CHADEMA moja ya mafanikio yao, wamefanikiwa kuichonganisha Serikali na wananchi wake. Chuki ipo juu sana


Embu toka huko. 32M unafikiri ni mchezo. Unaleta utani hapa
 
Chadema ndiyo ilifanya mauaji ya Watanganyika 500+ Oktoba? Chadema ndiyo inafanya huu ufisadi wa kihayawani unaoendelea? Chadema ndiyo imefanya maisha yawe magumu sana mtaani? Chadema ndiyo inateka na kupoteza watu hovyo hovyo? Chadema ndiyo.......?

Angalizo: Sijasoma gazeti lote. Si ajabu umeshayajibu hayo maswali 🚶🏿‍♂️
 
Embu toka huko. 32M unafikiri ni mchezo. Unaleta utani hapa
Gentleman,
mchezo ni huo wa kujidanganya eti chuki ni mafanikio, kwasababu tu unaemchukia kakukalia kimya dhidi ya chuki zako.

But patashika nguo kuchanika,
huyo unaemchukia akija kusema ng'we, ndio mtaona motro wake, otherwise endeleeni kujidanganya tu na itapendeza zaidi 🐒
 
Ni kweli Magufuli alikuwa nginjanginja na Mafisadi, alipambana sana. Hata mimi namsifu kwa hilo kwani wote tulikuwepo na tunajua hilo.
Hapa umedanganya. Magufuli yule yule aliyemtimua CAG aliyefichua ufisadi? Yuleyule aliyependelea Mayanga construction? Yuleyule aliyewatajirisha vijana wake kina conductor & co? Yuleule ambae hatujui pesa za plea- bargain zilienda wai?
 
Ndio. Lakini, sio kiivo kwasababu Pesa inaongea laiti CCM kingekuwa chama fukara pangekuwa hapatoshi...Japo Pia CHADEMA nao chamoto wamekiona. CHADEMA kama mnataka kuishinda CCM imarisheni pia uchumi wenu wa kifedha.
 
Hivi wewe Robert Heriel Mtibeli ni Popo, ndege au sio popo wala ndege - yaani neutral kama ambavyo hujinasibu mzee Pascal Mayalla?

Bila shaka umeelewa logic ya swali langu, au siyo..?
 
Mkuu mimi ni CCM wa siku nyingi lakini unakuwa mpumbavu kufikiri kuna mwana CCM au CHADEMA anayeunga mkono utekaji na kesi za kubambika.
 
Serikali imejichonganisha yenyewe kwa kuminya haki na demokrasia.
Hakuna alieituma serikali yenu kuengua wagombea 2020.
Hakuna alieituma serikali apige stop mikutano ya kisiasa chini ya JPM, na badae huyo mama.
Chadema hawateki watu, kuwaua na kuwatesa.
Chedema haihusiki na ukosefu wa ajira wa nchi hii.
Chadema haihusiki na maendeleo kiduchu ya nchi hii.
Chadema haihusiki na wizi, ufisadi na rushwa za nchi hii.
Chadema haihusiki na rasilimali z mvhi hii kuzinufaisha familia za viongozi.

Hiki ulichondika ni propaganda; na ni utopian.
 
We the people have known all along that Serikali ya mazafakas haipo pale kwa maslahi ya wote.

Kitu pekee ambacho CHADEMA wamekifanya (na wanaendelea kukifanya) ni kuwapa wananchi elimu ya jinsi ya kuibadilisha hiyo hali. Wananchi wameambiwa (na wanaendelea kuaambiwa) it’s possible to change what they already don’t like. Huo sio uchonganishi.
 
Matatizo haya yameanzia kwa watawala;kufumbia macho na kunyamazia utekaji. mambo kama hayo hata sisi huku vijijini yamesababisha watu kuichukia ccm. Kibaya zaidi ni ule utaratibu wa kulitumia jeshi la polisi kwa manufaa ya ccm,yani polisi kutumika kisiasa. Chuki imezidi mno na hakika kukiwa na katiba mpya naa tume huru ya uchaguzi hicho chama kinaaga dunia
 
Chadema haina wananchi, Mungu gani aliiumba Chadema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…