poa ila wewe umekurupuka huijui historia ya chama.
 
Umenena Mkuu! Mijitu mingine humu michawi tu hata haisomi alama za nyakati. Kama CHADEMA inakufa wasitumie mabavu wauone moto wake!
 

Petro E. Mselewa, na mimi nakubaliana na wewe kwamba Team Lowassa ndiyo inayousumbua uongozi wa CHADEMA, na ndio walio wengi hata humu JF. Lugha yao ni moja tu ya kupinga kila kitu kwa kebehi, dharau, lawama, lialia, uzushi, nk kwa kila aina ya lugha chafu.

Viongozi wa CHADEMA Team Lowassa, watambue kuwa Lowassa aliwaandaa angie Ikulu kwa kutumia migongo yao, kupitia tikiti ya CCM, kwa kuwa alikuwa amejekwisha jenga mizizi na mtandao wa ufisadi. CCM ililiona hilo, ikamkata na genge lake.

Viongozi wa CHADEMA Asilia wanalijua hilo ila walimpokea Lowassa kama mtaji wao kisiasa. Na hakika wamevuna siyo tu majimbo zaidi bungeni, pia wanaongoza halmashauri kubwa nchini.

Tofauti ya makundi haya mawili unaonekana sasa kwa jinsi ya utendaji wa Serikali ya CCM inayongozwa na Rais Magufuli, akitambua kuwa nguvu yake ni Watanzania wenyewe. Inapambana na kundi/genge la mafisadi chini ya Lowassa, na wakati ule ule ikiendesha mabadiliko ya kiuchumi, moja ya agenda kuu za CHADEMA asilia.

Team Lowassa, wengi humu, kila lifanyalwo na Magufuli kwao ni mwimba. Wanasahau kuwa matatizo anayopambana nayo Rais Magufuli mengi yamefanyika wakati wa awamu zilizopita, ambazo Sumaye na Lowassa walikuwa Mawaziri Wakuu. Baadhi ya matatizo hayo:
1) Kesi za kimataifa, ambazo leo zinapelekea mali za Taifa kukamatwa.
2) Mikataba mibovu ya usimamizi wa maliasili ya nchi.
3) Ukwepaji kodi na matumizi mabaya na mali ya umma.
4) Urasmu na uzembe Serikalini na Taasisi zake
5) Na mengine mengineyo anayopambana nayo.

Kila lililo na mwanzo lina mwisho. CHADEMA Asilia wakati ndio huu, ngoeni mizizi yote ya Team Lowassa!

nk: Vijana Mnyika, Lissu, na Msigwa unganeni na wazee akina Mwesigwa na Safari kwa kazi hiyo ya kuleta mabadiliko ndani ya CHADEMA au kuiondoa Team Lowassa. Tayari Katambi na Kafulila wameungana na Mkumbo kuonesha mlango, japo walipaswa kufanya mageuzi ndani. Tatizo alikimbiwi ila hukabiliwa. Tatizo lichukuliwe kama changamoto, mwishowe ni fursa ya mabadiliko.
 
Kwa uhandishi huu mkuu paskali wewe ndio unatakiwa uwe mwenyekiti wa chadema na mkuu wa mikakati,kwa kusema angalia nitakavyooga matusi na kejeli!
 

Inamaana hujui nanii aliyepelekea tukapata kesi za kimataifa ? au unaandika tu
 
Ujinga wenu ndio huu.. Sasa kama ccm inadunda na mafisadi ndio na ninyi makae nae huko?
 
Tutajie listi ya viongozi wa juu wa chadema na sehemu wanazotoka
 
Historia yako haijakamilika siwaoni Mtei, Shanga, Ndesamburo na mke wa Bob Makani, lakini najua umewaacha kwa makusudi ili kuwahadaa wasioijua Chadema! Lyatonga alipotoka CCM alikataa kuingia Chadema akidai " anaukwepa" ukabila akaenda chama cha kitaifa NCCR mageuzi!
 

1. Siamini kama wanachama wakiamua kuhama chama cha siasa na kujiunga na chama kingine ni lazima kwenye chama wanachohama kunakuwa kumefanyika makosa. Actually, wakati mwingine wanaohama wanaweza pia wakawa na sababu zao na wanaweza kusema sababu ni x, y na z, lakini je ni kweli ndizo sababu "hasa" zilizowafanya wahame au kuna pia sababu zingine ambazo hazitajwa hadharani - mfano kuahidiwa greener pastures kwenye chama kingine au kupata protection ya kutosha? Nakumbuka kuna mwanaCCM mmoja aliyehamia Chadema na wakati akiwa Chadema alikuwa akiikosoa serikali na kwa kutumia uzoefu wake serikalini, alikuwa akisema anajua mambo mengi. Alipoamua kurudi CCM, moja ya mambo aliyoyataja ni kuikosoa serikali kwamba si sahihi (jinsi nilivyomwelewa).

2. Kwa upande wangu, kwenye ushindani kila mtu anatumia mbinu mbalimbali na kwa bahati mbaya vyama vya upinzani kwa sasa vina mtihani mgumu kwa upande wa kujinadi na kupata wanachama wapya na hili si kosa la vyama hivi hata kidogo (maana liko nje ya matakwa yao). Na hili pia lina matokeo hasi kwa vyama vya upinzani. Hivyo, kwa baadhi ya mambo yanayotokea hatuwezi kusema vyama vya upinzani vimekosea. Inabidi pia tuone sehemu ambayo imekuwa kikwazo kikubwa kwa afya ya vyama vya upinzani na tuseme kwamba hali hii inaathiri ustawi wa vyama hivi ingawa kinachofanyika si kwa matakwa yao.

3. Na tusipokuwa na vyama vya siasa vyenye ushindani ili kuikosoa serikali na kuifanya iwajibike vizuri zaidi kwa wananchi, ina maana waathirika ni sisi wenyewe. Hivyo, mtu anayefurahia kufa kwa vyama vya upinzani ni sawa na anayekata tawi alilokalia.

4. Mwanachama akihama chama chake na kujiunga na chama kingine siyo kapi na asionekane kapi (labda iwe dhahiri kwamba hana au amekosa sifa za kuwa mwanachama wa chama cha siasa). Lakini kama sababu ni kutofautiana na chama chake na kufukuzana, kwangu mimi kwa mwanachama kama huyu si kapi hata kama chama chake cha awali kitamwona kama ni kapi. Kwangu mimi, kapi ni mtu asiye na sifa za kuwa mwanasiasa (hafai). Nasema hivi, kwa sababu hata sisi hapa tulipo tumetoka sehemu mbalimbali na kwa sababu tumetoka sehemu hizo hakutufanyi tukose sifa za kuwa tulipo leo hii unless kama tumepoteza sifa za kuwa kwenye ajira (kama hilo linawezekana).

5. Ukomavu wa kisiasa ni mchakato - inachukua muda kwa sababu kuna sababu nyingi zinachangia kufikia huu ukomavu. Mimi niseme tu kwamba vyama vya upinzani vimefanya kazi kubwa na visikate tamaa pamoja na kwamba vinakabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na kukosekana kwa a 'level political ground'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…