CHADEMA moja ya mafanikio yao, wamefanikiwa kuichonganisha Serikali na wananchi wake. Chuki ipo juu sana

Ndiyo......
Lakini, sio kiivo kwasababu Pesa inaongea laiti CCM kingekuwa chama fukara pangekuwa hapatoshi...
CCM sio "chama cha siasa" rafiki. Jifunze, tafuta na utaelewa kuwa ni hivyo....
Japo Pia CHADEMA nao chamoto wamekiona.
Yeah...

TANU na kabla ya hapo TAA walikiona kwelikweli lakini waliwashinda waliokuwa na fedha, bunduki na connections (mkoloni Mwingereza).............. AND HERE WE ARE..!!
CHADEMA kama mnataka kuishinda CCM imarisheni pia uchumi wenu wa kifedha.
Jina lako ni MONEY IS NOT EVERYTHING lakini Cha kushangaza unadhani pesa ni kila siku, na kwamba kila wakati na kila mahali pesa inaweza kukuokoa au kukusaidia..... YOU'RE ABSOLUTELY WRONG...!!

La pesa nyingi zingekuwa na uwezo wa kuokoa, basi kina Mzee Reginald Mengi, Abbas Gulamali, Manji na wengine wengine wangetumia pesa zao kujiokoa, wasitwaliwe na mauti. Yaani wangemhonga Mr Death asiwachukue...

Na kwa taarifa yako pesa inafanya kazi Retrospectively. Inaweza kukua na inaweza kukuokoa sometimes, NOT ALWAYS...

KWENYE SIASA NA CHAMA CHA SIASA, Pesa ni muhimu lakini SIO KILA KITU...

Pesa inachangia kwa 25% tu kukifanya chama cha siasa kiwe hai

Chama cha siasa ni watu kukiunga mkono. Na ili chama cha siasa kiungwe mkono na umma ni lazima itikadi, sera, mipango zibebe maslahi ya umma..

Ukipata watu = wanachama, wafuasi, wapenzi na wanaokuunga mkono, umepata pesa...

Hujui tu usemalo kwa sababu penginee maana yako yako ya "chama cha siasa" ni tofauti na tunayoelewa sisi wengine...

Kwa taarifa yako tu, CHADEMA ni very strong economically kwa sababu kina wanachama, wafuasi na wapenzi kwa maelfu ndani na nje ya nchi. HAWA NDIO PESA ZENYEWE...!

Si umewaona figisu figisu wanazofanyiwa na watawala wahuni, mafisadi na wauaji wa CCM lakini hakijawa shaken na badala yake ndio momentum inaongezeka...?

Tukiwaacha CCM (ambao kiukweli sio chama cha siasa), umeviona vyama vingine ACT Wazalendo, CHAUMA, UDP, CUF, TLP, NCCR MAGEUZI nk wakifanya hata mkutano na wakapata wananchi kuwasikiliza kama ishara ya kuuungwa mkono kwao..?

Hujiulizi?

CHADEMA hawana mbunge, hawana Rais, hawana diwani wala Mwenyekiti wa Kijiji au mtaa lakini still wako very active ktk politics za nchi hii, wanatembea nchi nzima kujitangaza, kutangaza sera zao na kusema kasoro na mapungufu ya chama dola - CCM kinachoongoza serikali...

Kwa sababu hii wahuni na mataikuni, mafisadi na wauaji ndani ya serikali na CCM yao wanachukia kweli na kuwasagia meno CHADEMA. Na ndio maana ya huu moto wanaoupitia kama ulivyosema. Lakini usifikiri kuwa utadumu. Utazimika na umma utashinda tu. Historia na nature haijawahi kukosea kwenye hili kwa sababu, DAIMA WEMA/HAKI HUSHINDA UBAYA NA DHULUMA. NURU HULISHINDA GIZA...!!

Hii imewashitua walioko madarakani, wameshindwa kabisa kuelewa nini Siri ya kilicho nyuma ya CHADEMA. Hawaamini kuwa Siri kubwa inayokibeba CHADEMA na kukiweka juu ya playlist ni kuungwa mkono na umma/wananchi kwa kuwa kimebeba ajenda na interests za wananchi...

Kwa hiyo, FUTA HIYO IMANI YAKO. JINA LAKO MONEY IS NOT EVERYTHING linapaswa kusadifu Imani yako....!
 
Hamjambo!

Walianza na harakati za ufisadi miaka hiyo. Enzi hizo.
Kukemea mafisadi, kuyataja mafisadi. Waliopo na ambao hawapo.

Enzi hizo kina Slaa na wenzake. Walipaza sauti.
Kipindi hicho utekaji na mauaji yalikuwa kama Hayapo alikuwepo Mzee Kikwete. Na kama yalikuwepo basi ni kwa kiwango cha chini ambacho hakikuwa critical.

Wakafanikiwa kuaminisha CCM ndio ufisadi na ufisadi ndio CCM yenyewe.

Miaka zaidi ya 10 tangu 2005 mpaka 2015 agenda kuu ya CHADEMA ilikuwa Kukemea Ufisadi. Masakata mengi kama Escrow, Richmond, Meremeta n.k. yaliibuliwa.

Wimbo unaiombwa kila siku huwa Sala. Huwa imani. Hiyo ni falsafa ya kitibeli.
Hivyo Watanzania wengi wakaamini Umaskini wao, ukosefu wa miundombinu, huduma za kijamii, mishahara duni, mazingira ya kazi hatarishi yote hayo yanasababishwa na watawala mafisadi.

Mzee Kikwete alisalimika. Halikuwa jina maarufu katika maandiko ya kifisadi. Hakutajwa tajwa kabisa. Isipokuwa marafiki zake akiwemo Marehemu Lowasa.

Hivyo Mpaka 2015 CCM ilikuwa inashambuliwa zaidi kwa Ufisadi na Rushwa.
Na ilitambulika hivyo.

Mwaka 2015 alipoingia Hayati magufuli, upepo ulibadilika sana.

Magufuli baada ya kunusurika kuangushwa na Lowasa katika uchaguzi ule wa 2015. Hofu ikawa kubwa hasa ukizingatia 2020 sio mbali yaani miaka mitano kisiasa sio mingi.

Mbinu aliyoitumia Magufuli ni kutembelea upepo wa upinzani CHADEMA, kwa kuanzisha vita kali na mafisadi. Lengo likiwa kuwaondoa CHADEMA kwenye line. Hii ingewafanya CHADEMA kukosa agenda.

Ni kweli Magufuli alikuwa nginjanginja na Mafisadi, alipambana sana. Hata mimi namsifu kwa hilo kwani wote tulikuwepo na tunajua hilo.

Na akadhihirisha kuwa nchi hii inaweza kuendelea. Maendeleo aliyoyaleta kwa Muda mfupi yalithibitisha kwamba ni kweli nchi hii ilikuwa na ufisadi na ukiritimba.

Sasa upinzani wangekosa agenda. Lakini kwa bahati Mbaya sana. Magufuli anafanya kosa kubwa zaidi kuliko mtangulizi wake Mzee Kikwete.

Kosa la kunyima watu Uhuru, na tunapozungumzia watu tunazungumzia wanasiasa wenzake wa Upinzani. Lilikuwa Kosa kubwa sana la kimedani.

Kimedani, ni bora mtu asile wali nyama lakini awe huru, kuliko umlishe wali nyama, na gari na kila kitu lakini umfungue kwenye gereza la kutokuwa huru.
Kikwete alikuwa mjanja sana eneo hilo. Acha watu waongee, kula na kipofu usimguse mkono. Waache waongee usiku watalala.

Sasa Agenda haikuwa ufisadi tena. Agenda ikawa Haki za binadamu.
CHADEMA wakalia haki za binadamu kwa miaka mitano.
Huku Magufuli naye akitumia mfumo ambao haukuwa rafiki kwa wapinzani wake.

Filimbi za utekaji, kupotezwa na mauaji ikapulizwa. Hofu ikatanda kila mahali.
Wengi wakakalishwa, plasta midomoni. Hofu juu ya hofu.

Tishio kubwa kwa wanadamu ni Kifo. Watu huogopa kifo kuliko jambo lolote.

CCM ikajikuta ikipata character nyingine, kutoka kuwa Chama cha kifisadi kwenda kuwa Chama cha majangili, watekaji, na wauaji. Hivyo ndivyo CHADEMA wakawa wanakitangaza.

Na ukweli ni kuwa chadema na wanaharakati kwenye vitaya kukutangaza na kuaminisha jamii wamefuzu. Wanaiweza.

Magufuli alikubalika na wananchi wengi kwa sababu ya umaskini wa wananchi wenyewe. Kuthamini vitu kuliko UTU. Lakini bado walimkubali huku wakimuogopa.
Wapinzani wao hawakumkubali bado walikuwa kwenye wimbo.

Wakiimba wimbo wa Muuaji, katili, dikteta, asiyejali maisha ya watu. Mwenye kuthamini vitu kuliko utu. Huo wimbo uliimbwa sana na wapinzani

Lakini Magufuli na hapa CCM haitajwi sana isipokuwa yeye mwenyewe. Ni kama aliachiwa hivi. Kwani Ile vita yake na mafisadi ilimpa uadui na baadhi ya wanachama na viongozi wenzake huko CCM.

Magufuli naye akawa anaimba kusema yeye anapambana na mafisadi na kujenga nchi.
Wakiimba naye anaimba.
Wakicheza naye anacheza.
Waliomzidi aliwatishia na kuwanyamazisha.

Jina la Mzee Kikwete lilirudi kwenye Chati ya Mafisadi huku Jina la Lowasa likianza kuyeyuka na kupotea polepole.

Sasa Lowasa hakuonekana tena Fisadi kama alivyoimbwa miaka nenda rudi.

Ndani ya CCM huko kukawa na CCM Maya. Ni kama kiliundwa Chama ndani ya Chama. Huku CCM Mpya ikijiona kama yakizalendo sana na inapenda nchi. Alafu CCM makada wakiona wao ndio wenye Chama na waliokijenga Chama.

Sijui kwa kweli. Nafikiri na sithibitishi ila ni kama madai ya kuwezekana. Nahisi CCM makada kwa siri Iliwabidi wajiunge na upinzani kwa kuwapa taarifa ili kuwakabili CCM mpya.

Hapo ndipo Siri za serikali zikawa zinavuja sana. Yaani nchi nzima ilikuwa inaweza kupata taarifa ya kikao cha siri kilichofanywa na wakuu wa nchi.

CCM mpya wakajichanganya kwa watamuongezea miaka. Hili lilikuwa kosa la kimkakati ambalo wazo hili halikupaswa kutolewa mapema.

CHADEMA wakafanikiwa kuilabel CCM kuwa Chama katili.

Mwaka 2021 akaingia Samia. Hii ni baada ya Magufuli kufariki.
Samia yeye alikuja na mpango wake. Mpango kabambe.
Ni 4R zake alizoamini kuwa zitampa nguvu, ushawishi, na zitamfanya aongoze nchi yake kwa utulivu.

Mpango wake ulikuwa Mzuri sana. Hilo wengi tunalijua. Sisi wafuatiliaji wa mambo. Sisi Watibeli tulijua ule mpango wa 4R ulitosheleza zile nguzo za utibeli ambazo ni HAKI, KWELI, AKILI NA UPENDO.

Binafsi nikajiuliza, mfupa walioushindwa Wanaume, je mwanamke atauweza?

Alipongezwa.

4R ilizima agenda za Upinzani. Upinzani walikuwa kwenye hatihati kuingizwa kwenye line.

Changamoto haikuwa nje tena. Changamoto ya CCM ilibakia ndani. CCM Mpya dhidi ya CCM 4R. Wapo CCM walioamini mwanamke hapaswi kuongoza hasa kwenye nafasi kubwa kama ya urais. Wengine hawakuishia kuteta sirini walisema hadharani.

Kuungana kwa Samia na Chadema dakika za awali kuliwaumiza CCM Mpya ukizngatia ligi kali iliyokuwa inaendelea baina ya Serikali ya Magufuli na Wapinzani. Ilikuwa nginjanginja.

Samia alitaka kufuta Ile dhana iliyojengwa na CHADEMA kuwa CCM ni chama cha wauaji, watekaji, watu wasio na huruma.
Ni kweli Samia alisifiwa.
Ni kweli alipigiwa zumari na mapambio. Mama anaupiga Mwingi. Tena walioimba ni Upinzani

Sasa kumbe mambo hayaendi hivyo. Sifa zile alizopewa Samia hazikufurahisha baadhi ya watu. Hasa wasiomtakia mazuri. Ndivyo siasa zilivyo. Kila mmoja anataka yeye ndiye awe bora. Asinine.

Kimedani, ukitaka umguse panapouma mtawala basi gusa kiti chake. Ndio mbinu iliyotimuka. Magazeti yakaanza kuchokoza na kujaribu frequency za Samia. Lengo ni kupata metreband yake. "Samia hatagombea urais 2025" hahaha! Gazeti fulani liliandika kitu mfano wa hicho. Ilikuwa kuchokoa chokoa. Hii ni kumaanisha mchokoaji alitaka kujua future ya 2025. Ili wajue game itachezwaje mpaka 2021-2025.

Baada ya Samia kuchokozwa. Akajibu. Tangu hapo kipenga kilipulizwa Rashmi.
Nyimbo zikasimama
Marimba yakaacha.
Mama anaupiga mwingi ikakoma.

Jaribio linalofuata ni kipimo cha kugusa maslahi ya kiti ili ndoto ya 2025 kuendelea ikatike. Kumjaza aingie kwenye laini.

Chadema wanatangaza mikutano ya kudai Katiba Mpya. Nchi Nzima. Kipenga kikiwa kimelia.

Bado Samia anahangaika na 4R zake lakini anagundua yeye sio mahiri sana kutumia 4R huku wenzake wanamjia Juu.

Yupo kwenye mtihani. CCM mpya Vs CCM 4R. CCM mpya inajaribu kusema tuone utatumia njia gani. Si unajifanya wewe sio katili. Unautu. Mama wa 4R. Haya Sasa kula chuma hiko.

Mikutano inaitika. CHADEMA inachanja mbuga. Wafuasi wa jpm inawabidi waungane na CHADEMA sasa.

4R mwaka uleule zinashindikana. Mwenyekiti wa Chadema anawekwa ndani kwa kesi mbaya na ngumu ya kigaidi. Dadeki.
Sasa moto unakuwa umewaka

Kwisha. Kila kitu kimekwisha. 4R chali. Nguvu zinaanza kutumika. Mabavu.

Baadaye huko 2022 mwenyekiti Anatolewa. Lakini bado vita inakuwa kubwa sana kutokea kwa wapinzani na ndani ya CCM.

CCM wanatumia Kete yao muhimu kutaka kukigawa Chadema kupitia uchaguzi wao wa ndani. Huku kundi kubwa linalomsapoti Mbowe likimeguka baada ya kushindwa na kuhamia Chaumma. Lengo likiwa kudhoofisha CHADEMA lakini pia kupata mbadala wa chama pinzani ikiwa chadema wangesusa kwelikweli

Kukatisha stori.
2025 inafika, hali inakuwa ngumu zaidi kuliko awali.
Chadema wanabaki na ushindi uleule wa kufanikiwa kuichonganisha serikali na wananchi wake.

Huku chadema hao wakipata msaada kutokea makundi ya ndani ya CCM.

Kitu pekee ninachoona. Kama makundi hayo ya CCM ambayo najua itasemwa hayapo ila ukweli uliopo Moyoni yapo. Hayatakuwa kitu Kimoja. Hii inawapa advantage kubwa Chadema siku zijazo za usoni.

Nimemaliza

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Umeua kaka
 
2030 najua wanamuandaa mtu mwingine wakuja ku-clear cache za watangulizi wake. Yale makosa ataya clear na huo ndio mchezo wa mara kwa mara wa CCM. Mchezo wa Nyoka kujivua gamba au tai kujitoa manyoya ili yaje mapya

..hiyo script wananchi wameshaiona mwaka 2015.

..Na iliwezekana kwasababu wapinzani / Chadema walikubali kula matapishi yao kwa kumsimamisha mgombea aliyekuwa na tuhuma za ufisadi.

..sasa 2030, wapinzani, na CCM, wote wakisimamisha mgombea anayepinga MAUAJI, unadhani mgombea wa upande upi ataaminika kwa wapiga kura?
 
Iv ndugu unatumiaga nini kwenye kuandika ni simu au pc maana makala ndefu
 
Wanasiasa duniani kote wanajulikana kwa ma deals, u lobbyist, kutajirika, uroho na ulafi! Hata wa ULAYA, MAREKANI, SCANDINAVIA NA NK NK.
Ila wale AT LEAST KAZI INAFANYIKA! kuanzia miundombinu, huduma za afya, elimu, ustawi wa jamii, haki na hata raia wao kupata vi slesi vya keki ya taifa.
WA KWETU WAO KAMA NGURUWE! NI WAO WAO WAO NA FAMILIA ZAO TU!
SASA ULAFI NA UROHO GANI HUO! ITS MUCH KIBINADAMU!
 
..Ssh alikuwa na uwezo wa kuiokoa, na kui-rebrand Ccm. Kwa bahati mbaya, uwezo wake mdogo wa kiuongozi ndio chanzo cha Ccm kupoteza muelekeo, na umwagaji damu wa Oct 29.
 
Msifanye watanzania ni wapumbavu hawaoni utekaji, uuaji, maisha magumu, ukosefu wa ajira, ongezeko la chawa wanaolipwa mamilioni wakati watoto wao hawana viti wala madawati shule, matokeo ya fomsiksi ya kupikwa wakati watoto hawana hata uwezo wa div 4 ya miaka ya 80, chadema hawana cha kusema kama keki ya taifa inagawanywa kwa usawa hata wa 50% tu sio sasa zaidi ya 90% ipo kwa familia za wakuu wa sisiemu

Chadema hawana chochote walichochangia zaidi ya kutamka tu mateso wanayoyaona wananchi, wanasisiemu na vyama vingine, uzuri umaskini wa wanakaya hauchagui chawa wala mwanasisiemu, zinafaidi matunda ya nchi familia zisizozidi 1000 kati ya watu milioni 70 kasoro! Acha uchawa hata kama umelipwa kumbuka baba yako na babu yako walipo wanateseka tu huko machakani vudee hata kama we upo mbagala unaandika na kihongoze anakurushia muamala
 
Serikali imejichonganisha yenyewe kwa kuminya haki na demokrasia.
Hakuna alieituma serikali yenu kuengua wagombea 2020.
Hakuna alieituma serikali apige stop mikutano ya kisiasa chini ya JPM, na badae huyo mama.
Chadema hawateki watu, kuwaua na kuwatesa.
Chedema haihusiki na ukosefu wa ajira wa nchi hii.
Chadema haihusiki na maendeleo kiduchu ya nchi hii.
Chadema haihusiki na wizi, ufisadi na rushwa za nchi hii.
Chadema haihusiki na rasilimali z mvhi hii kuzinufaisha familia za viongozi.

Hiki ulichondika ni propaganda; na ni utopian.
Sahihi kabisa.

Huyu mtoa mada anaitaja Chadema kama vile wao ndio wameshika Dola.
 
Mkuu kuna mambo yako wazi kabisa, wala hayaihusu chadema, mfano; ukosefu wa ajira, rushwa, huduma mbovu za kijamii, utekaji, mauaji ya wanaokosoa serikali, kiburi cha viongozi, ukiukwaji wa haki za binadamu, kusigina katiba kwa makusudi, mihimili yote ya serikali kugeuka taasisi za chama tawala n.k

Kwa hali hii, watakao ipenda serikali ni wachache wanaonufaika nayo.
 
Wala
Chadema ndiye kisababishi, watekelezaji wengine.
CCM hawataki uzungumze. Wewe ukazungumza.
Msababishi ni nani?

Kihaki sio sawa. Haki za kisiasa. Siasa za demokrasia
Chadema sio kisababishi maybe iwe umezaliwa mwanzoni mwa miaka ya 2000 but to me I know haya yanayo tokea ni tatizo la muda mrefu sana since nyakati za mkapa Huko watu wamekuwa wakiulalamikia utawala wa CCM kutokana na Matendo yao kilichotokea now ni chuki iliyopo muda mrefu Kwa wananchi dhidi ya gavoo kukithiri zaidi Pasipo gavoo Kuji rekebisha
Chadema ndiye kisababishi, watekelezaji wengine.
CCM hawataki uzungumze. Wewe ukazungumza.
Msababishi ni nani?

Kihaki sio sawa. Haki za kisiasa. Siasa za demokrasia
Kuna wakati Huwa unazingua mwanangu

Kwani raia wa Tanzania wameanza kuilaumu ccm na Matendo yake baada ya chadema kupata power !?

Malalamiko ya wananchi dhidi ya serikali ya ccm hayajaanza kwenye prime ya chadema ni kitu ambacho kina zaidi ya 2 decades but kilichotokea now ni Hali ya wananchi hao kuchoka kuvumilia Mateso ya muda mrefu yanayo wakumba , Mbaya zaidi licha ya utesi huo kupungua au kuisha kabisa ndio kwanza Hali ya utesi Kwa wananchi inazidi kuongezeka ,

So unataka kuwafanya raia wa Tanzania kwamba hawana akili wanashikiwa akili na chadema kiasi hicho Kuna raia wengine hawana chama chochote Mimi nikiwemo mmoja wapo but still natambua kwamba ccm it's a worse, na nimeanza kuichukia ccm before hata chadema Haiko kwenye prime Yao ,

Wananchi sio wajinga wamesoma they can reason they can see huduma mbovu za kijamii miaka zaidi ya 50 nchi tangu ipate uhuru Kuna baadhi ya maeneo Hadi Leo maji tu hakuna umeme hakuna Barabara hakuna , masoko ya bidhaa zao wanazo zilima hakuna na watu hao wanaotoka kwenye hayo mazingira wamezaa watoto wao na kuwasomesha watoto baada ya kusoma wamepata mwangaza katika Fikra zao , nakuanza kutambua kwamba kumbe hawakustahiki kukosa huduma za kijamii ktk vijiji vyao au miiji Yao kumbe Hawa kustahiki kukosa kazi na kuishi kwenye umaskini uliota kubuhu ,

Mwisho wa siku vijana hao hao ndio wana amua kuamka na kuanza kudai haki zao kwasababu wamesoma wame elimika wamepata exposure na kutambua kwamba maisha yanavyokwenda ktk nchi Yao hayaendi sawa so

unataka kuniambia kwamba yote hayo watu hawayaoni Kwa macho Yao na kuyapima Kwa Fikra zao mpaka chadema waongee !!!?

Serikali ingekuwa inatenda haki na kuzingatia utawala wa democracy na sheria zake hao chadema wangepata wapi Time ya kuongelea yanayo fanywa na serikali!? Unashindwa kuelewa ni kwamba hata kama chadema wasingekuwa wanaongea kuhusu yanayo fanywa na serikali Kwa stage ambayo serikali hii imefikia ni lazima tu Kuna makundi ya watu wengine yangeibuka na kuipigia kelele serikali,

So solution ni Moja tu gavooo kuacha kufanya Yale wanayo yafanya wafuate Sheria walizo zitunga ,Watende haki halafu uone kama Kuna team ya wapinga serikali itakayo jitokeza ,
 
Wewe ni ***** mpumbavu mwenye njaa na tamaa ya mafanikio.
Baada ya kujiion unajua kubwabwaja. Umeona utumike kama mtaji wa kutfta ulaji kwa wenye uchu wa madaraka wenzio
 
Mbona kwenye takwimu Samia ndio Rais anayeongoza kwa kupigiwa kura na wananchi wengi zaidi ? Ni wananchi gani wamechoganishwa ? nyoosha maelezo
 
Back
Top Bottom