CHADEMA mnajipanga vipi kuzikabili hujuma kama za uchaguzi wa Serikali za mitaa, maana ndiyo nguzo ya CCM uchaguzi wa Oktoba

CHADEMA mnajipanga vipi kuzikabili hujuma kama za uchaguzi wa Serikali za mitaa, maana ndiyo nguzo ya CCM uchaguzi wa Oktoba

kama kutakuwa na uchaguzi huru na haki, CDM itawika tena na wabunge wengi tu! Hilo nina uhakka nalo! Kitabaki kuwa chama kikuu cha upinzani.
Si kweli

Watu wamechoka

Wapinzani hawaaminiki tena, unachagua Leo kesho anahama chama. Lakini la pili kwenye majimbo yao watu wanaamini wamechelewa kupata maendeleo kwakuwa tu walichagua upinzani

Mfano ninaishi Jimbo la Mnyika watu wamekata tamaa wanasema watachagua upinzani wapate maji na barabara.

Mimi mwenyewe nilikuwa nawashangaa sana watu wasiopiga kura, nilikuwa naona wanapoteza haki yao kubwa lakini this time I won't bother kupiga kura,nitaacha watu wanichagulie atakayepita yoyote sawa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo maana tunasema CDM Makao Makuu iwe na mkakati wa kujaza fomu hizo, for example, kwa ku assign watu maalumu say wanasheria kusaidia kujaza hizo fomu under their strict supervision kwa kila mgombea!
Tulishatoa mapendekezo

Kila Jimbo kuwe na mwanasheria but hawachukulii maanani.

Hata kupitia tu hizo fomu kabla ya kuwasilishwa kwa mtu mwelewa nalo Jambo jema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la wanasiasa wali wengi hususani wa vyama vya upinzani hawawajui vizuri wateja was ambao kimsingi ndio wapiga kura.
Wananchi wako wengi wanauelwa mdogo sana wa mambo.Nachelea kusema ni wajinga.
Angalau Chama tawala wanaujua ukweli huo,ndio maana wanaweza kuwashawishi kirahisi walio wengi na kura zikatosha.
Uchache wa wananchi walio na uelewa mpana wa mambo ndio unaovigharimu vyama vya upinzani kwenye chaguzi.
Siasa ni pamoja na kujua wateja wako wanakuelewa,hata kama unafanya mambo ya kipuuzi.
Nadhani nimeeleweka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nimekuelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unadhani mizengwe inakuwa kwenye kujaza fomu tu? kumbuka wanaopokea hizo fomu huwa wanajificha chini ya meza baada yakupokea za ccm

Sent using Jamii Forums mobile app

Wanatakiwa kupeleka mapema hata wiki moja kabla ya deadline. Ukienda leo akajificha, utaenda kesho na kesho kutwa....hawezi siku zote kukimbia.

Sasa wewe unasubiri siku ya mwisho ndio unapeleka

Lazima wakufanyie figisu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alafu kutwa yako kwenye nyumba za ibada eti yanasali na kutuambia tumtangulize Mungu huku yenyewe yamemtanguliza shetani!
 
Kwa maana yako cdm isipo pata mbunge na diwani ndiyo itakuwa dawa ya corona?

In God we Trust
Ndio corona mtanzania Wa kwanza mwanaume kuumwa corona alikuwa mtoto Wa mbowe chadema imehusika kuleta corona
 
Unadhani mizengwe inakuwa kwenye kujaza fomu tu? kumbuka wanaopokea hizo fomu huwa wanajificha chini ya meza baada yakupokea za ccm

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahihi, nasema moja wapo ni kujaza fomu, kufunga ofisi, kukataa kuzipokea makusudi etc na mbinu nyingine watakazobuni hata za wazi wazi... unampa anazichana kuwa sijapokea etc etc
 
Chadema safari hii hampati mbunge wala diwani hata

Hata mmoja sababu kwenye maslahi na mambo ya nchi hamsimsmii kaxi yenu kutetea mataifa ya nje tu kukitokea issue ypyote ya Tanzania na nje ya nchi nyie mnasimama na nchi ya nje hata mshinde hamtatangazwa

Mimi nilidhani hawatashinda, kumbe ni hata wakishinda hawatatangazwa! Sasa tunaposema tume ya uchaguzi haipo huru, huwa mnatokwa na mishipa kwanini? Maslahi ya nchi hayalindwi kwa utashi wa ccm, na hakuna mwanacdm atatii utashi wa ccm kwa kichaka cha kujifanya eti maslahi ya taifa, ili kupata hisani ya kutangazwa iwapo atashinda. Inapokuwa maswala ya maslahi ya taifa acheni kutafungamanisha na uccm, ili maslahi ya taifa yasichanganywe na sifa za kiccm. Propaganda za kipuuzi haziwabebi kwenye mazingira haya boss.
 
Mimi nilidhani hawatashinda, kumbe ni hata wakishinda hawatatangazwa! Sasa tunaposema tume ya uchaguzi haipo huru, huwa mnatokwa na mishipa kwanini? Maslahi ya nchi hayalindwi kwa utashi wa ccm, na hakuna mwanacdm atatii utashi wa ccm kwa kichaka cha kujifanya eti maslahi ya taifa, ili kupata hisani ya kutangazwa iwapo atashinda. Inapokuwa maswala ya maslahi ya taifa acheni kutafungamanisha na uccm, ili maslahi ya taifa yasichanganywe na sifa za kiccm. Propaganda za kipuuzi haziwabebi kwenye mazingira haya boss.
Toka lini chadema mkatetea maslahi ya taifa? ndio.maana hatuwataki hata mshinde hamtatangazwa .Kama mna pesa za kupoteza gombeeni zipotee
 
Inawezekana pia wabunge wa upinzani watakaoshinda uchaguzi na kutangazwa, wakapitishwa kwa huruma.
Watu wanakaa mezani na kujadili,

Vp mbowe apite, HAPANA
Prof J vp, ahh huyo mwacheni hana mazara
Heche je, mmmh tutasoma upepo kule jimboni
Lema vp, fyekelea mbali
Mnyika, futa kabisaaa, tumembembeleza sana.
Kubenea, usiulize we delete huyo
Mdee na wenzake je, marufuku kuwasikia tena hao
Mbatia vp, We unaonaje, huyu tumuache tu, poa


Hata ushinde, watu wanapindua meza kibabe,
Focus ya upinzani iwe ni kwa namna gani watahakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki,
Na ikitokea ukawa sio huru na haki, wamejipangaje kuhakikisha hali hiyo inakomeshwa kabisa.

CDM atabaki Prof J tu

NCCR ndio itakuwa na wengi
 
Toka lini chadema mkatetea maslahi ya taifa? ndio.maana hatuwataki hata mshinde hamtatangazwa .Kama mna pesa za kupoteza gombeeni zipotee

Ndio nakuambia hivi maslahi ya nchi hii hayasimamiwi kwa utashi wa ccm, kama unatarajia maslahi ya nchi kusimamiwa kwa vionjo vya kiccm basi utangoja sana. Kama unadhani uchaguzi wa nchi huu unategemea fadhila za ccm na mambo yataishia hapo, ngoja impact yake. Ccm mmechoka kushindana kwa ushawishi wa kisiasa, mmebaki kujipachika sifa za kuwa walinzi wa maslahi ya umma, ili kujipa uhalali wa kukaa madarakani bila ridhaa ya umma. Hiyo ghiliba imebakiza muda mfupi maana wananchi wengi wana ufahamu wa kutosha.
 
CDM atabaki Prof J tu

NCCR ndio itakuwa na wengi

NCCR watakuwa wengi kwa matamanio ya ccm, ila wananchi wanajua wanataka nini. Kuna uwezekano wa kuchezea uchaguzi na kumtangaza mshindi asiye halali, lakini hakuna uwezekano wa kuwalazimisha watu kuikubali hiyo NCCR. Kama ccm yenyewe haina mvuto bali inatumia mabavu na vitisho kukubalika, ndio itaweza kuipa mvuto hiyo NCCR?
 
kama wabunge wetu walivyoenda lockdown "kwa hiari yao"?

Wawe wameenda kwa hiyari au kwa kulazimishwa hilo watajua wao, sisi tunachojua tunakubali cdm na hatuikubali ccm chama cha kizee fullstop.
 
Back
Top Bottom