Uchaguzi 2020 CHADEMA mkisema mtatoa Huduma za Afya bure, naomba mjibu hoja zifuatazo

Kilichosemwa ni kutoa BIMA YA AFYA kwa bei nafuu. Acha porojo za

Umekurupuka na jiuzi lako lirefu. Uwe unasikiliza na kuelewa. Unadhani wanaokulipa wanaokota hiyo pesa?
 
Lb7 ikiwa na jipya ndipo mtu unaweza anza kushangaa.

Hivi hizi ndege 5 nyingine zitakazokuja kununuliwa na jiwe bila kuangalia vipaumbele ni za nini na zitagharimu pesa ngapi?

Huu uwekezaji wa kupendezesha jiji la Dodoma wakati kwingine kupo hivi ni wa nini?

Barabara ya Rusahunga Rusumo mtaji kwa wagombea

CCM mnachukua ruzuku kiasi gani? Hizi pesa zinazoendelea hulipwa wasanii koko nazo vipi?

Hizi gharama za misafara ya jiwe ya magari 100+ vipi?

Gharama za kuendeshea serikali Chatto vipi?

Uwekezaji unaoendelea Chatto na geita vipi?

Kwa ufupi kwa kuweka vipaumbele tu sawa sawa, pesa lukuki mbona zitakuwapo?
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya maneno Afya bure na sentensi " kila raia wa Tanzania atakuwa mwenye mfumo wa bima ya afya".

CDM sera yao ya afya ni Bima ya afya kwa watanzania wote.
 
Si anaropola tu,yeye mwenyewe huwa analalamika kanyimwa pesa za matibabu na serikali,kumbe kwenye matibabu lazima uwe na pesa.Lissu ni muongo sana.
 
mkuu ebu ni jibu kwanza hili swali...trilioni 1.5 inaweza kutoa huduma za afya bure kwa watanzania wangapi?ukinijibu hili swali nitajua kama lissu ni muongo or mkweli
Mkuu mi sio mtu wa kufanya analysis za aina hiyo, labda unisaidie wewe nijue wapi nimefeli
 
Si anaropola tu,yeye mwenyewe huwa analalamika kanyimwa pesa za matibabu na serikali,kumbe kwenye matibabu lazima uwe na pesa.Lissu ni muongo sana.
Ndo hivyo hata Kama akitoa bima za gharama nafuu, ubora wa huduma za afya utadorora sana. Itakuwa more than worse
 
hiyo hata obama marekani alishindwa nchi tajiri itakuwa kwa huyu kibaraka wa mabeberu wameshamdanganya wamemtosa hata kampeni hawamsaidii
Wewe boya kweli. Sipendi watu wanaoongea mambo wasiyoyajua kwa undani. Nani alikuambia Obama alishindwa Medicare policy yake? Kwa taarifa yako Obama hakushindwa ila demokrasia ndani ya senete ndio ilimwangusha. Maseneta wa republican walipinga. Unaongea vitu usivyovijua unadhani kila mtu ni mbumbumbu kama wewe.
 
Kwani mkuu mapato ya chama unataka yatumikaje labda? Bajeti yao inaruhusu kufanya kampeni za aina hiyo
 


Chadema waliposema kwamba watatoa Elimu bure mlisema ni uongo kwamba haiwezakani, leo mnajinadi kuwa mnatoa elimu bure je imewezekanaje? ni jibu tafadhali sana
 
Mkuu sera ya kwamba bima zitatolewa kwa gharama nafuu, halafu aseme atawaondolea Kodi baadhi ya makundi ya wajasiriamali maana yake kuna makundi yataongezewa Kodi kwa kiwango kikubwa. Kufanya unafuu wa huduma za afya lazima taxes zitaongezeka pakubwa
 
kumbe wewe sio mtu wa kufanya analysis...unasemaje mtu muongo wakati huwezi kufanya analysis ya anachokiongea??
Mkuu ijulikane tu kuwa sera zinatolewa ili watu wapate kura tu, hapa hamna haha ya analysis unayoitaka wewe
 
Lissu amesema kila Mtanzania atakua na Bima ya afya ya bei nafuu na ataichangia. Si wote tutaumwa kwa pamoja hii inamaana pesa za wazima zitatibu wagonjwa.
Basi itakuwa kodi ya kichwa, sainunu LAIZER ana wake 32 watoto 76 house girl 48 walinzi 4 kwenye boma lake, akilipia bima ya laki kwa kila mtu kafirisika tayari
 
Mkuu ijulikane tu kuwa sera zinatolewa ili watu wapate kura tu, hapa hamna haha ya analysis unayoitaka wewe
kweli mkuu,kuna wengine waliahidi milioni 50 kila kijiji na ahadi nyingine kemkem alafu baada ya kupata kura wamejikausha kama si wao..wamerudi tena safari hii kutulaghai na uongo mwingine..wanafkiri tumesahau
 
Ukiwa unamtongoza dem utaongea lolote tu ila ukishampata u avimba[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nilizoziona kwenye tv Ni ndege tano bombardier 2, airbus 220 2 na dreamliner moja, hizi sita zingine zilikuja lini na zimeegeshwa wapi?
 
Chadema waliposema kwamba watatoa Elimu bure mlisema ni uongo kwamba haiwezakani, leo mnajinadi kuwa mnatoa elimu bure je imewezekanaje? ni jibu tafadhali sana
Suala la elimu bure linawezekana japo ubora pia umepungua, kwa sababu gharama za kulipia shuleni ni fixed kila mwaka zinajulikana, hivyo serikali inapata urahisi wa kupangia bajeti ambayo iko fixed pia.

Lakini suala la afya mkuu huwezi panga kwamba leo nitaumwa ama siumwi hivyo gharama zake sio fixed. Hata serikali ya Mh. Lissu ikijakupanga bajeti kuhusu hii ishu watasumbuka kwa sababu, bajeti itakuwa inabadilika kila mara .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…