MAGALEMWA
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 6,413
- 4,889
Haya maelezo ya Msigwa acha mauongo.Mchungaji Msigwa ambaye amedai anaiwakilisha Chadema katika mazishi ya kijeshi ya hayati Magufuli kule Chato amesema mtu akifa kinachopaswa kujadiliwa ni mazuri aliyoyatenda ili yaendelexwe na kamwe si mabaya yake.
Mtumishi wa Mungu mchungaji Msigwa amesema hayati Magufuli ana mengi maxuri aliyotuachia ikiwemo mapambano ya rushwa na ufisadi, ulinzi wa rasilimali, nidhamu serikalini na dhana ya Kujitegemea ambavyo ni lazima vienziwe bila kujali itikadi za kisiasa, dini au kabila.
Source ITV habari
RIP Magufuli!
"Asante Mungu kwa zawadi ya maisha ya JPM.
Na Peter Msigwa.
Inawezekana ukawa sio muumini wa ukristo lakini Bibilia ni kitabu Chenye hazina kubwa ya mambo mengi unayoweza kujifunza ukiamua kisoma.
Nashauri uwe unaisoma Bibilia.
Bibilia imerekodi watu wengi maarufu na mashuja kama Daudi, Samson,Abraham. Lutu nk.
Bibilia haijasita kurekodi mambo yao mabaya waliyoyafanya, na pia mambo yao mazuri waliyoyafanya wakati wa uhai wao. Ukijifunza maisha yao kuna wakati walifanya mambo ya hovyo sana , lakini hawa ni Mashujaa wa imani.
Inatufundisha Kuwa Kila binadamu ana pande mbili za maisha yake , upande mbaya na upande mzuri, na Huu ndio ubinadamu wenyewe.
Mtu Mwerevu atajifunza yote yaani mambo mabaya na mazuri, mambo yenye akili na mambo ya kijinga pia .
Atajifunza mambo mabaya na ya kijinga , ili asirudia kufanya mambo mabaya na ujinga kwa kuwa mambo mabaya na ujinga, Una madhara.
Atajifunza pia mambo mema na yenye akili ili kufanya kwa ubora zaidi kwa ajili yake na vizazi vijavyo.
Nakiwa njiani kutoka Chato kumzika Rais JPM , nimetafakari sana nikiwasikiliza waombolezaji na Nyimbo mbalimbali. Yeye amemaliza maisha yake hapa duniani.
Tusisahau Kuwa JPM alikuwa binadamu na alikuwa na pande mbili Yaani ubaya na uzuri!
Tusiige ubaya wake na wala tusi ufanye.
Tujifunze mazuri yake na tuyafanye kwa vizuri zaidi.
Katika uchumi aliweza wapi na alishindwa wapi?
Uhuru wa habari aliweza wapi alishindwa wapi?
Demkrasia aliweza wapi alishindwa wapi!
Kuilinda katiba ya nchi aliweza wapi alishidwa wapi?
Mahusiano ya kimataifa aliweza wapi alishindwa wapi!
Yapi tuyachukue katika uongozi wake ? Na yapi tusiyachukue?
Haya ni maswali tunapswa kujiuliza kama taifa kwa Kila anayetuongoza, ili Viongozi watakaofuata wasirudie makosa.
Tunapoendelea kuomboleza tuendelee kuyatafakari haya."