Chadema: Mtu akishakufa hatupaswi kujadili mabaya yake bali tunajadili mazuri yake ili tuyaendeleze

Kama isingekuwa mijadala tusingefahamu aliyoyafanya Bhokasa, Mobutu, Iddi Amin and so on. Historia ipo ili tujifunze yaliyopita, tuelewe yaliyopo na tupange yanayokuja.
 
Yule hakuiwakilisha Chadema, yeye ni mwanafamilia ,hivyo alichosema ni mtazamo wake kama mwanafamilia,sema tu una hamu sana kuitajataja Chadema, Mbowe na Lissu.
Yeye kasema akiwa mbele ya luninga kwamba ametumwa na mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe!
 
Kama isingekuwa mijadala tusingefahamu aliyoyafanya Bhokasa, Mobutu, Iddi Amin and so on. Historia ipo ili tujifunze yaliyopita, tuelewe yaliyopo na tupange yanayokuja.
Kwahiyo mchungaji Msigwa hayuko sahihi?
 
Wamehojiwa yeye na Prof Lipumba kila mmoja akiwakilisha chama chake!
Kwanini hawakupewa japo mmoja wapo kuongea kwa niaba ya Vyama Vya UPINZANI au kila mmoja kwa niaba ya Chama chake?!Mbona muda uliruhusu kabisa?
 
Mema na mabaya yote lazima yasemwe ili kuondoa unafiki kwani watu wana cha kujifunza kutokana na hayo yote..

Ukiona watu wanasisitiza mema tu ndio yasemwe basi ufahamu kuwa huyo marehemu alikuwa na maovu mengi kuliko mema na ndicho kinachosumbua kwenye swala la Magufuli kwani ametenda maovu mengi sana, hakujua angeweza kufa leo kwa kufikiria urais ungeendelea kumsaidia aendelee kuishi na hakujua kwamba Mungu hajui rais.
 
Kwanini hawakupewa japo mmoja wapo kuongea kwa niaba ya Vyama Vya UPINZANI au kila mmoja kwa niaba ya Chama chake?!Mbona muda uliruhusu kabisa?
Baba wa Demokrasia mzee Mwinyi aliwakilisha vyama vya siasa!
 
Mchungaji Msigwa amesema hakuna mtu aliye na mazuri tu, na mabaya yapo. Yanajadiliwa yote. Hiyo ITV inaripoti kujikomba lakini haibadilishi kitu.
Magufuli kaua, kavunja katiba na sheria za nchi, kateka na kawafanyia maovu mengi watu wasio na hatia. Katumia vyombo vya dola vibaya. Kajinufaisha na nagsi ya urais kujenga kwake.
Vyombo vya Habari viliandika kumsifia bila kukosoa.
Sasa angalia ukuu wa Mungu, kamchomolea betri na ndio mwisho wake. Wewe endelea na masifu yasiyo na mashiko.
 
Kwanza angeiwakilisha Chadema na angetambuliwa angepewa nafasi ya kuweka shada la maua kaburini. Yeye ni mwanafamilia.
Shada la maua limewekwa na mzee Mangula kwa niaba ya vyama vyote vya siasa!
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ really Mzee Mangula anaviwakilisha vyama vilivyouliwa na CCM.
Vyama vimejiua vyenyewe manka.

Kwa mfano chama kinafukuza uanachama wabunge 19 huko ndio kujiua kwenyewe!
 
Hata Mobutu Sese Seko Kuku Ngwendu wa Zabanga huwa yanasemwa Mabaya na Mazuri yake
 
Vyama vimejiua vyenyewe manka.

Kwa mfano chama kinafukuza uanachama wabunge 19 huko ndio kujiua kwenyewe!
Chama kinachounda serikali na kugundua kuwa kinahitaji wabunge wa upinzani bungeni baadae kimefilisika kisiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…