Uchaguzi 2020 CHADEMA mmekosea sana kumpitisha Tundu Lissu kuwa Mgombea Urais

MaCCM mtatema tu ndoano.. CCM ya Magufuli wajipange kukabizi nchi kwa nguvu ya Umma. Pushapu na kujamba majukwaani havitamsaidia kitu.

#LISSURAIS2020
Mtakula mitama ya kutosha
 
Unawashwa na nini? Yanakuhusu nini? wacha wakosee.. wewe si mmepatia kwa Jiwe, sasa huku kunakuwasha nini?
 
Nini maoni yako kuhusu Membe, Rungwe, Muttamwenga, Lipumba na wagombea wengine? Kwa nini TL tu? Inaonekana amewanyima usingizi kabisa. Na sisi wajanja huyo mnayemwandama ndiye tutampa kura. Kwa maneno mengine mnampigia kampeni.
Very good Kiongozi
 
Kwani ccm inategemea kura kukaa madarakani? Kama inategemea kura na inajua kumbembeleza wapiga kura, sema mlipata kura kiasi gani uchaguzi wa SM.
Mkuu uchaguzi wa selikali za mtaa si kinajulikana kilichotokea?
 
Mkuu uchaguzi wa selikali za mtaa si kinajulikana kilichotokea?

Kipi kiseme ili tuone mnavyoshinda, ili tujiridhishe na mwenendo wa uchaguzi kwa hii miaka mitano ya Magufuli.
 
Tunajuta aisee. Bora hata tungempitisha Profesa Kahigu
 
Tundu Lissu anawajambisha mbaya
 
Kipi kiseme ili tuone mnavyoshinda, ili tujiridhishe na mwenendo wa uchaguzi kwa hii miaka mitano ya Magufuli.
Chadema mlikosea kujaza form! Baada ya kuona wengi manaenguliwa kwa makosa ya kujaza form mkajitoa ccm ikabeba viti vyote
 
STILL LOT MORE TO COME FROM TL
 
Una uhakika na uraia wako baada ya kuandika haya?
 


Kwa sababu hujataka kutaja jina la mtu ambaye unafikiri angefaa zaidi kushika kibendera kwa niaba ya chama ulichotaja, basi, nafikiri mtoa mada wetu unatakiwa uwe ni mtu mwenye furaha kubwa sana wakati huu kwa kitendo cha chama ulichokitaja kuweka mtu ambaye unadhani ni dhaifu na asiye na maono yoyote.

Au hujawahi kusikia msemo wa Kiswahili kuwa "kifo cha panzi ni furaha ya kunguru"? Huu ni wakati wako wa kufurahi na kwenda kwenye majukwaa ya siasa kueleza mema mengi yaliyofanyika na viongozi wetu wa sasa na katika awamu zilizopita. Pia, kueleza mipango mathubuti iliyopangwa na wagombea wako wanaoomba ridhaa ya wananchi.

Ila wanasiasa na wafuasi wao ni viumbe wa ajabu mno, kizuri cha mwenzako, mwingine kwake ni kibaya.
 
Wewe ndiye KITUKO tuendolee UPUUZI WAKO.

 
Chadema mlikosea kujaza form! Baada ya kuona wengi manaenguliwa kwa makosa ya kujaza form mkajitoa ccm ikabeba viti vyote

Sio cdm maana vyama vyote vya upinzani vilisusia. Sasa huo ulikuwa ni uchaguzi au mtihani wa kujaza fomu za uchaguzi? Hizo ni fomu za aina gani ambazo watu wa vyama vyote vya upinzani wakosee, ila ccm tu ndio wapatiwe bila kukosea? Hao wagombea waliojaza hizo fomu, wameshajaza fomu nyingi sana kwenye maisha yao, mbona wasikosee au kunyimwa hizo huduma kwa kushindwa kujaza fomu?

Hivi unadhani watu ni wajinga wa hivyo boss? Ndio maana tunawachora tu mnavyokusanya makundi mbalimbali kama ya dini, wasanii nk kumsifia Magufuli na kuhubiri amani uchwara, huku makundi hayo yakifumbia mambo viashiria vya wazi kabisa vya kuingiza nchi hii kwenye machafuko. Nikuhakikishie, kama nchi hii itaingia kwenye machafuko, 50%+ itakuwa ni Magufuli. Acha watu waigize unafiki, huku wakifumbia macho ukweli.
 
Pumbavu,, wangempitisha Nyalandu tena mngesema CHADEMA haina wagombea? Subirini dawa iwaingie punda nyie! Mwaka huu mpaka mjambe cheche!
 
CCM mmekosea sana kumpitisha jiwe kwa sababu hauziki, wananchi wamechoka

Kwa nini hamkutoa atlist form za kutosha kila anaetaka kugombea achukue form, mmetoa form moja mnaogopa nini?

Halafu bila aibu mnakuja hapa kulaumu chama pinzani, pambaneni na mgombea wenu, huyu wa kweetu mwacheni hawahusu.
 
Ulimsikia Lisu wakati anaomba wadhamini!

Alisema mwaka huu madiwani na wabunge wajitahidi kusoma kwa makini wajazapo form za uchaguzi ili isiwe kama kwenye selikali za mitaa!

Kwa kauli hiyo unapata picha gani?
 
Kuna mtu alifuata form akaambiwa hazipo?
 
Kuna watu hawana karama ya kuwa wasimamizi wakuu bali ni wazuri kwenye utekelezaji/kutumwa na msimamizi husika.
Kama kaka Yohana ameweza kubuzibuzi hivyo hivyo miaka hii mitano hata TL ataweza basi.
 
Kuna mtu alifuata form akaambiwa hazipo?
Hata ningekua mimi singefata form kwa kweli unaweza kupokelewa na wasiojulikana

Mwenyekiti wenu akikosolewa tu hadharani au hata na vyombo vya habari ni kila aina ya figisu pamoja na wasiojulikana, unategemea kuna mtu atakua na ubavu wankuchukua form kupingana nae? Tatizo ccm mnajali matumbo yenu, hata pale mwenyekiti anapokosea nyie mpo busy mnamwimbia na kumwabudu, sijui akili huwa mnapeleka wapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…