figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 28,132
- 64,416
CCM wakiangalia mbele ni giza sababu haakuna walichofanya. Hivyo wanahofu ya kuondolewa madarakani. Mikutano ya CHADEMA inawatisha kwani walitegemea CHADEMA imekufa. Hata 29.10.2025 walipiga risasi wananchi sababu walihisi waliokuwa wanaandamana ni CHADEMA.
Nashauri CHADEMA tutumie mabavu, nguvu, fitina, na kila mbinu iwe safi au chafu kuhakikisha mikutano inaruhusiwa.
Msikimbilie mahakamani.. Huu ni mtego wa drafti. Wanajua mtaenda mahakamani..
Mkienda mahakamani mtakuwa mumefunga hata mijadala kwenye vyombo vya habari. Wakiulizwa kwanini mumefungia mikutano ya siasa, Jibu litakuwa kwamba hilo Swala hatuwezi kulijibu sababu lipo mahakamani. Na mahakama kesi watakuwa wanaahirisha hadi itafika 2030.
Wa kushitakiwa ni Katambii kwa matumizi mabaya ya madaraka. Lakini tukienda na kesi ya kikatiba, tutakesha. Na mahakama itapigilia msumali kwamba kesi isiendelee hadi kesi ya msingi itakapo sikilizwa. Mfano kesi ya Chadema, kesi ya msingi ilisikilizwa baada ya mwaka na wakashinda. Ilikuwa washinde baadda ya wiki moja.
Ushauri wangu ni Mikutano iendelee Nchi nzima. Na mtoe taarifa Polisi kama kawaida... Wakituzua kwenye mikutano tutapambana hapo hapo.
Nawashauri Watanzania kuanza mazoezi ya kujiweka fit. La mgambo limelia