Sija kusoma muda mrefu kidogo, kiasi nilianza kuwa na wasiwasi.
Mliopo huko ndani ya chama; hasa nyinyi mnao pitia sehemu mbalimbali mitandaoni, na hasa humu JF; kisaidieni chama na viongozi wenu kukusanya mengi yanayo elezwa sehemu hizi na kuyawasilisha kwa viongozi wenu ili wayachuje na yanayo faa chama kiyafanyie kazi.
Kwa mfano: Mikutano wanayo fanya viongozi sehemu mbalimbali inaonyesha kila mahali "nyomi" za kutisha yeyote; hata huyo CCM. Jiulizeni, hizi nyomi kwa nini zinaishia kwenye mikutano hiyo?
Kuna kitu gani kinahitajika kufanyika hizi nyomi ziwatishe kweli kweli CCM wakati zinapo hitajika kufanya hivyo.
Natumaini utanielewa ninapo lenga; na huo ni mfano mmoja tu wa ushauri tunao tamani chama na viongozi wake waufanyie kazi haraka kabla ya 2025.