Tetesi: CHADEMA muda wowote kusitisha Oparesheni UKUTA

Status
Not open for further replies.
Michezo mingine haihitaji hasira, sasa kuna watu mishipa imekaza kisa hasira kwa mchezo huu!
 
Nyie watu wa ajabu sana akitangaza UKUTA mnalialia sasa anataka kusitisha mnalialia, tuwaeleweje? Mnajua lengo la UKUTA? Hizi ni dalili kuwa mnapiga kelele tu bila kueLewa dhana nzima ya UKUTA

Wasira aliyesema CDM itakufa kabla ya sijui 2010 leo ametoka hadharani na kuona logic behind UKUTA lakini nyie wamezaji ndio hamuelewi
Kijana huyo ni Mbowe kasema.
 
This time watanzania tumechoshwa na udikteta. Yaani mtawala anataka atufunge mdomo hata tusipate nafasi ya kutoa maoni yetu. Kwa mfano Dr. Kimei alipobainisha kwamba CRDB wamesitisha mikopo kwa sababu uchumi umeyumba akaonekana ameisaliti serikali then ikakanushwa bila hata kuzingatia uhalisia wa taratibu za sasa za benki hiyo. Hali kadhalika watu wa bandari walipotoa taarifa ya kupungua kwa mizigo na kushuka kwa mapato pia walitakiwa kukanusha.
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kuwa chama chake kiko tayari kusitisha mikutano na maandamano ya Septemba 1 yaliyotajwa kuwa sehemu ya Operesheni UKUTA, endapo yataanzishwa mazungumzo kutafuta muafaka.

Mbowe-1.jpg

Freeman Mbowe akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chadema, Kanda ya Kaskazini

Mbowe ambaye hivi sasa yuko kanda ya Kaskazini akipanga mikakati na viongozi wa chama hicho kuhusu namna ya kuratibu na kutekeleza operesheni UKUTA, amesema kuwa wako tayari kusitisha mpango huo na kushiriki mazungumzo yoyote yatakayoanzishwa.

“Tutashiriki mazungumzo yoyote ya kusaka muafaka na kama matamko ya Rais Magufuli yakibalishwa. Tutawaeleza wanachama kusitisha mikutano ya Septemba 1 na kuendelea na mikutano ya kawaida,” alisema Mbowe.

Arusha.jpg

Baadhi ya viongozi wa Chadema Kanda ya Kaskazini wakimsikiliza Mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe

Kiongozi huyo wa Chadema alitangaza kufanyika kwa Operesheni Ukuta nchi nzima na kwamba Kamati Kuu ya Chama hicho imeridhia kufanya maandamano na mikutano nchi nzima kwa lengo la kupinga kile walichodai ni kuminywa kwa demokrasia ndani na nje ya Bunge.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amewataka kusitisha maandamano hayo akieleza kuwa kama walizoea kutikisa kiberiti, wakati huu hiki ni kiberiti cha gesi.
 
Hakika mkuu umeileta kama ilivyotakiwa...ninanukuu picha hizi kuongeza mvuto wa hoja.
 
1: hiyo kauli imetolewa wapi? Maudhui gani?

Polisi na hii serikali ya Magufuli inajua ni kiasi gani chadema imewekeza katika hiyo operation UKUTA na wanajua vyema Kuwa hili swala haliwezi pita kama wengi wenu mnavyojifariji humu ndani.

Kama ni kweli hiyo kauli imetolewa na Kamanda Mbowe, basi ni wazi Kuwa maandalizi ya UKUTA yameshakamilika kwa zaidi ya asilimia 95% na kinachofanyika ni kumalizia kujenga msingi wa kumfikisha Mfalme Inc tarehe husika
 
Kama wameamua kusitisha maandamano basi hiyo tarehe 1/9/2016 wana CHADEMA wafanye hata usafi wa mitaro na KUTA mbalimbali zinazozunguka majengo mbalimbali. Uchafu bado ni kero kubwa sana mitaani.
Tatizo CHADEMA hawana hata ofisi
 
1: hiyo kauli imetolewa wapi? Maudhui gani?

Polisi na hii serikali ya Magufuli inajua ni kiasi gani chadema imewekeza katika hiyo operation UKUTA na wanajua vyema Kuwa hili swala haliwezi pita kama wengi wenu mnavyojifariji humu ndani.

Kama ni kweli hiyo kauli imetolewa na Kamanda Mbowe, basi ni wazi Kuwa maandalizi ya UKUTA yameshakamilika kwa zaidi ya asilimia 95% na kinachofanyika ni kumalizia kujenga msingi wa kumfikisha Mfalme Inc tarehe husika
Mpigie simu Mbowe atakujulisja
 
Hatutakubali kusimamisha mikutano, tunachohitaji ni ulinzi tu basi full stop

Si mumesema maandamano ni ya amani sasa ulinzi wa nini?

Kumbe mnafahamu pia maandamano haya yanaweza kuhatarisha usalama wa watu na mali zao? Maana kufanya maandamano na mikutano nchi nzima tena kwa siku moja, sidhani kama kuna jeshi linaloweza kukuhakikishia usalama wako maana kuna waovu pia watatumia fulsa hiyo.

Na kwa kuwa maandamano haya yametawaliwa na itikadi za kisiasa hususan wa vyama hivi viwili, hivyo tegemea mambo kama ya kuchomeana ofisi za vyama, na hapa ndipo vurugu zitakapoanzia. Tusubili tu tuone, maana wakati mwingine matokeo ya kile unachotamani kukifanya hutoa majibu sahihi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom