CHADEMA mnatuchanganya. Tunataka Katiba inayosimamia haki na sio Katiba Mpya. Kamwe Katiba hiyo haiwezi kutengenezwa na Wanasiasa

Kitu wapinzani wanachofeli NI kuongozwa na hasira na ushindani na kupigania maslahi binafsi ya kisiasa hivyo kukosa logic na plan nzuri kufanikisha mipango yao.

Jk alianzisha mchakato wa Katiba mpya Ila mchakato mzima katika mazingira hayo ulitawaliwa na wanasiasa. Bunge lilijaa wanasiasa na kwa maamuzi yao lingeleta katiba mbovu Tena iliyoegemea kuibeba CCM kwani walikuwa wengi na wenye nguvu ya maamuzi. Wangekuja na katiba mpya lkn isiyofaa. Jk alijua akaitupilia mbali mwishoni.

Sasa mnavyoomba tuimalizie mchakato mnataka tuimalizie kwa staili hiyo hiyo?!

Je, mnataka katiba mpya au katiba nzuri?

Mi nadhani kwa busara CHADEMA ombeni tume huru na chaguzi za haki. Piganieni mabadiliko hayo ya Sheria na katiba Ila swala la katiba liacheni. Waacheni watu wasio wanasiasa watuundie katiba.

*Katiba itakayowasimamia na kuwawajibisha wanasiasa pia. Katiba hiyo wanasiasa hawawezi kuiunda.

*Katiba itakayojibu kila kitu na kuondoa mizengwe kwenye kila sekta kuanzia kilimo, biashara, Viwanda, madini na Mikataba yote isiyo ya kiusalama Kama madini na manunuzi, ubia, hesabu za taasisii na mashirika ya umma kuwa wazi kwa umma wakati wote.

*Katiba itakayomlazimisha mbunge kabla ya kwenda bungeni kwenye kikao chochote akae vikao vyenye maandishi angalau vitatu na wadau wote katika Jimbo lake na kuikusanya mawazo na Kisha kuyafikisha bungeni au serikalini na sio Sasa wabunge kwenda kuzungumza mawazo binafsi na marafiki zao wachache wanaokunywa nao bia vijiweni.

Bunge jipya la katiba lisizidi 10% ya wanasiasa. Waingie wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, bunge lijae wataalamu kwa 30% mfano walimu, madaktari, wanasheria na wachumi. Na wanaoshiriki kwenye bunge Hilo wakubali kutokugombea au kuteuliwa nafasi yoyote ya kisiasa au za kiuteuzi kwa miaka kumi ili kuondoa bunge Hilo Hilo kuja kugeuka chombo Cha utawala Mara baada ya kuunda katiba.
Bunge lililopita na mchakato mzima wa Katiba ndio uliowaibua akina polepole na Kabudi. Watu watashindwa kutoa mawazo kwa Uhuru wakitarajia hisani za watawala

Na nawaomba wimbo isiwe katiba mpya Bali tunataka katiba yenye kulinda haki. Na katiba yenye kutenda haki kamwe haiwezi kuletwa na wanasiasa. Kila sehemu wanasiasa huvutana tu kutafuta msindi. Kwenye katiba lazima kila mtu awe msindi.
Kila siku nauliza.

Wana uhakika gani kama hiyo katiba mpya itafuatwa?
 
Mataga ktk ubora wake
Ndio maana hayati JPM hakucheka na HAO JAMAA....

JPM alikuwa na maono....ni kweli vyama vingi vya UPINZANI BARANI AFRIKA viko kwa ajili ya kuchelewesha tu MAENDELEO....viko kuchochea UHASAMA...UTENGANO....VURUGU....

Vyama vingi vya Afrika viko kuona kila SERIKALI iliyoko madarakani INASHINDWA NA KUANGUKA hata Kama INAFANYA VYEMA....ni siasa mahsusi za "domokrasia" zilizoasisiwa KULETA SINTOFAHAMU HUMU AFRIKA...

Nitapingwa sana kwa kusema hayo....ila ukichunguza utamaizi kuwa kuna ukweli angalau 51%.....

#MamaSSHAnaupiga MWINGI
 
Hizi nchi za KIAFRIKA wakati mwingine zinahitaji misimamo kama ya watu aina ya hayati Magufuli.....

Mama SSH ni rais Bora mno....wanataka tu kumfelisha....hao jamaa hawana jema....kwao hayati JPM alikuwa mbaya....mama naye mbaya....yaani jamaa HOPELESS sana Khaaa 🤣🤣🤣
Sitaki kumbuka Magufuli kabisa
 
Yani mama apite mule mule kwa magu maana wanakosa adabu kwa hizi siku Mia za mama tumeona angalu vitu vinaanza kurudi kwenye mstari

Mwakani Kuna sensa unaitaji pesa, haya mchakato wa Katiba mpya unaitaji pesa mama anawambia uchumi wetu haupo sawa subilieni, wapi wao tunataka Katiba mpya

Haya akifanya ambayo wanayasema baada waseme sawa mama wanaanza mzodoa yani hawana wema so mama awanyooshe
CHADEMA wao wanataka hata leo bunge livunje, uchaguzi urudiwe ili na wao wapate madaraka.

Nchi hii ukisikiliza sana wanasiasa, unaweza kujikuta unatumika weee, mpaka unazeeka.

Kumbukeni wao siyo masikini.

Sasa hivi agenda za CHADEMA zote hazigusi maslahi ya mwananchi wa kawaida.

Huwezi kuwakuta wanaongelea Ajira, maji, afya, umeme, barabara, n.k

Wao siku zote wako busy na mambo ambayo ni ya faida kwao binafsi kama BUNGE LIVE, MIKUTANO YA HADHARA, TUME HURU, KATIBA MPYA.

Na kibaya zaidi kuna mambo ambayo unaona kabisa yalipaswa kushirikishwa watu wengi kama katiba, lakini unashangaa wao wanabagua watu na kujifanya wao ndio mabingwa wa hiyo agenda na wengine ni wasaliti.

Hamtaweza kufanikiwa kwa njia hii.

Mpaka sasa hata wananchi hawajashirikishwa kwenye hiyo agenda yao.

Ndio maana sasa hivi kila kundi lina agenda na mikutano yao.

Ukiwaita machinga, wanawake, wazee, wasanii, vyana vya wafanyakazi, vijana hawawezi kukwambia wanataka kwanza Tume huru na katiba mpya.
 
Ndio maana hayati JPM hakucheka na HAO JAMAA.

JPM alikuwa na maono....ni kweli vyama vingi vya UPINZANI BARANI AFRIKA viko kwa ajili ya kuchelewesha tu MAENDELEO, viko kuchochea UHASAMA...UTENGANO, VURUGU.

Vyama vingi vya Afrika viko kuona kila SERIKALI iliyoko madarakani INASHINDWA NA KUANGUKA hata Kama INAFANYA VYEMA....ni siasa mahsusi za "domokrasia" zilizoasisiwa KULETA SINTOFAHAMU HUMU AFRIKA.

Nitapingwa sana kwa kusema hayo....ila ukichunguza utamaizi kuwa kuna ukweli angalau 51%.

#MamaSSHAnaupiga MWINGI
Angekuwa na maono angeleftishwa na uviko?
 
Huu ndo ukweli ninaouamini siku zote. Chadema ikiingia madarakani hawawez kubadilisha katiba kwani itawabeba.

Wananchi tunataka uchumi mzuri, ajira, miundombinu ma uwekezaji na afya njema. Hivyo vikilatikana mengne yatafuata. Tatzo Chadema wanataka watimiziwe wao huju sisi tykiumia. Jiwe katunyoosha jaman watuache kidogo mama atupe neema wananchi. Haya mambo wanayoyataka sio kipaumbele chetu.
Huu ni mwaka wa ngapi tangu upate uhuru?
 
Kitu wapinzani wanachofeli ni kuongozwa na hasira na ushindani na kupigania maslahi binafsi ya kisiasa hivyo kukosa logic na plan nzuri kufanikisha mipango yao.

Jakaya Kikwete alianzisha mchakato wa Katiba mpya Ila mchakato mzima katika mazingira hayo ulitawaliwa na wanasiasa. Bunge lilijaa wanasiasa na kwa maamuzi yao lingeleta katiba mbovu Tena iliyoegemea kuibeba CCM kwani walikuwa wengi na wenye nguvu ya maamuzi. Wangekuja na katiba mpya lkn isiyofaa. Jk alijua akaitupilia mbali mwishoni.

Sasa mnavyoomba tuimalizie mchakato mnataka tuimalizie kwa staili hiyo hiyo?!

Je, mnataka katiba mpya au katiba nzuri?

Mi nadhani kwa busara CHADEMA ombeni tume huru na chaguzi za haki. Piganieni mabadiliko hayo ya Sheria na katiba Ila swala la katiba liacheni. Waacheni watu wasio wanasiasa watuundie katiba.

*Katiba itakayowasimamia na kuwawajibisha wanasiasa pia. Katiba hiyo wanasiasa hawawezi kuiunda.

*Katiba itakayojibu kila kitu na kuondoa mizengwe kwenye kila sekta kuanzia kilimo, biashara, Viwanda, madini na Mikataba yote isiyo ya kiusalama Kama madini na manunuzi, ubia, hesabu za taasisii na mashirika ya umma kuwa wazi kwa umma wakati wote.

*Katiba itakayomlazimisha mbunge kabla ya kwenda bungeni kwenye kikao chochote akae vikao vyenye maandishi angalau vitatu na wadau wote katika Jimbo lake na kuikusanya mawazo na Kisha kuyafikisha bungeni au serikalini na sio Sasa wabunge kwenda kuzungumza mawazo binafsi na marafiki zao wachache wanaokunywa nao bia vijiweni.

Bunge jipya la katiba lisizidi 10% ya wanasiasa. Waingie wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, bunge lijae wataalamu kwa 30% mfano walimu, madaktari, wanasheria na wachumi. Na wanaoshiriki kwenye bunge Hilo wakubali kutokugombea au kuteuliwa nafasi yoyote ya kisiasa au za kiuteuzi kwa miaka kumi ili kuondoa bunge Hilo Hilo kuja kugeuka chombo Cha utawala Mara baada ya kuunda katiba.

Bunge lililopita na mchakato mzima wa Katiba ndio uliowaibua akina polepole na Kabudi. Watu watashindwa kutoa mawazo kwa Uhuru wakitarajia hisani za watawala

Na nawaomba wimbo isiwe katiba mpya Bali tunataka katiba yenye kulinda haki. Na katiba yenye kutenda haki kamwe haiwezi kuletwa na wanasiasa. Kila sehemu wanasiasa huvutana tu kutafuta msindi. Kwenye katiba lazima kila mtu awe msindi.
Nadhani latina tunayoitaka haipo popote

Maana ni katiba, sera, miongozo, Sheria, taratibu, ushauri in one document

Must be a hell of a huge document
 
Kama si mh.Rais SSH hivi Hawa akina MDUDE NYAGALI wangetoka RUMANDE?

Kama si mh.Rais SSH hivi masheikh wa UAMSHO wangetoka RUMANDE?

Mungu ana funzo kubwa sana kwetu WATANZANIA.

Alimleta madarakani HAYATI JPM kuwa kama "REDEEMER".....JPM alikuwa FUNZO kwa makosa TULIYOFANYA ili tujirekebishe....baadaye akamleta Mh.Rais SSH....kwanza mwanamama....pili MPOLE NA MSIKIVU HASA kama lilivyo jina lake....hakika ni FUNZO NA ZAWADI KWETU WATANZANIA WENYE KUTAFAKARI....WENYE KUTAFAKARI....WENYE KUTAFAKARI.

Chadema wanataka kuiyumbisha NCHI....hawana lolote.....wana hadaa tu za KISIASA.

JPM mwamba,Mama SSH Mwamba!

#KaziInaendelea
#StaunchSupporterOfSSH
Wewe itakua ulizaliwa kabla ya muda yaani Njiti.rudi hospitali ukawekwe kwenye jokofu ukomae akili.
 
Chadema wanajisahaulisha kuwa TANZANIA ni nchi ya KIJAMAA...UJAMAA WA KIAFRIKA...na si ULIBERALI anaotuhadaa nao TUNDU LISSU.....

Tanzania si KENYA....na haitokaa iwe kama KENYA.....

Misingi ya UASISI wa taifa hili imeo ekana kama INAWACHELEWESHA baadhi ya "watu".....ila ndiyo INAYOLINDA AMANI....UMOJA WETU.....na UTU WETU....

Upekee wa WATANZANIA huupati popote pale....

Kenya imejaa UKABILA....
Kongo imejaa VURUGU....
Uganda nchi ya "KIJESHI"....
Burundi Kama "ilivyo".....
Rwanda Kama "ilivyo".....
Msumbiji uhasama na "UGAIDI"....
Ethiopia Kama "ilivyo"........
Somalia "ubaguzi wa KOO ,UGAIDI ,tabu tupu tabu tabu tupu"....
Nigeria UFISADI ULIOTOPEA ,UKABILA ,UGAIDI...tabu tupu tabu tupu"

KILA NCHI ni afadhi ya NYINGINE....

TANZANIA PEKEE ITABAKI NA UPEKEE WA AJABU......

TUENDELEE KUENZI TUNU ZETU KWA KUIUNGA MKONO CCM....

#ChadoomoWababaifu
#KaziIendelee
Umeongea ukweli mtupu. Tunao msingi mzuri tangu awamu ya Julius Nyerere.
 
Umeandika hoja nzito sana mkuu, hizi ndio fikra zilizoifanya JF ikapata jina.
 
Katiba ni jambo jumuishi ila tatizo ni kuwa wanasiasa ndio wenye uhitaji nayo sana ili kutimiza kiu yao kwa baadhi ya interest zao.

Wananchi watakapo ihitaji itakuja tu bila pressure za wanasiasa.

Ukitaka kujua kuwa madai ya katiba ni ya wanasiasa angalia wanachodai.

1. Tume huru ya Uchaguzi.

2. Kupunguzwa mamlaka ya Urais yatakayoathiri pia uwezo wa kuteua watendaji mbali mbali.

Madai yanayopigiwa chapuo mno ni ya wanasiasa tu wananchi wa kawaida wanatumika tu kuwabeba wanasiasa.
 
Swala la kitu gani kitakuwepo kwenye katiba ilo ni jambo jingine kwasababu ili uandae katiba lazima ushirikishe wananchi ili iandaliwe rasimu.ila kabla hatujafika uko lazima kuwe na kundi fulani kwenye jamii litakalo anza kupiga kelele uanzishwaji wa huo mchakato sasa nikuulize unadhani kwa nchi hii ilivyo tofauti na wanasiasa ni kundi gani jingibe linaloweza kupaza sauti kirahisi zikafika kwa wenye mamlaka ya kuanzisha huo mchakato?
 
CHADEMA wao wanataka hata leo bunge livunje, uchaguzi urudiwe ili na wao wapate madaraka.

Nchi hii ukisikiliza sana wanasiasa, unaweza kujikuta unatumika weee, mpaka unazeeka.

Kumbukeni wao siyo masikini.

Sasa hivi agenda za CHADEMA zote hazigusi maslahi ya mwananchi wa kawaida.

Huwezi kuwakuta wanaongelea Ajira, maji, afya, umeme, barabara, n.k

Wao siku zote wako busy na mambo ambayo ni ya faida kwao binafsi kama BUNGE LIVE, MIKUTANO YA HADHARA, TUME HURU, KATIBA MPYA.

Na kibaya zaidi kuna mambo ambayo unaona kabisa yalipaswa kushirikishwa watu wengi kama katiba, lakini unashangaa wao wanabagua watu na kujifanya wao ndio mabingwa wa hiyo agenda na wengine ni wasaliti.

Hamtaweza kufanikiwa kwa njia hii.

Mpaka sasa hata wananchi hawajashirikishwa kwenye hiyo agenda yao.

Ndio maana sasa hivi kila kundi lina agenda na mikutano yao.

Ukiwaita machinga, wanawake, wazee, wasanii, vyana vya wafanyakazi, vijana hawawezi kukwambia wanataka kwanza Tume huru na katiba mpya.
Unataka wayaongelee wapi hayo wkati unajua mikutano ya hadhara ilipigwa marufuku.Ata hivyo sio lazima chadema waseme kila kitu,ata wewe kwa nafasi yako unayo haki na wajibu wakusema hayo unayoyaona hayako sawa.Ata hivyo chadema wako smart kwasababu kama wameanza na hitaji la katiba maana yake wanataka kuwepo katiba bora itakayoweka na kurekebisha mambo mengi tunayoangaika nayo sasa yakiwepo hayo uliyoyataja.
 
Hayo ya Tume huru, katiba mpya na bunge live wanayasemea wapi ???
 
Wewe ni mpumbavu usiye na akili , mods futeni takataka hizi , unajua maana ya katiba we mbwa ? ,Au unadhani katiba ni Kwa ajili ya Chadema , ukawa au Act ? , Mazafaka
Daaah! Nimefafanua vizuri Sana, nahisi hujasoma Uzi wangu ata punje. Umesoma headlines tu ukajaa. MijadAla yenye tija haiitaji hasira. Jadili hoja Mzee. We ukiwa kiongozi si utachinjA kila mtu sasa
 
Swala la kitu gani kitakuwepo kwenye katiba ilo ni jambo jingine kwasababu ili uandae katiba lazima ushirikishe wananchi ili iandaliwe rasimu.ila kabla hatujafika uko lazima kuwe na kundi fulani kwenye jamii litakalo anza kupiga kelele uanzishwaji wa huo mchakato sasa nikuulize unadhani kwa nchi hii ilivyo tofauti na wanasiasa ni kundi gani jingibe linaloweza kupaza sauti kirahisi zikafika kwa wenye mamlaka ya kuanzisha huo mchakato?
Sijapinga swala la kupiga kelele. Kwanza wapiganie haki zilizopo kikatiba na wakapokonywa Kama mikutano ya hadhara, Uhuru wa habari na Sheria kandamizi.

Wakipata haki hiyo waende wakahubiri na kufundisha watu maana na mabadiliko ya Katiba Tena kwa namna ya kutafuta suluhu ya kisiasa na sio kwa vitisho na kushindana. Na mwisho m chakato wa uundwaji Katiba usitawaliwe na wanasiasa.
 
Kitu wapinzani wanachofeli ni kuongozwa na hasira na ushindani na kupigania maslahi binafsi ya kisiasa hivyo kukosa logic na plan nzuri kufanikisha mipango yao.

Jakaya Kikwete alianzisha mchakato wa Katiba mpya Ila mchakato mzima katika mazingira hayo ulitawaliwa na wanasiasa. Bunge lilijaa wanasiasa na kwa maamuzi yao lingeleta katiba mbovu Tena iliyoegemea kuibeba CCM kwani walikuwa wengi na wenye nguvu ya maamuzi. Wangekuja na katiba mpya lkn isiyofaa. Jk alijua akaitupilia mbali mwishoni.

Sasa mnavyoomba tuimalizie mchakato mnataka tuimalizie kwa staili hiyo hiyo?!

Je, mnataka katiba mpya au katiba nzuri?

Mi nadhani kwa busara CHADEMA ombeni tume huru na chaguzi za haki. Piganieni mabadiliko hayo ya Sheria na katiba Ila swala la katiba liacheni. Waacheni watu wasio wanasiasa watuundie katiba.

*Katiba itakayowasimamia na kuwawajibisha wanasiasa pia. Katiba hiyo wanasiasa hawawezi kuiunda.

*Katiba itakayojibu kila kitu na kuondoa mizengwe kwenye kila sekta kuanzia kilimo, biashara, Viwanda, madini na Mikataba yote isiyo ya kiusalama Kama madini na manunuzi, ubia, hesabu za taasisii na mashirika ya umma kuwa wazi kwa umma wakati wote.

*Katiba itakayomlazimisha mbunge kabla ya kwenda bungeni kwenye kikao chochote akae vikao vyenye maandishi angalau vitatu na wadau wote katika Jimbo lake na kuikusanya mawazo na Kisha kuyafikisha bungeni au serikalini na sio Sasa wabunge kwenda kuzungumza mawazo binafsi na marafiki zao wachache wanaokunywa nao bia vijiweni.

Bunge jipya la katiba lisizidi 10% ya wanasiasa. Waingie wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, bunge lijae wataalamu kwa 30% mfano walimu, madaktari, wanasheria na wachumi. Na wanaoshiriki kwenye bunge Hilo wakubali kutokugombea au kuteuliwa nafasi yoyote ya kisiasa au za kiuteuzi kwa miaka kumi ili kuondoa bunge Hilo Hilo kuja kugeuka chombo Cha utawala Mara baada ya kuunda katiba.

Bunge lililopita na mchakato mzima wa Katiba ndio uliowaibua akina polepole na Kabudi. Watu watashindwa kutoa mawazo kwa Uhuru wakitarajia hisani za watawala

Na nawaomba wimbo isiwe katiba mpya Bali tunataka katiba yenye kulinda haki. Na katiba yenye kutenda haki kamwe haiwezi kuletwa na wanasiasa. Kila sehemu wanasiasa huvutana tu kutafuta msindi. Kwenye katiba lazima kila mtu awe msindi.

Kudai Chadema wanakuchanganya kwenye hili ni kutokuwatendea haki.

Katiba inahitajika na wananchi ambao ndiyo watakayoiandika. Kumbuka katiba iliyopo iliandikwa na nani na kwenye mazingira gani?

Chadema hawajahitaji wanasiasa kuandika katiba bali wanataka mchakato wa katiba mpya kurejelewa.

Chadema kusukuma mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya uliosimama tangia 2015 tatizo liko wapi hapo? Labda kama wanakuchanganya kea kuuhitaji mchakato huu kurejelewa?

Kama wao wanakuchanganya kwa kutaka mchakato kurejelewa labda wewe ulipendelea nani basi waweke msukumo kwenye kulirejelea hili?
 
Back
Top Bottom