thegreat1510
JF-Expert Member
- Mar 2, 2021
- 1,523
- 4,040
Hii nchi inazidi kupotea kila kukicha , tunazidi kuingia gizani tusijue tutatokaje.
Wahuni wa CCM, wametudharau sana.
============
KUHUSU KUPELEKWA GEREZANI MWANACHAMA WETU DEOGRATIAS PIUS MUSHI KABLA YA KUFIKISHWA MAHAKAMANI.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tumepokea kwa mshtuko taarifa ya Mwanachama wetu Deogratius Pius Mushi, Mkazi wa Mbezi Kibanda cha Mkaa Jimbo la Kibamba aliyekamatwa tarehe 2 Novemba, 2025 na kupelekwa moja kwa moja gerezani kabla ya kufikishwa mahakamani.
Mushi aliyekamatwa nyumbani kwake Kibanda cha Mkaa, Jimbo la Kibamba Manispaa ya Ubungo amepelekwa gereza la Mkuza lililopo Kibaha mkoani Pwani.
Taarifa zetu zinaonesha kwamba, wako wananchi zaidi ya 30 wanashikiliwa Gereza la Mkuza lakini hawakuhukumiwa kwa mujibu wa sheria wala hawakuwahi kupelekwa mbele ya Mahakama.
Chadema tunamtaka Kamishina wa Magereza nchini kuueleza umma utaribu upi ulitumika kuwapokea na kuwahifadhi wananchi hao ambao hawakufikishwa Mahakamani.
Tunasisitiza wananchi hao kuachiwa mara moja na wote waliohusika na kuwashikilia kinyume na utaratibu wawajibishwe.
Imetolewa leo Jumamosi, tarehe 20 Desemba, 2025 na;
Brenda Rupia
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi