Mkuu sipingi angalizo lao, lakini kulingana na uhuru wa vyombo vya habari huwezi kuwazuia kuandika wanachotaka. Ni juu ya CDM kusimamia wanachoamini. Hata hivyo wananchi wengi sio wasomaji wa magazeti. Na wanaosoma wanaweza kuelewa malengo ya kinachosemwa.
Kwangu mimi kama ni kweli Lisu na Mbowe wanapishana tena hadharani, hiyo ndio afya kwa CDM kwani kwanza ndio demokrasia, na ni rahisi sisi Wafuasi kujua yupi ni kiongozi sahihi kwa chama. Haya mambo ya viongozi kukubaliana kila kitu, ndio ilipelekea Lowassa kupokelewa ndani ya CDM bila kupima madhara ya jambo lile.