CHADEMA mwendo mdundo

CHADEMA mwendo mdundo

Hili bomu jingine lisilojitambua. Alikuwa Mtanzania aliyejidai kutetea utawala bora. Ikaja kudhihirika ni mganga njaa tu wa CCM. Anataka ubunge huko Mbeya.

Nawe hauko tofauti sana na George Mwakalinga.

Mkuu,

Malizana na ya CHADEMA kwanza kabla hujaanza kurukia ya wengine.

Mtu anayejitegemea kwa kazi yake hawezi kuwa mganga njaa labda hata kama hujui maana ya maneno unayoyatumia.

Mtanzania ni mtetezi wa utawala bora na ataendelea kufanya hivyo popote pale atakapokuwa.

Tatizo la Tanzania sio vyama ni watu. Kuingia CCM au kuingia CHADEMA hakuwezi kumfanya mtu safi achafuke kama ambavyo hakuwezi kumfanya mtu mchafu asafishike.

Viongozi wetu ni refection ya sisi wananchi. Watanzania ninaowajua mimi, wengi ni wababaishaji tu. Prove here kwamba wewe sio mmoja wa wababaishaji hao. Maneno mengi, kubwabwaja kwingi, vitendo sifuri; hiyo ndio sifa ya wengi hapa JF.
 
Ngoja awaudhi wenye chama ndio atajua unachooongea..dogo bado anabebwa kwa nepi...
Siasa za Tanzania upande wa vyama vya upinzani zimejaa kila aina ya vibweka toka enzi za NCCR mpaka leo hii tunaona na Chadema pia. Lakini mi mtazamo wangu ni kuwa Chadema lazima kipitie majaribu makubwa ili kiwe chama imara. Sasa ni kwao Chadema kutuzihirishia kwamba they can survive the test of time. Maana ni kweli vyama vingi vya upinzani vimekuwa kama NGO za watu vile.Ukikosana kimtazamo na hao wakubwa then you are out!Na lingine ni hii infiltration ya watu wanaonia kuvusambaratisha
 
hivi wewe mbona unawashwa san na mambo ya CHADEMA??kama unapenda siasa si uanzishe chama chako.personally unini bore sana.Unakuwa kama voyeur ...kazikuchungulia mambo ya watu
walioandika ni gazeti la Mwananchi,usinisakame mimi?anayewashwa MBOWE na Asha Abdala adi leo hajaolewa na analipuliza.
 
Acha pumba zako chadema ndiyo maana mlimuondoa Zitto kuwa mwenyekiti kwasababu ni chama cha wakrisro na wachagga..angalia safu yake uongozi...MDINi mkubwa wewe...
akili fupi, mawazo duni , mdini, mshari, usie na dira, umekata tamaa, masikini wa fikra, shame on you.
 
akili fupi, mawazo duni , mdini, mshari, usie na dira, umekata tamaa, masikini wa fikra, shame on you.
Akili fupi, mnafiki,mdini, mpumbavu, huna dira, mlevi, unapenda vya bure hasa pombe, maskini wa fikra, shame on you lol.
 
Ungeniuliza ni kiongozi gani wa chama cha siasa una-appreaciate uongozi wake so far ningesema..ni "Ibrahimu Lipumba" wa CUF

Kwanini, chama kimelaumiwa sana kuwa na cha kidini lakini kila siku wanajitahidi na unaona viongozi wanafanya hivyo kwa vitendo...kuwa chama cha kitaifa...inapenetrate sehemu na kona zote za nchi.. hajalaumiwa uadilifu wake iwe katika kuonea mwanchama au kufisadi fedha za chama, hana njaa na ni msomi muadilifu..that is my take.

Umesahau walivyomfanya Prof. Safari alivyogombea nafasi ya mwenyekiti??
 
Umesahau walivyomfanya Prof. Safari alivyogombea nafasi ya mwenyekiti??
Walimfanyeje?
Prof. Safari kama lowassa kapewa nafasi ajieleze wananchi wakamuuliza maswali, akijibu alivyojibu, akakosa kura anazira ebo? kama lowassa alivyoambiwa atoa maelezo au apime mwenyewe akazira? ebo ..watu wanaendelea
 
na imani mmejitoa kufanya mapinduzi ya nchi hii kazeni buti tu acheni kusikiliza rongo rongo za watu ,migogoro ni sehemu ya maisha na ndio inasababisha kukua kwa chama imarisheni chama na kumbukeni tu si lazima upendwe na kila mtu ..
Pia katika msafara wa mamba na Kenge wamo
wish you all the best
mie sijaamua kuweka msimamo wangu wapi mpaka sasa ...
 
CHADEMA, mkubali-mkatae, viongozi mna matatizo!

Alianza aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Marehemu, Chaha Zakayo Wangwe, ambaye alizungumza waziwazi kuwa CHADEMA kuna matatizo ya kiuongozi. Viongozi wakuu wakamjia juu kuwa anakihujumu Chama na anataka kukigawanya. Agenda kuu ya Chacha Wangwe wakati akigombea Uongozi ilikuwa ni kufanya mageuzi katika Chama ili Chama kianzie chini matawini na kutaka kuwa ruzuku inayop[taikana pia ityumika kuimarisha Chama matawini (nao wagawiwe ruzuku). Viongozi wenzake hasa Mwenyekiti wa Chama walimuona Wangwe kuwa ni tatizo ndani ya Chama na wakaanza mikakati ya kumg’oa kutoka uongozi wa CHADEMA! Bahati mbaya alifariki kwa ajali kule Kongwa, ajali mabayo ilileta mtafaruku mkubwa na baadhi ya watu wakaunganisha tofauti baina yake Wangwe na Mwenyekiti wake Mbowe kuwa ndizo chanzo cha kifo-ati ajali ilipangwa na viongozi wa CHADEMA ili kuondoa tatizo (Wangwe)!

Hivi karibuni katika hali isiyyo ya kawaida, Zitto Kabwe alitangaza kugombea Uenyekiti wa CHADEMA dhidi ya Mbowe, hali ambayo si ya kawaida baina ya watu (viongozi wenye msimamo au mlengo unaofanana? Tukajiuliza kwanini Zitto achuane na Mwenyekiti wake Mbowe? Kwa nini asigombee nafasi ya Makamu Mwenyekiti au hata Uenyekiti wa Vijana? Wazee wa Chama kwa hekima wakamshinikiza Zitto ajiengue kwenye kinyang’anyiro hicho! Kwa wachambuzi wa mambo hatua ya Zitto kugombea dhidi ya Mbowe ilikuwa ni ishara kuwa CHADEMA kuna tatizo hasa kwenye safu ya Uongozi wa Kitaifa. Wapenda mageuzi tuliunga mkono hatua ya Zitto kujiengua kwa ajili ya mustakabali wa Chama. Katika kipindi hicho hicho cha uchaguzi wa Viongozi wa CHADEMA Kitaifa, Katibu Mkuu wa CHADEMA alitengua ushindi wa Davidi Kafulila baada ya kushinda Uenyekiti wa BAVICHA- Baraza la Vijana la CHADEMA kwa madai kuwa uchaguzi ulivurugwa! Hilo nalo lilikujwa ni doa kubwa kwa upande wa Viongozi wakuu wa CHADEMA maana wengine walimchukulia Kafulila kuwa ni mfuasi wa karibu wa Zitto na hilo ni kweli maana ni kama vile Zitto alishajipanga na timu yake kuchukua nafasi za juu za Uiongozi wa CHADEMA kitaifa.

Kitendo cha juzi cha Katibu Mkuu wa CHADEMA kumtimua Kafulia kazini na mwenzake Juju ni njia tu ya kuwaengua watu hao kwenye Uongozi wa CHADEMA na kwa kuwa wao ni watu wazima waliamua kujivua na Uanachama kabisa ingawa baadhi yetu tulimuona Kafulila kuwa hana hoja lakini kwa mtu mzima na kwa Kafulila hiyo ilikuwa ni rasharasha tu maana masika ilikuwa inakuja na kwa hekima akaamua kujivua na uanachama! Baadaye akafuatiwa na Juju. Wakati Kafulila akitimuliwa kazi na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mwasisi wa CHADEMA Mzee Mtei alikaririwa na gazeti moja akiunga mkono kutimuliwa kazi kwa madai kuwa Kafulia kwa nafasi yake hakuwa na haki ya kuhoji matumizi ya fedha za CHADEMA kwamba yeye Kafulila si Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA! Tujiulize hapo kwa kauli ya Mtei- yaani Mwanachama wa CHADEMA hana haki ya kuhoji juu ya mambo ambayo anaona hayaendi vizuri katika CHADEMA? Kwangu mimi naona kuna tatizo katika Uongozi wa CHADEMA na hata kwa Mwasisi wake Mzee Mtei.

Matukio hayo yaliyotokea CHADEMA na yanayoripotiwa juu ya watu kadhaa kujiengua kutoka CHADEMA si ajabu yakawa ni kweli na sitashangaa nikisikia watu mashuhuri ndani ya CHADEMA wakiendelea kujienguia kutoka chama hiki ambacho sisi wapenda mageuzi tunakiona kama nguzo ya upinzani nchini na hata kukichukulia kama Chama mbadala cha CCM.
 
Tujiulize hapo kwa kauli ya Mtei- yaani Mwanachama wa CHADEMA hana haki ya kuhoji juu ya mambo ambayo anaona hayaendi vizuri katika CHADEMA? Kwangu mimi naona kuna tatizo katika Uongozi wa CHADEMA na hata kwa Mwasisi wake Mzee Mtei.

Mkuu kwanini Tusianze kuhoji kwenye CHAMA TAWALA KWANZA ? Au mambo ya CCM yana kwenda vizuri ?
 
mimi naamini ninyi wanazi nado mna matatizo!....................
 
mbona hamhoji SHibuda anapotaka kugombea uenyekiti wa CCM na Urais?nyie watu vipi nyie?
 
NInashangazwa sana kuona jinsi ambavyo wasomi wengi Tanzania hawaoni namna CCM na serikali yake inavyofanya bidii kubwa kudhoofisha upinzani.

Kwa hakika mission kubwa zaidi ya CCM ni kuhujumu progress za vyama vya siasa. Mafisadi ndani ya CCM wanafadhili kwa wingi sana kazi ya kudhoofisha upinzani ili fursa yao ya kuifisadi nchi isiharibiwe.

Kibaya zaidi ni uhakika kuwa usalama wa taifa unafanya kazi kubwa ya kupambana na wapinzani na upinzani.

Vikwazo vilivyowekwa kwa kila atakayeingia upinzani ni mkakati muhimu sana wa kuhakikisha kuwa kambi ya upinzani inakimbiwa na kuepukwa na kila anayetaka maendeleo binafsi.

Kama kungekuwa na haki sawa katika uwanja wa siasa Tanzania, CCM isingekuwa madarakani.
 
Tujiulize hapo kwa kauli ya Mtei- yaani Mwanachama wa CHADEMA hana haki ya kuhoji juu ya mambo ambayo anaona hayaendi vizuri katika CHADEMA? Kwangu mimi naona kuna tatizo katika Uongozi wa CHADEMA na hata kwa Mwasisi wake Mzee Mtei.

Mkuu kwanini Tusianze kuhoji kwenye CHAMA TAWALA KWANZA ? Au mambo ya CCM yana kwenda vizuri ?

T Blister, Hicho Chama Tawala tumeshajua muda mrefu kuwa kinachechemea. Kwangu sinaoni hasara ikiwa kitaishia kama KANU ya Kenya na UNIP ya Zambia au MDC ya Malawi. Tatizo ni Chama Tawala kinaelekea kujifia halafu tunakosa Chama mbadala cha ku-take over na kutufikisha pale tunapopataka kwa ajili ya kutokuwa makini, kutoaminiana na kuendekeza visasi. Inatia uchungu!
 
Kwa hiyo; kwa vile CCM wana maruarua yao, basi ule uozo wa CHADEMA tuufungie macho? Kuna ubaya gani kuongelea upupu unaochanua CHADEMA hivi sasa bila kuacha kupiga vita ufisadi wa CCM?

CHADEMA tatizo ni moja tu, kuwepo madarakani kwa Mbowe akipigiwa kifua na Mzee Mtei. Mengine yote yanatokana na ubinafsi wa hao wawili.

CCM tatizo ni moja tu, JK. Aking'olewa halafu pakawa na uteuzi safi na wa haki wa kiongozi wake, CCM itanenepa na nchi itang'ara upya.

Tatizo ni kuwa Mbowe na JK wote hawako radhi kuachia utamu wanaoukalia. Zidumu fikra zao.
 
Matukio hayo yaliyotokea CHADEMA na yanayoripotiwa juu ya watu kadhaa kujiengua kutoka CHADEMA si ajabu yakawa ni kweli na sitashangaa nikisikia watu mashuhuri ndani ya CHADEMA wakiendelea kujienguia kutoka chama hiki ambacho sisi wapenda mageuzi tunakiona kama nguzo ya upinzani nchini na hata kukichukulia kama Chama mbadala cha CCM.

Ibrah bwana,

Mnakiona chadema kama nguzo ya upinzani nchini. - sio kama chama cha kisiasa chenye nia na uwezo wa kuongoza dola ya Tanzania?!

Posts zako huwa zinanifurahisha sana.
 
Kwa hiyo; kwa vile CCM wana maruarua yao, basi ule uozo wa CHADEMA tuufungie macho? Kuna ubaya gani kuongelea upupu unaochanua CHADEMA hivi sasa bila kuacha kupiga vita ufisadi wa CCM?

CHADEMA tatizo ni moja tu, kuwepo madarakani kwa Mbowe akipigiwa kifua na Mzee Mtei. Mengine yote yanatokana na ubinafsi wa hao wawili.

CCM tatizo ni moja tu, JK. Aking'olewa halafu pakawa na uteuzi safi na wa haki wa kiongozi wake, CCM itanenepa na nchi itang'ara upya.

Tatizo ni kuwa Mbowe na JK wote hawako radhi kuachia utamu wanaoukalia. Zidumu fikra zao.

Here we go again.

Katika wana ccm wooote, anayenifurahisha ni kubwajinga. Yaani akiona jina la mbowe anaruka kama kaombewa na Kakobe vile. Akihojiwa sana, anakimbilia kupondea wachaga (yaani ana chuki dhidi ya wachaga utadhani kuwa alipigwa kibuti na binti wa kimachame).
 
NInashangazwa sana kuona jinsi ambavyo wasomi wengi Tanzania hawaoni namna CCM na serikali yake inavyofanya bidii kubwa kudhoofisha upinzani.

Kwa hakika mission kubwa zaidi ya CCM ni kuhujumu progress za vyama vya siasa. Mafisadi ndani ya CCM wanafadhili kwa wingi sana kazi ya kudhoofisha upinzani ili fursa yao ya kuifisadi nchi isiharibiwe.

Kibaya zaidi ni uhakika kuwa usalama wa taifa unafanya kazi kubwa ya kupambana na wapinzani na upinzani.

Vikwazo vilivyowekwa kwa kila atakayeingia upinzani ni mkakati muhimu sana wa kuhakikisha kuwa kambi ya upinzani inakimbiwa na kuepukwa na kila anayetaka maendeleo binafsi.

Kama kungekuwa na haki sawa katika uwanja wa siasa Tanzania, CCM isingekuwa madarakani.

Kamende usisahau kuwa aliyeanzisha hii thread ni Ibrah na wachangiaji wengi watakuwa kina kanda2, chuma, Tumaini na kubwajinga.
 
...............

CHADEMA tatizo ni moja tu, kuwepo madarakani kwa Mbowe akipigiwa kifua na Mzee Mtei. Mengine yote yanatokana na ubinafsi wa hao wawili.............

Mbowe ni tatizo kwa lipi hasa?, kwa vile ni mchagga?
 
Back
Top Bottom