CHADEMA msicheze Upatu kwenye Uenyekiti wa chama mtakuja kujuta

Kwa taarifa yako hakuna anayejali matokeo halali. Sisi ni wataka mabadiliko, hivyo hatuna tatizo lolote na mchakato au matokea ya uchaguzi halali.
Kama hamtajali matokeo ya uchaguzi huo utakuwa uhuni kama uhuni mwingine kitu ambacho hakikubaliki.
 
Chadema ingekuwa imekufa wakati huu ungekuwa unajadili UDP ya Cheyo au NCCR ya Lissu.
Chadema haiwezi kufa Kwa sababu ni Chama Cha Serikali

Chadema ni Sawa na UVCCM

Sidhani kama utaelewa 😂🔥
 
Kwa hli ilivyo hiki Chama kujiweka juu ya taifa ni heri kife tu, maana kumbe hakina tofauti na CCM ambayo imepelekea waliopo serikalini watumikie zaidi Chama kuliko nchim
Watu wanaothubutu kusema urais is nothing compared na Uenyekiti wa Chama...??? Na kwamba urais huwa hawaupi u-serious?
 
Kuna vitu ukiwa mtazamaji usieyekuwa na chama lazima utakiona
1. Chawa wa mbogamboga wanaojiona hii nchi ni mali yao na wao ndio wanastahili keki ya taifa
2. Chawa wa mwenyekiti wanaoamini chama ni mali yao na hakuna mbadala zaidi ya mwenyekiti
Hitimisho: sioni ajabu watu kutokuwa na mwamko katika kudai haki zao maana option A na B ni zilezile unaona kabisa wote wanatetea mifumo yao inayowawezesha kwenda chooni
 
Chadema haiwezi kufa Kwa sababu ni Chama Cha Serikali

Chadema ni Sawa na UVCCM

Sidhani kama utaelewa 😂🔥
Hivi vyama ni vya hiyari kama unaona Chadema ni chama cha serikali na hakiwezi kukufikisha kwenye malengo yako so why ung'ang'anie kubaki kwenye hicho chama.
 
Reactions: Tui
Kwanini unataka Chadema kife na sio vyama vingine zaidi ya 20 vife, kwani vyenyewe vinatimiza malengo yako.
 
Hivi vyama ni vya hiyari kama unaona Chadema ni chama cha serikali na hakiwezi kukufikisha kwenye malengo yako so why ung'ang'anie kubaki kwenye hicho chama.
Chadema inaendeshwa Kwa Kodi za Watanzania maskini

Ndio sababu Wananchi wote Kwa sasa Wanataka Mambo ya chadema yawekwe hadharani
 
Kwanini unataka Chadema kife na sio vyama vingine zaidi ya 20 vife, kwani vyenyewe vinatimiza malengo yako.
Watu huwa wanawachukulia CHADEMA very serious na wanajitoa hasa. Leo wanaibuka watu ndani ya CHADEMA wanatoa kauli zinazoonyesh yale malalamiko ya wagombea kukatwa , kuibiwa kura, kuvurugwa kwa uchaguzi na huwa si za kweli kwa sababu wao wanajua kushinda hawawezi
 
Lissu alimnukuu nyerere kwamba waliniambia mwalimu unataka kung'atuka hii nchi bado changa,lakini nikagundua wao wanahofia familia zao kwakuwa hawana uhakika kama uongozi mpya utawachagua na kuendelea kuwa katika nafasi zao

kwahiyo tutegemee chawa kulialia kwakuwa hawajui kesho yao
 
Chadema inaendeshwa Kwa Kodi za Watanzania maskini

Ndio sababu Wananchi wote Kwa sasa Wanataka Mambo ya chadema yawekwe hadharani
Mambo yepi yawekwe hadharani kasome ripoti ya CAG kila kitu kinachohusu ruzuku kipo mle, au unataka Chadema wakichangishana hata michango ya sendoff waweke hadharani.
 
Huu ni ukweli uliomchungu wasiotaka kusikia watawala wetu.....
 
Na akimtayarisha mtu wa kumrithi mtasema kuwa anataka kuleta utawala wa kiimla. Kiongozi makini anawapa wanachama wenzake uwezo wa kujichagulia kiongozi ambae wao wanaona anafaa sio kujipendekeza kwake kwa kuchagua mtu ambae yeye anamtaka. Kama kuna mtu anamtaka ataweza kumfanyia kampeni lakini bila kulazimisha.

Amandla...
 
Mkuu umeliweka vizuri, akiwekwa na Mbowe watasema chama cha ukoo, msimamo wangu wote waingie kwenye sanduku la kura atakayeshindwa avunje kambi wawe kitu kimoja.
 
Kama hamtajali matokeo ya uchaguzi huo utakuwa uhuni kama uhuni mwingine kitu ambacho hakikubaliki.
Naoina umenichukua nje ya muktadha, naamanisha hatutajali matokeo halali ya atakayeshinda au kushindwa. Kiufupi tutaheshimu matokeo yoyote halali, zingatia neno halali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…