Mawazo mazuri na ushauri murua kabisa ila Pascal siasa za rd ni ngumu. Kikubwa kinachotakiwa kwa opposition ni kugombania tume huru ya uchaguzi yaani waache vitu vyote. Halafu wapambane kupata tume huru hata kama uchaguzi hautafanyika lkn wapaze sauti zao wakiwaelemisha wananchi mpaka kieleweke kwenye tume huru. Bila tume huru hakuna oppsition na kwa utawala huu. Wengi watapokonywa majimbo yao hata kama watashinda. Lingine Pascal watanzania pia wanapenda maisha ya starehe na rahisi, wanapenda maisha ya juu bila kuifanyia kazi. Uoga wa watanzania pia inachangia sana oppsition kutokuwa na nguvu. Kuna vitu vya msingi ambayo wamenyimwa lkn wako kimya tu. Lazima udai haki yako kwa nguvu hata kwa kupoteza uhai. Wananchi wangekuwa waelewa mengi yangefanyika hata Magufuli mwenyewe asingeweza kuyazuia. Bila demokrasia ya kweli hakuna maendeleo Paskali. Tunaumia sana ce tunaoona wenzetu wanavyoishi. Inaniuma sana, Pascal ukisafiri au ukiishi nje ya Tanzania ukaishi ktk nchi hizi kubwa zilizoendelea sio rahisi kuishabikia ccm. Mie siwezi kuishabikia ccm kwa sababu kuna mambo mengi ambayo wanafanya bila kujali haki za binadamu. Na marais wetu na viongozi wetu bado hawajajua thamani ya mtu. Wanaona binadamu wote ni wanyama. Wangejua thamani ya binamu, kwass Tanzania ingekuwa mbali. Hivi mazingira ya vyama vya opposition unavyoiona ipo sawa hebu tizama wanavyoonewa. Wanajitahidi sana, wanao huwezo wa kukaa kimya bungeni lkn wanapigana bila kuogopa. Ni safari ndefu ndugu yangu. Mwisho watanzania walinyimwa elimu na ccm na viongozi wa serikali na ccm bado wanajua na wataendelea kutaka watanzania wazidi kuwa mambumbumbu, ili waendelee kuwatawala. Ila ipo siku watatoka tu hata Magufuli ipo siku atatoka. Kwanini Magufuli hataki kuwajengea watanzania uongozi thabiti ambayo itawasaidia hata akiondoka madarakani??? Anaogopa nini