GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Taarifa ambazo ni za SIRI mno na ambazo zimepatikana kwa ugumu mkubwa sana tena wa kujitoa mhanga kutokana na unyeti wake zinasema kwamba muda wowote kuanzia sasa Uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA unakusudia kutangaza kusitisha mpango wake wa kufanya maandamano ya UKUTA yaliyopangwa kufanyika tarehe 1 September 2016.
Taarifa hiyo imedai kwamba sababu kubwa ya CHADEMA kuamua hivyo ni kuona kuwa kwa sasa Uongozi wa CCM unafanya Kazi yake vizuri tu na kwamba hayo mapungufu mengine ni madogo sana ambayo yanaweza tu kuzungumzika bila hata ya kufanya maandamano.
Wakati hayo yakiendelea inasemekana pia kuwa muda wowote kuanzia sasa CHADEMA wanajipanga kuitisha Mkutano na Waandishi wa Habari nchini Tanzania ili kuwaomba radhi Watanzania kwa usumbufu wowote waliowapa na kwamba sasa yameisha na CHADEMA inaenda kuwa ya AMANI, UTU na UPENDO.
Mwisho mnyetishaji wangu amesema kuwa sasa CHADEMA walichoamua kukifanya ni kwamba siku hiyo ya tarehe 1 September 2016 wataomba tu kuonana na Mheshimiwa Rais ili kuitumia kama kumpongeza kwa Uongozi wake mzuri na madhubuti na wakitoka hapo wataelekea pia Makanisani na Misikitini kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumwombea mafanikio mema Rais na kutubu dhambi zao zote kwa Maulana.
Kama hii taarifa ni ya UKWELI basi naomba nichukue fursa hii adhimu kuwasifu na kuwapongeza sana Wanachama wote wa CHADEMA na Uongozi wao wote wa juu na labda niseme tu kama CHADEMA wameamua kuwa na hii busara nina uhakika kuwa sasa Saisa za Tanzania zimekomaa na CHADEMA imeonyesha AFYA katika Demokrasia.
Hongereni sana CHADEMA, tusameheane na tujenge nchi yetu hii kwa pamoja na kwa wale ambao walikuwa pengine wakijipanga kwa Oparesheni UKUTA sasa ni rasmi kuwa CHADEMA imeusitisha na HAUTAKUWEPO tena. Ngoja nitege sikio nisikilize hiyo Press Conference yao ya muda mfupi ujao ambapo watatangaza rasmi kusitisha UKUTA.
CCM na CHADEMA sasa ni Ndugu moja kwa maslahi ya Mama Tanzania.
Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki CCM na CHADEMA
Pepo baya la UKUTA potea,shindwa na lilegee.
===========
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kuwa chama chake kiko tayari kusitisha mikutano na maandamano ya Septemba 1 yaliyotajwa kuwa sehemu ya Operesheni UKUTA, endapo yataanzishwa mazungumzo kutafuta muafaka.
Mbowe ambaye hivi sasa yuko kanda ya Kaskazini akipanga mikakati na viongozi wa chama hicho kuhusu namna ya kuratibu na kutekeleza operesheni UKUTA, amesema kuwa wako tayari kusitisha mpango huo na kushiriki mazungumzo yoyote yatakayoanzishwa.
“Tutashiriki mazungumzo yoyote ya kusaka muafaka na kama matamko ya Rais Magufuli yakibalishwa. Tutawaeleza wanachama kusitisha mikutano ya Septemba 1 na kuendelea na mikutano ya kawaida,” alisema Mbowe.
Kiongozi huyo wa Chadema alitangaza kufanyika kwa Operesheni Ukuta nchi nzima na kwamba Kamati Kuu ya Chama hicho imeridhia kufanya maandamano na mikutano nchi nzima kwa lengo la kupinga kile walichodai ni kuminywa kwa demokrasia ndani na nje ya Bunge.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amewataka kusitisha maandamano hayo akieleza kuwa kama walizoea kutikisa kiberiti, wakati huu hiki ni kiberiti cha gesi.
Source: Dar24