Hao wabunge 70 walipatikana enzi za JK wakati huo demokrasia na utawala bora ulikuwa na afadhali kwa mbali. Toka ameingia Magufuli madarakani tumeona na kumsikia akitishia maafisa wa tume kutokumtangaza mpinzani kisa yeye ndio anawalipa. Mimi binafsi na watu wengine tuliona kupitia kituo cha ITV kwenye kituo cha uchaguzi wa marudio maboxi ya kura yakitolewa kituoni na kwenda kujazwa kura za ccm, hali hii ilitokea mbele ya vyombo vya dola na msimamizi wa uchaguzi, na bado msimamizi wa uchaguzi alimtangaza mgombea wa ccm mbele ya huo uhayawani. Mtindo ulitumika kwenye vituo vingine vyote vya uchaguzi, na aliyetoa maagizo hayo ni rais ili kuhadaa umma kuwa ccm inakubalika.
Pia niliona baadhi ya vituo karatasi zisizo halali za matokeo, mawakala wa upinzani wakilazimishwa kujaza tena kwa kipigo cha polisi. Haya yalifanyika kwenye vituo vyote vya uchaguzi kwa maagizo maalumu. Wasimamizi wa uchaguzi walikuwa wakifunga ofisi ili wasipokee fomu za wagombea wa upinzani. Fomu za wagombea wa upinzani hata zile zilizopokelewa zikifanyiwa hujuma za wazi. Tabia hii ya kwenye chaguzi za marudio zilifanyika hata kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Ukiangalia hizi tabia za kwenye chaguzi zetu ni tabia binafsi za Magufuli hata alipokuwa mbunge. Ninaposema Magufuli ndio anayenajisi chaguzi za nchi hii kwa matumizi mabaya ya madaraka, sisemi hivyo kwa kubahatisha. Ndio tunasema tunataka tume huru ya uchaguzi, kwani ccm chini ya Magufuli haiwezi ushindani wala sio imara, bali inaendesha ukatili kwenye chaguzi zetu ili kutangazwa washindi. Nitawashangaa wapinzani kushiriki huu ushenzi wa mtu mweusi uitwao uchaguzi. Na sisi wananchi tunaojitambua hatutashiriki huo upuuzi bila tume huru ya uchaguzi fullstop.