CHADEMA mnajipanga vipi kuzikabili hujuma kama za uchaguzi wa Serikali za mitaa, maana ndiyo nguzo ya CCM uchaguzi wa Oktoba

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056
Unaona wimbi kubwa la wana Chadema njaa kukimbia kwenda CCM. Si kwamba wanaipenda CCM, la hasha. Wanasoma trend kuwa wabunge wote walionunuliwa wame-retain nafasi zao bungeni.

Na wanajua kuwa hata uchaguzi wa October mbinu hiyo itatumiwa na serikali/CCM kupora ushindi wa Chadema. Au mbinu ya kihuni iliyotumika kuengua wagombea kama ilivyotumika serikali za mitaa itawabeba/itawalinda.

Hata Ndugai anaweza akasema hutaingia bungeni mimi sikutaki! Akijua hakuna la kumfanya! Courage hiyo wanayo sana utawala huu!.

Kama jana Mkuu wa wilaya amemuweka Wakili (ambaye yuko mahakamani kutetea wateja wake) kwa vile anamtetea mtu wa CDM, lolote watalifanya!


Wanaamua ku-pretend kuunga juhudi, wakijua watapata favour kama wenzao waliotangulia.

Mnajipangaje kukabili hujuma hizo? short of that, kama alivyosema Ndugai hata wabunge watatu hamtawapata, maana wataengua kila mmoja kwa njia hiyo.

Achana na malumbano na Ndugai, (yeye anajua fika atarudi), capitalise on that!
 
Kama wao ccm /wenye maamuzi na nchi hii, wana nguvu nyingi yaani ni un touchable wameamua hivyo unadhani wana cdm watafanya nini?

Kikubwa ni kuendekeza mshikamano ndani ya chama kupitia wanachama na wapenzi wa cdm ili huu upepo upite na maisha mengine yasonge.

Retired

In God we Trust
 
Chadema inaungwa mkono na wananchi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka mkubwa heshima kwako. Kuna kitu nakiona hapo mbeleni. Kama kitatokea kila kitu kitabadilika!

Jr[emoji769]

Kiseme kaka. Uzuri kwangu hata ccm wajitangaze washindi wapendavyo, lakini hawawezi kulazimisha wananchi kuwapenda, na hali hiyo ya kushinda kwa njia zisizo sahihi ndio zitakazowatoa kwa aibu. Cdm watumie kila njia kuhakikisha uchaguzi huu kama utakuwa wa kihuni ni kuuharamisha, hali itakayopelekea Mbinyo mkubwa wa kimataifa.
 
Kaka mkubwa heshima kwako. Kuna kitu nakiona hapo mbeleni. Kama kitatokea kila kitu kitabadilika!

Jr[emoji769]
Hata Mimi nakiona kwa jicho la tatu. Ila nikitokea hilo vijana kama hawa Lijualikali au Waitara watajiweka wapi na nyuso zao maana ulikotoka umenyea kambi na ulikoenda wanajua huna mapenzi nao ni ulafi wako wa mlo tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka mkubwa heshima kwako. Kuna kitu nakiona hapo mbeleni. Kama kitatokea kila kitu kitabadilika!

Jr[emoji769]
kama kile tulichoombea kitokee bungeni wakati tunaenda karantini Daresalaam?
 
Yap, tena kwa hiyari yao na sio kutumia vitisho vya kundi la watu wasiojulikana, wala mabavu na vitisho vya taasisi zozote za kimamlaka.
kama wabunge wetu walivyoenda lockdown "kwa hiari yao"?
 
Inawezekana pia wabunge wa upinzani watakaoshinda uchaguzi na kutangazwa, wakapitishwa kwa huruma.
Watu wanakaa mezani na kujadili,

Vp mbowe apite, HAPANA
Prof J vp, ahh huyo mwacheni hana mazara
Heche je, mmmh tutasoma upepo kule jimboni
Lema vp, fyekelea mbali
Mnyika, futa kabisaaa, tumembembeleza sana.
Kubenea, usiulize we delete huyo
Mdee na wenzake je, marufuku kuwasikia tena hao
Mbatia vp, We unaonaje, huyu tumuache tu, poa


Hata ushinde, watu wanapindua meza kibabe,
Focus ya upinzani iwe ni kwa namna gani watahakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki,
Na ikitokea ukawa sio huru na haki, wamejipangaje kuhakikisha hali hiyo inakomeshwa kabisa.
 
Hata ushinde, watu wanapindua meza kibabe,
Exactly, kwa ubabe wa Magufuli, atafanya hivyo! Hilo liko wazi! Hata Ndugai anaweza akasema hutaingia bungeni mimi sikutaki! Akijua hakuna la kumfanya!
 

Umeongea point sana

Ubaya wa chadema huwa wanaacha wagombea wapambane kivyao, watajaza fomu bila kusaidiwa, watafanya kampeni kwa pesa zao kwa asilimia mia, wataachwa na viongozi wa kata tu ikibahatika mkoa.


Hawatachukua huu ushauri hata kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…