Naomba nijibu baadhi hata kama mimi sio miongoni mwa wanachadema ila mfuasi wa sea mbadala.
1.Kuhusu sera ya afya ni rahisi sana,kipaombele kitapewa makundi maalumu hapa ni watoto chini ya miaka 18 na wanafunzi wa vyuo kwa muda watakaokuwepo shule,wazee miaka 55 na kuendelea,walemavu wote na wamama wanyonyeshao/wazazi ndani ya miaka 3.
-Pesa kwa kipindi cha mpito itapatikana kwa kupunguza bajeti ya miradi mikubwa isiyo na tija kwa sasa inayofanywa na ccm ikiwa ni pamoja na kununua ndege,sgr na stiglaz na mingine ya dizaini hiyo.Pili ku cut down admnistrative expenditures,ukiangalia bajeti ya utawala ya Magu ni kubwa kuliko marais wote waliowahi kuwa ofisini licha ya kujigamba kutoenda ulaya nk lakini impacts ya kutosafiri haijaonekana bali hasara zaidi,huu ni kati ya mfano mja tu wa maeneo yatakayotoa pesa kwa kipindi cha mpito.
2.Kuna pesa nyingi sana zinaibiwa au kufujwa na ccm kwa namna mbali mbali ikiwa ni pamoja na baadhi ya taasisi na miradi ambayo inafanyiwa matumizi nje ya bajeti na mingine haikaguliwi na CAG,kisa cha Prof.Assad na 1.5T nadhani kila mtu anakikumbuka,hapo hatujazungumzia maeneo mengine ikiwamo viwanja vya michezo ambavyo ccm wamejimilikisha.
3. Mwisho kabisa katiba ya Warioba itakuwa ni kichocheo kikubwa sana cha ufanisi na utawala usiotegemea mtu mmja kama uko jeshini ndio maana kila siku utasikiawatu wanamlalamikia rais mara hakuna vyoo stendi mara vyumba vya madarasa nk nk
Mwisho atayeichagua ccm ni dhahiri hajielewi anachofanya maana shida kuu ya watu wa ccm ni kutojua watekeleze jambo gani na kwa wakati gani,hawna akili za kutambua mambo ya mda mfupi,mda wa kati na mda mrefu watakachokurupuka nacho ndio hicho hicho.
Wewe kama zinakutosha unaanzaje kujenga reli ya matrion ya shilingi sehemu ambayo hakuna uzalishaji wa maana si ndani ya nchi wala nchi za jirani,si bora ingeenda DRC,mwisho wa siku hii reli itakuwa liability kama zilivyo zingine ikiwamo Tazara.
Wewe kama zinakutosha unaanzaje kununua mandege ya matilioni ambayo hayana ruti zinazoeleweka na hata watu wako uwezo wa kuyapanda ni olmost haupo,hadi sasa kila mwaka serikali inatoa pesa ya walipakodi kama ruzuku ya kuendeshea mashirika yasiyo na faida kama hili la ndege.
Wewe kama zinakutosha unaanzaje kuwekeza kwenye umeme kwa matilioni ya dola bila kubainisha huu umeme wote unahitajika kwa sasa au hata kwa miaka 30 ijayo? imagine nchi ina miaka 60 lakini tunatumia mgwt 1560 huku tukiwa na ziada ya zaidi ya mgwt 200 sasa hizo mgwt 2015 si zitabaki kuwa mzigo tu wa maintanance? Hii ni baadhi ya mifano mingi michache ambayo ni tembo mweupe na mzigo kwa wananchi.Ningekuwa mimi ndio kiongozi wa ccm ningeunganisha mikoa yote kwa barabara kuu,ningeunganisha nchi yetu na nchi jirani na ningejenga barabara nyinginezo amabazo zinatija kwa wananchi ili wafanye biashara,barabara zina matokeo ya haraka kwenye uchumi wa mtu mja mja na taifa kuliko reli na ndege.
Ningekuwa mimi ni ccm wala nisingehangaika na stiglaz goji badala yake ningewekeza bwawa angalau la mgwt 400 ambazo zina uwezo wa kuishi ndani ya miaka 20 ili pesa inayookolewa nikafanye mengine.
Ningekuwa mimi ni ccm kama sitaki katiba mpya ili niwapumbaze watu,hata nisingehangaika na ndege maana bajeti ya ndege 2 inatosha kupata zaidi ya bln 500 ambazo ningeziweka kwenye benki ya kilimo na uwekezaji na benki ya vijana ili zitumike kama dhamana kwa mikopo ya wawekezaji waanzishe viwanda nk,pili ningewakopesha vijana hasa kwa kuwapa mikopo ya vifaa au vitendea kazi ili wajiajiri na soko kuu ningekuwa serikali,,mfano mradi wa kuhamia Dodoma ulifaa wenye viwanda vya matofali serikali ingekuwa inanunua wanapata kipato sasa badala yake serikali inafyatulisha yenyewe matofali nk nk. Kwa hali na sera za hovyo kama hizo naanzaje kuchagua ccm kwa mfano