Hili bomu jingine lisilojitambua. Alikuwa Mtanzania aliyejidai kutetea utawala bora. Ikaja kudhihirika ni mganga njaa tu wa CCM. Anataka ubunge huko Mbeya.
Nawe hauko tofauti sana na George Mwakalinga.
Mkuu,
Malizana na ya CHADEMA kwanza kabla hujaanza kurukia ya wengine.
Mtu anayejitegemea kwa kazi yake hawezi kuwa mganga njaa labda hata kama hujui maana ya maneno unayoyatumia.
Mtanzania ni mtetezi wa utawala bora na ataendelea kufanya hivyo popote pale atakapokuwa.
Tatizo la Tanzania sio vyama ni watu. Kuingia CCM au kuingia CHADEMA hakuwezi kumfanya mtu safi achafuke kama ambavyo hakuwezi kumfanya mtu mchafu asafishike.
Viongozi wetu ni refection ya sisi wananchi. Watanzania ninaowajua mimi, wengi ni wababaishaji tu. Prove here kwamba wewe sio mmoja wa wababaishaji hao. Maneno mengi, kubwabwaja kwingi, vitendo sifuri; hiyo ndio sifa ya wengi hapa JF.