Sasa kama ni mafisadi na nyie mna madaraka si muwawajibishe,au wao ni untouchable wako juu ya sheria.Lowasa na kundi lake ni mafisadi kulingana na list of shame iliyo tolewa na chadema na sasa wanaona aibu kukemea ufisadi.....
Katambi huyo tangu ashinde BAVICHA umemsikia kafanya lolote? Sisi vijana hatujamuona hata katika ziara akipitia mikoa yote wenzake kina Heche walipita. Kama unamuona Katambi ameua chama lets wait and see mwisho wake. Wengi walihama CHADEMA awaone walivyoshuka kisiasa. Base on facts not non-sense
You're an advocate and would like you to answer this.
1. Lowassa na kundi lake wamekoea/ wanataizo gani kwa umma wa watanzania?
2. Lowassa na kundi lake wanatatizo/ubaya gani kuwepo CdM?
OK. Twende pole pole.Tatizo kubwa ni kuwafunga mdomo CHADEMA kuzungumzia na kukemea ufisadi. Sasa CCM inajifanya ndiyo inayopambana na ufisadi kutokana na CHADEMA kuzibwa mdomo.
Sawa mkuu...nikuamini maana ata style ya alivojibu amejibu as if amepewa ahadi ya uDCHUYU MTU NI MZIGO SIKU HIZI SIONI MAARIFA NA TAFAKURI TOKA ROHONI TENA, UMEMUULIZA MASWALI YA MUHIMU ILA HATOSHI KUWA MUULIZWAJI
Huenda ni kweli lkn nani amethibitisha? Hata serikali hii inayopigana vita vitakatifu bado imeshindwa kuthibitisha au hata kuwafikisha panapopaswa.Lowasa na kundi lake ni mafisadi kulingana na list of shame iliyo tolewa na chadema na sasa wanaona aibu kukemea ufisadi.....
Mawazo mazuri na ushauri murua kabisa ila Pascal siasa za rd ni ngumu. Kikubwa kinachotakiwa kwa opposition ni kugombania tume huru ya uchaguzi yaani waache vitu vyote. Halafu wapambane kupata tume huru hata kama uchaguzi hautafanyika lkn wapaze sauti zao wakiwaelemisha wananchi mpaka kieleweke kwenye tume huru. Bila tume huru hakuna oppsition na kwa utawala huu. Wengi watapokonywa majimbo yao hata kama watashinda. Lingine Pascal watanzania pia wanapenda maisha ya starehe na rahisi, wanapenda maisha ya juu bila kuifanyia kazi. Uoga wa watanzania pia inachangia sana oppsition kutokuwa na nguvu. Kuna vitu vya msingi ambayo wamenyimwa lkn wako kimya tu. Lazima udai haki yako kwa nguvu hata kwa kupoteza uhai. Wananchi wangekuwa waelewa mengi yangefanyika hata Magufuli mwenyewe asingeweza kuyazuia. Bila demokrasia ya kweli hakuna maendeleo Paskali. Tunaumia sana ce tunaoona wenzetu wanavyoishi. Inaniuma sana, Pascal ukisafiri au ukiishi nje ya Tanzania ukaishi ktk nchi hizi kubwa zilizoendelea sio rahisi kuishabikia ccm. Mie siwezi kuishabikia ccm kwa sababu kuna mambo mengi ambayo wanafanya bila kujali haki za binadamu. Na marais wetu na viongozi wetu bado hawajajua thamani ya mtu. Wanaona binadamu wote ni wanyama. Wangejua thamani ya binamu, kwass Tanzania ingekuwa mbali. Hivi mazingira ya vyama vya opposition unavyoiona ipo sawa hebu tizama wanavyoonewa. Wanajitahidi sana, wanao huwezo wa kukaa kimya bungeni lkn wanapigana bila kuogopa. Ni safari ndefu ndugu yangu. Mwisho watanzania walinyimwa elimu na ccm na viongozi wa serikali na ccm bado wanajua na wataendelea kutaka watanzania wazidi kuwa mambumbumbu, ili waendelee kuwatawala. Ila ipo siku watatoka tu hata Magufuli ipo siku atatoka. Kwanini Magufuli hataki kuwajengea watanzania uongozi thabiti ambayo itawasaidia hata akiondoka madarakani??? Anaogopa nini
Ni kweli 100%Its a one man Army fight and he won't prosper. Ukitizama kwa umakini mkubwa pia utagundua kuwa wale wapiganaji ni kama wamesusia na kukaa kando.
Ccm ya sasa hawawezi kushindana kwa hoja. Na hao waliowapokea juzi hawana uwezo tena kuwashawishi wananchi ni bora cdM nyarandu anaeleweka kwa wananchi
Leo sina la kusema zaidi ya kukupongeza kwa makala nzuri.Maana makala nyingi za nyuma umekua ukikosoa bila kutoa way forward.Sasa hivi umeiva hasa. Lazima ukipinga kitu uje na mawazo mbadala nini kifanyike.MTU akiamua kukubeza Huyo Ni mpuuzi.Hongera tena.Wanabodi,
Declaration of Interest.
Mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, hivyo ni kawaida, ukifanya ukosoaji wowote kuihusu Chadema humu jf, utanyooshewa vidole kuwa wewe ni CCM. Nafanya ukosoaji wangu constructively, truthfully with objectivity, impartiality and balancing, hivyo nawashauri Chadema, wawe tayari kupokea na kuuzingatia ushauri wowote, hata kama ushauri huo unatoka kwa kichaa au kwa shetani, ili kujitafakari na kujitathinini, kama inajidhania imesimama, na uiangalie isianguke. CHADEMA msipuuzie ushauri hata kama ni kutoka kwa shetani!, S ...
Utangulizi
Hili ni bandiko la ushauri wa bure kwa Chadema, na unatolewa na mtazamaji wa muda mrefu wa mchezo wa siasa nchini Tanzania, ambaye ameangalia tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini Tanzania, uchaguzi wa jimbo la Kwahani, 1994, uchaguzi mkuu wa 1995, 2000, 2005, 2010, na 2015. Ushauri wenyewe ni kuhusu hii hama hama ya wanachama na viongozi wa Chadema kuhamia CCM. Naishauri Chadema Wajitafakari!, Wasiwabeze Wanaohama Kama Wafanyavyo CCM, Wanaohama Chadema, Wana Hoja za Msingi, Chadema Wanadhani Adui Yao Mkuu Anaowanya Kushindwa Kwenda Ikulu ni CCM, Kiukweli Adui Mkuu wa Chadema Sio CCM, Nitawatajia Adui Mkuu wa Chadema, na Mwisho Nitawapa Ushauri Chadema Wafanye Nini, Waweze Kuingia Ikulu 2025 Magufuli atakapomaliza and only if Magufuli atamaliza 2025!, kwa sababu haya ninayoshauri, kwa uchaguzi wa 2020, saa hizi tayari ni too little too late, na Magufuli ni just too powerful kiasi kwanza hakutakuwa na uchaguzi wa rais 2020, uchaguzi wa rais wa 2020 utakuwa ni igizo tuu la uchaguzi, lakini mshindi tayari ni Magufuli, hivyo wote watakaompinga Magufuli 2020, itakuwa ni kujifurahisha tuu, hivyo Chadema Watake Wasitake, Lazima Wabadilike, Vinginevyo...its the end of the road kwa Chadema, tunarudi kwenye nchi ya Chama Kimoja.
Why Chadema?
Tanzania japo tuna vyama vya siasa zaidi ya 22, lakini vyama vikubwa ni CCM, Chadema na CUF, by now CUF is already a gone case, hivyo tunapozungumzia upinzani Tanzania, tunazungumzia Chadema. Kifo cha CUF hichoo... chaja! Upinzani kubaki CHADEMA pekee ...
Justification ya Kuikosoa Chadema kwa Mtu Ambaye Sii Mwanachama.
Mashabiki na manazi wa Chadema humu jukwaani, ukifanya ukosoaji wa Chadema, au kutoa ushauri wowote kuhusu Chadema, watakubeza unashauri kama nani?. Kwa sababu Chadema ni public party paid by taxpayers money, then the taxpayers have the right to know the conduct of their tax, hivyo Watanzania wote wana right kujua mambo yote ya Chadema, public na private, ni haki yao kwa sababu kinaendeshwa kwa kodi zao!.
Kwanini Uishauri Chadema, Kwa Wao Wenyewe Hawajioni na Kujishauri?.
Ushauri huu nautoa kwa dhana kuwa Viongozi wa Chadema, wanachama wao, wafuasi wao, washabiki wao na manazi wa Chadema humu jf, wote ni pro Chadema, wako ndani ya box la Chadema, hivyo wanaweza wasiwe na uwezo wa kuona nje ya box, soso tulioko nje ya box ambao ni watazamaji, tunaweza kuwa tunaiona Chadema vizuri Zaidi kwa nje, kuliko waliomo ndani ya chama, lakini pia kuna walioko ndani, wanayaona madhaifu na mapungufu ya Chadema from within, lakini kwa vile wamo, wanakosa objectivity ya kujiambia, kujitathinini na kujikosoa, hata hivyo tathmini ya kweli, inapaswa ifanywe na watu wa nje na sio kujitathmini yenyewe.
Chadema Isiwabeze Wanaohama, Ni Haki Yao, Ila Pia Izingatie Hoja Zao, Wana Hoja za Msingi
Kati ya wanachama na viongozi wa Chadema wanaohamia CCM, kuna wengine wanahama kimya kimya bila kusema sababu, kuna wengine wananunuliwa, na kuna wengine na haswa baadhi ya viongozi, wanapohama, wanaandika barua Chadema na kuaga kwa kutoa sababu, ziwe ni sababu za kweli au ni visingizio tuu, lakini kuna kitu wanasema, na wengine hawasemi chochote kuhusu Chadema lakini siku wanapokelewa CCM, Chadema, japo ni kweli wengi kinachowahamisha Chadema ni njaa zao tuu, na wanakwenda CCM kufukuzia fursa, lakini kuna baadhi, wana hoja za msingi sana, hivyo Chadema inatakiwa kutozipuuza hoja zao, isisikilize na kujitathmini kuhusu ukweli wa hoja hizo.
A Way Forward, Chadema Ifanye Nini.
Ni hayo kwa uchache, nikikumbuka mengine nitayaongeza.
- Kwanza Chadema ijitathmini, is it on the right track?, itambue makosa yake, ikubali makosa, ijirekebishe, isonge mbele. CHADEMA ni sikio la kufa? Iambiwe vipi ili isikie? Masha ana hoja za msingi, zisikilizwe, zizingatiwe, zisipuuzwe!
- Ianzishe grassroots recruitment ya wanachama wake waaminifu, isije kujikuta imewakumbatia CCM ndani, Chadema nje hadi ndani ya CC yake, kama ilivyotokea kwa Mwenyekiti wa Bavicha.
- Ianzishe headhunting na spotting leadership talents na able people toka kwenye jamii kujiunga Chadema na kujenga kada ya viongozi wake wa kesho, born and breed in Chadema, kwa kuwafanyia grooming, ili kupata wagombea wake wa nafasi mbalimbali za uongozi.
- Ipunguze kushobokea makapi kutoka CCM, wana CCM wanaojitoa CCM na kujinga Chadema, wawe wanachama wa kawaida tuu kama wanachadema wengine na sio kupapatikiwa na kupewa uongozi moja kwa moja.
- Chadema I invest on people na mass mobilization, na sio ku invest on vitu na mikutano tuu ya hadhara, kupitia social media na kumiliki media yake yenyewe, kutawafikia watu wengi Zaidi kuliko kutegemea mikutano na maandamano pekee.
- Chadema irudishe ukomo wa uongozi, hata kiongozi awe mzuri vipi, anafikia kiwango cha ukomo wake na kuwa kama saturated solution, he can do no more than what he can!, anakuwa hana jipya!, pia Chadema waandae succession plan, by now, wawe na a pool of able people from within kushika nafasi zote za uongozi, na kuendesha serikali, kungekuwa na ukomo, by now watu wangejua Mbowe amefikia ukomo wa uwezo wake, hivyo nani watampokea.
- CCM ni chama dola, hivyo Chadema isitumie model ya CCM kuitafuta ikulu, iandae model yake yenyewe ya kupata viongozi wake na wagombea wake, mtindo wa the democrats ya US ni mzuri kuanzia kwenye primaries.
- Kuondokana na viongozi ving'ang'anizi na miungu watu, maadamtarget ni kuingia ikulu, umeshindwa kuuingiza Chadema ikulu, unapisha wengine wanaendeleza, sio umeshindwa hala unang'ang'ania!.
- Kuwafanyia tathmini wabunge wake na kukubalika kwao, na kuwe hakuna haki miliki ya majimbo, mfano 2020, Mdee anatathminiwa amefanya nini Kawe for 10 years, na jee bado anakubalika?, Wanachadema wote wenye uwezo, wawe huru kumchallenge Mdee, akitokea mwanachama mwingine mwenye sifa Zaidi, uwezo Zaidi na kukubalika Zaidi, Mdee anawekwa pembeni, vinginevyo 2020, kuna majimbo kibao Chadema mtayarudisha CCM!.
- Chadema kionyeshe ukomavu na kuwa ni chama mbadala kwa kuachana na cheap politics ya siasa za matukio, na kujikita kwenye real politics ya kushindanisha sera, sio kwa kupinga kila kitu, CCM ikifanya mazuri, mfano elimu bure, Chadema ikubali hili ni zuri, lakini ionyeshe ingekuwa Chadema ingefanya bora zaidi kwa elimu bure hadi chuo kikuu, kwa kuonyesha how CCM inatapanya fedha kwa mambo yasiyo na maana, halafu inanyanyasa Watanzania masikini kwa kuwanyima mikopo. Chadema wajifunze kuibomoa CCM kwa hoja na sio siasa za matukio, mfano mwaka 2020, Magufuli anaingia ulingoni akiwa na elimu bure, ndege za ATCL zinapaa dunia nzima, flyovers, reli ya SGR, na Tanzania ya viwanda. Chadema lazima waje na sera mbadala kuonyesha jinsi ATCL, flyovers na SGR zilivyowatia umasikini Tanzania, kama fedha hizo zingewekezwa kwenye sekta ya kilimo nini kingepatikana, bila kuinua sekta ya kilimo, hiyo Tanzania ni Tanzania ya viwanda gani vinavyotumia malighafi gani?. Ijikite kwenye hoja kama hizi Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas ...
- Chadema ipiganie a level playing field kwenye the political ground, kupitia tume huru ya uchaguzi na katiba mpya, haiwezekani watu wawili wanagombea urais, mgombea mmoja anakuja na vingora, na full government media team, paid by public money for the advantage ya CCM, halafu, mwingine with nothing, halafu utegemee kushinda!.
- Chadema ipiganie true free and fair elections with maximum transparency, kama hakuna manouvers zozote zinazofanywa na Tume ya Uchaguzi, kwa nini wazueie party tallying?, wanaogopa nini, kama matokeo yote hadi ya urais yanabandikwa vituoni mbele ya mawakala wa vyama, kuna kosa gabi kama mawakala wote watakuwa na smart phones, ku scan matokeo na kutuma makao makuu kwenye tallycenters za vyama, kama haki itatendeka, then tallying za vyama zitafana na tallying ya NEC, what is it there to hide kuzuia tallying?.
- Chadema kutimiza majukumu yake kikamilifu kama Chama cha upinzani kazi yake sio tuu kuikosoa serikali, bali ku I check serikali kuhakikisha inafuata katiba na kutekeleza sharia, taratibu na kanuni, mfano, katika kuzuia mikutano ya kisiasa, rais Magufuli amevunja katiba wazi wazi kabisa mchana kweupe!, chama chochote makini, by now, kingeifungua shauri mahakamani, ili mahakama itoe tafsiri rasmi, kama itathibitisha rais amevunja katiba, anashitakiwa na bunge, na kuondolewa madarakani!. Mfano hata suala dogo tuu kama Daudi Bashite, nilishauri Je, wajua suala vyeti vya Bashite, linaweza kabisa kumng'oa Rais ...
- Chadema waipinge CCM kwa kujikita kwenye hoja zenye maslahi kwa taifa, ujinga, umasikini, maradhi, rushwa na ufisadi, kwa kuonyeshea CCM katika kipindi chote cha miaka 50, CCM imeshindwa, na katika rushwa na ufisadi, Chadema iwaeleze wananchi, CCM ndio shina na mlezi wa rushwa zote na mafisadi karibu wote ni CCM!, ili wananchi waelewe kuwa CCM inapigana vita ilivyovilea na kuvijenga.
Paskali
Never, unataka kusema tanzania hii kuna anayeyaona hayo, never, ni njaa zinawasukuma kuondoka. Mbaya katika Tanzania hii ni Lowasa, Fisadi kuliko wote ni Lowasa (kama kweli tuhuma ni ya kweli). Nakuapia kama hawatapata wilaya na mikoa, watarudi Chadema. Usilete shallow analysis, hawa wanahama baada ya Magufuli kusema atahakikisha anaua upinzani. Njia moja wapo ni kuwanunua (madiwani), sasa anaona wenye njaa kama Kafulila, atawapa vyeo.... etc. Petro, akiwapa vyeo utasemaje? Time will tell. Yule binti tayari ni waziri, na akina kafulila and Co. Ltd wanategemea watafanyiwa hivyo.Kaka Pascal Mayalla, nakubaliana na hoja yako. Lakini, ugonjwa mkubwa uliobaki na kuwasumbua CHADEMA ni kuwepo kwa Lowassa na kundi lake. Kundi la Lowassa likiondoka kwa kuhamia chama kingine au kuanzisha chama chao, CHADEMA itarejea kwenye njia yake. Hakika, uwepo wa Lowassa na kundi lake ni jambo gumu sana kwa CHADEMA kwakuwa inakuwa na muda mwingi wa kujibu tuhuma kuliko kujijenga.
Umekosea mayalla adui mkuu wa upinzani ni FISIEM[emoji196] Hawa wengine ni wamekumbwa na mifadhaiko hawawezi na hawatoweza kuiyumbisha cdm. Kaondoka kigogo slaa je umekionaje chama kimeyumba?
Chama hakiwezi kuendelea kwa kununua wanachama ona fisiem wanavohangaika kaondoka Nyalandu tazama idadi ya wanaowarubuni imefikia ngapiii... ukipata jibu hapo ndo ujue Nyalandu ananguvu ya idadi hiyo wanayonunua mpaka ifikie idadi YA MAUMIVU YA KUKIMBIWA na MH. NYALANDU nnaimani NYALANDU atakuwa mbali na hawatomfikia.
watambue kuwa kila kichwa watakachofika bei ndio sawa na gharama ya kumrudisha NYALANDU kama fisiem watammaind.[emoji196]