CHADEMA moja ya mafanikio yao, wamefanikiwa kuichonganisha Serikali na wananchi wake. Chuki ipo juu sana

Ndiyo......
Lakini, sio kiivo kwasababu Pesa inaongea laiti CCM kingekuwa chama fukara pangekuwa hapatoshi...
CCM sio "chama cha siasa" rafiki. Jifunze, tafuta na utaelewa kuwa ni hivyo....
Japo Pia CHADEMA nao chamoto wamekiona.
Yeah...

TANU na kabla ya hapo TAA walikiona kwelikweli lakini waliwashinda waliokuwa na fedha, bunduki na connections (mkoloni Mwingereza).............. AND HERE WE ARE..!!
CHADEMA kama mnataka kuishinda CCM imarisheni pia uchumi wenu wa kifedha.
Jina lako ni MONEY IS NOT EVERYTHING lakini Cha kushangaza unadhani pesa ni kila siku, na kwamba kila wakati na kila mahali pesa inaweza kukuokoa au kukusaidia..... YOU'RE ABSOLUTELY WRONG...!!

La pesa nyingi zingekuwa na uwezo wa kuokoa, basi kina Mzee Reginald Mengi, Abbas Gulamali, Manji na wengine wengine wangetumia pesa zao kujiokoa, wasitwaliwe na mauti. Yaani wangemhonga Mr Death asiwachukue...

Na kwa taarifa yako pesa inafanya kazi Retrospectively. Inaweza kukua na inaweza kukuokoa sometimes, NOT ALWAYS...

KWENYE SIASA NA CHAMA CHA SIASA, Pesa ni muhimu lakini SIO KILA KITU...

Pesa inachangia kwa 25% tu kukifanya chama cha siasa kiwe hai

Chama cha siasa ni watu kukiunga mkono. Na ili chama cha siasa kiungwe mkono na umma ni lazima itikadi, sera, mipango zibebe maslahi ya umma..

Ukipata watu = wanachama, wafuasi, wapenzi na wanaokuunga mkono, umepata pesa...

Hujui tu usemalo kwa sababu penginee maana yako yako ya "chama cha siasa" ni tofauti na tunayoelewa sisi wengine...

Kwa taarifa yako tu, CHADEMA ni very strong economically kwa sababu kina wanachama, wafuasi na wapenzi kwa maelfu ndani na nje ya nchi. HAWA NDIO PESA ZENYEWE...!

Si umewaona figisu figisu wanazofanyiwa na watawala wahuni, mafisadi na wauaji wa CCM lakini hakijawa shaken na badala yake ndio momentum inaongezeka...?

Tukiwaacha CCM (ambao kiukweli sio chama cha siasa), umeviona vyama vingine ACT Wazalendo, CHAUMA, UDP, CUF, TLP, NCCR MAGEUZI nk wakifanya hata mkutano na wakapata wananchi kuwasikiliza kama ishara ya kuuungwa mkono kwao..?

Hujiulizi?

CHADEMA hawana mbunge, hawana Rais, hawana diwani wala Mwenyekiti wa Kijiji au mtaa lakini still wako very active ktk politics za nchi hii, wanatembea nchi nzima kujitangaza, kutangaza sera zao na kusema kasoro na mapungufu ya chama dola - CCM kinachoongoza serikali...

Kwa sababu hii wahuni na mataikuni, mafisadi na wauaji ndani ya serikali na CCM yao wanachukia kweli na kuwasagia meno CHADEMA. Na ndio maana ya huu moto wanaoupitia kama ulivyosema. Lakini usifikiri kuwa utadumu. Utazimika na umma utashinda tu. Historia na nature haijawahi kukosea kwenye hili kwa sababu, DAIMA WEMA/HAKI HUSHINDA UBAYA NA DHULUMA. NURU HULISHINDA GIZA...!!

Hii imewashitua walioko madarakani, wameshindwa kabisa kuelewa nini Siri ya kilicho nyuma ya CHADEMA. Hawaamini kuwa Siri kubwa inayokibeba CHADEMA na kukiweka juu ya playlist ni kuungwa mkono na umma/wananchi kwa kuwa kimebeba ajenda na interests za wananchi...

Kwa hiyo, FUTA HIYO IMANI YAKO. JINA LAKO MONEY IS NOT EVERYTHING linapaswa kusadifu Imani yako....!
 
Umeua kaka
 
2030 najua wanamuandaa mtu mwingine wakuja ku-clear cache za watangulizi wake. Yale makosa ataya clear na huo ndio mchezo wa mara kwa mara wa CCM. Mchezo wa Nyoka kujivua gamba au tai kujitoa manyoya ili yaje mapya

..hiyo script wananchi wameshaiona mwaka 2015.

..Na iliwezekana kwasababu wapinzani / Chadema walikubali kula matapishi yao kwa kumsimamisha mgombea aliyekuwa na tuhuma za ufisadi.

..sasa 2030, wapinzani, na CCM, wote wakisimamisha mgombea anayepinga MAUAJI, unadhani mgombea wa upande upi ataaminika kwa wapiga kura?
 
Iv ndugu unatumiaga nini kwenye kuandika ni simu au pc maana makala ndefu
 
Wanasiasa duniani kote wanajulikana kwa ma deals, u lobbyist, kutajirika, uroho na ulafi! Hata wa ULAYA, MAREKANI, SCANDINAVIA NA NK NK.
Ila wale AT LEAST KAZI INAFANYIKA! kuanzia miundombinu, huduma za afya, elimu, ustawi wa jamii, haki na hata raia wao kupata vi slesi vya keki ya taifa.
WA KWETU WAO KAMA NGURUWE! NI WAO WAO WAO NA FAMILIA ZAO TU!
SASA ULAFI NA UROHO GANI HUO! ITS MUCH KIBINADAMU!
 
..Ssh alikuwa na uwezo wa kuiokoa, na kui-rebrand Ccm. Kwa bahati mbaya, uwezo wake mdogo wa kiuongozi ndio chanzo cha Ccm kupoteza muelekeo, na umwagaji damu wa Oct 29.
 
Msifanye watanzania ni wapumbavu hawaoni utekaji, uuaji, maisha magumu, ukosefu wa ajira, ongezeko la chawa wanaolipwa mamilioni wakati watoto wao hawana viti wala madawati shule, matokeo ya fomsiksi ya kupikwa wakati watoto hawana hata uwezo wa div 4 ya miaka ya 80, chadema hawana cha kusema kama keki ya taifa inagawanywa kwa usawa hata wa 50% tu sio sasa zaidi ya 90% ipo kwa familia za wakuu wa sisiemu

Chadema hawana chochote walichochangia zaidi ya kutamka tu mateso wanayoyaona wananchi, wanasisiemu na vyama vingine, uzuri umaskini wa wanakaya hauchagui chawa wala mwanasisiemu, zinafaidi matunda ya nchi familia zisizozidi 1000 kati ya watu milioni 70 kasoro! Acha uchawa hata kama umelipwa kumbuka baba yako na babu yako walipo wanateseka tu huko machakani vudee hata kama we upo mbagala unaandika na kihongoze anakurushia muamala
 
Sahihi kabisa.

Huyu mtoa mada anaitaja Chadema kama vile wao ndio wameshika Dola.
 
Mkuu kuna mambo yako wazi kabisa, wala hayaihusu chadema, mfano; ukosefu wa ajira, rushwa, huduma mbovu za kijamii, utekaji, mauaji ya wanaokosoa serikali, kiburi cha viongozi, ukiukwaji wa haki za binadamu, kusigina katiba kwa makusudi, mihimili yote ya serikali kugeuka taasisi za chama tawala n.k

Kwa hali hii, watakao ipenda serikali ni wachache wanaonufaika nayo.
 
Wala
Chadema ndiye kisababishi, watekelezaji wengine.
CCM hawataki uzungumze. Wewe ukazungumza.
Msababishi ni nani?

Kihaki sio sawa. Haki za kisiasa. Siasa za demokrasia
Chadema sio kisababishi maybe iwe umezaliwa mwanzoni mwa miaka ya 2000 but to me I know haya yanayo tokea ni tatizo la muda mrefu sana since nyakati za mkapa Huko watu wamekuwa wakiulalamikia utawala wa CCM kutokana na Matendo yao kilichotokea now ni chuki iliyopo muda mrefu Kwa wananchi dhidi ya gavoo kukithiri zaidi Pasipo gavoo Kuji rekebisha
Chadema ndiye kisababishi, watekelezaji wengine.
CCM hawataki uzungumze. Wewe ukazungumza.
Msababishi ni nani?

Kihaki sio sawa. Haki za kisiasa. Siasa za demokrasia
Kuna wakati Huwa unazingua mwanangu

Kwani raia wa Tanzania wameanza kuilaumu ccm na Matendo yake baada ya chadema kupata power !?

Malalamiko ya wananchi dhidi ya serikali ya ccm hayajaanza kwenye prime ya chadema ni kitu ambacho kina zaidi ya 2 decades but kilichotokea now ni Hali ya wananchi hao kuchoka kuvumilia Mateso ya muda mrefu yanayo wakumba , Mbaya zaidi licha ya utesi huo kupungua au kuisha kabisa ndio kwanza Hali ya utesi Kwa wananchi inazidi kuongezeka ,

So unataka kuwafanya raia wa Tanzania kwamba hawana akili wanashikiwa akili na chadema kiasi hicho Kuna raia wengine hawana chama chochote Mimi nikiwemo mmoja wapo but still natambua kwamba ccm it's a worse, na nimeanza kuichukia ccm before hata chadema Haiko kwenye prime Yao ,

Wananchi sio wajinga wamesoma they can reason they can see huduma mbovu za kijamii miaka zaidi ya 50 nchi tangu ipate uhuru Kuna baadhi ya maeneo Hadi Leo maji tu hakuna umeme hakuna Barabara hakuna , masoko ya bidhaa zao wanazo zilima hakuna na watu hao wanaotoka kwenye hayo mazingira wamezaa watoto wao na kuwasomesha watoto baada ya kusoma wamepata mwangaza katika Fikra zao , nakuanza kutambua kwamba kumbe hawakustahiki kukosa huduma za kijamii ktk vijiji vyao au miiji Yao kumbe Hawa kustahiki kukosa kazi na kuishi kwenye umaskini uliota kubuhu ,


Mwisho wa siku vijana hao hao ndio wana amua kuamka na kuanza kudai haki zao kwasababu wamesoma wame elimika wamepata exposure na kutambua kwamba maisha yanavyokwenda ktk nchi Yao hayaendi sawa so

unataka kuniambia kwamba yote hayo watu hawayaoni Kwa macho Yao na kuyapima Kwa Fikra zao mpaka chadema waongee !!!?

Serikali ingekuwa inatenda haki na kuzingatia utawala wa democracy na sheria zake hao chadema wangepata wapi Time ya kuongelea yanayo fanywa na serikali!? Unashindwa kuelewa ni kwamba hata kama chadema wasingekuwa wanaongea kuhusu yanayo fanywa na serikali Kwa stage ambayo serikali hii imefikia ni lazima tu Kuna makundi ya watu wengine yangeibuka na kuipigia kelele serikali,

So solution ni Moja tu gavooo kuacha kufanya Yale wanayo yafanya wafuate Sheria walizo zitunga ,Watende haki halafu uone kama Kuna team ya wapinga serikali itakayo jitokeza ,
 
Wewe ni ***** mpumbavu mwenye njaa na tamaa ya mafanikio.
Baada ya kujiion unajua kubwabwaja. Umeona utumike kama mtaji wa kutfta ulaji kwa wenye uchu wa madaraka wenzio
 
Ushaanza kupokea buku saba ewe jobless Herietha? takataka kabisa
 
Mbona kwenye takwimu Samia ndio Rais anayeongoza kwa kupigiwa kura na wananchi wengi zaidi ? Ni wananchi gani wamechoganishwa ? nyoosha maelezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…