CHADEMA mnatuchanganya. Tunataka Katiba inayosimamia haki na sio Katiba Mpya. Kamwe Katiba hiyo haiwezi kutengenezwa na Wanasiasa

Kila siku nauliza.

Wana uhakika gani kama hiyo katiba mpya itafuatwa?
 
Mataga ktk ubora wake
 
Sitaki kumbuka Magufuli kabisa
 
CHADEMA wao wanataka hata leo bunge livunje, uchaguzi urudiwe ili na wao wapate madaraka.

Nchi hii ukisikiliza sana wanasiasa, unaweza kujikuta unatumika weee, mpaka unazeeka.

Kumbukeni wao siyo masikini.

Sasa hivi agenda za CHADEMA zote hazigusi maslahi ya mwananchi wa kawaida.

Huwezi kuwakuta wanaongelea Ajira, maji, afya, umeme, barabara, n.k

Wao siku zote wako busy na mambo ambayo ni ya faida kwao binafsi kama BUNGE LIVE, MIKUTANO YA HADHARA, TUME HURU, KATIBA MPYA.

Na kibaya zaidi kuna mambo ambayo unaona kabisa yalipaswa kushirikishwa watu wengi kama katiba, lakini unashangaa wao wanabagua watu na kujifanya wao ndio mabingwa wa hiyo agenda na wengine ni wasaliti.

Hamtaweza kufanikiwa kwa njia hii.

Mpaka sasa hata wananchi hawajashirikishwa kwenye hiyo agenda yao.

Ndio maana sasa hivi kila kundi lina agenda na mikutano yao.

Ukiwaita machinga, wanawake, wazee, wasanii, vyana vya wafanyakazi, vijana hawawezi kukwambia wanataka kwanza Tume huru na katiba mpya.
 
Angekuwa na maono angeleftishwa na uviko?
 
Huu ni mwaka wa ngapi tangu upate uhuru?
 
Nadhani latina tunayoitaka haipo popote

Maana ni katiba, sera, miongozo, Sheria, taratibu, ushauri in one document

Must be a hell of a huge document
 
Wewe itakua ulizaliwa kabla ya muda yaani Njiti.rudi hospitali ukawekwe kwenye jokofu ukomae akili.
 
Umeongea ukweli mtupu. Tunao msingi mzuri tangu awamu ya Julius Nyerere.
 
Umeandika hoja nzito sana mkuu, hizi ndio fikra zilizoifanya JF ikapata jina.
 
Katiba ni jambo jumuishi ila tatizo ni kuwa wanasiasa ndio wenye uhitaji nayo sana ili kutimiza kiu yao kwa baadhi ya interest zao.

Wananchi watakapo ihitaji itakuja tu bila pressure za wanasiasa.

Ukitaka kujua kuwa madai ya katiba ni ya wanasiasa angalia wanachodai.

1. Tume huru ya Uchaguzi.

2. Kupunguzwa mamlaka ya Urais yatakayoathiri pia uwezo wa kuteua watendaji mbali mbali.

Madai yanayopigiwa chapuo mno ni ya wanasiasa tu wananchi wa kawaida wanatumika tu kuwabeba wanasiasa.
 
Swala la kitu gani kitakuwepo kwenye katiba ilo ni jambo jingine kwasababu ili uandae katiba lazima ushirikishe wananchi ili iandaliwe rasimu.ila kabla hatujafika uko lazima kuwe na kundi fulani kwenye jamii litakalo anza kupiga kelele uanzishwaji wa huo mchakato sasa nikuulize unadhani kwa nchi hii ilivyo tofauti na wanasiasa ni kundi gani jingibe linaloweza kupaza sauti kirahisi zikafika kwa wenye mamlaka ya kuanzisha huo mchakato?
 
Unataka wayaongelee wapi hayo wkati unajua mikutano ya hadhara ilipigwa marufuku.Ata hivyo sio lazima chadema waseme kila kitu,ata wewe kwa nafasi yako unayo haki na wajibu wakusema hayo unayoyaona hayako sawa.Ata hivyo chadema wako smart kwasababu kama wameanza na hitaji la katiba maana yake wanataka kuwepo katiba bora itakayoweka na kurekebisha mambo mengi tunayoangaika nayo sasa yakiwepo hayo uliyoyataja.
 
Hayo ya Tume huru, katiba mpya na bunge live wanayasemea wapi ???
 
Wewe ni mpumbavu usiye na akili , mods futeni takataka hizi , unajua maana ya katiba we mbwa ? ,Au unadhani katiba ni Kwa ajili ya Chadema , ukawa au Act ? , Mazafaka
Daaah! Nimefafanua vizuri Sana, nahisi hujasoma Uzi wangu ata punje. Umesoma headlines tu ukajaa. MijadAla yenye tija haiitaji hasira. Jadili hoja Mzee. We ukiwa kiongozi si utachinjA kila mtu sasa
 
Sijapinga swala la kupiga kelele. Kwanza wapiganie haki zilizopo kikatiba na wakapokonywa Kama mikutano ya hadhara, Uhuru wa habari na Sheria kandamizi.

Wakipata haki hiyo waende wakahubiri na kufundisha watu maana na mabadiliko ya Katiba Tena kwa namna ya kutafuta suluhu ya kisiasa na sio kwa vitisho na kushindana. Na mwisho m chakato wa uundwaji Katiba usitawaliwe na wanasiasa.
 

Kudai Chadema wanakuchanganya kwenye hili ni kutokuwatendea haki.

Katiba inahitajika na wananchi ambao ndiyo watakayoiandika. Kumbuka katiba iliyopo iliandikwa na nani na kwenye mazingira gani?

Chadema hawajahitaji wanasiasa kuandika katiba bali wanataka mchakato wa katiba mpya kurejelewa.

Chadema kusukuma mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya uliosimama tangia 2015 tatizo liko wapi hapo? Labda kama wanakuchanganya kea kuuhitaji mchakato huu kurejelewa?

Kama wao wanakuchanganya kwa kutaka mchakato kurejelewa labda wewe ulipendelea nani basi waweke msukumo kwenye kulirejelea hili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…